Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
mkandara.nilitumia jina la nyerere kwavile wewe ulitumia jina la nyerere kwamba ndilo lililoweka uhuru wa kweli zanzibar.hivyo madam umemhusisha nyerere na uhuru wa zanzibar ni lazima ukubali kumhusisha vile vile katika kusimamia haki za binadamu zanzibar.pia usisahau kwamba baada ya mapinduzi, na zanzibar na tanganyika kuungana ,nyerere alikuwa rais wa tanzania na sio wa tanganyika,hivyo apende asipende suala la zanzibar lilikuwa linamuhusu.lakini je nyerere aliweka usawa zanzibar? jibu liko wazi sina haja ya kujibu. je wanamapinduzi wameweka usawa zanzibar? jibu liko wazi haina haja ya kujibu. kuhusu suala la kwamba hata mikoani tanzania bara kuna kudumaishwa kimaisha na kielimu nakubaliana na wewe ila labda kidogo nitumie lugha utakayoifahamu zaidi.pemba kuna ukiukwaji wa haki za binadamu kwa maksudi mazima yaliotokana na siasa mbovu na potofu.na sio pemba tu bali hata sehemu za unguja.siasa ya zanzibar huwezi kuijua kama hujaishi zanzibar.
kuhusu sultani kukataza weusi kuoana na weupe sina uhakika nalo isipokuwa nawajuwa wazanzibari wengi ambao baba mweusi mama mweupe na kinyume chake.labda utupe ushahidi. hata hivyo mie hapa siongei kwa kumtetea sultani wala okello.ninachoongelea kwamba mapinduzi yale yameongeza athari kwenye visiwa vya zanzibar kuliko faida.kwani kile tunachoambiwa kiliondoshwa kwa sultani sasa kiko vile vile au kimezidi , ni sawa na kwamba "mbwa" tumemuita "dog". muhimu ni kwamba miaka mingi imepita na umefika muda sasa wa kuanza ukurasa mpya na kuachana na historia hii ilioichafulia jina na heshima, zanzibar.kuungana kwa watanzania wa upande wa zanzibar ni suala muhimu sana kwasasa,kwa maslahi ya zanzibar yenyewe na hata kwa maslahi ya watanzania wanaopenda usawa na uadilifu.
pia usisahau mkandara ,yule unaemuona wewe ni shujaa kuna wengine wanamuona msaliti,hivyo usilazimishe mtu fulani lazima akubalike na watu wote.muelezee mtu kwa unavyomjua wewe na acha mwengine amuelezee anavyomuelewa.
 
Jembajemba,
Nimezungumzia mwanaume wa kiafrika(weusi) kumwuoa binti wa Kiarabu. Ushahidi gani unataka zaidi ya kutazama kizazi cha wakati Ule!... waarabu waliwaoa wake weusi lakini sio mwanaume mweusi kumuoa binti mwarabu, mzungu wala Mchina. Hawa walikuwa watawala mzee wangu!.. huwezi kula meza moja na boss wako hata siku moja.
Hata leo hii nchi za Kiarabu bado zinaendekeza jadi hizo ambazo mwanaume mweusi hawezi kumuoa mwanamke mweupe wa Kiarabu bila idhini ya wazazi, tena jkwa wakoloni ni uchafu kwao! na hata ukija oa akushtakiwa na wazazi unapotezwa jela ama kurudishwa ulikotoka!.. hakuna haja ya kuonyesha Ushahidi kwani mabo haya yapo na sisi wenyewe ndio waathirika.

Under_age
hapana ndugu yangu matatizo ya Zanzibar Nyerere kwa mguu wake alikuwa akienda na kuongea nao. Wakakaa meza moja kutafuta suluhu na mara nyingi alikubalika na viongozi wa pande zote. Babu, Salim na Seif Shariff ni moja ya vipenzi wa Mwalimu kwa hiyo usitake kumpaka marehemu wakati hao jamaa wanafahamu fika jinsi mwalimu alivyopenda kuungana na kuwa kitu kimoja. Matatizo makubwa yamekuja jitokeza baada ya kifo chake na kama angekuwepo leo hii nadhani hata Katiba mpya ingewezekana kuundwa.
nakumbuka kuna hotuba moja ambayo alisema kuwa ktk makosa makubwa alowahi kuyafanya hapa duniani ni huo MUUNGANO! sielewi hadi leo nini alichokuwa akimaanisha.
 
