Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Hali ya hewa zanzibar ni mbaya ndege ya rais imeshindwa kutua kuja kumchukua kwa maana hiyo imerejea dar lakini kwa habari zaidi soma magazeti ya kesho utapata uhondo zaidi.

Na leo kuna kipindi cha chenel ten kuna mahojiano yale ya hamza kasongo kuhusu muungano msikose kuangalia waungwana na pia radio ujerumani (dw) jioni kuna roundtable na bbc pia kuna hivyo vipindi vya muungano binaendelea.

Kila la kheri
 
Bulesi,

Pointi kubwa hapo!

Ni nani hao wanaoupinga Muungano? Ni Waunguja? Wapemba? Je waliokimbia nje 1964? Ni Wazanzibari walioko nje ya Tanzania?

Je ni Watu wote wa Visiwani?
 
Hatuwezi kuendelea kula na ndugu anaemwaga mchuzi kila siku.tutapika mchuzi mwingine mpaka lini?,inabidi kaka mtu nifike mahali nami nimwage wali na maji ya kunawa ili ndugu asidhani ni mimi tu mwenye njaa.Halafu tujue mambo si shwari huko zenj na sasa hivi tatizo linaonekana muungano lakini kama haupo huko visiwani machafuko yatakayo tokea Somalia na Darfur tutaona kuna 'picnic'.
 
tupe mfano?
niko na wewe GAME THEORY. Watanganyika na Wazanzibari watakua na uhusiano mzuri bila ya huu muungano. kwasababu hakutokua na sababu ya kulaumiana. wanaofaidika nahuo muungano ni wachache. it's time to let it go.
 
kinacho kera zaidi ni ile system ya utawala ya muungano kuipeleka Zanzibar. imeua sekta zote za biashara na sasa wazanzibar wanalazimiswa kufuata utawala wa CCM. Rais wa Zanzibar anachaguliwa bara. sasa wazanzibar wamesha amka. kama ni fadhila basi inatosha. kama ni ujanja basi wamesha shtuka. miaka 10 nyuma zanzibar ilikua bora kuliko sasa hivi. system ya utawala mbovu wa bara imepelekwa Zanzibar. Wasisahau kama Zanzibar inamuamko wa kisiasa tangu enzi za kale. cha kujiuliza bara ,mali zote zilizokuwepo bara kwanini watu bado wana suffer hali ya maisha ngumu sana. wanZanzibar sio matata bali wana muamko tu wa kisiasa. the real change is coming,...coming soon!
 
Kwani faida yakuwa na idara ya hali ya hewa sio kujuwa taarifa zote za mwenendo wa hali ya hewa kila saa na dakika? hivi idara haikujuwa tokea jana au juzi kuwa mvuwa zitamwagika kwa wingi visiwani ili wao wampashe taarifa Mkuu wa Nchi ili atangulie siku moja kabla ya Sherehe?

Leo Muungano umesheherekewa na Vionozi wa Tanganyika peke yao wa Zanzibar hakuwepo ni dalili tosha kuwa sasa Muungano huu unakataliwa na Viongozi wenyewe wa Juu.

Kwa wale walioko Zanzibar ni Mashahidi kuwa hapakuwa na dalili yoyote kama pana Sherehe kubwa ya Kitaifa kwani hata Bendera Mbovu imeshindwa kupambwa ili kubadilisha mandhari ya kuonyesha kuwa tunasheherekea Muungano miaka 45.

SMZ haina habari na Muungano huu, na wananchi wananagalia

Kwani MFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUWAAAAAA
 
Taabu kubwa Visiwani ni watu wavivu ktk kazi!!!

Kubwa Visiwani wanalojua ni Kulalamika tu na kuomba msaada!!!

Wabara mnaojituma kufanya kazi mbona bado umaskini unawaandama? kwani mnatofauti kubwa ya kiuchumi na wa zanzibari?
 
Sasa hali ya hewa imeshasemwa ni mbaya ,hivi mlitaka afe ?

Mjadala wa Muungano sasa wageuka kama kaa la moto

ITV usiku, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Juma Duni Haji, alisema bila ya kuwa na serikali tatu kero za Muungano zitaendelea kudumu."Serikali ya Zanzibar ni ya watu na kila penye watu pana ardhi na pia ukisikia kuwa kuna harusi unategemea kumkuta mwanamke na mwanamume ukiwakuta wanaume watupu utashtuka," alisema Duni.
"Shughuli za serikali ni tatu (jurisdiction) kuna Muungano, Zanzibar na Tanzania Bara, hivyo kila shughuli hapa inahitaji serikali na hapo tutamaliza kero za Muungano kama walivyo wenzetu wa Uingereza.

Naye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Samuel Ruhuza alisema, serikali zinajaribu kupotosha historia kwa kuwa wanaitangaza tarehe tisa ya Uhuru wa Tanganyika kuwa ni ya Uhuru wa Tanzania na wanafunzi wanafundishwa na kupotoshwa hivyo shuleni, jambo ambalo si kweli.Ni uwongo mkubwa tunaowadanganya watoto wetu ili tuendeleze ufisadi.


