Junius,
Mkuu unaposema hakuna Mzanzibar anayetaka Muungano ufe unakuwa tofauti na hoja nyingi nazozisoma humu..Mwiba, geme Theory na wengine wengi tu maelezo yao ni kutokuwepo kwa Muungano. Sasa nnachoelewa mimi sababu zote zinatokana na Muungano uliopo kutotambuliwa na wengi Wazannzibari..
Madai mengi yanahusu Bara na utawala wake wakati mimi nachofahamu ni kwamba Zanzibar iinataliwa na CCM Zanzibar hao kina Karume ambao sio tu wameiba Mapinduzi bali wamechukua hata mali zote na kuzifanya mali zao.. hata kidogo alichojenga marehemu baba yake kwa faida ya Wazanzibar leo hii ni mali yao (baraza la mapinduzi) na wajukuu wao..Tatizo sio Muungano uwe wa vyama ama nchi isipokuwa ni viongozi wabovu wanaoshindana kuchuma umaskini tuliokuwa nao.. Hizi ni sera za chama CCM ktk kujiandaa na Ubapari kwani wanataka kizazi chao kiwe ktk hali nzuri pindi Ubepari utakapo shamiri nchini.....It's simple as that. Hakuna chama hata kimoja nje ya CCM kinakubaliana na mfumo wa serikali yetu hivi sasa iwe bara au Visiwani hivyo tatizo haliwezi kuwa Muungano wenyewe hata kama ukivunjwa au kufanyiwa marekebisho ambayo bado yatakuwa for the interest of Party..
Nakubaliana sana na mtazamo wako ktk swala zima isipokuwa tu unachoshindwa kuelewa ni kwamba Muungano as Union hauna matatizo kabisa ila matumizi ya Muungano wenyewe..Wanachoomba wengi ni samli wakati hakuna maziwa, na kutokana na hasira za kukosa samli, suluhu rahisi kwao ni kuua ng'ombe kwa sababu maziwa hayawafikii wananchi..Hapa ndipo naposhindwa kuelewa mawazo mengi humu ndani kwani kama hutakuwa na ng'ombe kuna uwezekano gani wa kupata hata hayo maziwa acha mbali hiyo samli unayoitaka!..
Utasikia wakityoa mifano ya Jumuiya ya Afrika mashariki kama vile kuna uhusiano wowote kati ya Jumuiya ya nchi tawala na Muungano.
Mwiba,
Mkuu wangu sio kweli Zanzibar haitambuliwi duniani kwa sababu ya Muungano bali ukweli ni kwamba Tanganyika ndiyo isiyofahamika duniani..Na sidhani kama kuna mtu anataka kujua state za Missouri, Iowa, Mississippi au Ohio zinafahamika kiasi gani kulingana na New York, Florida, Michigan au California ili muungano wao uwe wa haki!
Pia, unapozungumzia Muungano wa nchi uliobomoka mkuu wangu ni muhimu ufuatilie pia kile kilichofuatia.. Yugoslavia ya jana sii ya leo, Urusi ya jana sii ya leo, Chec ya juzi sii ya jana na kadhalika, Uhasama uliopo kati ya nchi hizo huwezi hata kupima..kila moja yake ina historia mpya ya mauaji na ukabila kuliko wakati wowote, hivyo ni lazima nasi tuyaweke maswala haya bayana ili kila Mtanzania atakaye amua kuvunjika kwa Muungano apate kuelewa athari zake.. Ni rahisi sana kuzungumzia lakini inapotokea mkuu wangu ni sawa na swala la ndoa.. lazima mmoja wetu atapata mke/mme mwingine na mara zote wivu huingia kati na kuzua uhasama.