mkandara.nilitumia jina la nyerere kwavile wewe ulitumia jina la nyerere kwamba ndilo lililoweka uhuru wa kweli zanzibar.hivyo madam umemhusisha nyerere na uhuru wa zanzibar ni lazima ukubali kumhusisha vile vile katika kusimamia haki za binadamu zanzibar.pia usisahau kwamba baada ya mapinduzi, na zanzibar na tanganyika kuungana ,nyerere alikuwa rais wa tanzania na sio wa tanganyika,hivyo apende asipende suala la zanzibar lilikuwa linamuhusu.lakini je nyerere aliweka usawa zanzibar? jibu liko wazi sina haja ya kujibu. je wanamapinduzi wameweka usawa zanzibar? jibu liko wazi haina haja ya kujibu. kuhusu suala la kwamba hata mikoani tanzania bara kuna kudumaishwa kimaisha na kielimu nakubaliana na wewe ila labda kidogo nitumie lugha utakayoifahamu zaidi.pemba kuna ukiukwaji wa haki za binadamu kwa maksudi mazima yaliotokana na siasa mbovu na potofu.na sio pemba tu bali hata sehemu za unguja.siasa ya zanzibar huwezi kuijua kama hujaishi zanzibar.
kuhusu sultani kukataza weusi kuoana na weupe sina uhakika nalo isipokuwa nawajuwa wazanzibari wengi ambao baba mweusi mama mweupe na kinyume chake.labda utupe ushahidi. hata hivyo mie hapa siongei kwa kumtetea sultani wala okello.ninachoongelea kwamba mapinduzi yale yameongeza athari kwenye visiwa vya zanzibar kuliko faida.kwani kile tunachoambiwa kiliondoshwa kwa sultani sasa kiko vile vile au kimezidi , ni sawa na kwamba "mbwa" tumemuita "dog". muhimu ni kwamba miaka mingi imepita na umefika muda sasa wa kuanza ukurasa mpya na kuachana na historia hii ilioichafulia jina na heshima, zanzibar.kuungana kwa watanzania wa upande wa zanzibar ni suala muhimu sana kwasasa,kwa maslahi ya zanzibar yenyewe na hata kwa maslahi ya watanzania wanaopenda usawa na uadilifu.
pia usisahau mkandara ,yule unaemuona wewe ni shujaa kuna wengine wanamuona msaliti,hivyo usilazimishe mtu fulani lazima akubalike na watu wote.muelezee mtu kwa unavyomjua wewe na acha mwengine amuelezee anavyomuelewa.