Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?

Unajuwa mpaka sasa sijaona mchangiaji kutoka bara aliechangia bila kuweka jazba na kupofuliwa na jazba.

Wewe ni mnafiki sijapata ona, unadai wachangiaji wana jazba, na hiki hapa nini, ni lugha ya utulivu hii?

Kama hujui maana ya Muungano si uzibe mdomo na ungojee utakaloweza kulifahamu? Unafikiri huo ukubwa wa Tanganyika una maana gani kiinchi, mbona kuna visiwa vidogo vidogo tu duniani vilivyo huru na kwa vile Zanzibar ni nchi sawa na Tanganyika Kistatus suala la ukubwa unabidi mlione nyie mnaowabana walio wadogo. Eti Masasi? Ina Status gani ulimwenguni?

Unakasirika kuambiwa kwamba Unguja na pemba (1660 sq. km) ni ndogo kuliko Masasi (8,940 sq. km) ndani ya Mtwara, mkoa mdogo kuliko yote ya Bara next to Dar? Kwamba Wazanzibar wako over-represented bungeni, na kwamba wanamaliza Oxygen ya uongozi huku Bara? Wanzanzibar ndio mara nyingi wana matatizo, hata makala ya Salim Said Salim ulioibandika humu inawapiga madongo Wanzanzibar wenzako.
175px-Tanzania_Mtwara.png

 
Kero za Muungano zitakwisha lini?

Salim Said Salim

....Mara nyingi husikika manung'uniko juu ya Muungano kutoka Visiwani. Ni kawaida nchi moja kubwa na nyingine ndogo zikiungana mdogo ndiye husikika akilalama - baadhi ya wakati bila ya sababu za msingi.

Si siri kuwa Muungano hutumiwa kama karata ya mwisho na baadhi ya watu, hasa wa Zanzibar, kulazimisha jambo wanaloliona linawanufaisha kisiasa kwa kutishia kuvunja Muungano pale wanapoona hoja zao zinawekewa vikwazo ndani ya CCM.

Wanaposakamwa kwa kufanya mambo yasiokubalika katika mfumo wa kidemokrasia, utawasikia tuachieni Zanzibar yetu na nyie mkae na Bara yenu. Lakini wanapobembeleza kura za maoni za Bara utawasikia wanausifu Muungano.

Kinachosikitisha ni kuona baadhi ya wazee, kwa vile walikuwa waasisi wa Muungano, ijapokuwa ulipoundwa hawakushauriwa, wanahisi vijana wa leo hawana haki ya kuuliza lolote isipokuwa kukubali kila kilichoamuliwa na kinachoakubaliwa na wakubwa. Huu sio mwendo mzuri katika dunia ya leo.

Sasa zinasikika kelele kutoka Visiwani kutaka masuala ya uchimbaji na biashara ya mafuta na bahari kuu yatolewe katika orodha ya Muungano. Mamlaka ya Kodi ya Mapato pia inalalamikiwa. Sijui kesho tutasikia malalamiko gani.

Ni vizuri pakachukuliwa hatua za uhakika na si propaganda kumaliza kero za Muungano na watu wa upande mmoja wasihisi wenzao wa upande wa pili wamependelewa. Vile vile ieleweke kuwa kama ilivyokuwa mkubwa hana haki ya kumuonea mdogo na mdogo naye hana haki ya kudeka ili mwenzake mkubwa amuonee imani.

Muungano una matatizo, lakini unaweza kukarabatiwa isipokuwa unataka mafundi stadi na waadilifu. Tukiwa tumetimiza miaka 45 tuifanye kazi hiyo kwa uadilifu na tuache kupiga kelele za kuwa mbioni wakati tumebweteka na hatufanyi lolote kumaliza matatizo ya Muungano.
Huyu mwandishi Mzanzibari Salim Salim ni very clear-thinking, anawakosoa wenzake. Na anajua nyeti za historia ya Muungano kwa kuelezwa ana kwa ana na watu kama Kassim Hanga kabla hawajapotea kimazingira.
 
