Ukifanya cross-multiplication kuwa kulinganisha idadi ya watu Visiwani ingebidi wapate tu 2.5% ila sasa hivi hupata karibu mara 2 yaani 4.5%!

Sasa Mwiba anasema hawapewi hata ndururu na kupendekeza 50% sijui anatumia vigezo gani!
 
Anaeweza kuvunja Muungano ni Zanzibar anytime wakiamua tu ,ila wanawaonea huruma waTanganyika ,hivyo wanachojaribu ni Kuirudisha Tanganyika ,ili WaTanganyika wasije wakawalaumu hapo baadae mlichukua Zanzibar yenu mkatuwacha na mafisadi.

So you really believe Tanganyika needs Zanzibar badly that we can't survive w/out you? Na kingine hata isipo kuwepo Tanganyika kwa sasa muungano ukifa tu automatically Tanganiyka inarudi so point yako haijaenda shule. Kwani land ina seize to exist? ukizingatia most government assets zipo bara so huruma yenu inatoka wapi? Watu wengine hapa wanaongea kwa jazba na wanaendeshwa na misguided patriotism. They are doing their best to make points but wanashindwa in the end ndiyo wanaongea mambo ambayo hawana hata uhakika nao. Who told you Tanganyika hata sasa haipo? Kwani eneo la Tanzania bara ni nini? Muungano ukifa we have all the assets & infrastructure of the union on our land so the only thing left to do will be to construct a constitution & elect leaders. Jamani kweli shule muhimu na isipo kuepo walau akili za kuzaliwa mtu awe nazo.
 
Hizi kelele zimezidi! Bora uvunjike..kieleweke! Maana hizi kelele bara watavumilia hadi lini?

Taabu sasa Wapemba na Waunguja na shughuli nyingi bara kutokana na soko kubwa: sasa itabidi watafute passport na work permits?

Maana watu wa bara walioko Visiwani sii wengi!
 
Referendum tu ndiyo itakayokata mzizi wa fitna! Waulizwe wazanzibari na wale wa iliyokuwa Tanganyika kama wana haja na Muungano. Upande mmoja ukikataa basi Muungano uvunjwe na kila mmoja aangalie ustaarabu wake. Pande zote zikikubali basi wasioutaka wanyamaze na kuheshimu maoni ya wengi.

Amandla....
 
Mimi kwa mawazo yangu kusiwe na nchi ya Zanzibar bali tuwe na serikali moja ya Tanzania
 
Mimi kwa mawazo yangu kusiwe na nchi ya Zanzibar bali tuwe na serikali moja ya Tanzania

Je Visiwani watakubali ndugu na hizi kelele zilivyo nyingi kwa sasa??

Mie not optmistic at all over Muungano..yaani sijui kwa nini!!!
 
Wandugu heshima kwenu

Naomba niwahakikishie tu kuwa ingawaje hakuna ushahidi wa wazi lakini udongo inasemekana kuwa ulichotwa Machame Moshi kwa upande wa bara na ule wa visiwani ulichotwa Pemba Kusini
 
Tatizo kubwa la Zanzibar ni elimu na si serikali ya muungano ni tabia. Zanzibar hawawezi kulalamikia muungano kwa wa bara kwani kwenye huu muungano wabara wanafaidi nini?
 


Sasa naona tunarudi tena 1984 alipojiuzulu Aboud Jumbe na hesabu ya Nyerere ya 1+1=3. Tutalikimbia hili suala lakini bado litarajea tu sasa kazi kwetu kama tunataka kulishughulikia sasa au tutasubiri miaka 25 mingine.
 

Leo mushawachuna waZanzibari kwa miaka 45 na weshafilisika munawatafuta wacomoro nao muwachune- you people are the real Nyang'aus. "Mnaonea gombe tu ila simba pana chezea", kama kweli munataka umoja basi kwanini munasita na EAF, munajua the bigger Nyang'au yuko tayari kukuchuneni sio.