Aidha, alifafanua kuwa wanaiacha Desemba 12 ya Uhuru wa Zanzibar na kusherehekea siku ya Mapinduzi ya Zanzibar na watu hawajui siku ya Uhuru wa Zanzibar.
"Tunapotosha na kufuta historia yetu ya Tanganyika, hali hii ni mbaya sana," alisema Ruhuza

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera alisisitiza kuwa makubaliano ya msingi ya Muungano yamekorogwa na kuingiliwa bila ya makubaliano ya pande mbili husika.
"Mambo ya msingi ya Muungano yalikuwa 11 tu, lakini sasa yameongezwa na kufikia 24 haya ndiyo yanayoleta mijadala na migogoro isiyokwisha," alisema Kimesera

Naye Kiongozi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar, Enzi Talib Aboud alisema wakati umefika serikali ya Tanganyika ni lazima ikarejeshwa au hapatalalika na kupatikana usingizi.

Wale watoto wanasema baba yao Nyerere alikuwa na haya :- Mzee Abeid Karume alikubali kuungana kwa sababu alikuwa anahitaji amani na usalama kutokana na hofu aliyokuwa nayo ya kuvamiwa na mataifa ya Magharibi; na huku Mwalimu Nyerere alikuwa na hofu ya kuathirika iwapo Zanzibar ingevamiwa. Si unajua machafuko yakiwa Zanzibar na Bara pia yana gharama zake," alisema Lwaitama na kuongeza:


"Tatizo la Muungano sio jina, jina si chochote. Tatizo linakuzwa kwa utashi wa wanasiasa tu, na ardhi ya Zanzibar kwa sababu ni ndogo ndio maana kukawa na vikwazo kwa watu wa Bara kumiliki, lakini kwetu sisi ardhi ni kubwa hata wakija Wazanzibari wote hawawezi kuimaliza."

"Mwalimu alikubali hayo ili Wazanzibari wasijione kama vile wamemezwa na ndio maana hata serikali, bendera na wimbo wa taifa wanavyo. "]Ukimwona mtu wa bara anapigia kelele hilo huyo ni mangi wa Tanganyika.
_________________________________

Nini maana ya Mangi wa Tanganyika ?
 
ananikumbusha Marehemu Mzee Karume alivyokuwa ana muIGNORE nyerere akimletea mamabo ya kipuuzi puuzi


safi sana sasa kilichobaki wabara waanze kuandika Makala ndefuuu kwenye magazeti yako yanayomilikiwa na Mafisadi

Labda na wao walitaka sherehe za Muungano zifanyike ZNZ kwa nini kila siku zifanyike Bara?
 
..hakuna haja ya kuanzisha serikali ya Tanganyika.

..masuala ya Tanganyika yanashughulikiwa na serikali ya Muungano.

..kama Zanzibar hawako tayari kuvunja SMZ na masuala yote yashughulikiwe na serikali ya Muungano basi wachukue hatua za kujitoa ktk Muungano.

NB:

..msimamo wangu mimi huu Muungano uvunjwe tu.


Mbona unajikanya kanyaga sasa ikiwa tuseme leo SMZ wajitowe kwa manaa hiyo Mnarudisha hiyo Tanganyika mliokuwa hamuitaki hata kuisikia wachilia mbali kuitwa nyinyi ni watanganyika ambayo ndio asili yenu .
 
Karume sasa ameamua kuwasikiliza ndugu zake, anajua mwisho wake unakaribia. kama nilivyo sema Zanzibar wana muamko wa kisiasa kuliko bara. change is coming,soon.
 
Yakhe kwanini tuandikie mate wakati wino upo? Nenda pale forodhani na utaona magunia ya vyakula .mayai tungule(nyanya) na vyakula tele vinavyovushwa kwenda Zenj.
Si kama tunasikitika , hasha ila ndio kielelezo cha ukulima wa Zenj.
Mtu ukufikia hata nyanya unaagiza nje basi umekwisha!!
Mkipata mafuta yenu na mtakapokuwa mmezoea mtavilipia vitu hivi kwa dola!


wale wanoishi mabara barani na kuomba huku na kule huwa tunawaita nini vile ?na nchi ikiwa inafanya kama hivyo huwa inaitwa ???nisaidie hapo neno limenitoka .
 
Hili litakuwa ni tatizo la hali ya hewa. Hii hutokea hata kwa nchi za wenzetu zilizoendelea hali kubadilika ghafla na ndege kushindwa tua kwa muda fulani. Sidhani kama ni mgomo. Lakini suala lina baki pale pale kuwa Muungano unalazimishwa na viongozi wakati hali halisi hautakiwi kuwa kama ulivyo.
 
