kichuguu,jembajemba,mtumwitu,mkandara,
Habari ya Karume kum-consult Nyerere wakati wa mazungumzo ya Uhuru naweza kuita ni "smoking gun." Sasa ndiyo maana nimepumzika huu mjadala, nikijaribu kupitia upya, na kuchunguza tena, uelewa wangu kuhusu kipande hiki cha historia ya ZNZ.
Tunavyoambiwa lengo la mapinduzi ilikuwa kumuondosha mtawala mweupe ambaye alikuwa akifanya ubaguzi na kutowapa haki wengi tunambiwa haki ilikuwa ikipatikana kwa wachache lakini hadi hii leo ubaguzi upo tena unauma zaidi kwa kuwa anayetubagua ni mweusi mwenzetu. na miaka zaidi ya 40 sasa haki inapatikana kwa wacheche ambao wana madaraka yaani wakubwa na familia zao ndio
wanaonufaika hivi sasa.
Stonetown,
Njembanjemba,
Nadhani huko nyuma nimeeleza vizuri sana kutokuwepo kwa usawa wa ktk chaguzi zetu na kusema kweli tatizo kubwa la Kisiasa nchi Zanzibar limeletwa na kurudishwa kwa vyama vya Upinzani, yaani tumurusisha uhasama ule wa mwanzo ambao ulifikia Mapinduzi! Yawezekana kabisa wakati wa vyama vingi nchini humo haukuwa tayari kama ilivyo bara ambako bado watu wanafikiria kuwa Nyerere yuu hai kiasi kwamba unapokuwa na mtazamo tofauti ktk mrengo basi wewe ni adui wa nchi.
Sina budi kumpongeza JK kuweza kustahimili mikiki ya sasa hivi hasa ktk magazeti na pengine kuacha wananchi watumie nafasi kama hizi kujieleza. Hofu yangu sio JK na nina hakika sii yeye mwenye nguvu nchini ila ni CCM na hilo baraza la Mapinduzi. kwa hiyo zikusanyeni nguvu zenu sio kwa uhasama bali ktk njia iliyonyoooka kama vile unavyosoma Surat L'Fatah!
Tatizo lenu mnawapa CCM kisa sababu ya kutumia maguvu kwani wakitangaza Uchaguzi tu nyie mnaanza kusema damu zitamwagwa! mara msione Polisi mawe!.. vigenge vya kihuni ndivyo viunavyowapa hawa jamaa kila sababu. Tumiieni chama chenu kuweka mikutano ya amani na kutoweka tofauti zenu za rangi ama Upemba! msiwe wajinga kama ndege kurushiwa mtama mkafikiri ndio mnapendwa sana. Wenzenu wana njaa na njaa hii haiwezi kuondoka hadi Kiyama kwani shibe ya binadamu huenda kwa masaa!.. na ndinyo ilivyo tamaa ya Utajiri!..
Tumiieni chama chenu kuweka mikutano ya amani na kutoweka tofauti zenu za rangi
Under_age,
Kuna sehemu nimekuuliza kama sii wewe basi itakuwa Njembanjemba kama una rangi?... ilikuwa utani lakini sasa ngoja nikupe ukweli.
sidhani kama kuna umuhimu wa kujua rangi yangu katika hii mada.ila kama utaihitajia nambie nitakutumia PM, ila tukianza kuulizana rangi hapa ukumbini nadhani tutapoteza lengo la kutaka kuwaunganisha waliotengana.
ama kuhusu siasa ya zanzibar ,nitaungana na jemba jemba kwamba bado mkandara ni mgeni saaaaaaana wa siasa ya zanzibar , na ningekueleza mifano mingi, ila napenda niwaunganishe wazanzibari kwa kampeni ya nyumba kwa nyumba ,kuliko kudhihirisha utengano wetu hapa ukumbini. ila kama utapendelea nikupe mifano kadhaa wa kadhaa ya siasa ya zanzibar basi nijulishe na nita ku PM.kama unafikiri wazanzibari wa sasa wanabaguana kwa rangi, basi umekwenda mchomoo, hilo neno warabu na sultani linatumika kwa kampeni tuuu lisikusumbue.
jemba jemba,kichuguu,mzalendohalis,stonetown,mtumwitu, na wengineo , ahsanteni na kwa pamoja ,basi ipo siku tutafanikiwa.dhulma zimezidi kila kona ya ulimwengu,ila tujitahidini kwa ajili ya vizazi vijavyo,kama hatukufaidi sisi watafaidi watoto wetu.
ni mdogo wenu underage.
Kuhusu mauaji ya Karume, kweli yalikuwa ni ya kulipiza kisasi. Kijana mmoja aliyekuwa ASP aliuliwa na baba yake ambaye hakuwa ASP katika mapinduzi yale pia. Baada ya kijana huyo kupata kamisheni ya jeshi na kuwa Luteni ndipo akaamua kulipiza kisasi.
Under_age,
Tena nashukuru sana unaposema kwamba Zanzibar leo hii watu hawatazamani kwa rangi zao... hii ni alama kubwa sana na mafanikio ya Mapinduzi yale. Na kama umewahi nisoma mara nyingi mimi sipendi kabisa tunapo jadili kitu kwa kuzitazama nafsi zetu, rangi zetu, jinsia zetu bali hupenda kujadili issue zinazotuhusu sote kwa ujumla.
Kwa nilivyowahi sikia mimi ni kuwa muungano huu Karume aliutaka kwa muda wa miaka 10 tu - sasa huu muungano wa kupeana muda maalumu sijui muungano gani?
Hii nilikuwa sijaisikia, kama ni hivyo basi aliuwawa miaka miwili kabla hajatimiza azima yake ya kumaliza muungano huo katika miaka kumi.
There was also a period when the government stopped importation of food and encouraged self reliance. Some allege that the govermnent used foreign currency to import large arsenals of weapon in preparation for the eventual pull out of Nyerere's support. It is claimed that the union was originally planned for only 10 years and was to end in 1974.
Ukiwasikiliza wazanzibari utachanganyikiwa.madai yao ni zaidi ya laki moja hasa ukikaa kwenye vijiwe vya kahawa.Mpaka sadani wanadai iko zanzibar ndio maana hata kwenye TV hawaonyeshi hali ya hewa ya huku bara lakini sadani wanaionyesha.Kero za muungano kero za muungano hakuna kero yeyote.Hayo mafuta hayajapatikana wanataka kupwewa mgao wa dhahabu ya shinyanga.je yakipatikana.jamani tujaribu kuwa wakweli zanzibar watu si zaidi ya milioni moja.baadhi wengi wao wanaishi huku bara mpaka vijini huko hakuna anayemzui mzanzibari katika shughuli yeyote.wengine wameajiriwa bara kama vile ni wabara.fedha za kigeni wanatumia za bara kununua mahitaji yao nje lakini wao hawana export kubwa yote haya hawaoni.lakini ukisikiliza manung'uniko yao utadhani bila zanzibar bara hakuna kitu kumbe ni kinyume chake.mimi ninaona hakuna haja kuwa na nci mbili zanzibar iwe ni mkoa/mikoa.