Mkubali msikubali katika huu muungano Zenj is the junior partner kwa mantiki ya sababu zote, Kwa population kwa maliasili hata kwa eneo tu.
For a long time Zenj wamekuwa wakitutake for a ride kwa udogo wao na sasa wanataka kingi.
Ni vyema muungano ukafilia mbali ili wenzetu warudi 1964.
Ila wajue kwamba
Ubaguzi wa rangi zanzibar upo
Ubaguzi wa kiitikadi usio na mfano Zbar upo
Matatizo ya kisiasa kati ya waliopindua na waliopinduliwa 1964 bado yapo
Umaskini uliokithiri ( kama huku bara ) Zbar uko







Kabla hamjatoka katika muungano yatatueni hayo la sivyo vibaraka wa sultani watakapokuja kwenu wabara itabidi tushirikiane nao tu.

Kuna jamaa kasema hapa angependa kuungana na Kenya na kuweka makao Nairobo-RUKSA and see how fast nyang'aus devour you.
Ina bidi wenzetu waelewe kuwa kwa temperature iliyopo tumeanza kuwachoka kwa manun'guniko yasiyo kwisha wakati umaskini wanajiletea wenyewe

Bado hujaleta hoja ya maana ambayo inaweza kutusaidia. Kama Mapinduzi, Kuuliwa na Kuuwana, Usultani na Ubwana na kila ovu unalolifikiria kuwa Wazanzibari wanalo wameshajipima na kwa umoja wao wanasema wanataka mabadiliko ya mfumo wa Muungano basi na uwepo kwani si mnawaonea huruma ka kuwapenda? Busara za Wazee husema mtoto akililia wembe mpe na wewe kama unahisi kuundwa kwa Serikali ya Muungano itakayoacha kushughulikia masuwala ya Tanganyika peke yake yataleta usultani na mauwaji basi na iwe hivyo wao wenyewe wako tayari.
Undeni Upya Serikali yenu ya Tanganyika na Pinda hatokwazana tena na DR Taarab kwani Bunge atakaloongoza Pinda litakuwa halina Wazanzibari.
 
Unajua Bara wanasita kuona Visiwani pakikosa amani kama Comoro! Na jirani sana toka Tanga au Dar?

Hakuna ushahidi kuwa Visiwani will do any better than Commoro maana hata
wale wa Visiwani wanaochuma raslimali bara huwa hawapendi kuwekeza kwao!

Kama mnajali kiasi hicho nashindwa kufahamu kwa nini mnawakwaza kwa maendeleo yao. Kama mtawapa haki ndani ya Muungano basi mtaonaaibu watakavyokupiteni kwa maendeleo.
 
"For a long time Zenj wamekuwa wakitutake for a ride kwa udogo wao na sasa wanataka kingi.
Ni vyema muungano ukafilia mbali ili wenzetu warudi 1964.
Ila wajue kwamba
Ubaguzi wa rangi zanzibar upo
Ubaguzi wa kiitikadi usio na mfano Zbar upo
Matatizo ya kisiasa kati ya waliopindua na waliopinduliwa 1964 bado yapo
Umaskini uliokithiri ( kama huku bara ) Zbar uko

Kabla hamjatoka katika muungano yatatueni hayo la sivyo vibaraka wa sultani watakapokuja kwenu wabara itabidi tushirikiane nao tu".




Nadhani huelewi kuwa Zanzibar ilikuwa nchi kamili kabla ya 1964 na iliweza kujiendesha kiuchumi bila matatizo yoyote yale, vile vile kama unaweza angalia GDP au statistics zozote za kimaendeleo na kiuchimi za Zanzibar na Tanganyika kabla ya Muungano na ilivyo hivi sasa utaona ni nani anadhurika zaidi na huu muungano. Matatizo yote unayowatisha waZanzibari yapo pia Tanganyika na sehemu nyengine duniani na musione kuwa nyinyi ni wakombozi wa Zanzibar.