mkandara, usilolijua ni usiku wa giza.kuna jambo moja kubwa sana lilitokea zanzibar, alipokufa nyerere.ningetamani kulitaja hapa ili kupinga unachosema lakini najua kuna wanaomuona nyerere ni shujaa katika ukumbi huu ,hivyo naheshimu hilo. nakwambia tena siasa ya zanzibar na ya tanganyika ni kusini na mashariki,hazifanani na wala hazikutani, pale unapomuona kijana wa miaka 14 zanzibar anajifanya miaka 18 ili tu apate kupiga kura na yuko tayari kusekwa jela kwa uhaini huo basi ujue hali sio shwaari ndani ya visiwa.mfano acha tukubaliane na wewe kwamba usultani ulikuwa na dhulma,sasa nikuulize suali, jee huu utawala wa sasa na siasa zao, ziko na uadilifu? ndio narudia tena na tena cha msingi ni kuanza ukurasa mpya leo kabla ya kesho.na pia jaribu kunifahamu,mimi simtetei wala kumshutumu yeyote katika historia hii,wakati wa sultani sikuwepo mie nahadithiwa tu na kusoma ,ila kama alikuwa na dhulma yeyote basi sikubaliani na yeye kwani sijali mwarabu wala nani,ninachojali ni pale ninapomuona mmoja anamnyanyasa mwengine.ya sasa hapa zanzibar, nayaona kwa macho yangu na maadam bado niko hai basi inaniumiza sana kuona binadamu anambagua binadamu mwenziwe kirangi,asili,lugha,itikadi n.k. bila ya sababu yeyote ya msingi.
mweupe atakufa na mweusi atakufa, mchaga atazeeka na mpemba atazeeka, mtanzania anaumwa na mkenya anaumwa.tukiangalia kwa undani sote ni wamoja kwanini turuhusu mambo flani yenye maslahi ya kidunia, ikiwemo historia na siasa ,yatubague na kusahau ubinadamu wetuu. ujanja wetu wote mwisho tunaishia kuzikwa chini ya ardhi,kwanini tuziendeleze chuki kisa ni historia! umefika wakati wa kujitambulisha kwa identity ya umoja,wema,upendo,usawa na uadilifu. kiama tukifufuliwa(kwa wale wanaoamini mungu) hutoulizwa kama ulikuwa mchaga,mzaramo,mtanzania,mpemba n.k? utaulizwa kama ulitenda haki na uadilifu duniani au laa,na kama uliishi kwa matakwa ya muumba au vyenginevyo?.
naamini hii ni ndoto inayowezekana ,inshallah iko siku wazanzibari watasahau tofauti zao na kuwa kitu kimoja ili chuki ilokuwepo zanzibar ibaki katika historia tu na sio reality.
 
UnderAge,
Hayo maneno hapo juu mazito-yanafaa kwenye tume ya Muafaka-bahati mbaya mimi sina ufaham mkubwa sana wa mambo ya Zbar! Ila naamni Z'bar will once again be a giant in a near future- ifikie heights za Dubai!
 
Aliyosema Under_Age ndiyo ninayodhani kuwa madhara yaliyoletwa na yale mapinduzi haramu. Tutasema mengi leo lakini lazima tukubali kuwa wale waliopanga, kusaidia na kufanikisha mapinduzi yale ndio walioharibu zaidi maisha ya wazanzibari. Demokrasi ilionekana haina maana kuanzia siku hiyo hadi leo. Yaliyompata Salim Ahmed Salim sote tunayajua, asili yake ni hayo hayo mapinduzi. Nilishasoma sehemu nyingi kuwa Mwinyi hakuwa chaguo la Nyerere mwaka 1985 lakini uvundo wa mapinduzi yale ulimzuia Salim na kuwekwa Mwinyi. Inawezekana Salim angeleta suluhu katika mgogoro wa Zanzibar na hata kutatua mgogoro wa muungano lakini ndiyo hivyo tena.
 
Kichunguu,

Kwa kweli faida ya Mapinduzi yale ni ndogo sana kulinganisha na madhara yake, madhara yake ni makubwa kupindukia kwani haya yote ya chuki, dhulma na demokrasia ya upande mmoja ni madhara ya Mapinduzi yale.

Lakini kama alivyosema under_age hapo juu kuwa tujaribu kuyasahau yaliyopita na tujenge Zanzibar mpya yenye uwelewano na mapenzi kwa sababu naamini hata hao walioshiriki katika mapinduzi yale (ambao bado wahai) sasa hivi wanajuta kwa mauwaji waliyoyafanya wakati ule ya kuuwa watu wasiokuwa na hatia yoyote.

Zanzibar sasa hivi ipo katika hali mbaya kiuchumi watu wamechoka unaweza ukamkuta kijana mdogo lakini jinsi alivyochoka utadhani ni kibabu kizee. So baada ya kusifia mapinduzi au kulaumu it is a high time now ya kukaa pamoja kwa nia safi kabisa ili kuzika yale yote mabaya yaliyotokea wakati ule wa Mapinduzi na baada ya mapinduzi.
 
