Mchukia Fisadi, Bubu Ataka Kusema, n.k.,
Mimi sioni ni vipi kiongozi wa Tanzania Bara, fisadi and such, anaweza kunufaika binafsi na Muungano. Kwa mfano kivipi, hebu nipeni nadharia moja. Nionavyo mimi, kama wewe ni kiongozi wa Tanzania bara, ungetaka huu muungano ufe, sababu moja ikiwa ni kwamba Wazanzibari wanamaliza Oxygen ya uongozi huku kwetu.
Wazanzibari tumewapa ki affirmative action fulani hivi, wanatengewa nafasi za uongozi lukuki wakati wanatoka kwenye kiwilaya kimoja tu, I mean, Unguja, Pemba zote (1660 sq. km) zinamezwa na Masasi (8,940 sq. km). zaidi ya mara tano. Lakini tunawapa V.P. wa muungano, mawaziri kibao, yani ni bwena, na wabunge lukuki wakati wanawakilisha watu kiduchu. Can't believe it, I mean, there are more Mtwarans than Zanzibaris. Sasa ni kwa nini waachwe wamalize Oxygen ya uongozi huku kwetu bara?