Unapozungumza kubebwa kwa serikali ya Zanzibar kumbuka pia kuwa serikali ya Zanzibar ilianza kufilisika wakati wa vita vya Kagera na mara baada ya vita wakati Nyerere alipotangaza miezi 18 ijayo itakuwa ya taabu, ukweli ni kwamba Nyerere alikuwa akibadilisha pesa Zanzibar, akichukua pesa za kigeni toka Zanzibar na kutupa pesa za madafu kwa exchange rate ambayo anaijua mwenyewe. Jumbe akienda baraza la mawaziri na kuwaambia tu ametoa kiasi fulani kuwapa bara bila ushauri wa mtu yoyote yule, sio kuwa tukihitaji pesa za madafu lakini tuliamini umoja na kuwasaidia wenzetu wala hatukusema kuwa tunawabeba hadi leo, leo tumefilisika mumesahau mpaka fadhila eti munatubeba na kutusimanga, sijui ni watu wa aina gani ndugu zetu nyinyi, kutusaidia hamutaki mpaka mutusimange tukitaka kutafuta misaada kwengine munanuna na kutuzuia, mfano OIC.

Hizi siasa za kisultani zimemalizika tangia 1964, hivi bado unafikiri kuna muarabu ambaye atataka kuja kutawala Zanzibar leo? afanalek!!!!!


hawajarudisha tena mali zetu. vifaa vya kifita kwani walimpiga idiamini peke yao wakashindwa ndio wakaja kuiba vifaa vyetu.

wameipa ngòmbe farasi wakabakisha punda tu mpaka mitambo ya sim waliivunja walivyo kuwa watu wabaya na choyo wakatengeneza wao eti na sie tuwalipe wao
 
Mchungajimakini!

Unapoandika punguza jazba

- Ni kweli kuwa wakristo ndio wenye nguvu katika utawala wa Zanzibar?

- Je ni kweli Zanzibar kuna Wakristo 40% na Wazanzibar 60%?

-Na hapo unamaana gani Wazanzibar wote ni waislam au wabara wote ni wakristo?

- Una uhakika kwamba wanaotoka bara kuja Zanzibar ni Wakristo tu au ndio ubaguzi wenyewe?

imekuuma murudi makwenu na mumbebe karume ndugu yenu.

nimesema kweli imekuwa ubaguzi
 
Nauliza tena hiyo serikali ya Muungano atagharamiwa na nani?

Hali ilivyo sasa: Idadi ya Watu Bara 40m na Visiwani 1m yaani 97% wa Watz Bara 03% Watz Visiwani

Sasa hiyo serikali ya 3 Muungano ambayo Visiwani watachangia 03%..(Wabunge, Pesa kuiendesha, Mawaziri, Majaji n.k) je hapo visiwani watakuwa na nguvu gani? Sii wataonekana wamemezwa na bara?

Kuna ungumu kidogo: hata zikiwa serikali 3 Visiwani bado wataona bado wanaonewa kwa vile ni wachache!
 
Vipi Viswani ina watu mil. 1 na Bara 40!

Je hiyo serikali ya Muungano nani atagharamia? Mtasema Bara itoe 95% ya budgeti ya Muungano..maana uchumi wa Visiwani mdogo! Sii bora tu kuendelea na serikali mbili za sasa?

Kubwa mie nalililiona ni nani agharamie huu Muungano wa serikali ya 3!

Hii ndo rationale ya kuwa na selikali 2 kulingana na udogo wa Visiwani!

Mfano Visiwani wangekuwa na uchumi mkubwa na watu wengi..Nyerere na Karume wangeanzisha serikali 3 wakati ule!


Jambo ambalo hujalitia maanani ni kuwa ukubwa wa nchi ndio ukubwa wa kugharamia na haja ya kuwa na uchumi mkubwa na udogo wa nchi na population una maana kiwango cha pato ndiyo ukubwa wa uchumi wao.
Angalia sasa msaada wa kama $ 500 milioni unaweza ukamaliza barabaa zote za Zanzibar wakati kiasi hicho kwa Tanganyika pengine Mkowa mmoja usitoshe.
Na kwa mantiki hiyo kiasi kinachohitajika kwa shughuli za Muungano hazitokuwa kubwa kwani tayari mambo mengi yatakuwa yashashughulikiwa na Serikali za Tanganyika na Zanzibar.
 
unamaanisha nini zanzibar haijatoa hata raisi mmoja? Mwinyi alikuwa nani?

