Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
kichuguu,
1.hivi ni kigezo gani kilitumika kumfanya Sultani kuwa Head of State wa ZNZ? Zaidi, vigezo hivyo vina uhalali gani?

2.Zaidi, HIZBU na ZPPP walikuwa na msimamo gani kuhusu kuwepo kwa Sultani ZNZ, na mamlaka yake?

3.Nini kiliwazuia ASP kuunda serikali baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 1957? Why were the elections called again in 1961, and 1963?
 
kichuguu,
tayari yapo maelekezo ya Zanzibar kupewa 4.5%, na wamekuwa wakipewa kiwango hicho. yale manunguniko uliyosikia, yalitokana na Zhakia Meghji kuahidi "kuwachotea" zaidi kutokana na "huruma" zake tu.

kuna kajarida kameandikwa na Prof.Teddy Malyamkono, pamoja na watafiti wengine wa taaluma mbalimbali. Naomba ukatafute, kwasababu kanaelezea mambo mengi yanayohusu mahusiano ya kichumi baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Mimi nadhani Zanzibar waachiwe wachimbe mafuta yao bila kuingiliwa na Tanzania Bara. Ni AIBU kwa Taifa la watu millioni 37 kuanza kusumbuana na waZanzibari millioni 1.
 
JokaKuu
Hayo Mafuta yapo? au yapo kisiasa?
Hivi kwa mfumo wa sasa- ni nani ana anufaika zaidi? Manake naskia Zenj hata hawatoi mchango wa sekta za Muungano. Halafu hii debate ya Muungano mbona ni one sided? Kwa nini mara nyingi malalamiko hutoka tu visiwani?
Kuna hisia toka visiwani kuwa bara wanainyonya Zenj- ila sijui kwa nini bara nao huwa hawalalamiki!
 
mzalendo wa bara nao wanalalama sana tu, mfano kama ww unaona zanzibar inapendelewa kwa kutotoa mchango wa muungano
 
MzalendoHalisi,
Kuna habari kwamba Zanzibar walisaidia kifedha wakati wa vita vya Kagera. Zaidi ya hapo hawajakuwa wachangiaji wazuri ktk kuendesha masuala ya Muungano.

Lakini tukumbuke kwamba Wazanzibari wako millioni 1, wakati Watanganyika tuko millioni 37.Wazanzibar wakichangia, au wasipochangia, sioni kama it will make any difference.

Kuna uwezekano there are as many Tanganyikans as Zanzibaris who are not happy with our Union. Sasa hiyo peke yake haitoshi kusema kwamba Watanganyika hawautaki Muungano. Watanganyika wengi hawana habari na huu Muungano na hauathiri moja kwa moja maisha yao ya kila siku.

Hili suala la mafuta usije ukashangaa WaZanzibari wakakaa kimya ikiwa Tanganyika wataanza kuchimba kabla yao. Sasa hivi Zanzibar wana kitete kwasababu wanafikiri the prospects are better on their side.

Naitafuta ile hoja ya G-55 kuona wale wabunge walikuwa na hoja gani. vilevile kuna ripoti ya kamati ya william shelukindo nayo itatueleza vizuri nini kinaendelea ktk muungano huu.

Binafsi nafikiri ZNZ wasiingiliwe katika matumizi ya rasilimali zao kama Madini na Mafuta.
 
