Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
nitajitahidi kuweka wazi maana ya neno hili la hizbu alwatwani zenjibar.

kiswahili cha zanzibar na hasa wakati ule kiliathiriwa zaidi na kiarabu, na mara nyingi watu wa kisiwa kile walikuwa katika maongezi yao huchanganya zaidi baina ya kiswahili na kiarabu, sawa na leo kuona baadhi ya miji yetu kuchanganya kiswahili na kiingereza.

mfano utasikia nnmpeleka mtoto madrasa ikimaanisha nnampeleka mtoto shule.

wizara ya ya ziraa maana yake wizara ya kilimo, na hadi leo bado athari hizo zipo, kwa mfano kule kwetu zanzibar ktk kipindi hiki kuna wizara inaitwa wizara ya elimu na mafunzo ya amali neno amali ni la lugha ya kiarabu likimaanisha vitendo au kazi za mikono.

sasa rurudi kwenye neno letu, hizbu kama ulivyosema lina maana ya army, lakini kwa nyongeza lina maana ya movement, party

mfano hizbollah( hizb maana yake party na allah maana yake god) kwa hiyo maana kamili itakuwa Party of God pia yaweza kuitwa Army of God (for ref: www.yeshuatyisrael.com/Powerpoint/Hezbullah.ppt

mfano mwengine ni chama cha HAMMAS cha wapelistina hiki urefu wake Hizbu Almuqqawamat Al-islamiyy
nacho kina maana hizbu ni movement, na almuqawamat Resistance na Al- islammiy iko wazi sasa utaona wanakiita Islamic Resistance Movement hapa imetumika kama movement.

na hata kule Sudan chama kinachoongoza nchi kinaitwa Almuutamar hizbu alwattwan ikiwa na maana almuutammar ni congress, na hizbu party na wattan ni National utapata kinaitwa ni National Congress Party.

turudi kwenye alwattaniy, zanzibar hadi kesho neno hjili tunalitumia kumaanisha utaifa au mzawa, japo sasa kuna harakati za kuliondoa na kutumia mzanzibari halisi lakini ukitaka kusema mimi ni mzawa kindaki ndaki unasema mimi ni muwattin , yule alwattwan.

sasa nnataka kusema kuwa chama cha hizbu urefu wake hasa ni hizbu alwatwani zenjibar na maana yake ni Zanzibar National Party (ZNP). watu kwa ufupi wakawa wanakiita Hizbu na hii ndio maana yake.

na kuitwa Hizbu haimaanishi kuwa waliokuwa hizbu ni waarab tu, hata kwenye quraan neno hili limetumika na wazanzibar wengi ni waislam na wameathiriwa na lugha ya kiarabu ktk matumizi yao.

nnategemea nitakuwa nimejaribu kufafanua maana ya hizbu na any comment zinakaribishwa

Mtumwitu,
Ahsante kwa shule yako bwana! Tunaifurahia! Mimi naona kuna double standard- kwa nini Afro-Shiraz Party (ASP) ni Kiingereza au ukisema Zanzibar National Party (ZNP)- yoote ni Kiingereza inaonekana sawa. Ila Ukisema 'hizbu alwattwan' ambayo ni Kiarabu na maana yake ni hiyo hiyo- kwa nini hizbu alwattwan inaleta negative cannotation? Manake kweli Bara wakati wa Mchakato wa Salim kuwa kugombania Uraisi- walisema tu- yeye ni 'hizbu'- na hii kweli ilimponza Salim kupita na kukubalika! Any stigma associated with hizbu au walionekana ni Waarabu? Kwa nini Kiingereza iwe ok ila Kiarabu maana hiyo hiyo kuwe na stigma!
 
Kweli JF ni shule!
Thanks wachangiaji.. maana hapa napata mambo ambayo sikufundisha shule, chuo wala mtaani!
 
Mtumwitu;

Nashukuru sana kwa ufafanuzi wa HIZBU-WATAN. Haitofautiani sana na jinsi nilivyokuwa nafikiria, niliposema jeshi au kundi la watu sikuwa na maana ya wapiganaji, ila neno zuri zaidi ni hilo movement. Kwa vile Zanzibar walikuwa wakitumia kiingereza, na kiswhaili chenye kujaa kiarabu sishangani kwa nini Chama cha HIZBU kilikuwa kina jina la kiarabu na la kiingereza: ni kama JWTZ na TPDF.

