Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mbona mnazungumzia kuunda serikali ya tanganyika kama suluhisho la muungano....kama tatizo kila upande uwe na serikali yake basi kwanini tusiondoe serikali zote ijulikane kuwa wote tumekosa na ibaki hii ya Jamhuri ya Muungano maana naona tu wazanzibar wanatuamulia mambo yetu kama vile sie hatuna hisa kama hii UNION....nilichangia kwenye thread zilizopita na naendelea na msimamo wangu kuwa wanazenji acheni kutumika kisiasa kwani hakuna mantiki ya hoja mnazozitoa.

Kama ni usawa basi uanze kwa kuvunja serikali yenu afu ndo tuanze kuongelea haja ya serikali mbili. Mambo ya kumangamanga kisiasa hayatasaidia.
 
walioko Zenj tuelezeni kama kweli weather ndio problem au mkuu wa kisiwa analake?
 
Muungano huu ni wa wana TANU na ASP maana kimsingi hao ndo waloungana kiukweli.

Najitahidi kufahamu Nyerere alikuwa anatega kitu gani huko Zanzibar wala sipati picha. maaana kilichotokea ni kuwa imekula kwake. Karume alimchezea ile gemu inayoitwa "Chako Chetu" "ChanguChangu"

Au pengine Nyerere alikuwa na hamu ya kuwa Rais wa Nchi mbili. Lakini iko siku Watanganyika tutarudishiwa Serikali yetu tu. na hapo ndo itakuwa mwisho wa malalamiko haya ya Muungano.
 
Tayari Rais Kikwete kaingia uwanjani. Mshereheshaji hajaeleza bado kilichosibu hadi viogozi hawa wakuu wa juu kuamua kuendelea na hii shughuli bila ya Mwenzao wa Zanzibar kuwepo.

Ngoja niamini kwamba leo kunahotuba ya maana.
 
Zanzibar hawautaki huu muungano mbona mnakuwa wagumu kuelewa?

sijui nyie wabara muelezwe vipi mtaelewa

sherehe kubwa kama hiyo jamaa anaamua kuingia leo kwani inamaana rais mzima hana watabiri wa hali ya hewa?

nyie ndio mnaungangania huu muungano ni aibu kubwa
 
GT, you are damn right about haka ka-muungano--- sio Zenjibar pekee hata baadhi yetu wa bara hatuutaki na dhana kwamba we need it ni potofu
 
Katika siku kama ya leo (Muungano) utaona clip ya marehemu Mwl Nyerere kwenye tv mbalimbali, akichanganya udongo kuashiria muungano wa Tanganyika na Zanzibar (au zanzibar na Tanganyika).

Swali langu ni; udongo huo ni wa wapi?? Dar na Zanzibar?; Butiama na Zanzibar? Butiama Unguja? Songea na Zanzibar? Rukwa Na Pemba?? Bagamoyo na kusini unguja?! oohps!!
I am confunsed, naombeni jibu.
 
Kweli kabisa Karume hayupo uwanjani...na mambo yanaendelea kama kawa.....tusubiri hotuba ya vijembe ambayo haina meno.
 
Shughuli hizi kwa kawaida haziambatani na hotuba, labda kama mwaka huu kuna mabadiriko. Ni ukaguzi wa gwaride na kuondoka. Sana sana watu wa posho ndiyo watapata na baadaye kuwa na sherehe ikuru (Kikwetu na wateule wake na wageni).
 
Wabara je si Wavivu? Kwani kinachokuhamisheni vijijini na kujijaza mijini nini?
Huo uhodari wenu wa Kilimo mpaka sasa haujakutoweni katika kufa kwa njaa. Mko ndani ya Basi moja na Zanzibar angalau wao wana sababu kuwa hawapewi uhuru wa kufanya kazi zinazostahiki. Hivyo dhana yako kuwa maendeleo ya nchi zote yataletwa kwa kilimo? Hata hivyo kuna wakati Zanzibar iliwasaidia majirani wake kwa Fedha iliyotokana na Kilimo na sio kitu chengine.

😡 😕 😀
jamani, uhuru wa namna gani mpewe? kariakoo nzima imejengwa na wapemba, ilala yote wapemba, magomeni yote wapemba, tandika yote wapemba, kigamboni yote wapemba..
"Zanzibar angalau wao wana sababu kuwa hawapewi uhuru wa kufanya kazi zinazostahiki."

UPI TENA HUO?!! usimwamshe aliolala,utalala wewe!! wazanzibari wamewakejeli sana wabara. fimbo ni muungano. hatuoni manufaa ya muungano, bora uvunjwe!! lakini isiwe hodihodi tena. Hakuna kabila ya mpemba wala muunguja, wengine wamakonde, wengine wanyamwezi, kasumba tu ya kusema,"mimi mwarabu,mimi mwarabu!" hakuna lolote!!🙄

mmesahau wote mlikotokea!ni wizi wa fadhila, wenyewe kwanza hampendani, na pia mnaleta kasumba ya ubaguzi hata huku bara!
Muungano ufe, halafu tuone mtafikia wapi!!!!!!! hatuna haja nao, mnatunyonya tu!!!!
 
sasa ole wake mtu 2010 mtu aje alete pua yake huku, kupiga kura.........CCM, tapikwa supu anywewe....ya popo bawa yatakuwa madogo.

Mambo ya popo bawa niyo mnayafahafu kwa ufanisi mkubwa sana .Mungekuwa mnalima hivyo hivyo msingekuwa na shida ya kulilia muungano unakasoro kwa vile mwashinda kuganga njaa.
Hatuna haja ya kuja huko kwenye shida tupu na ila nyie ndo mmejazana huku bara-kweli si kweli?
 