Mtumwitu,

  1. Niliwahi kuisoma ile hotuba ya Sheikh Shamte aliyoitoa kule umoja wa mataifa ila nilikuwa najaribu kukumbuka niliisoma wapi. Hotuba ile ilikuwa ni ya kitaifa kweli kweli. Sikuwahi kuona hotuba yoyote iliyotolewa na Sheikh Karume kwenye umoja wa Mataifa.
  2. Ukweli kuwa HIZBU/ZPPP vilikuwa vyama inclusive vilivyokuwa na mwelekeo wa kitaifa ni wa wazi kabisa. Hii hotuba ya Muhsin inaonyesha hivyo, sikujua kuwa Rais Mwinyi aliwahi kuteuliwa na HIZBU/ZPPP kuwakilisha Zanzibar huko Indonesia licha ya kuwa wa ASP. Je kweli ASP walikuwa na ubavu wa kumteua mtu kutoka HIZBU/ZPPP kama walifikia kuipindua serikali yao na kuuwa watu wengi vile?
  3. Nashukuru kwa hiyo historia fupi ya Zanzibar. Binafsi, nimekuwa nahangaika kuiweka pamoja kuonyesha jinzi gani ilivyokuwa makosa kwa ASP kuwabagua waarabu wa Zanzibar kulingana na historia ya Zanzibar.

JokaKuu

Kipindi chote ambacho Zanzibar ilikuwa chini ya himaya ya Uingereza, bado kulikuwa na Sultani pale. Orodha yao ni kama ifuatavyo (nimeitoa Wikipedia)
  • Sa'id ibn Sultan - 14 September 1806–19 October 1856
  • Majid ibn Sa'id - 19 October 1856–7 October 1870
  • Barghash ibn Sa'id - 7 October 1870–26 March 1888
  • Khalifa ibn Sa'id - 26 March 1888–13 February 1890
  • Ali ibn Sa'id - 13 February 1890–5 March 1893
  • Hamid ibn Thuwayni - 5 March 1893–25 August 1896
  • Khalid ibn Barghash - 25 August–27 August 1896
  • Hamud ibn Muhammad - 27 August 1896–18 July 1902
  • Ali ibn Hamud - 18 July 1902–8 December 1911
  • Khalifa ibn Kharub - 9 December 1911–9 October 1960
  • Abd Allah ibn Khalifah - 9 October 1960–1 July 1963
  • Jamshid ibn Abd Allah - 1 July 1963–12 January 1964
  1. Ingawa masultani hawa walikuwa na asili ya Oman, kuanzia Sultani Khalifa bin Kharoub masultani wote walikuwa ni Wazanzibar waliozaliwa na kukulia Zanzibar na wala hawakuwa na uhusianao na usultani wa Oman. Hii inategemewa kwa vile Zanzibar ilikuwa imeshachukuliwa na waingereza walioitawala kuanzia mwaka 1890 hadi 1963, kwa hiyo usultani haukuwa na nguvu tena: walikuwa wapo wapo tu. Kama Zanzibar ilikuwa chini ya Sultan wa Oman, isingekaribishwa kwenye Umoja wa Mataifa baada ya uhuru wake.
  2. Mara zote wakati uingereza ilipokuwa inatoa uhuru kwa makoloni yake, ilikuwa inabuni mfumo wa serikali itakayobaki pale. Ilifanya hivyo kwa Tanganyika tukapewa Waziri Mkuu chini ya malkia, ilifanya hivyo hata kwa Zimbabwe mwaka 1980 na ilifinya vivyo hivyo kwa Zanzibar. Ila badala ya kuacha Zanzibar chini ya malkia waliamua ibaki chini ya sultani. Nchi nyingine kama Australia zilikubaliana na muundo huo zikabaki na Waziri Mkuu chini ya malkia wakati nchi nyingine kama Tanganyika hazikukubali mfumo huo hivyo zikajitoa baada ya muda mfupi tu. Zanzibar nayo ingeweza kujitoa kutoka kwenye usultani kama haikuwa inaupenda, lakini siyo kwa kumwaga damu na kuvunja misingi ya demokrasi iliyokuwa imeanza kujengwa.
  3. Inawezekana kweli HIZBU na ZPPP walikuwa wanashabikia usultani. Kama nilivyosema hapo juu, kwa vile Sultani ilikuwa ceremonial post tu, ingeweza kufutwa kwa kufanya marekebisho ya Kikatiba. Kama Nyerere aliondoa machifu wote walioachwa na mkoloni, ni nini kingezuia ASP kumwondoa sultani kama ingekuwa na mandate ya wananchi?
  4. Uchaguzi wa mwaka 1957 haukuwa wa kuunda serikali bali ulikuwa wa kupata wajumbe wa kuingia kwenye baraza la kutunga sheria. Kwa hiyo ingawa ASP ilishinda viti vyote haikuunda serikali kwa vile walikuwa wamegombea viti vhichahe tu kati ya viti vyote vya baraza. Majority ya viti vilikuwa chini ya mwingereza

