Under_age,
Kuna sehemu nimekuuliza kama sii wewe basi itakuwa Njembanjemba kama una rangi?... ilikuwa utani lakini sasa ngoja nikupe ukweli.
sidhani kama kuna umuhimu wa kujua rangi yangu katika hii mada.ila kama utaihitajia nambie nitakutumia PM, ila tukianza kuulizana rangi hapa ukumbini nadhani tutapoteza lengo la kutaka kuwaunganisha waliotengana.
ama kuhusu siasa ya zanzibar ,nitaungana na jemba jemba kwamba bado mkandara ni mgeni saaaaaaana wa siasa ya zanzibar , na ningekueleza mifano mingi, ila napenda niwaunganishe wazanzibari kwa kampeni ya nyumba kwa nyumba ,kuliko kudhihirisha utengano wetu hapa ukumbini. ila kama utapendelea nikupe mifano kadhaa wa kadhaa ya siasa ya zanzibar basi nijulishe na nita ku PM.kama unafikiri wazanzibari wa sasa wanabaguana kwa rangi, basi umekwenda mchomoo, hilo neno warabu na sultani linatumika kwa kampeni tuuu lisikusumbue.
jemba jemba,kichuguu,mzalendohalis,stonetown,mtumwitu, na wengineo , ahsanteni na kwa pamoja ,basi ipo siku tutafanikiwa.dhulma zimezidi kila kona ya ulimwengu,ila tujitahidini kwa ajili ya vizazi vijavyo,kama hatukufaidi sisi watafaidi watoto wetu.
ni mdogo wenu underage.