Hili litakuwa ni tatizo la hali ya hewa. Hii hutokea hata kwa nchi za wenzetu zilizoendelea hali kubadilika ghafla na ndege kushindwa tua kwa muda fulani. Sidhani kama ni mgomo. Lakini suala lina baki pale pale kuwa Muungano unalazimishwa na viongozi wakati hali halisi hautakiwi kuwa kama ulivyo.

kwani hiyo weather forecast inafanywa asubuhi tuu? Ile mitambo yote walionunua ya haifanyikazi?

Mbona siku ya Jumanne walisema kuwa kutakuwa na mvua sasa usiniambie walikuwa hawajui kama hilo litatokea hivyo siamini kuwa washauri wake walikuwa hawajui hili

nadhani it was good for Zanzibaris to snub this idiotic ceremeony ambayo at most insherekea wao kuwa colonised na wabara


kila siku sherehe wanazifanyia Bara halafu wazanzibari wakilalamika mnawaambia ohhhh hawa nao wamezidi

mimi naona sawa tuuu walivyosnub hii shughuli
 


:twisted:
Wayi!!!! hilo ni dogo kwa mbara nairobi imepakana naye .TANGA,ARUSHA.MUSOMA.haina gharama.bara tutaweka . BUJUMBURA. kwanza wengine watafia hapa na mstuko wakisikia muungano umevunjika.labda ewe masikini hana alichowekeza hapa lakini walio wengi matajiri.watarudi na ugonjwa wa moyo.
kwa taarifa yako "vijisenti" vilivyowekezwa hapo ni sehemu ya faida ya pesa za dakaa, wazenj bwana ruti zao "umangani", " masteti" na london, hakuna atakae pata presha, wote walikuwa huku huku visiwani ufisadi tu wa SMT kuiharibia zanzibar biashara ndo vimewasukuma huko, na nyinyi mlikuwa mkija huku kuchukua vitu na kuviuza huko,na mkaona gere komandoo alipofanya bandari huru, sasa achilieni muone kama zanzibar haitafika 2025, kama singapore.
 
MOJA WAPO YA matatizo makubwa kule Zenj ni uvivu ulio kithiri.
Hawalimi maana wanasema si jadi yao ni ya WATWANA kulima.Kila aliyepo anataka kufanya biashara ya kununu bidhaa nje na kwenda KUUZA BARA.
Ardhi ya Zanzibar na Pemba , hasa Pemba ni nzuri mno kwa kilimo.Katika miaka ya 80 Mzee Kawawa alipo watembelea kule Pemba risala ilisomwa kuwa wanasikitika kuwa ski hizi(siku hizo) wanyamwezi hawaruhusiwi au wamepungua kuingia Zanzibar. Hivyo kilimo kimeathirika.Mzee Kwawa alishangaa sana na kuwa uliza kuwa , hivi nyinyi hamli mpaka mlimiwe.
Hiki ni kielelezo cha utegemezi kwa upande wa bara ambako vile vile kuna umaskini wa kutisha.Sasa ukimtegemea mtu/taifa jingine wakati wewe mwenyewe hujifanyii maendeleo yoyote ndio mwanzao wa kudai talaka kwa ajili ya kukosa matunzo.
Suala la kutenga na Zanzibar linaweza kuwa si suluisho la kudumu kwa matatizo ya Zanzibar maana baada ya matatizo haya ya reja reja bado kunatatizo kubwa sana la tofauti kubwa ya Zanzibar(mainisland) na Pemba.
Mimi nejihakikishia kuwa muungano ukivunjika leo wawili hawa hawaivi chungu kimoja.



Nyinyi sio wavivu lakini kiboko wao hata kumi hawafiki sasa wewe huoni akili za mamilioni ya watu huko hazifanyi kazi, kiboko Rostam na wenziwe kwa hilo inaonesha kuwa nyinyi mumelala usingizi mzito halafu ukiwangalia jamaa wapo tafauti na nyinyi.
 
yaani ujanja wote na maneno mengi wahindi saba unusu tu, wanatia ufukara nchi nzima, halafu mmebaki kama wapofu eti KIDUMU, na kidumu kweli , wala wazanzibar hawatakubali kukupeni mafuta yao muyahonge kwa majizi mnayalea.
 
Wanatuonea sisi wazanzibari tu ,kumbe waindi saba wanawaendesha puta ,hasila zao wanakuja kumalizia visiwani ,siku hizi hata mmasai anakwambia ana asili ya Zanzibar hii too much .afu unamkuta amevaa buibui yeye na mumewe ambae amevaa kanzu ya kialabu na kibalaghashia wanaenda kwenye taalabu ,yaani hana habali ya ng'ombe zake kabisa ,hatari ukija kumuita Mtanganyika anaweza kukuuwa.
 
jamani mbona hii hadithi iko upande mmoja tu? Je inamaanisha ni wazanzibari tu wanaokerwa na muungano? Azimio la G 55 linamaana gani? Nadhani mpaka tutakapokuwa wakweli na kuona mitizamo na hisi ya Tanzania na zanzibar ndipo tutaweza kutatua tatizo hili. Maana mjadala wetu bado unarudia makosa yale yale ya kikatiba ya kusahau Tanganyika.
 
Back
Top Bottom