Nimesoma kwa utuvu sana huu mjadala.Jinsi unavyousoma ndio maswali mengi yanavyoibuka kuliko majibu. Siasa za Zenj;Ni kama kitabu cha Daniel katika biblia,the more you read it the more you get confused, it applies to Zenj`s politics & history, by the way hivi mauaji ya Karume na yenyewe hayana mkono wa mtu?

Jambo lingine nililoliona ni uhusika wa Tanganyika katika siasa za majirani zetu.Hivi inatusaidia nini kutengeneza watawala hapa Tg na kuwaexport kwenda kutawala katika nchi "ZAO" Mifano ipo mingi tu ya watawala waliotengenezwa hapa Tanganyika, Kaguta,Kabila,Chamora etc etc Why? Huko Comoro tunatafuta nini? Ah hebu Wataalam wa JF pawekeni sawa hapa.
 
Ag,
Ah siasa za Zanzibar bwana zimejaa usiri so zinataabu sana kuzielewa ni kizungumkuti kitupu, kwa maana utasikia malengo ya Mapinduzi ni kumuondoa sultan lakini watu waliouliwa baada ya Mapinduzi walikuwa hawausiani na Mapinduzi hata kidogo.Kwa hiyo nadhani cha msingi sasa hivi ni kusahau yaliyopita na hayo Mapinduzi yabaki kama histori tu watu kusameheana na kujenga Zanzibar mpya. Lakini kitu kibaya kilichojitokeza mpaka sasa hivi bado watu hawajawa tayari kusahau tofauti zao sasa kuna kazi kweli kweli hapa.
 
Jembajemba, History is about the past. Ingawa waswahili husema mavi ya kale hayanuki, kama yamenyewa sebuleni ni vema kumtafuta aliyefanya hivyo ili asije akarudia. Historia ni kama mzimu fulani ambao kama hutautafutia maridhiano utakutafuna kila siku. Kwa Zanzibar nadhani ipo haja ya kuunda tume ya maridhiano kwa ajili ya kuupunga huu mzimu ambao maumbikizi yake tunayaskia hata huku Tanganyika kwani wenyewe husema zumari likipigwa Zenj bara wanacheza
 
Ag
Junior Member Join Date: Mon Jun 2007
Posts: 4
Rep Power: 0

Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts

--------------------------------------------------------------------------------

Nimesoma kwa utuvu sana huu mjadala.Jinsi unavyousoma ndio maswali mengi yanavyoibuka kuliko majibu. Siasa za Zenj;Ni kama kitabu cha Daniel katika biblia,the more you read it the more you get confused, it applies to Zenj`s politics & history, by the way hivi mauaji ya Karume na yenyewe hayana mkono wa mtu?

Jambo lingine nililoliona ni uhusika wa Tanganyika katika siasa za majirani zetu.Hivi inatusaidia nini kutengeneza watawala hapa Tg na kuwaexport kwenda kutawala katika nchi "ZAO" Mifano ipo mingi tu ya watawala waliotengenezwa hapa Tanganyika, Kaguta,Kabila,Chamora etc etc Why? Huko Comoro tunatafuta nini? Ah hebu Wataalam wa JF pawekeni sawa hapa.
 
Nilichokubaliana kabisa na Ag ni mambo maweili:

(1) Historia na siasa za Zanzibar zina utata mwingi sana, kadri unavyosoma historia ile ndivyo inavyozidi kukuchanganya. Unahitaji kuwa neutral kabisa katika kuangalia historia ya Zanzibar ndipo utajua kuwa kweli mapinduzi yale yalikuwa na walakini. Ukiyatazama kwa kuchanganya na historia tuliyofundishwa katika "SIASA" utaishia kusema kuwa mapinduzi yale yalikuwa ni halali ili kumwondoa sultani, na ndipo utashindwa kujiuliza kuwa kama kweli lengo lilikuwa ni kumwondoa sultani tu, je watu wote waliouwawa na kuzikwa makaburi ya pamoja walikuwa ni watu wa sultani tu. Kama ungeweza kuona ile kile kipande cha video kilichoonyesha jinsi watu walivyokuwa wanauwawa, mawazo yako kama yangu yangebadilika kabisa kuwa hii haikuwa ishu ya usultani tu. Ni kutokana na nia mbaya ya mapinduzi yale ndiyo maana uhasama bado uko Zanzibar hadi leo. Mambo yote wanayofanyiwa wapenba na watu wengine ambao hawakuwa wanachama wa ASP wakati wa mapinduzi yale ni matokeo ya mapinduzi yale. Kwenye Uchaguzi wa mwaka 2000 au 2005 (sikumbuki vizuri) Karume alyekuwa balozi wetu huko ujerumani wakati huo alisikika akisema kuwa "CCM kwa gharama yoyote haitaachia chama kingine kiungoze Zanzibar kwani itakuwa ni kurudisha usultani; ni lazima CCM italinda mapinduzi kwa njia zozote zile." Maneno yale yalinishtua sana, na nadhani Zanzibar imekuwa ni mali ya CCM hata bila ridhaa ya wananchi kwani hata kama wakishindwa uchaguzi watatumia mabavu kama walivyofanya mwaka 1964.