Wabara je si Wavivu? Kwani kinachokuhamisheni vijijini na kujijaza mijini nini?
Huo uhodari wenu wa Kilimo mpaka sasa haujakutoweni katika kufa kwa njaa. Mko ndani ya Basi moja na Zanzibar angalau wao wana sababu kuwa hawapewi uhuru wa kufanya kazi zinazostahiki. Hivyo dhana yako kuwa maendeleo ya nchi zote yataletwa kwa kilimo? Hata hivyo kuna wakati Zanzibar iliwasaidia majirani wake kwa Fedha iliyotokana na Kilimo na sio kitu chengine.

Yakhe kwanini tuandikie mate wakati wino upo? Nenda pale forodhani na utaona magunia ya vyakula .mayai tungule(nyanya) na vyakula tele vinavyovushwa kwenda Zenj.
Si kama tunasikitika , hasha ila ndio kielelezo cha ukulima wa Zenj.
Mtu ukufikia hata nyanya unaagiza nje basi umekwisha!!
Mkipata mafuta yenu na mtakapokuwa mmezoea mtavilipia vitu hivi kwa dola!
 
safi sana Karume

kilichobaki tugawane kila mmoja kivyake

Dunia ya leo naamini ZNZ wanaweza kusuyrvive tuu bila matatizo na sie tukaendelea kubaki na MAFISADI wtu

SIJUI TUNANGANGANIA NINI

Sherehe kubwa kama hizo Rais analala mpaka saa 2 abubuhi kama si uhuni nini?
 
Lole Gwakisa, nakuunga mkono mia kwa mia, popo bawa wanajua wao! bara hakuna!
kila siku tunaona, anakataa nini? ndivyo walivyo, hawataki kupewa ukweli wao!Tuvunje Muungano, wapate mafuta, waingie kwa viza hapa Bara, waje wanunue vitu kwa dola. Vitu vyenyewe ni hivi vifuatavyo: nyama mbuzi, ng'ombe, kuku, bata, mchicha, vitunguu maji, vitunguu saumu, viazi mbatata, nyanya, njugu mawe, mahindi, mbaazi, maboga, ngano, etc.. Je, hivi vyakula vinatoka baharini? Muungano unawanufaisha wao!
wanapenda dhahabu kama nini! wanaipata wapi?! kama si bara?

:twisted:
 
Swala la kurudisha Serikali ya Tanganyika lina-justfy kuwa Wanzanzibari hawataki muungano. Sijui ni kwa nini CCM wanaung'ang'ania sana huu muungano. Hizo siri za muungano ziwekwe hadharani ili tuzijue, tuzione kama ni za msingi na zinatosha kutushawishi kuendelea na muungano. Kwa upande wangu naona huu muungano uvunjwe kila upande ujiendeshe kivyake. Au kama kuna ulazima wa kuwepo basi kusiwe na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tubaki na Serikali moja ya Tanzania na Zanzibar iwe ni sawa na mkoa kama mikoa mingine iliyoko Tanzania bara.
 
Sioni kuwa serikali 3 ndio jibu la matatizo ya muungano, na uchumi wetu huu tutamudu kweli serikali hizo? imagine mawaziri 120, marais 3, makamu wa marais 3, mawaziri wakuu 3, wote hao tuwanunulie mashangingi, tuwajengee ma office. Je hii serikali kuu ikipewa msaada katika mfumo wa 3 prez, huo msaada ndio unakuwa pasu pasu au serikali kuu inakukua 50%, tanganyika 25% na Zenj 25%? Nashangaa tunavyo umiza vichwa na kasehemu kadogo sana. Muafaka wa wenyewe kwa wenyewe umeshindikana, sasa mnategemea hili la muungano (bara vs zenj )ndio mtalimaliza? Kuna solution 3 hapo.(1) bara wawakatie wazenj pochi la uhakika na ajira za kumwaga (maisha bora kwa kila mzenj) bila kujali hali ya wabara (wabara unajua niwavumilivu bwana, wamemwaga damu Uganda, Msumbiji, Namibia achilia mbali ya IPTL, RM, BOT etc) SIIKUBARI HII
(2) Kuvunja muungano.... naunga mkono 100%
(3) SMZ kama kweli wapo serious watangaze kujitoa kwenye muungano, Karume atimue polisi na wanajeshi wa bara walioko zenj, swap wabara walioko zenj na wazenj walioko bara..hatakuwa na lawama kwa viongozi wa bara kuwa wamevunja muungano wa Nyerere na Karume 100%.......baada ya hapo Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanganyika. Huenda ikasadia pia kupunguza mafisadi, maana kuna mafisadi ya kizenj ukiyagusa tu, utaambia muungano.......
 
Wazanzibar wanawaombea watanganyika serikali, kwa ajenda gani? Nafikiri ingekuwa vyema kama wangedai wanavyovikosa. Tatizo la Zanzibar ni uroho wa viongozi wake na wala si wananchi. CUF wanajua chini ya muungano huenda wasiitawale Zanzibar Miaka 50 ijayo, na wale wa SMZ wanajiona kama ma DC chini ya muungano, na tetesi za kupatikana kwa mafuta kunazidi kuwatoa udenda. Wataangaisha sana, lakini hawataki kutaja manufaa ya muungano kuliko kulalamika kila siku. Wapemba pale Ilala na Tanganyika kote wanamiliki kiulaini rasilimali za kutisha pamoja na ardhi kuliko wa bara kule Zanzibar. Wa bara sasa hivi ni sifa tu ya kuwa na Zanzibar, kama ni mafuta hata huku bara yapo ya kuisha nusu milenia ijayo. Mtatoana macho muungano ukivunjika!
 
Back
Top Bottom