Zanzibar kuwa mkoa nadhani huwafahamu waZanzibari - jaribuni muone, itakuwa hadithi ya tembo kummeza chura hiyo.
 

Kwa kweli hili la misaada WaTanganyika wamezoeshwa vibaya tangu tokea enzi za mzee Abeid Karume, wakati huo uchumi wa Zanzibar ulikuwa mzuri na wala hawakutaka misaada hivyo wakiaachiwa tu waombe misaada na waitumie wanavyotaka, kama unaweza kuzipata basi sikiliza hotuba za mzee Karume anavyojinata kwa kusema Zanzibar haidaiwi na haitodaiwa maisha!!!, baada ya miaka 20 ya muungano mambo yamebadilika Zanzibar imefilisika na inahitaji misaada lakini wenzetu wa Tanganyika weshazoea kuchukua misaada yote na kutegemea Zanzibar kukaa kimya. Hawaelewi kuwa kama Zanzibar ingelikuwa haimo kwenye muungano basi ingeliweza kujipatia misaada yake kivyake na hii ingelikuwa ni zaidi sana ya hizo 2.5% wanazodai tunastahiki kutokana na watu wetu, pale tulipojaribu kupata misaada yetu wenyewe kwa kujiunga na OIC wamekuja juu hawataki, wao hawataki kutusaidia maana tumekuwa mzigo tukitaka kujikwamua kivyetu basi inakuwa nongwa - ndugu zetu hawa jamani hata hawaeleweki wee acha tu.
Pia huwezi kufananisha Zanzibar na mkoa kama Mwanza, Zanzibar ni nchi (entity ya JMT), muungano ni baina ya nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar na sio baina ya Zanzibar na kila mkoa wa Tanganyika, sasa sijui kwanini bado watu wanaifananisha Zanzibar na mikoa ya Tanganyika, au hii ndio sera ya siri ya Tanganyika kwenye muungano?, kuifanya Zanzibar kajimkoa?.
 
Hii dhana ya Mwiba kuwa kuwa maendeleo visiwani yataletwa kwa misaada (hand outs!), itafanya visiwa hivi kuwa nyuma kiuchumi miaka mingi ijayo!

Chapeni kazi: wakati wa utwana na mtumwa ulishaisha zamani!

Kama misaada haileti maendeleo basi wapeni Zanzibar misaada yote inayokuja Tanzania na nyinyi muchape kazi, kwa nini basi inakuwa issue wanapodai chao?, angalia historia na uone lini visiwa hivi vimeanza kuwa nyuma kiuchumi utashangaa, is it a mere coincidence or?
 


Ndugu yangu fanya research ya uendeshwaji wa muungano kwa njia ya federation na utapata majibu ya yote haya, ningependa kukuelezea kwa urefu lakini naona utaniumiza kichwa tu na sijui nitaandika page ngapi. Anyway - kwa ufupi kiti kitakuwa kimoja umoja wa mataifa, kutakuwa na hazina ya serikali ya muungano na hazina ya serikali ya Tanganyika na hazina ya serikali ya Zanzibar, mambo ya nje yatakuwa chini ya muungano. TRA itakuwepo au haitakuwepo itategemea na makubaliano yalivyo.

Kuhusu Tanganyika kuvunja uhusiano na West Germany ilikuwa zaidi ni Nyerere mwenyewe alotaka ku prove a point kuwa tuko huru na tutaamua nani awe rafiki yetu na sio kuwa accommodate wa Zanzibar.
 
Hamad says talks way out of current Union�s problems

2009-04-27 10:00:36
By Joyce Kisaka


The Civic United Front (CUF) secretary general, Seif Shariff Hamad, has said the present problems facing the Union can only be resolved through national dialogue.

He made the remarks during an exclusive interview with \'The Guardian\' on Friday ahead of the Union celebrations yesterday.