(2) Serikali hiyo ya mapinduzi imeshindwa kabisa kukiri makosa yake na kuomba radhi ili kuwaweka wananchi wote wawe kitu kimoja tena; wanaona vizuri kuwa na wananchi waliotengana kwa vile inawarahisishia wao kuwatwala: Divide and Rule. Inajulikana wazi kabisa kuwa leo hii baada ya miaka zaidi ya 40, ni mambo machache sana yanayoweza kufanywa kurekebisha maovu ya mapinduzi yale, kwani wahusika wengi wameshafariki. Hata hivyo serikali ya mapinduzi iliyoundwa wakati ule bado ipo ingawa wahusika wamebadilika. Ninadhani kuwa Karume hawezi kusema kuwa baba yake alikosea, kwa hiyo ni vizuri Zanzibar ipate kiongozi ambaye hana madoa ya mapinduzi yale ndiye aunganishe wanachi wa visiwa vile tena. La ajabu ninasikia kuwa kuna fununu kuwa mtoto wa Mwinyi ndiye anyeandaliwa kuwa Rais wa Zanzibar, sijui kama naye ataweza kukemea maovu ya mapindzi yale kwa vile baba yake naye ana madoa yatokanayo na mapinduzi yale.
 
Ninasoma kijitabu hapa cha "MASIMULIZI YA SHEIKH THABIT KOMBO JECHA"Kama kilivyoandikwa na Minael-Hosana O Mdundo DUP 1999.Dibaji na Mwl J K Nyerere. Copyright hairuhusu kunakili sehemu yoyote ya kitabu hicho. Ukiona masimulizi ya mzee huyu halafu ukilinganisha na ya yule bwana Thani wa Oman kuhusu mambo yaleyale utaona kuna MPASUKO mkubwa sana wa kisiasa Zanzibar ambao kama Hawa jamaa hawatakubaliana kutokubaliana basi MPASUKO huu Raisi JK atakuwa anajaribu kupatanisha usiku na mchana ama mbingu na ardhi vitu ambavyo vina uhusiano lakini havitakutana milele. KAZI KWELI
 
Under_age,
Kuna sehemu nimekuuliza kama sii wewe basi itakuwa Njembanjemba kama una rangi?... ilikuwa utani lakini sasa ngoja nikupe ukweli wa hizi hoja zetu.
Utawala wa Sultan ulikuwa na kila hali ya kibaguzi kuliko serikali yoyote ile unayoweza kuifikiria wewe leo hii Afrika labda Darfur peke yake naweza kusema kwa ukaribu. Na sidhani kama kuna kipimo cha ubora wa maisha hayo!

Kutawaliwa na Sultan, Mreno, Mjarumani amaMuingereza kulikuwa na unafuu ambao mimi nausema kwamba mwananchi unakuwa ukijua kwamba Upo JELA kwa hiyo matatizo yote unayoyapata ukiwa kifungoni ni matatizo unayotarajia kukutokea kuliko kuwa huru nje chini ya tawala zetu Ukakosa Uhuru, haki undugu na nafasi sawa ya kufurahia Uhuru huu. Huko jela huna uhuru, haki wala ndugu kwani nyote ni criminals ktk macho ya mtawala. Lakini pamoja na yote haya huwezi kunambia ni afadhali maisha yako yote uishi Jela kuliko kuwa huru ukinyimwa baadhi ya haki zako za msingi. Na kama wewe ulikuwepo Zanzibar chini ya utawala wa Sultan na kweli wewe ni mweusi nadhani utaliona gereza nalozungumzia wakati wa Sultan.