Kwani ndugu yangu hujui kwo ni wapi? kule alilowea tu na sasa angalau angerudi wangemtambuwa kuwa ni mwenzao lakini wamemjengea nyumba pale Maisara inakaliwa na Maghost yeye yuko nyumbani.
 
hawajarudisha tena mali zetu. vifaa vya kifita kwani walimpiga idiamini peke yao wakashindwa ndio wakaja kuiba vifaa vyetu.

wameipa ngòmbe farasi wakabakisha punda tu mpaka mitambo ya sim waliivunja walivyo kuwa watu wabaya na choyo wakatengeneza wao eti na sie tuwalipe wao


Wanadhani watu hawajui yaliyotokea - sema wa Zanzibari wastaarabu hawapendi kuwasimanga watu, watuambie sasa ndege zetu za kivita za Mig zimeishia wapi?, ile meli ya jeshi MV Kasa wamejaribu kila njia kuifuta nembo isemayo Zanzibar lakini wapi, watafuta lakini hivi vitu vinajulikana na kama wanataka tupigiane hesabu basi na tuanze, fungu la pesa zetu za za kuundia Central Bank baada ya uhuru ziko wapi?.
 
Jambo ambalo hujalitia maanani ni kuwa ukubwa wa nchi ndio ukubwa wa kugharamia na haja ya kuwa na uchumi mkubwa na udogo wa nchi na population una maana kiwango cha pato ndiyo ukubwa wa uchumi wao.
Angalia sasa msaada wa kama $ 500 milioni unaweza ukamaliza barabaa zote za Zanzibar wakati kiasi hicho kwa Tanganyika pengine Mkowa mmoja usitoshe.
Na kwa mantiki hiyo kiasi kinachohitajika kwa shughuli za Muungano hazitokuwa kubwa kwani tayari mambo mengi yatakuwa yashashughulikiwa na Serikali za Tanganyika na Zanzibar.

Ahsante Ngekewa, hii ndio point nilokuwa naizungumzia lakini watu wengine bado wapo kwenye uendeshaji wa nchi wa siasa za chama kimoja.
 
Junius,
Mkuu unaposema hakuna Mzanzibar anayetaka Muungano ufe unakuwa tofauti na hoja nyingi nazozisoma humu..Mwiba, geme Theory na wengine wengi tu maelezo yao ni kutokuwepo kwa Muungano. Sasa nnachoelewa mimi sababu zote zinatokana na Muungano uliopo kutotambuliwa na wengi Wazannzibari..
Madai mengi yanahusu Bara na utawala wake wakati mimi nachofahamu ni kwamba Zanzibar iinataliwa na CCM Zanzibar hao kina Karume ambao sio tu wameiba Mapinduzi bali wamechukua hata mali zote na kuzifanya mali zao.. hata kidogo alichojenga marehemu baba yake kwa faida ya Wazanzibar leo hii ni mali yao (baraza la mapinduzi) na wajukuu wao..Tatizo sio Muungano uwe wa vyama ama nchi isipokuwa ni viongozi wabovu wanaoshindana kuchuma umaskini tuliokuwa nao.. Hizi ni sera za chama CCM ktk kujiandaa na Ubapari kwani wanataka kizazi chao kiwe ktk hali nzuri pindi Ubepari utakapo shamiri nchini.....It's simple as that. Hakuna chama hata kimoja nje ya CCM kinakubaliana na mfumo wa serikali yetu hivi sasa iwe bara au Visiwani hivyo tatizo haliwezi kuwa Muungano wenyewe hata kama ukivunjwa au kufanyiwa marekebisho ambayo bado yatakuwa for the interest of Party..

