Sula la kuwapo mafuta Zanzibar si ndoto tena hivi sasa ni ukweli kabisa, anayekataa na akataye.
Hakuna mafuta ZNZ, na hata kama yapo si sababu tosha kuvunja muungano nafikiri ndiyo sababu hasa ya kuungana??? who told you kwamba ZNZ kukiwa na mafuta Mainland hayatapatikana??? si ndo yatakuwa mengi zaidi ndugu
 
...si sababu tosha kuvunja muungano nafikiri ndiyo sababu hasa ya kuungana??? who told you kwamba ZNZ kukiwa na mafuta Mainland hayatapatikana??? si ndo yatakuwa mengi zaidi ndugu
Mimi sijazungumzia habari za kuvunja muungano wala hiyo hotuba ya Waziri wa MUNA katika BLW, Bw. Mansour Y. Himid, haijazungumzia habari hizo. Sikusema wala haijasemwa kuwa kukiwa na mafuta Zanzibar basi Mainland hayatopatikana,hayo nasikia kutoka kwako, naomba uisome vizuri hiyo habari pengine hujaielewa vizuri.
 
Eee mungu hebu wanyime mafuta hawa wasipate hata kwenye "kisoda", hapa hawajapata wanabwabwaja je yakipatikana si ... yatalia mbwata!
 
Eee mungu hebu wanyime mafuta hawa wasipate hata kwenye "kisoda", hapa hawajapata wanabwabwaja je yakipatikana si ... yatalia mbwata!
Tuoembeane dua ya kuku basi!
Bismillahi.
Eeeee Mungu we!!! mafisadi papa kumi na nyangumi mmoja hawatoshi kule bara, hebu jaalia wazaliwe wengine mara kumi na moja.
Amin.
 
Tuoembeane dua ya kuku basi!
Bismillahi.
Eeeee Mungu we!!! mafisadi papa kumi na nyangumi mmoja hawatoshi kule bara, hebu jaalia wazaliwe wengine mara kumi na moja.
Amin.

yaani kinachofanya muanze kukataa muungano mnaogopa mafisadi wa bara?. Kwa style hii basi hayo mafuta hayatapatikana na cloves zimeshuka bei kinoma, labla mjiunge OIC waarabu wajenge bomba la mfuta kuja Zanzibar ili na Zanzibar muanze kuchimba na kuuza.

Tatizo la zanzibar kumejaa watu wenye hasira ya kunyimwa vyeo katika serikali ya muungano na hivyo kuona kama wanaonewa vile!. Huu nao ni ufisadi
 
Kumbe nini? nchi imejaa marasilimali ya kufa mtu bado wanafunzi Kigoma kule wanakalia magogo na mifuko ya plastiki, hamna maana,si bora mngeuzwa nyote na nchi yenu kule Marekani mkawa watumwa!
Karafuu ilikuwa inauzwa kwa jina la Zanzibar tokea enzi za Wafalme Watukufu na ilikuwa ni karafuu bora kuliko ile ya Malaysia na nchi za jirani, kwa ufisadi wa SMT na vibaraka wake kule Zanzibar ikauzwa kwa jina la Tanzania, 'Comepetitors' wakapata la kusema kuwa Tanzania haijawahi kuzalishwa karafuu, wakazidi kuiharibia soko, saivi mnataka mpewe na mafuta muyagawe kama mnavyogawa bwerere madini yenu kwa mafisadi wenzenu.
Wazanzibar hawapo tayari kufa njaa kuneemesha matumbo ya walioshiba.
Hakuna mwenye shida ya cheo wenye shida ya vyeo wapo huko wame'nga'ngani kurudi majimboni mwao hawataki eti wametingwa na shughuli za uwaziri tutawaona 2010 wakagombee jimbo la ikulu, kule visiwani wasijipeleke bure na vyombo vyao vya habari wakitaka wavihamishie uko uko kwa mafisadi wenzao.
 
Zanzibar hakuna cha kufisadi ndio maana husikii kuna ufisadi, ila hao akina Karume naona wameshaanza kujizolea viwanja kwa kwenda mbele.
 
Zanzibar siyo nchi ni kitongoji cha Tanzania. Wanapoteza muda kujidanganya!
 
Hivi kweli swala hili bado linajadiliwa Bungeni?.. Mafuta yakipatikana Pemba au Unguja ni mali ya serikali ya Zanzibar hilo wazi kabisa..
Kinachotakiwa sasa hivi ni kuundwa mfumo mpya wa kodi ambao utatambua mgawanyo wa kodi kwa kila serikali. Mathlan, asilimia 5 ya kodi za serikali ya jimbo hilo, na pengine asilimia 8 ni kodi ya serikali ya Muungano. Hivyo jumla ya kodi kwa mwekezaji ni asilimia 13..