Mateso wanayoyapata Wazanzibar leo hii ni matatizo ya Ubinafsi. Matatizo mengine yanatokana na mahitaji yetu sisi kama vile mtoto anayepinga masharti ya baba kutokwenda disco, kuwa na boyfriend, kurudi nyumbani saa 12 jioni, shule bila kukosa kipindi na homework kila siku yaani gate kali na ukikosea bakora!.. haya ndio malezi alotupa hata sisi Nyerere na tulimlaani vibaya sana na kumwita mkoloni lakini leo hii wengine hapa tumejifunza mengi kuweza kuelewa nini ilikuwa hekima nyuma ya mafunzo ya mwalimu. Lakini katika mafunzo yake kuna mengi ambayo mimi sintaweza kumlea mwanangu ktk mazingira yale na kwa sababu hiyo haiwezi kumfanya mwalimu kutokuwa mlezi mzuri. Haya ni matakwa yangu na pengine mimi ndiye mkosa na mwanangu atakuwa ktk kiza cha maisha zaidi, hata hivyo I'm ready to take that risk!..
Sasa ebu nambie Karume sio Mzanzibar?. huyo Shein sio Mzanzibar na imekuwaje awe mbaya kwenu kuliko huyo Sultan!...na ikiwa unachodai ni CCM basi nina hakika malalamishi yako yamesimama kisiasa kwani hata Seif Sharrif atayafanya haya haya kwa Wazanzibar wanaompinga ama wasiokuwa Wapemba!.

Huu ndio Utawala wa kiafrika na pengine naweza kusema welcome to the club!... nikiwa na maana ya kwamba hakuna nchi yoyote Afrika yenye Uhuru wa raia zake tofauti na Zanzibar! wewe si unaona Botswana wameendelea! basi kaulize maisha ya Watswana kule maporini ambao wanaishi vibaya kuliko hata masai ama mang'ati wetu wakati nchi hiyo tariji ina population ya mkoa mmoja tu wa Tanzania!
Kwa hiyo sii swala la Mapinduzi ni swala la viongozi wetu ambao ni wabinafsi sana na hawa hawa wana ndugu zao ambao wanaishi Tandale Uwanja wa Fisi wakiuza samaki wa kuchoma. Huu ndio Ubinafsi wa Mtanzania unapoanzia na huwezi kuubadilisha kwa mapinduzi ya aina yeyote ile na kamwe nakuhakikishia hakuna kiongozi atakaye kuwa bora kwetu isipokuwa yule atakaye weza kumwogopa Mungu kwanza!
Kuna kitabu cha Obama kakiandika nakuomba kitafute na utie mwanga kidogo labda mwakani utaweza kutukomboa sote!...ndio maisha tulokulia sote mjomba sii Zanzibar, Dar, Ukerewe wala Chicago south east!.. ni maisha ya mtu mweusi!
 
Nilichokubaliana kabisa na Ag ni mambo maweili:

(1) Historia na siasa za Zanzibar zina utata mwingi sana, kadri unavyosoma historia ile ndivyo inavyozidi kukuchanganya. Unahitaji kuwa neutral kabisa katika kuangalia historia ya Zanzibar ndipo utajua kuwa kweli mapinduzi yale yalikuwa na walakini. Ukiyatazama kwa kuchanganya na historia tuliyofundishwa katika "SIASA" utaishia kusema kuwa mapinduzi yale yalikuwa ni halali ili kumwondoa sultani, na ndipo utashindwa kujiuliza kuwa kama kweli lengo lilikuwa ni kumwondoa sultani tu, je watu wote waliouwawa na kuzikwa makaburi ya pamoja walikuwa ni watu wa sultani tu. Kama ungeweza kuona ile kile kipande cha video kilichoonyesha jinsi watu walivyokuwa wanauwawa, mawazo yako kama yangu yangebadilika kabisa kuwa hii haikuwa ishu ya usultani tu. Ni kutokana na nia mbaya ya mapinduzi yale ndiyo maana uhasama bado uko Zanzibar hadi leo. Mambo yote wanayofanyiwa wapenba na watu wengine ambao hawakuwa wanachama wa ASP wakati wa mapinduzi yale ni matokeo ya mapinduzi yale. Kwenye Uchaguzi wa mwaka 2000 au 2005 (sikumbuki vizuri) Karume alyekuwa balozi wetu huko ujerumani wakati huo alisikika akisema kuwa "CCM kwa gharama yoyote haitaachia chama kingine kiungoze Zanzibar kwani itakuwa ni kurudisha usultani; ni lazima CCM italinda mapinduzi kwa njia zozote zile." Maneno yale yalinishtua sana, na nadhani Zanzibar imekuwa ni mali ya CCM hata bila ridhaa ya wananchi kwani hata kama wakishindwa uchaguzi watatumia mabavu kama walivyofanya mwaka 1964.