Mzalendohalisi;

Nia yangu kubwa kufuatilia background ya mapinduzi ilikuwa ni kutafuta chanzo cha mfarakano kati ya Pemba na Unguja. Nina imani kabisa mfarakano huo chanzo chake ni kwenye mapinduzi. Kumbuka kuwa Shamte alikuwa ni mpemba, na kati ya watu wengi walioathirika sana na mapinduzi yale inaelekea walikuwa ni wapemba. Nikisha pata picha kamili ya mapinduzi nitaweza kuunganisha dots kujua chanzo cha mpasuko huu sasa hivi. Kitu ambacho kinajulikana wazi ni kuwa katika siasa za CCM huko visiwani kuna wanasiasa wameendelea kuwapiga vita watu wengi waliokuwa wanachama wa ZPPP na ZNP. Kuna simulizi kuwa wakati Nyerere anastaafu alitaka Salim amrithi kama Rasi wa Muungano lakini alipigwa vijembe sana kutoka kwa wajumbe wa Zanzibar kuwa asimpe Salim madaraka kwa vile aliwahi kuwa mwanachama wa Hizbu, ndiyo mwishoni akapewa Mwinyi.
 
sasa nnataka kuchangia kidogo kuhusu siasa za zanzibar kabla ya mapinduzi,

watu wengi huwa wanajiuliza hivi hichi chama cha hizbu ni cha waarabu? na jee wao ndio walioanzisha chama hiki kwa kuwatumia wazawa?

kwanza kama kitabu kinavyoeleza ambavyo sawa na nilivyoelezwa na wazee wangu chama cha hizbu kilianzishwa na watu wa unguja na hasa watu wa vijijini kwa lengo la kupinga matabaka yaliokuwepo zanzibar wakati huo, na ndio chama cha mwanzo kabla ya vyama vyengine cha ASP na ZPPP.

chama hichi kilijikita zaidi katika kutetea uzawa kiliamini kuwa wazanzibar wale wa asili hasa ndio wenye zanzibar na ndio wanaostahiki kutawala nchi yao.

nnapenda hapa ifahamike kuwa hata hao waarabu wako waliokuwa wakionekana kuwa ni wageni kwa mtizamo wa hizbu.

hizbu kilikuwa na mchanganyiko mkubwa wa watu wa mashamba ya unguja( ambayo ndio ikijulikana kama zanzibar, na sio mkusanyiko wa unguja na pemba kama invyojulikana leo), na watu wenye asili ya asia na baadhi ya wapemba wachache.

hizbu ilikuwa ikiamini mkoloni kwa kushirikiana na sultani hawawapi haki wazawa.

ASP wao waliamini kila mwafrika ana haki kubwa tu zanzibar, kwa hiyo hata mtu aliekuja mwaka mmoja basi huyo ni mzanzibari.

ukiangalia nadharia hizi mbili utaona kuwa ASP kilikuwa ni chama chenye mvuto zaidi kwa watu walio na asili ya kiafrika zaidi na hasa wageni. na hata ukiangalia viongozi wake wa juu wengi walikuwa wenye asili ya mrima(tunaposema mrima tunakusudia bara hapa iwe kenya, nyasa land, uganda, kongo au tanganyika kwa wakati ule).

na Hizbu kilikuwa ni chama ambacho kikiamini watu hawa ni wageni, japokuwa wanadai uhuru wa kujitawala lakini uhuru huo usiangukie mikononi mwa wageni.

baada ya ASP kugawika, napenda kusema kiligawika kwa misingi hiyo ya juu na kuzaliwa ZPPP ambacho kiliungwa mkono sana na watu wa pemba utaona Zanzibar kulikuwa na vyama vyenye kuwakilisha watu wa aina tatu:-

moja ZNP ambacho kiliwakilisha watu ambao walikuwa wakijidai wao ndio wazanzibari halisi au alwattan.

pili ASP ambacho kiliwakilisha waafrika wengi waliohamia Zanzibar kwa namna moja au nyengine.

na kundi la tatu ni ZPPP ambacho ni chama kilichokuwa kikiwakilisha zaidi watu wa pemba.

kutokana tofauti hizo za mielekeo hio watu wa hizbu kilikuwa kiwakejeli watu wa ASP kuwa wao ni magovi, yaani watu wa bara( na wakati huo watu wengi wa bara walikuwa wakiitakidiwa ni wakristo na hawatahiriwi, mfano kama alivyokuwa akitaniwa mkjj na swahiba yake mswahili humu).

chaguzi zilipofanyika na hasa huu wa mwisho ASP walienda kumuomba Shamte waungane ili waunde serikali, lakini Hizbu wakamfuata na kumwambia usikubali kuipeleka nchi kwa wageni.

mara nyengine walipoenda ASP Shamte akawaambia munipe utume mie basi siko tayari kuuungana na nyinyi, ndio akaungana na Hizbu kuunda serikali.

baada ya mapinduzi watu wa pemba walitengwa kwa kuwa waliiunga mkono Hizbu.