Nakubaliana sana na mtazamo wako ktk swala zima isipokuwa tu unachoshindwa kuelewa ni kwamba Muungano as Union hauna matatizo kabisa ila matumizi ya Muungano wenyewe..Wanachoomba wengi ni samli wakati hakuna maziwa, na kutokana na hasira za kukosa samli, suluhu rahisi kwao ni kuua ng'ombe kwa sababu maziwa hayawafikii wananchi..Hapa ndipo naposhindwa kuelewa mawazo mengi humu ndani kwani kama hutakuwa na ng'ombe kuna uwezekano gani wa kupata hata hayo maziwa acha mbali hiyo samli unayoitaka!..
Utasikia wakityoa mifano ya Jumuiya ya Afrika mashariki kama vile kuna uhusiano wowote kati ya Jumuiya ya nchi tawala na Muungano.

Mwiba,
Mkuu wangu sio kweli Zanzibar haitambuliwi duniani kwa sababu ya Muungano bali ukweli ni kwamba Tanganyika ndiyo isiyofahamika duniani..Na sidhani kama kuna mtu anataka kujua state za Missouri, Iowa, Mississippi au Ohio zinafahamika kiasi gani kulingana na New York, Florida, Michigan au California ili muungano wao uwe wa haki!
Pia, unapozungumzia Muungano wa nchi uliobomoka mkuu wangu ni muhimu ufuatilie pia kile kilichofuatia.. Yugoslavia ya jana sii ya leo, Urusi ya jana sii ya leo, Chec ya juzi sii ya jana na kadhalika, Uhasama uliopo kati ya nchi hizo huwezi hata kupima..kila moja yake ina historia mpya ya mauaji na ukabila kuliko wakati wowote, hivyo ni lazima nasi tuyaweke maswala haya bayana ili kila Mtanzania atakaye amua kuvunjika kwa Muungano apate kuelewa athari zake.. Ni rahisi sana kuzungumzia lakini inapotokea mkuu wangu ni sawa na swala la ndoa.. lazima mmoja wetu atapata mke/mme mwingine na mara zote wivu huingia kati na kuzua uhasama.

Bado sio kweli kuwa Wazanzibari wengi wanataka uvunjike Muungano. Hebu tuwe brief,Zanzibar wanataka nini ndaninya Muungano;
- Wawe na haki ya kujiamulia mambo ya kuwaendeleza kiuchumi na sio kubanwa wakati hakuna kipingamizi kwa Tanganyika kwa vile Muungano ni Tanganyika
- Wanataka rasilimali zao ziwe chini yao kama vile rasilimali za Tanganyika zilivyo chini ya Tanganyika na kwa hili hata serikali ya Muungano imetamka kuwa mali asili kama almasi na dhahabu ni za Tanganyika pekee.
- Wazanzibari wanataka serikali ya Muungano ishughulikie mambo ya Muungano tu isichanganye na ya Tanganyika
Sasa ikiwa muundo wa Muungano ndio unaokwaza matakwa yao ya haki iweje useme Muungano hauna matatizo. Pasingekuwepo muungano pasingekuwepo interaction na matatizo haya ya sasahivi.
Kwa hivyo Muungano unatakiwa usahihishwe ili uwe hauna matatizo lakini kwa sasa una matatizo.
 
www.youtube.com

zanzibar 1964 part 1

tafuta hii uone nyerere alivyowafanya wazanzibar (waislam) pamoja na waarabu

juzi yule kafiri bungeni anasema wazanzibar ni watumwa hajui kuwa watumwa ni akina karume na akina nyuni jumbe na wenzake ni wauaji?
mtumwa anajulikana zanzibar kwani mtumwa hana kwao zanzibar kama karume?

na wauaaji wanajulikana wote na wakuja kwa mwenge
 
Nkazahau,

Fed. gov. unayozungumzia kwa Visiwani na Bara..hizo 97% ya pesa kuendesha Fed. Gov. zitatoka bara!

Maana ukiangalia idadi ya watu: 97% ya Watanzania wanatoaka Bara na 03% ndo wanatoka visiwani!

Na kwa hiyo hata mawaziri atatoka tu mmoja au may be wawili, Wabunge yaani watakuwa 03% ya wabunge wa sasa yaani Visiwani watatoa tu Wabunge kama 10 wakati Bara watatoa zaido ya 300!

Bado tuko pale2: je hiyo serikali ya 3 nani ataiharamia? kama ni Bara: basi mfumo wa sasa bado una faida zaidi Visiwani!