Kama nilivyoandika huko nyuma, tatizo lilikuwapo mbele ya ASP ni kuwa hakikuwa na viongozi articulate, na nadhani ndiyo maana hata hawakuona kuwa mgawanyo wa majimbo ulikuwa unapunguza nguvu ya kura za mafuasi wake. Kwenye mikutano ya katiba walikuwa hawajui ni nini kinaendelea ndiyo maana hawakulazimisha majimbo yagwanywe upya.
 
kichuguu,
1.Mamlaka ya Sultani baada ya "Uhuru" wa ZNZ yalikuwa yapi? Haiwezekani ASP wakurupuke tu kumpindua. Lazima kulikuwa kuna kitu with Sultani ambacho kilikuwa kinawakwaza ASP.

2.Nyerere aliweza kuwaondoa Machifu kwasababu walikuwa chini yake. Vilevile aliweza kuleta Jamhuri kwasababu TANU walikuwa MAJORITY na Nyerere alikuwa anaongoza SERIKALI. Ni wapi panapoelekeza kwamba ASP walikuwa wanaweza kubadili KATIBA wakati wao walikuwa MINORITY?

3.Umeona wapi MINORITY party wakibadilisha KATIBA? Vilevile tumeisha elezwa kwamba ZNP & ZPPP walikuwa Pro-Sultan, sasa huoni kwamba mabadiliko ya Katiba yalikuwa hayawezekani bila MAPINDUZI?

4.Sidhani kama mkutano wa Katiba ya Zanzibar uliridhia madai yote ya ASP. Nadhani tangu mwanzo ASP hawakukubaliana na hiki kipengele cha Zanzibar nchi ya Kiafrika kuwa na Sultani.

5.Mimi sioni mantiki yoyote ya ZNZ kuwa na Sultani. Ndiyo maana nimekuuliza tena na tena kulikuwa na ulazima gani kwa ZNZ kuwa na Sultani, even a ceremonial one?
 
JokaKuu
Hayo Mafuta yapo? au yapo kisiasa?
Hivi kwa mfumo wa sasa- ni nani ana anufaika zaidi? Manake naskia Zenj hata hawatoi mchango wa sekta za Muungano. Halafu hii debate ya Muungano mbona ni one sided? Kwa nini mara nyingi malalamiko hutoka tu visiwani?
Kuna hisia toka visiwani kuwa bara wanainyonya Zenj- ila sijui kwa nini bara nao huwa hawalalamiki!

jawabu ni rahisi - kwa sababu wao ndio wanaofaidika sasa walalamike kwa nini
 
sawa sawa wakati umefika tupige mbinja za kudai haki setu, ila nnasikitika sana na ndugu zangu wa CCM zanzibar, wakiwamo kwenye madaraka hutetea sana muungano, hao hao wakitupwa nje judai muungano unawaonea.

wewe subiri watakaoachwa kuwa na nafasi 2010 halafu wafate pembeni uwasikie watakavyokuhadithia jinsi muungano inavyoionea zanzibar.

kazi tunayo


Ni kweli mtuMwitu hawa CCM Zanzibar ni wanafiki wakubwa wapo pale kwa maslahi yao tu na wala si kwa ajili ya nchi (Mungu awanakamishe), wakisha kutolewa kwenye madaraka tu utawasikia wanavyolalamika kuhusu Muungano jinsi unavyoiyumiza Zanzibar. Halafu utamsikia mtu anasema hawachangii kitu kwenye Muungano? sasa wachangie kitu gani wakati kila kitu kimehodhiwa na Serikali ya Muungano?.
 
kichuguu,
1.Mamlaka ya Sultani baada ya "Uhuru" wa ZNZ yalikuwa yapi? Haiwezekani ASP wakurupuke tu kumpindua. Lazima kulikuwa kuna kitu with Sultani ambacho kilikuwa kinawakwaza ASP.