chama cha CUF kimerithi baadhi ya sera za Hizbu kwa mfano wao leo hutumia sana neno mzanzibari na mzanzibara.

sasa mmoja katika babu zangu wa upande wa hizbu ambaye ni mshirazi hunambia sana wenzetu wa pemba wao wameweza na kuwa na chama chao ila sisi watu wa unguja tumeshindwa kuwa na chama chetu.

ndio utaona Hizbu wamejigawa wengine wanaiuunga mkono CCM na wengine wanawaunga mkono ndugu zao wa pemba.

hadi leo wako wanaoaamini CCM si chama cha wazanzibari kama ilivyokuwa ASP, ila wazanzibari hutumiwa tu.

husema kuwa ukiangalia kwa kina sehemu nyingi za utawala zimekamatwa na watu wasio na asili ya zanzibar.

nnapenda kuwasilisha mchango wangu huu, na nnaomba tuchangie kwa kuvumiliana na tukosoane kwa upendo maana hii ni mada hassasi sana .

lakini ni wakati wake wa kuijadili ili tuweze kuijenga tanzania yenye upendo
 
Hizbu ni chama cha mwanzo cha wananchi kuasisiwa zanzibar. Wananchi waasisi hao walikuwa ni, Sheikh Vuai Kiteweo, Sheikh Miraj Shaalab, Maalim Zaid Mbarouk, Maalim Maksud Fikirini, Maalim Mwandoa Khamis, Maalim Wazir Ali bin Maalim, Sheikh Haji Hussain Ahmed, Sheikh Othman Soud, Sheikh Abdulla Mahmoud Kombo (wa Makunduchi), Sheikh Ramadhan Tosir (Ramadhan Madafu), Maalim Hija (wa Ndijani), Sheikh Ame, Sheikh Abdulla Mali, Sheikh Haji Kombo (wa Kiboje), Sheikh Abdalla Mahmoud na wenziwe wachache. Kwahivyo wale wenye kusema na kutangaza kuwa Hizbu (ZNP) iliasisiwa na Waarabu au kilikuwa chama cha Waarabu, hapana shaka wanakosea, amma kwa ku- tokujuwa ukweli ulivyo au wana-sema hivyo kwa makusudio ya kutafuta maslaha yao. Uk-weli na hakika ilivyo ni kuwa Hizbu haikuasisiwa na Waarabu wala hakijapata kuwa Chama cha Waarabu
 
kichuguu,
1.maelezo ya mtumwitu yanaonyesha kwamba kulikuwa na hali ya Mwafrika kutokukubalika kama Mzanzibari halisi. Yaani mzao wa Mwarabu aliyekuja Afrika kufanya biashara ya Utumwa, ulianza kuwadharau na kuwatenga Waafrika, ndani ya Afrika.

2.Zaidi, maelezo ya Mtumwitu yanaonyesha kwamba ZPPP na HIZBU walikuwa na sera za kibaguzi dhidi ya Waafrika. Vilevile maelezo yake yanaelekeza kwamba ASP ilijaribu zaidi ya mara moja kuunda serikali ya mseto na ZPPP, lakini wakakataliwa kwasababu ambazo nalazimika kuamini zilikuwa za kuwabaguwa kwa RANGI na UTU wao.

3.Mtumwitu anaeleza kwamba SHAMTE aliwahi kutamka kwamba hata angepewa UTUME ndani ya Muungano wa ASP na ZPPP angeukataa. Hayo ni maneno mazito sana ukizingatia kwamba Shamte ni Muislamu. Ni elimu kubwa hiyo Mwafrika alikuwa ktk daraja gani huko ZNZ.

4.Sasa turudi kwenye huu utaratibu wa uchaguzi ZNZ, na jinsi mshindi alivyokuwa akipatikana. Kwanza utaratibu huu wa electoral votes mara nyingi huwepo mahali penye "tensions" za namna moja au nyingine. Mara nyingi ni utaratibu unaowekwa kuwahakikishia minorities na underpriviledged a say in the political decisions.

5.Nalazimika kuamini kwamba mfumo wa Uchaguzi ZNZ kabla ya Mapinduzi ulikuwepo pale kuhakikisha kwamba Mwafrika hatotawala ZNZ.

6.ASP walikuwa "naive" kufikiri kwamba chama cha Waafrika kitaweza kuunda serikali na hivyo wakashiriki uchaguzi ktk mazingira yaliyokuwepo. Walishiriki uchaguzi mara 3, nadhani hiyo ilitosha kuwashawishi Waafrika kwamba wasingeweza kuunda serikali kwa mfumo wa demokrasia uliokuwepo.