(2) Serikali hiyo ya mapinduzi imeshindwa kabisa kukiri makosa yake na kuomba radhi ili kuwaweka wananchi wote wawe kitu kimoja tena; wanaona vizuri kuwa na wananchi waliotengana kwa vile inawarahisishia wao kuwatwala: Divide and Rule. Inajulikana wazi kabisa kuwa leo hii baada ya miaka zaidi ya 40, ni mambo machache sana yanayoweza kufanywa kurekebisha maovu ya mapinduzi yale, kwani wahusika wengi wameshafariki. Hata hivyo serikali ya mapinduzi iliyoundwa wakati ule bado ipo ingawa wahusika wamebadilika. Ninadhani kuwa Karume hawezi kusema kuwa baba yake alikosea, kwa hiyo ni vizuri Zanzibar ipate kiongozi ambaye hana madoa ya mapinduzi yale ndiye aunganishe wanachi wa visiwa vile tena. La ajabu ninasikia kuwa kuna fununu kuwa mtoto wa Mwinyi ndiye anyeandaliwa kuwa Rais wa Zanzibar, sijui kama naye ataweza kukemea maovu ya mapindzi yale kwa vile baba yake naye ana madoa yatokanayo na mapinduzi yale.

Mwl Kichunguu,

Mimi nadhani CCM wana tafsiri nyengine kuhusu maana halisi ya usultani, sio kama sisi hapa tunavyoouona usultani. Inaonyesha tafsiri yao kuhusu usultani ni mtu yeyote au chama chochote ambacho sio CCM kuja kutawala Zanzibar. Ukiona yale mauwaji na kauli zao hizo ambazo wanazitoa kila siku utashuhudia kwamba CCM hawamchukulii sultani kuwa ni muarabu ila ni mtu yoyote ambae anatishia maslahi yao, so huyo ndie atakuwa muarabu (sultani).

Ag,

Mauwaji ya sheikh Karume kwa nilivyosikia mimi ni yalikuwa ya kulipiza kisasi. Kuna jamaa mmoja anaitwa Humudi ndie aliyemuua Karume kwa sababu za kulipiza kisasi cha Baba yake ambae aliuliwa na Karume.
 
NjembaNjeba na Kichuguu,

"CCM kwa gharama yoyote haitaachia chama kingine kiungoze Zanzibar kwani itakuwa ni kurudisha usultani; ni lazima CCM italinda mapinduzi kwa njia zozote zile."

Hizi ni politcal games na CUF wanatakiwa kuzitumia zaidi inapopasa hasa wakifahamu kwamba ndani ya CCM wamo Wazanzibar wenye uchungu na nchi yao. Karume aliposema maneno hayo siyatofautishi kabisa na Bush alivyotumia udhaifu wa Demokratic ktk national security kiasi kwamba Bush alidai kuwaachia Demokratic ni sawa na kuiuza nchi yetu!
Yalikuwa maneno mazito sana na yalichukua mijadala mingi yenye matusi ndani ayke. At the end wananchi wenyewe walikubaliana na hukumu za Bush waamini kweli Kelly na Demokratic walikuwa weak ktk kulinda nchi yao dhidi ya wageni!..Now, come to think of it wageni hawa walihusiana vipi na Demokratic?... hakuna uhusiano wowote ila ndio mkenge wananchi walisha uvaa. Ni jukumu la Wazanzibar kujibu mapigo ya namna hii kwa vishindo pia!..
Wee subiria utasikia cha moto Chadema tukianza hizo kampeni ! labda wanifunge mdomo viongozi wangu.. itakuwa mshikemshike!..Huu ni wakati wa sisi kufanya majambo na sio kukaa pembeni na kunyoosha vidole, Lipumba anakuhitaji sana maanake dhoruba zikitoka kila kona hilo mande CCM hana pa kujichimbia!
 
Hiyo point niliyoweka uzito ndiyo yenyewe hasa; umeipatia bila makosa. Hata yale mapinduzi mimi bado nayaangalia katika mtazamo huo huo; kwamba Karume alitaka ndiye awe bosi lakini siyo mzanzibari mwingine. Baada ya kugundua kuwa mapinduzi yale yasingedumu ndipo akaona aungane na Tanganyika haraka haraka kusudi yeye awe mtawala wa Zanzibar huku akipata ulinzi kutoka kwa Nyerere.

Kuhusu mauaji ya Karume, kweli yalikuwa ni ya kulipiza kisasi. Kijana mmoja aliyekuwa ASP aliuliwa na baba yake ambaye hakuwa ASP katika mapinduzi yale pia. Baada ya kijana huyo kupata kamisheni ya jeshi na kuwa Luteni ndipo akaamua kulipiza kisasi. Testimony ya jamaa huyo aliyempiga risasi Karume iko hapa.
 