�To hold a national debate is very crucial in order to strengthen the Union and corrective measures should be taken thereafter, otherwise it would be difficult to deal with matters of the union,� he said.

He said the Zanzibar founding President Abeid Amani Karume wanted a three governments formula for the Union - Tanganyika, Zanzibar and the Union governments.

He said the Father of the Nation, Julius Nyerere, held a different view for the reason that Zanzibar�s identity must be maintained.

He said: �No one has doubts with what our leaders have signed in the Articles of the Union that formed Tanzania, but for the sake of the Union and its people, we have to see the original certificate of Articles of the Union.
Imagine, as we are talking now, no one in Zanzibar has seen them,� he said.

Hamad, who had held several posts in the Revolutionary Government of Zanzibar, including chief minister, said the Union itself had brought stability in the region as it had rendered its peoples to be much closer and that the advantages of the Union outweighed the disadvantages.

He added; a strong political will is what was needed on the part of the government and that people should be told clearly the truth about the problems. He said it was the national dialogue that would give them the chance to present their views.

Hamad said the three government sformula would have been the perfect one adding that what was happening now to the Union matters was unfortunate. He said their discussion was taking place in the national parliament involving few law-makers from the Isles.

He said it was very unfair for 20 people to speak on behalf of the whole of Tanzania.

Speaking on the burning issue of oil he said evidence exited that the matter was not discussed by the respective parties and that the Isles Attorney General during that period, Abubakar Hamisi, went to see Mwalimu Julius Nyerere on the same, but the latter said they would consider it in a meeting to be organised later.

Hamad said Zanzibaris were therefore of the stand that the matter was added to the list silently for reasons which they were yet to know todate.

He compared the matter with that of gas, which started to be the Union matter but since exploration of the same began at Songo Songo and Mnazi bay, Zanzibar had not benefited a single cent. He asked why was the arrangement put that way.
  • SOURCE: Guardian
 
 

Hebu jiulize hivi ni nani alieanza kuondoa au alietaka kuondolewa travel documents unaposafiri toka Zanzibar kwenda Tanganyika?, hizi travel documents zilikuwepo zamani tu na wala haziku affect kitu chochote. Soko sio Tanganyika pekee Kenya na nchi nyengine zipo, angalia uchumi wa Zanzibar kabla ya muungano na utaona kuwa kulikuwa na masoko mengine mengi tu kwa hivyo acheni kujidanganya.
 
Mimi kwa mawazo yangu kusiwe na nchi ya Zanzibar bali tuwe na serikali moja ya Tanzania

E bwana wee?, njozi za Alinacha hizo kama hamuitaki hata hiyo Changanyika basi jaribuni kuiondoa serikali ya Zanzibar tutabaki kuwa na nchi kama Somali vile.
 
Tatizo kubwa la Zanzibar ni elimu na si serikali ya muungano ni tabia. Zanzibar hawawezi kulalamikia muungano kwa wa bara kwani kwenye huu muungano wabara wanafaidi nini?

Wabara hawafaidiki kitu sasa na ndio maana hata hai make sense kuung'ang'ania muungano mbali na hiyo sifa tu kuwa ni nchi pekee ya Afrika ilo baki na muungano, kufaidika wameshafaidika zamani na ndio maana wana kiburi maana wanajua mua weshaufyonza sukari yaliobaki maganda tu, wee hushangai kwa nini wazanzibari wamekuja juu kwenye mafuta?, weshaumwa na nyoka hao............., natamani Nyerere angelikuwa hai akalijibu suali lako, angeliweza kukuambia jinsi gani mulivyofaidika.
 
Muungano waibua malumbano makali katika televisheni ya taifaNa Salim Said

MVUTANO mkali umeibuka miongoni mwa wasomi, wanasiasa na serikali katika mjadala kuhusu kero za Muungano uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Katika mjadala huo, baadhi ya washiriki walikua wakinyoosheana vidole na kutuhumiana kuwa, ndio wanaosababisha kukua na usugu wa kero za Muungano wa Tangayika na Zanzibar.

