Unajuwa mpaka sasa sijaona mchangiaji kutoka bara aliechangia bila kuweka jazba na kupofuliwa na jazba.

Wewe ni mnafiki sijapata ona, unadai wachangiaji wana jazba, na hiki hapa nini, ni lugha ya utulivu hii?


Unakasirika kuambiwa kwamba Unguja na pemba (1660 sq. km) ni ndogo kuliko Masasi (8,940 sq. km) ndani ya Mtwara, mkoa mdogo kuliko yote ya Bara next to Dar? Kwamba Wazanzibar wako over-represented bungeni, na kwamba wanamaliza Oxygen ya uongozi huku Bara? Wanzanzibar ndio mara nyingi wana matatizo, hata makala ya Salim Said Salim ulioibandika humu inawapiga madongo Wanzanzibar wenzako.

 
Huyu mwandishi Mzanzibari Salim Salim ni very clear-thinking, anawakosoa wenzake. Na anajua nyeti za historia ya Muungano kwa kuelezwa ana kwa ana na watu kama Kassim Hanga kabla hawajapotea kimazingira.
 

Bado hujaleta hoja ya maana ambayo inaweza kutusaidia. Kama Mapinduzi, Kuuliwa na Kuuwana, Usultani na Ubwana na kila ovu unalolifikiria kuwa Wazanzibari wanalo wameshajipima na kwa umoja wao wanasema wanataka mabadiliko ya mfumo wa Muungano basi na uwepo kwani si mnawaonea huruma ka kuwapenda? Busara za Wazee husema mtoto akililia wembe mpe na wewe kama unahisi kuundwa kwa Serikali ya Muungano itakayoacha kushughulikia masuwala ya Tanganyika peke yake yataleta usultani na mauwaji basi na iwe hivyo wao wenyewe wako tayari.
Undeni Upya Serikali yenu ya Tanganyika na Pinda hatokwazana tena na DR Taarab kwani Bunge atakaloongoza Pinda litakuwa halina Wazanzibari.
 
Unajua Bara wanasita kuona Visiwani pakikosa amani kama Comoro! Na jirani sana toka Tanga au Dar?

Hakuna ushahidi kuwa Visiwani will do any better than Commoro maana hata
wale wa Visiwani wanaochuma raslimali bara huwa hawapendi kuwekeza kwao!

Kama mnajali kiasi hicho nashindwa kufahamu kwa nini mnawakwaza kwa maendeleo yao. Kama mtawapa haki ndani ya Muungano basi mtaonaaibu watakavyokupiteni kwa maendeleo.
 


hawajarudisha tena mali zetu. vifaa vya kifita kwani walimpiga idiamini peke yao wakashindwa ndio wakaja kuiba vifaa vyetu.

wameipa ngòmbe farasi wakabakisha punda tu mpaka mitambo ya sim waliivunja walivyo kuwa watu wabaya na choyo wakatengeneza wao eti na sie tuwalipe wao
 

imekuuma murudi makwenu na mumbebe karume ndugu yenu.

nimesema kweli imekuwa ubaguzi
 
Nauliza tena hiyo serikali ya Muungano atagharamiwa na nani?

Hali ilivyo sasa: Idadi ya Watu Bara 40m na Visiwani 1m yaani 97% wa Watz Bara 03% Watz Visiwani

Sasa hiyo serikali ya 3 Muungano ambayo Visiwani watachangia 03%..(Wabunge, Pesa kuiendesha, Mawaziri, Majaji n.k) je hapo visiwani watakuwa na nguvu gani? Sii wataonekana wamemezwa na bara?

Kuna ungumu kidogo: hata zikiwa serikali 3 Visiwani bado wataona bado wanaonewa kwa vile ni wachache!
 


Jambo ambalo hujalitia maanani ni kuwa ukubwa wa nchi ndio ukubwa wa kugharamia na haja ya kuwa na uchumi mkubwa na udogo wa nchi na population una maana kiwango cha pato ndiyo ukubwa wa uchumi wao.
Angalia sasa msaada wa kama $ 500 milioni unaweza ukamaliza barabaa zote za Zanzibar wakati kiasi hicho kwa Tanganyika pengine Mkowa mmoja usitoshe.
Na kwa mantiki hiyo kiasi kinachohitajika kwa shughuli za Muungano hazitokuwa kubwa kwani tayari mambo mengi yatakuwa yashashughulikiwa na Serikali za Tanganyika na Zanzibar.
 
unamaanisha nini zanzibar haijatoa hata raisi mmoja? Mwinyi alikuwa nani?

Kwani ndugu yangu hujui kwo ni wapi? kule alilowea tu na sasa angalau angerudi wangemtambuwa kuwa ni mwenzao lakini wamemjengea nyumba pale Maisara inakaliwa na Maghost yeye yuko nyumbani.
 