7.Utumwa uliisha miaka mingi sana kabla ya Mapinduzi. Lakini ukichunguza and reading btn the lines utaona kwamba Mwafrika aliendelea kudharauliwa ndani ya ZNZ. Mfano mzuri ni WAAFRIKA kuitwa MAGOVI, wenyewe wakiita "utani."

8. Kwa kifupi Muarabu akikuita govi maana yake amekufananisha kitu kichafu,kisichofaa, au na-jisi. Katika jamii za Kiafrika zinazotahiri[tena nyingine hata wanawake] mtu govi hafai kuongoza familia, na zaidi jumuiya.

9.Ulizungumzia kitendo cha wajumbe wa Baraza la Mapinduzi kuoa wanawake wa kiarabu, zaidi ukakielezea kama ishara ya amani,upendo,na utangamano. WRONG. Wale 14 boyz waliamua kuoa Waarabu kama ishara ya kulipiza kisasi kwamba sasa "magovi" wanalala na mabinti wa Kiarabu. Hata Iran walipata kulalamikia kitendo cha wasichan wa Kiarabu kuolewa kinguvu Tanzania. Suala hilo lilimuaibisha sana Nyerere ktk mkutano wa Non-Alligned Movement.

10.ZNP kuwa na jina la Kiarabu we are not arguing about the interpretations in the dictionary. Tunajadili mantiki ya chama hicho kuwa na jina la kiarabu in the social and political psychic ya Wazanzibari wa wakati huo. Kwa kifupi Hizbu was not for Africans[magovi]. Chama hicho kilikuwa kipo hapo kuhakikisha Mwarabu anaendelea kuwa bwana na Mwafrika anakuwa mtwana siku zote.

11. Ukisikiliza hotuba nyingi za Mzee Abeid Karume alikuwa akitumia sana maneno, MWANA-WA-NCHI, MWA-FRIKA, na HESHIMA. Naomba tulitafakari suala hilo.
 
ahsante kichuguu kwa kuileta hii mada na ahsanteni kila anaetuelimisha katika hii mada,nilielezwa mengi sana na mababu waliokuwepo wakati wa mapinduzi na nikatajiwa majina mengi mengi kama akina washoto,rashid abdalla,shamte,okello,abrahman babu,karume ,thabit kombo,ameir tajo, na wengi wengineo.ila acha nikiri ukweli ,haya nilioyasoma tangu hii mada ianzishwe basi yamenifanya hata niwe na woga wa kuchangia,nimefurahi kuona watu wamekuwa wanayaelewa mapinduzi ya zanzibar kwa utaalamu zaidi na wako tayari kuyajadili kwa njia ya kisasa na kiuwazi zaidi na acha niseme ukweli kwamba nimeelimika mengi sana ambayo nilikuwa siyajui kupitia hii mada.mtumwitu,mzalendohalisi,jembajemba,jokakuu,kichuguu na wengineo, well done guyz. ni hatua ya kwanza ya kutetea haki za wanyonge ,acha tufichue yaliofichikana.kwa pamoja ,tunaweza.iko siku tutamfunga paka kengele.hongereni vijana.endeleeni
 
Kichuguu,

Kwanza nashukuru sana kama tumeelewana ktk lengo la mapinduzi yenyewe ambayo yalikuwa ni LAZIMA yatokee kwa sababu mtawala alikuwa bado Sultan.
Mimi sintagusia sana maswala ya vyama hivi kwani wakati huo vyama havikuwa na mrengo zaidi ya kusimamia kundi la watu. Na wala siwezi kuwalaumu Hizbu ama ASP kwa sababu hizo hizo. Tatizo kubwa wengi hapa wanajaribu kutazama vyama hivi kwa hali iliyopo leo hii na pengine kushangaa kwa nini Hizbu kilikuwa chama cha waarabu zaidi ya weusi, lakini wakati huo huo ukitazama nchi zote zilizotawaliwa duniani zenye mchanganyiko wa rangi zilikuwa na vyama vinavyosimamia jumuiya zao kutafuta haki ya watu ama kundi lao, Zanzibar was not exceptional.