Sultani hakuwa na mamlaka yoyote, that was a ceremonial post. Ni kama alivyokuwa Rais Canan Banana kule Zimbabwe.

2.Nyerere aliweza kuwaondoa Machifu kwasababu walikuwa chini yake. Vilevile aliweza kuleta Jamhuri kwasababu TANU walikuwa MAJORITY na Nyerere alikuwa anaongoza SERIKALI. Ni wapi panapoelekeza kwamba ASP walikuwa wanaweza kubadili KATIBA wakati wao walikuwa MINORITY?

Katika demokrasi maoni ya majority hufuatwa ingawa maoni ya minority nayo husikilizwa. Kwanza, kwa vile ASP walikuwa minority, walitakiwa wafuate mawazo ya majority. Pili ASP walipewa nguvu ya "veto" kwenye maandalizi ya katiba, wakai-blow up. Halafu hakuna palipoandikwa kuwa ASP wangekuwa minority miaka yote. Kama kweli walikuwa na mvuto kwa raia wangekuwa majority siku moja; ninachosisitiza ni ujenzi wa misingi thabiti ya demokrasi na kuheshimu haki za binadamu.

3.Umeona wapi MINORITY party wakibadilisha KATIBA? Vilevile tumeisha elezwa kwamba ZNP & ZPPP walikuwa Pro-Sultan, sasa huoni kwamba mabadiliko ya Katiba yalikuwa hayawezekani bila MAPINDUZI?
Nadhani nimeshajibu hapo juu. Hebu fikiria katika muundo wa leo ambapo CCM wanadai wanajenga nchi ya kijamaa na wanapata asilimia 80 ya kura. CHADEMA wanasema hapana nchi hii siyo ya kijamaa na wanapata asilimia 20 ya kura, lakini ukweli ni kuwa kila mtu anajua kuwa CCM haijengi ujamaa na raia wengi hawataki kusikia kitu ujamaa, je ni halali kwa CHADEMA kupindua serikali na kuuwa watu wengi kwa madai kuwa CCM inapendelea ujamaa wakati watu wengi hawautaki ilhali hawakushinda uchaguzi?

4.Sidhani kama mkutano wa Katiba ya Zanzibar uliridhia madai yote ya ASP. Nadhani tangu mwanzo ASP hawakukubaliana na hiki kipengele cha Zanzibar nchi ya Kiafrika kuwa na Sultani.
ASP hawakuwa na viongozi articulate kwenye mikutano ile ingawa kuna wakati walipewa hata uwezo wa kura ya trufu (Veto). Kwenye mkutano wa mwisho walikubali kila kitu, kumbe walikuwa wameshapanga kuchukua nchi kwa nguvu.
5.Mimi sioni mantiki yoyote ya ZNZ kuwa na Sultani. Ndiyo maana nimekuuliza tena na tena kulikuwa na ulazima gani kwa ZNZ kuwa na Sultani, even a ceremonial one?

