Wanaotakiwa kudai serikali ya Tanganyika ni Watanganyika wenyewe na si Wazanzibar.
Wazanzibar wana haki ya kudai mambo mengine yote, hili la kudai serikali ya Tanganyika si lao wala hawatakiwi kuwa na uchungu nalo.
Mimi kama Mtanzania kutoka ilokuwa Tanganyika sijawahi kumwomba hata mzanzibari mmoja kunisemea ili kudai serikali ya Tanganyika.
Hoja hii ya baadhi ya Wazanzibari ni hoja ya kukemewa vikali, kwa sababu lengo lake ni kurudisha nyuma hoja nzima ya kujadiri kero za muungano ambazo wote tunajua zipo na kamwe hazitakaa ziondoke mpaka sisi Watanzania wenyewe tuweke makalio yetu chini na kuzijadiri kwa kina na kuzitolea ufumbuzi wa kisheria.
Wote tumechoka kukoromewa na watu wanaojifanya kutetea muungano kwa misuli yao bila kuweka akili zao katika utetezi.
Lakini hatuwezi vumilia vitendo vya kuvuruga mambo na kuingilia haki za watu wengine na kuleta madai ambayo kisheria wasemaji hawana uwezo wa kuajadiri.
Kama hoja ya kudai Zanzibar hruru isiyokuwa mshiriki wa Muungano wa Tanzania haiwezi simama kwa miguu yake yenyewe mpaka hoja ya kudai Tanganyika iwekwe mezani, basi hoja ya kudai Zanzibar haina nguvu na pengine itakufa kwa kujikaba yenyewe kuliko kuuawa na watu.
Labda tu kama kuna maana nyingine ambayo mtoa hoja anaweza kuianisha, Sivyo "Shut Up and Drive".
Kama tungekuwa na tabia ya mtu kujiamulia jambo linalomuhusu basi tungekuwa Wastaarabu lakini hili halipo na ndio maana Wazanzibari wnaamuwa kuwalisheni dawa ile ile mnayoitumia nyie YA KUINGILIA MAMBO YASIYOWAHUSU>