Sasa hali ya hewa imeshasemwa ni mbaya ,hivi mlitaka afe ?
Mjadala wa Muungano sasa wageuka kama kaa la moto
ITV usiku, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Juma Duni Haji, alisema bila ya kuwa na serikali tatu kero za Muungano zitaendelea kudumu."Serikali ya Zanzibar ni ya watu na kila penye watu pana ardhi na pia ukisikia kuwa kuna harusi unategemea kumkuta mwanamke na mwanamume ukiwakuta wanaume watupu utashtuka," alisema Duni.
"Shughuli za serikali ni tatu (jurisdiction) kuna Muungano, Zanzibar na Tanzania Bara, hivyo kila shughuli hapa inahitaji serikali na hapo tutamaliza kero za Muungano kama walivyo wenzetu wa Uingereza.
Naye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Samuel Ruhuza alisema, serikali zinajaribu kupotosha historia kwa kuwa wanaitangaza tarehe tisa ya Uhuru wa Tanganyika kuwa ni ya Uhuru wa Tanzania na wanafunzi wanafundishwa na kupotoshwa hivyo shuleni, jambo ambalo si kweli.Ni uwongo mkubwa tunaowadanganya watoto wetu ili tuendeleze ufisadi.
Aidha, alifafanua kuwa wanaiacha Desemba 12 ya Uhuru wa Zanzibar na kusherehekea siku ya Mapinduzi ya Zanzibar na watu hawajui siku ya Uhuru wa Zanzibar.
"Tunapotosha na kufuta historia yetu ya Tanganyika, hali hii ni mbaya sana," alisema Ruhuza
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera alisisitiza kuwa makubaliano ya msingi ya Muungano yamekorogwa na kuingiliwa bila ya makubaliano ya pande mbili husika.
"Mambo ya msingi ya Muungano yalikuwa 11 tu, lakini sasa yameongezwa na kufikia 24 haya ndiyo yanayoleta mijadala na migogoro isiyokwisha," alisema Kimesera
Naye Kiongozi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar, Enzi Talib Aboud alisema wakati umefika serikali ya Tanganyika ni lazima ikarejeshwa au hapatalalika na kupatikana usingizi.
Wale watoto wanasema baba yao Nyerere alikuwa na haya :- Mzee Abeid Karume alikubali kuungana kwa sababu alikuwa anahitaji amani na usalama kutokana na hofu aliyokuwa nayo ya kuvamiwa na mataifa ya Magharibi; na huku Mwalimu Nyerere alikuwa na hofu ya kuathirika iwapo Zanzibar ingevamiwa. Si unajua machafuko yakiwa Zanzibar na Bara pia yana gharama zake," alisema Lwaitama na kuongeza:
"Tatizo la Muungano sio jina, jina si chochote. Tatizo linakuzwa kwa utashi wa wanasiasa tu, na ardhi ya Zanzibar kwa sababu ni ndogo ndio maana kukawa na vikwazo kwa watu wa Bara kumiliki, lakini kwetu sisi ardhi ni kubwa hata wakija Wazanzibari wote hawawezi kuimaliza."
"Mwalimu alikubali hayo ili Wazanzibari wasijione kama vile wamemezwa na ndio maana hata serikali, bendera na wimbo wa taifa wanavyo. "]Ukimwona mtu wa bara anapigia kelele hilo huyo ni mangi wa Tanganyika.
_________________________________
Nini maana ya Mangi wa Tanganyika ?