Mjadala huo ambao ulirushwa na Kituo cha Televesheni TBC1 uliwashirikisha baadhi ya wasomi, viongozi wa serikali na wanasiasa..

Waziri wa Nchi katika ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhmmad Seif Khatib alisema muungano umeimarika na kwamba ndoto za waasisi wake, ambao ni mwalimu Julius Nyerere na hayati Abeid Aman Karume zimetimia.

Kauli hiyo pia, iliungwa mkono na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azaveli Lwaitama ambaye alisema muungano umeimarika na kwamba, falsafa ya waasisi imetimia.

“Hata ukimuuliza ndugu yangu Duni hapo, atakwambia yeye ni Mtanzania, kero zinakuzwa na wanasiasa ambao hawajaelewa, yaliyokuwamo katika vichwa vya waasisi wa muungano huu” alisema Dk Lwaitama

Kauli hizo zilionyesha kumkera Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Juma Duni Haji ambaye katika kujibu hoja hiyo alisema, “kama kuimarika kwa muungano ni kuwepo kwa kero nyingi na matatizo, basi umeimarika lakini kama ni utatuzi wa matatizo na kero hizo, basi bado haujaimarika”.

“Katika mambo ambayo siyapendi na yananikera sana ni kuufananisha muungano huu kuwa ni wa mke na mume au mkubwa na mdogo. Huu ni muungano wa nchi mbili. Mimi nikiwa Katibu wa Wizara ya Fedha tuliisaidia serikali ya muungano dola 15 milioni za Marekani kulipa deni la Benki ya Dunia,” alisisitiza Duni.

Jambo hilo, lilimfanya muongoza mjadala huo ambaye ni mtangazaji wa TBC1, kumuomba radhi mwanasiasa huyo na kuruhusu mjadala huo kuendelea.

Duni aliendelea kutoa mifano ya kutoimarika kwa muungano huo kuwa, ni pamoja na kufukuzwa katika chama, kwa Rais mstaafu, Aboud Jumbe na maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alikuwa waziri kiongozi wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kutoka na kesi za muungano.

“Muungano lazima ulete faida kwa wananchi kisiasa, kiusalama na kiuchumi lakini Wazanzibari wanahoji kuhusu fedha za misaada na mikopo zinazoingia nchini kwa jina la Tanzania, kwa nini hawapati,” alihoji Duni

Alisema, jambo muhimu ni kushughulikia kero za muungano na si kuwa, mtu akisema aitwe katika vikao vya kamati kuu ya chama na kunyamazishwa au kuadhibiwa.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari, Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (Misa- Tan), Ayoub Rioba alisema, kama kuna mawasiliano yanayoeleweka, baina ya viongozi na wananchi, matatizo ya kero za muungano yatamalizika.

“Kama tutakuwa na mawasiliano imara baina ya pande mbili hizi, tatizo ni dogo sana lakini pia tuthamini michango ya mijadala kama hii, kwa kuwa bado sisi tunayo fursa ya kujadiliana, wenzetu wanatafuta lakini hawapati fursa ya kujadiliana” alisena Rioba.

Katika hilo, Dk Lwaitama alisistiza kuwa, dhamira ya waasisi ilikuwa ni umoja na mshikamano wa Watanzania na Waafrika lakini matatizo na kero ni jambo la kawaida.

Kwa upande wake waziri Khatibu alisisitiza kuwa, uhuru, usalama, amani na uchumi wa Zanzibar unategemea serikali ya muungano iliyopatikana baada ya kuungana kwa Zanzibar na Tanganyika mwaka 1964. “Muungano ni wa binadamu wala si wa malaika, matatizo hayaepukiki lakini tunafanya jitihada mbalimbali za kutatua kero na matatizo hayo” alisema Khatib.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…