Hata mimi sioni mantiki hiyo, ila nitakurudisha nyuma kuwa ilikuwa ni system ya Uingereza kutawala kwa monarchy kwa hiyo wakati wanaondoka walikuwa wanaacha namna fulani ya monarchy. Unaweza kujiuliza vile vile kuwa kwani Tanganyika ilikuwa na ulazima gani wa kubaki chini ya Malkia baada ya uhuru? Zimbabwe iliendelea chini ya malkia kwa karibu miaka minane tangu wapate uhuru wao kabla hawajajiondoa. Zanzibar ilikuwa na uharaka gani wa kuondoa usultani overnight kwa mauaji yale tena katika siku 33 tu na kuvunja misingi yote ya demokrasi ambayo sasa wanahangaika kuijenga; na sasa itawachukua muda mrefu sana kuifikia tena.
 
kichuguu,
1.Haya masuala ni complicated na nafikiri unajaribu kuya-trivialize. ASP walikuwa minority by the number of constituencies they won.If you look at the number of votes they gunnered it is totally a different story.

2.Mfumo wa democrasia wa electoral votes lengo lake siyo kuhujumu matakwa/maoni ya majority ktk uchaguzi. Yes, the minority should be listened to, but the majority must have their way. Binafsi naona mfumo wa uchaguzi ZNZ ulikuwepo pale kuwakandamiza ASP.

3.Upumbavu wa viongozi wa ASP usiwe ni kisingizio cha kutokusikiliza sauti na matakwa ya Wazanzibari waliokuwa wakiwapa "ushindi" ktk chaguzi 3 mfululizo. Mimi nadhani Mapinduzi yalichelewa kufanyika. They waited too long.

4. Hali ya Tanganyika na Zimbabwe ni tofauti na ile ya Zanzibar. ZANU na TANU walikuwa majority bungeni hivyo walikuwa wanaweza kubadilisha katiba ya kuondoa Monarchy wakati wowote. Kwa upande wa Zanzibar, ASP walishakata tamaa ya kuwa majority bungeni, na hivyo kuwa na influence kubwa ktk kubadilisha katiba.
 
Kama kweli ASP walikuwa wanaonewa, wangejitoa katika uchaguzi ule au wangelalamikia matokeo yale. Katika mikutano yote ya uhuru hawakuwahi kuongelea mgawanyo wa majimbo kwa hiyo wote walikuwa wamekubaliana. Majimbo yale yaligawanywa kwa kufuata ukubwa wa eneo, siyo idadi ya watu. Ninahisi kuwa wakati huo hakukuwa na takwimu thabiti za makazi ya watu; inawezekana sehemu zilizokuwa na waafrika wengi zilikuwa na poupulation density kubwa kuliko zile walizokuwa wakiishi waarabu.

Ninachosema ni kuwa hata kama lengo la mapinduzi hayo lilikuwa ni zuri, mapinduzi yale hayakuwa halali kabisa kwa vile siyo tu kuwa yalisababisha mauaji mengi bali yaliondoa kabisa utawala wa kidemokrasi nchini Zanzibar na kusababisha haki za binadamu kuwa ndoto; kibaya zaidi ni kuwa mapinduzi yale yalifanywa na watu wa nje. Ni chini ya mfumo huo huo ndiyo maana hadi leo hii watu wote wanaopingana na serikali wamekuwa wanauwawa bila sababu yoyote.
 
Kichuguu,
Duh Mjomba, hiyo ya Sultan kuwa kama rais wa Zimbabwe umeipata wapi mjomba!
Je, Unajua kama Sultan anakuwa na heshima, kifungu chake cha mapato ya taifa!..Na lazima serikali ya nchi yoiyote ile iheshimu falme!...tazama leo Canada na Australia wanazo serikali zao lakini bado ni chini ya Malkia na hawawezi kujiondoa hivi hivi. Ya Faukland huko Argentina unayakumbuka uncle!... Jamshid ni Mu-Oman kwanza kama alivyokuwa Ian Smith, uraia hata wewe ni raia wa Marekani lakini huwezi kuwatawala nchi hiyo hata siku moja!...
Je, unajua ya kwamba kwa desturi na mila za wa Oman, huyo Sultani Jamshid ibn Abdallah ndiye mrithi halali leo hii wa U -Sultan wa Oman kuliko Quabus?, haya linganisha na huyo Banana.
 