NjembaNjeba na Kichuguu,

"CCM kwa gharama yoyote haitaachia chama kingine kiungoze Zanzibar kwani itakuwa ni kurudisha usultani; ni lazima CCM italinda mapinduzi kwa njia zozote zile."

Hizi ni politcal games na CUF wanatakiwa kuzitumia zaidi inapopasa hasa wakifahamu kwamba ndani ya CCM wamo Wazanzibar wenye uchungu na nchi yao. Karume aliposema maneno hayo siyatofautishi kabisa na Bush alivyotumia udhaifu wa Demokratic ktk national security kiasi kwamba Bush alidai kuwaachia Demokratic ni sawa na kuiuza nchi yetu!
Yalikuwa maneno mazito sana na yalichukua mijadala mingi yenye matusi ndani ayke. At the end wananchi wenyewe walikubaliana na hukumu za Bush waamini kweli Kelly na Demokratic walikuwa weak ktk kulinda nchi yao dhidi ya wageni!..Now, come to think of it wageni hawa walihusiana vipi na Demokratic?... hakuna uhusiano wowote ila ndio mkenge wananchi walisha uvaa. Ni jukumu la Wazanzibar kujibu mapigo ya namna hii kwa vishindo pia!..
Wee subiria utasikia cha moto Chadema tukianza hizo kampeni ! labda wanifunge mdomo viongozi wangu.. itakuwa mshikemshike!..Huu ni wakati wa sisi kufanya majambo na sio kukaa pembeni na kunyoosha vidole, Lipumba anakuhitaji sana maanake dhoruba zikitoka kila kona hilo mande CCM hana pa kujichimbia!

Mkandara,

Tatizo lenyewe CCM hawasemi kwa maneno tu bali wanatumia na vitendo pia. Kweli wewe hujasikia zahma zinzowafika wapinzani Zanzibar? hebu wewe nenda Zanzibar wakati wa uchaguzi ndipo utakapoona kuwa hawa jamaa (CCM)huwa wanaposema hawatanii, yaani ni kipigo tu mtindo mmoja (wakitumia ASKARI POLISI, JKU, KMKM, MAFUNZO, NA JANJAWID) sasa unataka kuniambia hali kama hiyo kweli CUF watakuwa na ubavu kweli?

Siasa za Zanzibar Bob sio kama za Bara - Zanzibar ni machinjioni mkuu ukifanya mchezo unawahishwa akhera. Na hata huko Bara sasa hivi naona wanafuata style wanazotumia wenzao (CCM) Zanzibar za kutumia vyombo vya dola (Askari) kuwatia adabu wananchi ambao hawaitaki CCM.

Ok ngojea tuwaone hao chadema watakavyopambana na CCM
 
ASALAMU ALAYKUM.

Nimeusoma mjadala huu kwa makini sana.

kwa hakika kuna mambo yamenigusa sana hasa hili la ukiukwaji wa haki za binaadamu.

kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu kwa wapinzani na sio wapemba pekee maana hapa ni wapinzani ila wapemba ndio wamezidi kuonewa.

Mimi ni miongoni mwa watu waliokwenda kufanya utafiti juu ya madhara waliopata wananchi wa kisiwa cha Pemba wakati wa uchaguzi wa 1995 ambapo sikuwepo nchini lakini miaka miwili baadae nilikwenda na nimekuta mambo mengi sana sana yamefanyika huko pia wakati wa uchaguzi 2000 ndio hayasemeki yaani sikuamini kilichotokea. na report kamili imo katika report ya Hashim Mbita. ila kilichowasaidia watu wa visiwani ni waumini wazuri wa dini yao na imani ya dini unaposhindwa kufanya lolote kwa mtu aliyekuzidi ikiwa ni kwa ukubwa wake au kicheo basi unashukuru Mungu na unamtaka yeye akusaidie kutokana na dhulma inayokukabili.

na ndio mkaona hata watu walivyokuwa wanapigwa wanasema Alhamdulillah "tunamshukuru Allah" hiyo ni moja ya imani.