Wanadhani watu hawajui yaliyotokea - sema wa Zanzibari wastaarabu hawapendi kuwasimanga watu, watuambie sasa ndege zetu za kivita za Mig zimeishia wapi?, ile meli ya jeshi MV Kasa wamejaribu kila njia kuifuta nembo isemayo Zanzibar lakini wapi, watafuta lakini hivi vitu vinajulikana na kama wanataka tupigiane hesabu basi na tuanze, fungu la pesa zetu za za kuundia Central Bank baada ya uhuru ziko wapi?.
 

Ahsante Ngekewa, hii ndio point nilokuwa naizungumzia lakini watu wengine bado wapo kwenye uendeshaji wa nchi wa siasa za chama kimoja.
 

Bado sio kweli kuwa Wazanzibari wengi wanataka uvunjike Muungano. Hebu tuwe brief,Zanzibar wanataka nini ndaninya Muungano;
- Wawe na haki ya kujiamulia mambo ya kuwaendeleza kiuchumi na sio kubanwa wakati hakuna kipingamizi kwa Tanganyika kwa vile Muungano ni Tanganyika
- Wanataka rasilimali zao ziwe chini yao kama vile rasilimali za Tanganyika zilivyo chini ya Tanganyika na kwa hili hata serikali ya Muungano imetamka kuwa mali asili kama almasi na dhahabu ni za Tanganyika pekee.
- Wazanzibari wanataka serikali ya Muungano ishughulikie mambo ya Muungano tu isichanganye na ya Tanganyika
Sasa ikiwa muundo wa Muungano ndio unaokwaza matakwa yao ya haki iweje useme Muungano hauna matatizo. Pasingekuwepo muungano pasingekuwepo interaction na matatizo haya ya sasahivi.
Kwa hivyo Muungano unatakiwa usahihishwe ili uwe hauna matatizo lakini kwa sasa una matatizo.
 
www.youtube.com

zanzibar 1964 part 1

tafuta hii uone nyerere alivyowafanya wazanzibar (waislam) pamoja na waarabu

juzi yule kafiri bungeni anasema wazanzibar ni watumwa hajui kuwa watumwa ni akina karume na akina nyuni jumbe na wenzake ni wauaji?
mtumwa anajulikana zanzibar kwani mtumwa hana kwao zanzibar kama karume?

na wauaaji wanajulikana wote na wakuja kwa mwenge
 



Kwani mambo ya Muungano ni mangapi? Hayo ndiyo yatagharamiwa na kama Urais basi Rais wa sehemu moja atakuwa Rais wa Tanzania kwa kupokezana.
 
Mwiba!
Mmh! Sikujua Jumuiya ya Uamsho ina malengo zaidi ya kuamsha waumini kuhusu mambo ya dini!
Au swala la Muungano limeshakuwa la kidini huko Zanzibar?
Au hii Jumuiya imebadili malengo?


Wale waliosema Kikwete ni chaguo la Mungu walikuwa walevi wa tende?
 


Ndugu yangu ukipata nafasi jaribu ku research uendeshwaji wa serikali za nchi zenye mfumo wa federation, maoni yangu kama kutakuwa na serikali ya Zanzibar/Tanganyika ambayo itashughulikia mambo ya Zanzibar/Tanganyika sasa huu uonevu utatokea wapi?, uendeshaji wa serikali ya muungano utatokana na mapato ya kwenye federal taxes ambazo zitakuwa sawa kwa kila mtu au company regardless anatokea zanzibar au la, pia kumbuka pia kuwa serikali ya muungano itatumia zaidi pesa hizi kule ambako kuna watu wengi hivyo watakuwa wanachangia mambo ambayo ingewabidi wachangie kama wangelikuwa hawamo kwenye muungano vile vile, kasoro ndogo ndogo zitakuwepo lakini hazitakuwa na nguvu kama ilivyo sasa.
 


Naam sina jazba kwani nalipa kulingana na deni. Penye kejeli malipo yake kejeli ikifuatiwa na hoja na panapo hoja malipo ni hoja moja kwa moja.
 
Huyu mwandishi Mzanzibari Salim Salim ni very clear-thinking, anawakosoa wenzake. Na anajua nyeti za historia ya Muungano kwa kuelezwa ana kwa ana na watu kama Kassim Hanga kabla hawajapotea kimazingira.

Naam! Niliiposti hiyo baada ya kuisoma na kama yuko mtu anaona hoja anazotowa hazina mwelekeo basi atapata kazi kuleta zake za maana zaidi ya hizi.
Usifikiri kuwa hakuna Wazanzibari ambao hawakuwasaliti wenzao lakini walifanya hivyo wakati ule lakini sasa wazanzibari watawaweka sawa.
 
WATANGANYIKA tutakuja kujuta kwa kuikataa TANGANYIKA yetu.tumekuwa tunaipiga vita kwa nguvu zote ,kule visiwani wanamsemo usemao usimtupe jongoo na kijiti chake, kwani ipo siku kile kijiti utakihitajia tena .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…