Sasa turudi ktk case ya Mapinduzi yenyewe ambayo umezungumzia sana kuhusu Karume.
Binafsi sikumpenda Karume kama kiongozi wa ASP ama Zanzibar kwa sababu moja kubwa ambayo pia aliitumia mtu kama Idd Amin. Na kwa vile Idd Amin aliyafanya mapinduzi sina haki ya kupinga mapinduzi hayo dhidi ya Obote na wakati huo huo itafsirike kuwa maana yangu ni kwamba namtetea Idd Amin kama ni kiongozi mzuri. Kwa hiyo ndugu Kichuguu sina maana kabisa kwamba nakubaliana na Utawala wa ASP kuwa ni bora kuliko Hizbu isipokuwa kosa kubwa la Hizbu lilikuwa ni wakati....wakati huo nina hakika hata uchaguzi wa kwanza wa Rhodesia kama Ian Smith angeshinda nadhani kungetokea mapinduzi ya aina hiyo hiyo hata kama Ian Smith angeweza kuwa mtu mzuri... tatizo ni watu gani wanaowakilishwa na chama kile - minority! hivyo basi viongozi wa Hizbu wanaweza kuwa wazuri sana kuliko ASP lakini the timing was right for ASP... not for Hizbu na viongozi wake!
Na mwisho labda nigusie kuhusu Wale wahuni waliooweza kuyafanya mapinduzi ambao umeuliza kwa nini wameonekana wahuni tu.
Ni kweli na sidhani kama Karume na baraza lake la mapinduzi wangeweza kushika Bunduki na wala usitegemeee kumwona Bush, viongozi maseneta, congress wakitokea ktk picha za mapinduzi ya Iraq.
Na hata sisi tulipomwondoa nduli Idd Amin hatukuweza kuona picha za Nyerere na viongozi wa Tanzania wameshika silaha mbele ya mapinduzi hao.
Kwa hiyo pamoja na kuwepo kwa utata wa nani hasa wahusika wa mapinduzi hayo bado tukubali kuwa aliyepinduliwa hapa ni Sultan mtawala na sio Hizbu pamoja na kwamba utawala wa wizara za nchi hiyo ulikuwa chini ya serikali ya Hizbu. Hivi ndivyo navyoelewa mimi na ndio maana nimekupeni mfano mzuri wa nchi kama Zimbabwe na South Afrika.

Labda tukirudi leo hii na kutazama upya sababu ya mapinduzi hayo tumekuja gundua kuwa Hizbu ndio walikuwa the biggest looser! na hata walipoweza jiunga na ASP bado kulikuwepo na viongozi weusi wa ASP wenye usongo na jamaa wa Hizbu. Chuki ambayo hadi leo hii imeweka chachu kubwa ktk kujenga Umoja wa Wazanzibar. Hawa jamaa wamekuwa wakitengwa kila siku na kila juhudi zao kushika nafasi nyeti hasa za visiwani imekuwa kama vile ni laana. Do I support that? jibu lake ni NOOO! na ndio maana hata ktk muungano wa Tanzania bara na visiwani sipendi kabisa jinsi bara tunavyo wa treat visiwani ktk upande wa uongozi. Na kama utazama zaidi kutafuta sababu kubwa ya matatizo haya utakuta kwamba sisi waafrika nafasi ya kutawala nchi ni nafasi pekee ya kuvuta UTAJIRI!.. Kwa hiyo mjomba utanikuta siku zote nimekuwa consistant na mtazamo wangu ktk swala la Watawala wetu.
Hawa watawala wetu ni wabaya kuliko hata wakoloni kwani ile dream yetu ya kutotawaliwa na kuwa watu huru wenye uwezo wa kujichagulia maendeleo yetu imegeuka na kuwa jinamizi!.. bado tunatawaliwa na kibaya zaidi ni kwamba tunatawaliwa na ndugu zetu wenyewe wa damu ambao hatuwezi kuwaepuka...
Tazama mauaji ya Pemba! hawa ni Watanzania wakiua Watanzania wenzano kwa sababu ya kutawala tu. Ebu fikiria kama mauaji yale yangefanywa na mkoloni mwarabu! Je, kweli tungekubali hadithi kama inayotolewa na CCM leo hii?.. jibu lake ni hapana na magazeti yote duniani yangechapisha mauaji hayo na pengine taifa kuyapa sikukuu!

Hiyo ndiyo Afrika yetu! tunaipenda lakini hatuwezi kuepuka ukweli ambao wananchi wanau face kila siku ya maisha yao.
!
 
Nashukuru sana michango iliyotolewa. Nimeangalia jambo hili kwa undani nitatoa maoni yangu mengine labda kesho. Hata kama ASP walikuwa na nia njema, bado sijakubaliana na hatua waliyotumia katika mapinduzi yale hasa ukizingatia kuwa Zanziba lilikuwa ni taifa lenye sovereignty kama Tanganyika, Kenya na Uganda. Kutumika kwa Okello, Mfaranyaki na Injini katika mapinduzi yale si halali na kiliharamisha zaidi mapinduzi yale licha ya kuondoa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia tena baada ya siku 33 tu kabla hata hatujaona kama kweli ilikuwa serikali mbaya au vipi. Nitatoa details zaidi hapo kesho
 