Mimi nimezaliwa Unguja na sina jamaa Pemba ila rafiki zangu wengi ni watu wa Pemba lakini kwa ufupi watu wa pemba wanadharauliwa kweli na sio kwenye elimu tu bali katika kila kitu hata ajira wanabaguliwa hukumbuki walipofukuzwa wengi tu wakati wa Dk. Salmini alipokuwa Rais wa zanzibar?.

wakati alipotangazwa RAIS karume watu wengi walikuwa na matumaini na kumuhesabu kama ni mtu asiyependa ubaguzi na alionekana kuwa unapendelea usawa kutokana na kauli zake wakati wa kampeni lakini kilichotokea tofauti na walivyofikiria wengi.

mwana CCM mkubwa ambaye aliwahi kuwa waziri alinambia kwamba alimsupport karume yeye na wenzake kutokana na kumuona na nia ya kuwaunganisha watu lakini bahati mbaya hakuweza kutekeleza ahadi zake na badala yake yeye ndio amefanya makubwa zaidi.

alipoingia tu mauaji ya 2001 yalitokea makumi ya wananchi wlaipoteza maisha yao, tanzania kwa mara ya kwanza tukapata wakimbizi na ukiukwaji mkubwa wa haki za binanadamu wa wazi wazi ulifanyika katika kipindi chake cha awali.

katika kipindi cha pili ndipo alipoanza kuwafyeka mawaziri wake wanaotoka pemba na akabakisha wa unguja watupu hivi leo serikali nzima ya Rais Karume kuna mpemba mmoja tu ambaye waziri asiyekuwa na wizara maalumu Bi Zainab tena ni mtu aliyekuwa hajasoma sina uhakika wa elimu yake darasa la ngapi lakini nina hakika hajafika hata sekondari na hili halina ubishi wowote.

la kujiuliza hivyo kweli hakuna wapemba ambao wanafaa kuwa mawaziri? hivyo wapemba wakilalamikia hilo waonekane wabaya au waambie ahhh CUF tu hao, it is not good.

Sisi tuliozaliwa baada ya mapinduzi tunapata mashaka na haya mapinduzi maana bado lengo lake halijapatikana hadi leo.

tunavyoambiwa lengo la mapinduzi ilikuwa kumuondosha mtawala mweupe ambaye alikuwa akifanya ubaguzi na kutowapa haki wengi tunambiwa haki ilikuwa ikipatikana kwa wachache lakini hadi hii leo ubaguzi upo tena unauma zaidi kwa kuwa anayetubagua ni mweusi mwenzetu. na miaka zaidi ya 40 sasa haki inapatikana kwa wacheche ambao wana madaraka yaani wakubwa na familia zao ndio
wanaonufaika hivi sasa.

kuna watu zanzibar inapofika maadhimisho ya siku ya mapinduzi wao hujifungia nani na kulia wanalilia nini? wanakumbuka uvamizi uliofanywa wakati wa mapinduzi maana haikuwa mapinduzi tu bali kulifanyika uhuni wa hali ya juu wapo baadhi ya waliokuwa na nia ya kweli ya kupindua lakini wengine dhamira yao ilikuw akupindua na kufanya uasi tu kwa kulipiza kisasi, kuchukuwa watoto wa kike wa kiarabu, wengine walibaka, wengine waliiba n.k. kwa hivyo mapinduzi yatabakia kama historia lakini wapo wanaoona mapinduzi hayajaleta mabadiliko yoyote nikiwemo mie. naunga mkono kuondoshwa kwa utawala wa kisultani na kupewa wananchi wazalendo nchi yao lakini siuongi mkono yaliofanyika wakati wa mapinduzi na baada ya mapinduzi maana hadi leo watu wanapata matese na manyanyaso na kwa mana hiyo tunaona lengo bado halijatimia la mapinduzi.

haki bado haijapatikana kwa usawa wachache ndio wanaomiliki ardhi sasa wachache ndio wanaofaidi matunda ya mapinduzi, wananchi wanaishi katika maisha duani kabisa, wachache ndio maisha ya raha huku mamia ya wananchi wakihaha na maisha, njaa, umasikini ukosefu wa lishe bora, ukosefu wa matibabu, ukosefu wa maji na umeme pamoja na huduma muhimu za maisha zinakosekana katika miaka zaidi ya 40 sasa wananchi wanahangaika na maisha sasa yako wapi malengo ya mapinduzi? ya kumpuguzia mzigo wa maisha mwananchi? yako wapi malengo ya Rais wa kwanza wa zanzibar Abeid Karume ya kutaka elimu, maji na huduma za kijamii na matibabu bure? hivi sasa hakuna cha bure kila kitu kinalipiwa.

stonetowner.
 
kuchukuwa watoto wa kike wa kiarabu, wengine walibaka, wengine waliiba n.k.

..hili nishawahi kulisikia.

..nikaambiwa kuwa ilikuwa amri/maagizo ya karume kuwa waswahili wajitwalie mabinti wa kiarabu,asiye na uwezo wa kuoa na serikali itamsaidia.

..kisa cha hili naambiwa kilikuwa kuondoa dhana ya si waarabu si weusi...kuchanganya kizazi.

..sasa labda maelezo ya kina yanahitajika!

asalaam aleykhum!
 
Back
Top Bottom