JokaKuu,

naomba ungelituwekea mahesabu (matokeo) ya kura yalivyokuwa katika chaguzi zote tatu.
 
kichuguu,


4. Hali ya Tanganyika na Zimbabwe ni tofauti na ile ya Zanzibar. ZANU na TANU walikuwa majority bungeni hivyo walikuwa wanaweza kubadilisha katiba ya kuondoa Monarchy wakati wowote. Kwa upande wa Zanzibar, ASP walishakata tamaa ya kuwa majority bungeni, na hivyo kuwa na influence kubwa ktk kubadilisha katiba.


JokaKuu,


Hii ya kuwa ASP walikata tamaa mkuu umeipata wapi? wao wenyewe walitamka hivyo? au unawasemea wewe tu?

Unasema hivyo kua wamekata tamaa kwa sababu walishiriki chaguzi mara tatu na wakashindwa ndio wakaona watumie nguvu? basi kama ni hivyo na wapinzani sasa hivi ni halali kwa wao kufanya mapinduzi kumuondoa sultan (mkoloni) CCM na serikali yake kwa sababu mkoloni huyu ni mbaya zaidi kuliko hata hao waliopita huko nyuma.


ASP walishindwa katika njia za kidemokrasia wakaona bora watumie njia ya mkato (iliyokuwa inagharama kubwa) ya kuchukuwa serikali period.
 
Jembajemba,

basi kama ni hivyo na wapinzani sasa hivi ni halali kwa wao kufanya mapinduzi kumuondoa sultan (mkoloni) CCM na serikali yake kwa sababu mkoloni huyu ni mbaya zaidi kuliko hata hao waliopita huko nyuma.

Taratibu ndugu yangu viongozi wetu hawapendi kuitwa Wakoloni!
 
Mkandara,

Ninaelewa adha ya kipengere cha usultani. Nilipomlinganisha na Banana nilikuwa natafuta figure ya kuonyesha kuwa alikuwa ni ceremonial, na wala hakuwa commander in chief. Najua kabisa kuwa position ya Banana na ya Sultani zilikuwa tofauti kabisa, lakini zote zilikuwa ceremonial.

Naelekwa kuwa katika mapambano ya uhuru ASP walikuwa na front mbili: kuondoa ukoloni wa mwingereza na kuondoa usultani, wakati ZNP walikuwa na lengo moja la kuondoa mwingereza tu na labda kuimarisha usultani. Kwa upande wake ZPPP ilikuwa na lengo moja tu la kuomwondoa mwingereza na kuiweka serikali mikononi mwa wazanzibari; swala la usultani halikuwamo kwenye ajenda yao: kwepo au kutokuwepo kwa sultani ilikuwa siyo tatizo kwao. Ndiyo maana Shamte alikuwa ASP na baada ya kuondoka na kuanzisha chama chake aliweza kuungana na ZNP.

Jamshid alikuwa raia wa Zanzibar kwa vile baba yake alizaliwa Zanzibar na yeye mwenyewe alizaliwa na kukulia Zanzibar. Ni kama Kennedy aliyezaliwa Marekani na baba yake pia alizaliwa Marekani lakini Babu yake alitoka Ireland.

Tukiachana na huo mlolongo wa koo za sultani, ninalotaka lieleweke ni kuwa mapinduzi yale yawe ni ya kumng'oa sultani au ya kuindoa serikali ya Shamte kutoka madarakani, hayakuwa halali.

Ni kweli usultani ulikuwa hauhitajikin tena katika Zanzibar huru, hata hivyo njia zilizotumiwa na ASP zilikuwa za kinyama sana na za kupinga demokrasi. Nimeifutilia historia ya harakati za uhuru wa Zanzibar kwa makini sana na kugundua kuwa kilichosababisha kifungu cha Sultani kubaki kwenye katiba ni failure ya ASP yenyewe kwenye mazungumzo yale ya katiba. Wangeweza kabisa kudai sultani uondolewe lakini madai yao yalikuwa vague sana, wao waling'ang'ania kutaka uchaguzi urudiwe tena na tena bila kweka madai ya msingi kama kugawanya majimbo ya ucahguzi kufuatana na idadi ya watu, na kuondokana na mamlaka ya usultani.
 
