MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,679
- 1,612
nitajitahidi kuweka wazi maana ya neno hili la hizbu alwatwani zenjibar.
kiswahili cha zanzibar na hasa wakati ule kiliathiriwa zaidi na kiarabu, na mara nyingi watu wa kisiwa kile walikuwa katika maongezi yao huchanganya zaidi baina ya kiswahili na kiarabu, sawa na leo kuona baadhi ya miji yetu kuchanganya kiswahili na kiingereza.
mfano utasikia nnmpeleka mtoto madrasa ikimaanisha nnampeleka mtoto shule.
wizara ya ya ziraa maana yake wizara ya kilimo, na hadi leo bado athari hizo zipo, kwa mfano kule kwetu zanzibar ktk kipindi hiki kuna wizara inaitwa wizara ya elimu na mafunzo ya amali neno amali ni la lugha ya kiarabu likimaanisha vitendo au kazi za mikono.
sasa rurudi kwenye neno letu, hizbu kama ulivyosema lina maana ya army, lakini kwa nyongeza lina maana ya movement, party
mfano hizbollah( hizb maana yake party na allah maana yake god) kwa hiyo maana kamili itakuwa Party of God pia yaweza kuitwa Army of God (for ref: www.yeshuatyisrael.com/Powerpoint/Hezbullah.ppt
mfano mwengine ni chama cha HAMMAS cha wapelistina hiki urefu wake Hizbu Almuqqawamat Al-islamiyy
nacho kina maana hizbu ni movement, na almuqawamat Resistance na Al- islammiy iko wazi sasa utaona wanakiita Islamic Resistance Movement hapa imetumika kama movement.
na hata kule Sudan chama kinachoongoza nchi kinaitwa Almuutamar hizbu alwattwan ikiwa na maana almuutammar ni congress, na hizbu party na wattan ni National utapata kinaitwa ni National Congress Party.
turudi kwenye alwattaniy, zanzibar hadi kesho neno hjili tunalitumia kumaanisha utaifa au mzawa, japo sasa kuna harakati za kuliondoa na kutumia mzanzibari halisi lakini ukitaka kusema mimi ni mzawa kindaki ndaki unasema mimi ni muwattin , yule alwattwan.
sasa nnataka kusema kuwa chama cha hizbu urefu wake hasa ni hizbu alwatwani zenjibar na maana yake ni Zanzibar National Party (ZNP). watu kwa ufupi wakawa wanakiita Hizbu na hii ndio maana yake.
na kuitwa Hizbu haimaanishi kuwa waliokuwa hizbu ni waarab tu, hata kwenye quraan neno hili limetumika na wazanzibar wengi ni waislam na wameathiriwa na lugha ya kiarabu ktk matumizi yao.
nnategemea nitakuwa nimejaribu kufafanua maana ya hizbu na any comment zinakaribishwa
Mtumwitu,
Ahsante kwa shule yako bwana! Tunaifurahia! Mimi naona kuna double standard- kwa nini Afro-Shiraz Party (ASP) ni Kiingereza au ukisema Zanzibar National Party (ZNP)- yoote ni Kiingereza inaonekana sawa. Ila Ukisema 'hizbu alwattwan' ambayo ni Kiarabu na maana yake ni hiyo hiyo- kwa nini hizbu alwattwan inaleta negative cannotation? Manake kweli Bara wakati wa Mchakato wa Salim kuwa kugombania Uraisi- walisema tu- yeye ni 'hizbu'- na hii kweli ilimponza Salim kupita na kukubalika! Any stigma associated with hizbu au walionekana ni Waarabu? Kwa nini Kiingereza iwe ok ila Kiarabu maana hiyo hiyo kuwe na stigma!