Kwani mambo ya Muungano ni mangapi? Hayo ndiyo yatagharamiwa na kama Urais basi Rais wa sehemu moja atakuwa Rais wa Tanzania kwa kupokezana.
 
Mwiba!
Mmh! Sikujua Jumuiya ya Uamsho ina malengo zaidi ya kuamsha waumini kuhusu mambo ya dini!
Au swala la Muungano limeshakuwa la kidini huko Zanzibar?
Au hii Jumuiya imebadili malengo?


Wale waliosema Kikwete ni chaguo la Mungu walikuwa walevi wa tende?
 
Nauliza tena hiyo serikali ya Muungano atagharamiwa na nani?

Hali ilivyo sasa: Idadi ya Watu Bara 40m na Visiwani 1m yaani 97% wa Watz Bara 03% Watz Visiwani

Sasa hiyo serikali ya 3 Muungano ambayo Visiwani watachangia 03%..(Wabunge, Pesa kuiendesha, Mawaziri, Majaji n.k) je hapo visiwani watakuwa na nguvu gani? Sii wataonekana wamemezwa na bara?

Kuna ungumu kidogo: hata zikiwa serikali 3 Visiwani bado wataona bado wanaonewa kwa vile ni wachache!


Ndugu yangu ukipata nafasi jaribu ku research uendeshwaji wa serikali za nchi zenye mfumo wa federation, maoni yangu kama kutakuwa na serikali ya Zanzibar/Tanganyika ambayo itashughulikia mambo ya Zanzibar/Tanganyika sasa huu uonevu utatokea wapi?, uendeshaji wa serikali ya muungano utatokana na mapato ya kwenye federal taxes ambazo zitakuwa sawa kwa kila mtu au company regardless anatokea zanzibar au la, pia kumbuka pia kuwa serikali ya muungano itatumia zaidi pesa hizi kule ambako kuna watu wengi hivyo watakuwa wanachangia mambo ambayo ingewabidi wachangie kama wangelikuwa hawamo kwenye muungano vile vile, kasoro ndogo ndogo zitakuwepo lakini hazitakuwa na nguvu kama ilivyo sasa.
 
Wewe ni mnafiki sijapata ona, unadai wachangiaji wana jazba, na hiki hapa nini, ni lugha ya utulivu hii?



Unakasirika kuambiwa kwamba Unguja na pemba (1660 sq. km) ni ndogo kuliko Masasi (8,940 sq. km) ndani ya Mtwara, mkoa mdogo kuliko yote ya Bara next to Dar? Kwamba Wazanzibar wako over-represented bungeni, na kwamba wanamaliza Oxygen ya uongozi huku Bara? Wanzanzibar ndio mara nyingi wana matatizo, hata makala ya Salim Said Salim ulioibandika humu inawapiga madongo Wanzanzibar wenzako.
175px-Tanzania_Mtwara.png



Naam sina jazba kwani nalipa kulingana na deni. Penye kejeli malipo yake kejeli ikifuatiwa na hoja na panapo hoja malipo ni hoja moja kwa moja.
 
Huyu mwandishi Mzanzibari Salim Salim ni very clear-thinking, anawakosoa wenzake. Na anajua nyeti za historia ya Muungano kwa kuelezwa ana kwa ana na watu kama Kassim Hanga kabla hawajapotea kimazingira.

Naam! Niliiposti hiyo baada ya kuisoma na kama yuko mtu anaona hoja anazotowa hazina mwelekeo basi atapata kazi kuleta zake za maana zaidi ya hizi.
Usifikiri kuwa hakuna Wazanzibari ambao hawakuwasaliti wenzao lakini walifanya hivyo wakati ule lakini sasa wazanzibari watawaweka sawa.
 
WATANGANYIKA tutakuja kujuta kwa kuikataa TANGANYIKA yetu.tumekuwa tunaipiga vita kwa nguvu zote ,kule visiwani wanamsemo usemao usimtupe jongoo na kijiti chake, kwani ipo siku kile kijiti utakihitajia tena .
 
Back
Top Bottom