Kichuguu,

Lakini umejaribu kuangalia Muingereza kaingia vipi Zanzibar?
Je, umewahi kusoma mkataba wao wa Pretectorate na Sultan Seyyid Alli Said!.na toka hapo nafasi ya Sultan ktk utawala huo ilikuwa vipi.

Hawa jamaa leo hii wanapiga makelele mengi tu kuhusu hata Muungano na kusema kweli hata pretectorate ya Muingereza ilikuwa na malengo sawa kabisa na hayo ya Muungano. Tazama basi utawasikia wakisema muungano lakini wanashindwa kutaja makubaliano ya Sultan na Muingereza kuwa ni makubaliano ambayo hayakupendekezwa na Wazanzibar!..

Nitarudia kusema kwamba yote yazungumzwe ya leo kwa mabaya yanayoonekana leo lakini tusijaribu kurudisha historia nyuma kwa visingizio. Bahati mbaya ni kwamba watawala wetu weusi wamekuwa wanyama na wasiokuwa na dira ya wapi tulikotoka na tunakwenda wapi.
Uhuru wa Tanganyika ulikuwa muhimu pia pamoja na kwamba yaonyesha wazi kuwa hatukuwa tayari na pengine hadi leo hatupo tayari kuwa huru. Lakini yote haya tunayazungumza leo kwa sababu ya tawala zetu wenyewe kuwa mbovu na pengine mbaya kuliko hizo za wakoloni kwa sababu zimepotosha kabisa maana ya Uhuru.

Kwa nini nasema hivyo?... ni kwa sababu mtu ukiwa umefungwa Magereza siku zote hutegemei mazuri huko na ndio maisha yetu yalivyokuwa chini ya kutawaliwa lakini kama upo huru na unaishi kama mfungwa basi ni bora uwe Ukonga ukijua unatumikia kifungo kwa makosa uloyafanya.. makosa ya kumkaribisha Mkoloni.
Sii Zanzabiar wala bara hakuna penye nafuu hata kidogo kwani pato la taifa linapogawanywa na kuwa chini ya dola moja inaonyesha dhahiri kuna distribution mbaya sana ya Utajiri wetu..Moja ya malengo ya Uhuru wetu yaliyotupwa ktk pipa la taka!
 
Kichuguu,


Hawa jamaa leo hii wanapiga makelele mengi tu kuhusu hata Muungano na kusema kweli hata pretectorate ya Muingereza ilikuwa na malengo sawa kabisa na hayo ya Muungano. Tazama basi utawasikia wakisema muungano lakini wanashindwa kutaja makubaliano ya Sultan na Muingereza kuwa ni makubaliano ambayo hayakupendekezwa na Wazanzibar!..


Bob

Ahsante mkuu kwa maelezo yako mazuri.

Mimi naona makubaiano yote mawili sio halali (Muungano - Zanzibar na Tanganyika na yale ya Muarabu na Muingereza) kwa sababu yote mawili hayakupata ridhaa ya wazanzibari (wananchi).
 
Nitakuja kufungua mada kuhusu muungano kwa vile wakati ninatafiti kuhusu mapinduzi, nimegundua flaws nyingi sana kuhusu jinsi muungano huu ulivyofikiwa. Kwa sasa hivi ningependa tusafishe ufahamu wetu kuhusu mapinduzi, halafu baadaye tusafishe ufahamu wetu kuhusu muungano. Baada ya kuwa na mazingira mazuri kuhusu mapinduzi na muungano ndipo tuangalie twende wapi kuanzia hapa tulipo.
 
Back
Top Bottom