Mzee Mkandara,

Sasa nakuona umebadilika na kuwa fair katika mawazo yako. Ahsante nimekusoma Bob
 
Kichuguu,

Kwanza nashukuru sana kama tumeelewana ktk lengo la mapinduzi yenyewe ambayo yalikuwa ni LAZIMA yatokee kwa sababu mtawala alikuwa bado Sultan.
Mimi sintagusia sana maswala ya vyama hivi kwani wakati huo vyama havikuwa na mrengo zaidi ya kusimamia kundi la watu. Na wala siwezi kuwalaumu Hizbu ama ASP kwa sababu hizo hizo. Tatizo kubwa wengi hapa wanajaribu kutazama vyama hivi kwa hali iliyopo leo hii na pengine kushangaa kwa nini Hizbu kilikuwa chama cha waarabu zaidi ya weusi, lakini wakati huo huo ukitazama nchi zote zilizotawaliwa duniani zenye mchanganyiko wa rangi zilikuwa na vyama vinavyosimamia jumuiya zao kutafuta haki ya watu ama kundi lao, Zanzibar was not exceptional.

Sasa turudi ktk case ya Mapinduzi yenyewe ambayo umezungumzia sana kuhusu Karume.
Binafsi sikumpenda Karume kama kiongozi wa ASP ama Zanzibar kwa sababu moja kubwa ambayo pia aliitumia mtu kama Idd Amin. Na kwa vile Idd Amin aliyafanya mapinduzi sina haki ya kupinga mapinduzi hayo dhidi ya Obote na wakati huo huo itafsirike kuwa maana yangu ni kwamba namtetea Idd Amin kama ni kiongozi mzuri. Kwa hiyo ndugu Kichuguu sina maana kabisa kwamba nakubaliana na Utawala wa ASP kuwa ni bora kuliko Hizbu isipokuwa kosa kubwa la Hizbu lilikuwa ni wakati....wakati huo nina hakika hata uchaguzi wa kwanza wa Rhodesia kama Ian Smith angeshinda nadhani kungetokea mapinduzi ya aina hiyo hiyo hata kama Ian Smith angeweza kuwa mtu mzuri... tatizo ni watu gani wanaowakilishwa na chama kile - minority! hivyo basi viongozi wa Hizbu wanaweza kuwa wazuri sana kuliko ASP lakini the timing was right for ASP... not for Hizbu na viongozi wake!
Na mwisho labda nigusie kuhusu Wale wahuni waliooweza kuyafanya mapinduzi ambao umeuliza kwa nini wameonekana wahuni tu.
Ni kweli na sidhani kama Karume na baraza lake la mapinduzi wangeweza kushika Bunduki na wala usitegemeee kumwona Bush, viongozi maseneta, congress wakitokea ktk picha za mapinduzi ya Iraq.
Na hata sisi tulipomwondoa nduli Idd Amin hatukuweza kuona picha za Nyerere na viongozi wa Tanzania wameshika silaha mbele ya mapinduzi hao.
Kwa hiyo pamoja na kuwepo kwa utata wa nani hasa wahusika wa mapinduzi hayo bado tukubali kuwa aliyepinduliwa hapa ni Sultan mtawala na sio Hizbu pamoja na kwamba utawala wa wizara za nchi hiyo ulikuwa chini ya serikali ya Hizbu. Hivi ndivyo navyoelewa mimi na ndio maana nimekupeni mfano mzuri wa nchi kama Zimbabwe na South Afrika.

Labda tukirudi leo hii na kutazama upya sababu ya mapinduzi hayo tumekuja gundua kuwa Hizbu ndio walikuwa the biggest looser! na hata walipoweza jiunga na ASP bado kulikuwepo na viongozi weusi wa ASP wenye usongo na jamaa wa Hizbu. Chuki ambayo hadi leo hii imeweka chachu kubwa ktk kujenga Umoja wa Wazanzibar. Hawa jamaa wamekuwa wakitengwa kila siku na kila juhudi zao kushika nafasi nyeti hasa za visiwani imekuwa kama vile ni laana. Do I support that? jibu lake ni NOOO! na ndio maana hata ktk muungano wa Tanzania bara na visiwani sipendi kabisa jinsi bara tunavyo wa treat visiwani ktk upande wa uongozi. Na kama utazama zaidi kutafuta sababu kubwa ya matatizo haya utakuta kwamba sisi waafrika nafasi ya kutawala nchi ni nafasi pekee ya kuvuta UTAJIRI!.. Kwa hiyo mjomba utanikuta siku zote nimekuwa consistant na mtazamo wangu ktk swala la Watawala wetu.
Hawa watawala wetu ni wabaya kuliko hata wakoloni kwani ile dream yetu ya kutotawaliwa na kuwa watu huru wenye uwezo wa kujichagulia maendeleo yetu imegeuka na kuwa jinamizi!.. bado tunatawaliwa na kibaya zaidi ni kwamba tunatawaliwa na ndugu zetu wenyewe wa damu ambao hatuwezi kuwaepuka...
Tazama mauaji ya Pemba! hawa ni Watanzania wakiua Watanzania wenzano kwa sababu ya kutawala tu. Ebu fikiria kama mauaji yale yangefanywa na mkoloni mwarabu! Je, kweli tungekubali hadithi kama inayotolewa na CCM leo hii?.. jibu lake ni hapana na magazeti yote duniani yangechapisha mauaji hayo na pengine taifa kuyapa sikukuu!

Hiyo ndiyo Afrika yetu! tunaipenda lakini hatuwezi kuepuka ukweli ambao wananchi wanau face kila siku ya maisha yao.
!

kwa mara ya kwanza tunakubaliana mie na wewe katika hoja.maelezo matamu sana na yamejaa ukweli.uafrika sio rangi, na nikiyatizama haya mapinduzi hao waliopinduliwa walikuwa na haki ya kuitwa wazanzibari zaidi kuliko hao waliopindua, lakini kama alivyosema mkandara watu walitumia right timing na pia walijua wapi kuna upenyo wa kuyafanya mapinduzi hayo yakubalike! na wamefanikiwa ,kwani pale walipotumia neno "uafrika" na "rangi nyeusi" na kwa upande wa pili wakatumia "uarabu" "usultani" na "utumwa" (ukizingatia sana utaona hata siasa za leo za zanzibar zinatumia vipengele hivyo hivyo).utashangaa pale utakaposkia mpaka leo zanzibar kuna chama kinaitwa chama cha waarabu.na nikiwatizama hao waarabu walokuwemo kwenye hicho chama basi nakuwa nachanganyikiwa kidogo.natamani hii mada ingeweza kumfikia kila mtanzania katika kila kona ,kwani kwa kweli vijana mnafichua ukweli ambao wengi hawaujui mpaka leo.iko siku! iko siku! iko siku!
 
....kuna hiki kipengele ambacho nimebadilisha on my previous posting. samahani kwa usumbufu.

3.Mtumwitu anaeleza kwamba SHAMTE aliwahi kutamka kwamba hata angepewa UTUME ndani ya Muungano wa ASP na ZPPP angeukataa. Hayo ni maneno mazito sana ukizingatia kwamba Shamte ni Muislamu. Ni elimu kubwa hiyo, Mwafrika alikuwa ktk daraja gani huko ZNZ.
 
Kwani Shamte alikuwa mwarabu? Mimi ninadhani kuwa alikuwa mshiraz, na washiraz na waafrika walikuwa kundi moja.

Shamte alikuwa ASP ambako hakuelewana na Karume kisera, ndipo akaondoka na wala hakwenda kuungana na HIZBU bali alianzisha chama chake cha ZPPP. Ilipokuwa ni lazima afanya coalition na chama kingine, kwake yeye HIZBU ilikuwa ni bora kisera kuliko ASP; kwa hiyo hakutaka tena kuungana na ASP siyo kwa kudharau waafrika ila kwa kutokubaliana nao kisera.
 
kichuguu,
ni sera zipi hizo ambazo alikuwa hakubaliani nazo? lakini sera ya Hizbu ilikuwa kuwadharau waafrika, and that was their main difference with ASP. je, inawezekana hiyo ndiyo iliyompendeza Shamte?
 
JokaKuu,

Nafikiri kosa unalofanya wewe ni kuchukulia kuwa kila mwafrika alikuwa ni Mzanzibar. Tuwe wakweli tu kuwa kuna waafrika kama akina Okello na Mfarinyaki hawakuwa wazanzibar; Shamte alimtaka Karume kuhakikisha kuwa ASP inakuwa ni ya Wazanzibar tu, lakini Karume akafanya kuwa kila mwafrika ilikuwa rukusa kuwa ASP. Tunaweza kujadiliana kuhusu uhalali wa jambo hilo
hasa kama utaleta mfano unaoonyesha kuwa kulikuwa na waarabu waliotoka Tanganyika au Oman wakaruhusiwa kuwa katika HIZBU pia.

Kulikuwa na waafrika wengi katika ASP wengine wakiwa viongozi ambao hawakuwa Wazanzibar. Kumbuka tena kuwa kama ambavyo wakenya na waganda walikuwa hawakaribishwi katika TANU ndiyo vivyo hivyo ilivyotakiwa kwa ASP. Kwa hiyo tofauti kati ya Karume na Shamte ilikuwa kwenye namna wanavyohalalisha uzanzibar; ASP kilikuwa cha kumfurahisha kila mwafrika hata kama siyo mzanzibar. Ingawa hiyo ni sahihi kwa mazingira ya leo, tuseme ukweli katika mazingira vyale ya kupigania uhuru ambapo Zanzibar lilikuwa ni taifa linalojitegemea.

Halafu hii ya HIZBU kuwadharau waafrika nayo inakuwa exagerated sana kwa vile HIZBU ilikuwa na viongozi wengi waafrika. Jembajemba kakutajia baadhi yake hapo juu. Mmojawapo wa viongozi wa kiafrika ndiye aliyesababisha Babu kuhama HIZBU kwa vile alikuwa ni mzee sana ambaye hakuwa na elimu.

NYONGEZA: Kama ambavyo hata leo hapa kwetu watu wa pwani akina Mswahili bado wanawatania watu wa Bara, nadhani utani huo wa Wazanzibar kuwaona wabara kama magovi ulikuwapo lakini sidhani kuwa HIZBU iliwatenga waafrika wote hata wale ambao hawakuwa wabara.
 
kichuguu,
1.Col.Ally Mahfoudh alikuwa Mzanzibari, lakini kwa jinsi alivopigania uhuru wa Msumbiji, alipewa heshima kama vile ni mzalendo wa Msumbiji. Karume na wenzake wana haki kama Wazanzibari kumuenzi mtu yeyote aliyewasaidia ktk harakati zao za kurudisha heshima ya Mwafrika ZNZ.

2.Tunaweza tukabishana kuhusu Shamte,Karume,Mfaranyaki,ASP,HIZBU, lakini ukweli utabaki palepale kwamba Mwafrika alikuwa ni second class ZNZ.

3.Chama kuwa na viongozi "Waafrika" haitoshi. ZNZ is very complicated. Kuna mchangiaji hapa ameshangaa kwanini wapo watu wanaitwa Waarabu lakini they dont really look like Arabs. Sasa usije ukawa umechanganyikiwa hapa.

4.Hiyo dharau ya HIZBU dhidi ya Waafrika inakuwa exagerrated na nani? Inakuwa exagerated hapa JamboForums? Inakuwa exagerated na wanamapinduzi who acted so violent against Arabs and their perceived supporters? Inakuwa exagerated na wananchi waliounga mkono Mapinduzi?
 
Jokakuu,

Niliahidi kuliongelea hili kwa kirefu zaidi leo jioni baada ya kazi. Nitajitahidi kufanya hivyo, nadhani baada ya hapo utaelewa nina maana gani.
 
Katika ujumbe wake wa mwaka mpya wa 1968 kwa mabalozi, Mwalimu Nyerere alizungumzia haya ya mataifa yote kuishi kwa amani. Na ni katika hotuba yake hiyo hekima yake ya kidiplomasia bado inaonekana. Maneno yake hata hivyo yalikuja kutiwa majaribuni baadaye na kuhakikisha kuwa yalikuwa na ukweli. Akizungumzia mataifa kwenda kuyakomboa mataifa mengine Mwalimu alisema:

It is impossible for one people to free another people, or even to defend the freedom of another people. Freedom won for a people by outsiders is lost to those outsiders, however good their intentions, or however much the outsiders had desired to free their oppressed brothers. That is the nature of freedom; it has to be won, and protected, by those who desire it.

Of course, others can help a people who are struggling for freedom; they can give refuge, facilities for action, and they can give moral and diplomatic support to an oppressed people. But no group or nation - however powerful- can make another group or another nation free.

The struggle must be waged by those who expect to benefit from it. If the persecuted and the oppressed have really been denied their human rights, and if there is really no peaceful means of progress availabe to them, then they have the the right to demand of the rest of us that we should support their struggle - and not join their oppressors on the grounds of maintaining peace. But we can not replace their struggle, and we should not try.

For if we do so, we are not trying to free our brothers; we are simply trying to replace one oppression by a different one. It may be less harsh, it may take different forms; but it will not mean freedom for those who lack it.

mawazo hayo unaweza kuyaweka kwenye context ya mapinduzi ya Zanzibar au vita vya Iraq.
 
NYONGEZA: Kama ambavyo hata leo hapa kwetu watu wa pwani akina Mswahili bado wanawatania watu wa Bara, nadhani utani huo wa Wazanzibar kuwaona wabara kama magovi ulikuwapo lakini sidhani kuwa HIZBU iliwatenga waafrika wote hata wale ambao hawakuwa wabara.

kichuguu,

MAVOGI was a racial slur towards people of African descent in ZNZ. Kama ingelikuwa ni utani kwa mtu yeyote asiyetahiri basi, ungesikia Waingereza/Wazungu wakiitwa magovi pia. After all, btn Mzungu na Mwafrika, nadhani it the former ambao wamekubuhu kwa kutokutahiri.
 
Asante kwa kunifahamisha hivyo
 
Back
Top Bottom