Kibaya cha mfumo huu ni kutokana na Bara kutokuwa na serikjali hivyo ile asilimia 8 bado Zanzibar watakuwa na kisu chao iwe kutokana na hesabu ya watu au mahitaji ya fedha toka seriokali kuu kwa ujumla wa kodi zote.

Inachekesha sana kusikia kwamba Mkapa alijenga misingi bora ya Ukusanyaji wa kodi wakati matatizo makubwa kama haya yanajitokeza kila siku. Alichofanya Mkapoa ni sawa na hao RITES wanaosifika India kwa huduma ya reli kutokana na hesabu ya watu wengi kupanda treni..
Nchi zilizoendelea wanasifika kwa kuweka mpango bora wa usafiri kwa kugawanya usafiri wa ndani mijini (Underground, trums na mabus) kisha kuna usafiri wa nje ya miji kwa kutumia treni, sasa ukija chukua ubora wa huduma zao ndipo unapoweza kuona quality ya investment hiyo lakini sio hesabu ya Wahindi kupanda usafiri wa aina moja nchi nzima..
 
Last edited:
Kwa hili nawaunga mkono wana wa znz.
Iweje almasi ya Mwadui isiwe suala la muungano,au chumvi ya Uvinza isiwe suala la muungano,au gesi ya Mchuchuma isiwe suala la mungano au makaa ya mawe ya Kiwira-Kyela isiwe suala la Muungano ,lkn MAFUTA ambayo hata hayajathibitishwa kuwa yapo na ma-Geologists kule Gando au Mtambwe au Ziwani au Makadara au Mfenesini yawekwe kwenye suala la Muungano?
 
Point noted and taken cheers!
 
Kwani mafuta yapo huko kwenu. Hivi nani ameshathibitisha kuwa ameyaona? Kazeni kamba kupalilia mikarafuu yenu, piganeni utalii ukunemeesheni badala ya kuwatononoa wawekezaji tu, limeni mpunga mjitosheleze kwa mtee. Acheni kuota mchana.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika, mafuta yaligundulika Unguja na Pemba katika miaka ya 50's na 60's na si leo wala jana. Kampuni zilizofanya utafiti huo zikiitwa Shell/BP.
 
Kwani mafuta yapo huko kwenu. Hivi nani ameshathibitisha kuwa ameyaona? Kazeni kamba kupalilia mikarafuu yenu, piganeni utalii ukunemeesheni badala ya kuwatononoa wawekezaji tu, limeni mpunga mjitosheleze kwa mtee. Acheni kuota mchana.

Mkuu, mafuta yapo Z'bar!
 
Asha:'Nina hamu kweli ya kumuona kipenzi changu , yupo bomba ni mwaarabu haswa, akinikubali tunaachana, sawa la aziz?'

John:"Hamna noma, hata ivo si unakumbuka siwezi kukuoa kwasababu dini zetu ni tofauti? mimi sina shida wewe kaliwe tiGO tuu"
 
Nimekuwa nikifuatilia matatizo yanayojitokeza mara kwa mara kuhusu muungano wetu wa Zanzibar na iliyokuwa Tanganyika. kwa mtizamo wangu naona kuna haja ya kuifufua serikali ya Tanganyika ili kubainisha mambo ya muungano na yale ya Zanzibar au Tanganyika peke yake.

Sasa hivi kuna suala la mafuta; Zanzibar wanadai siyo suala la muungano wakati katiba inasema ni suala la muungano.

Zanzibar ina bendera ya taifa na wimbo wa taifa, Tanganyika haina vitu hivyo.

Zanzibar ina Rais, Tanganyika kama nchi haipo hivyo hakuna Rais wa Tanganyika.

Kila jimbo la uchaguzi Zanzibar lina Mwakilishi na mbunge, upande wa bara ambao ungekuwa ndiyo Tanganyika una mbunge tu.

Pamoja na kuwa na mwakilishi na mbunge, majimbo ya zanzibar ni madogo madogo sana kiasi kwamba jimbo linaweza kuwa na wapiga kura hata chini ya 3,000 wakati majimbo ya bara yana mbunge tu na ni makubwa kiasi cha kuwa na wapiga kura zaidi ya 120,000!!

Wana JF nadhani ni wakati mwafaka sasa kuirejesha Tanganyika ndani ya muungano. Tujadili

Nawakilisha
 
SMZ hawajasema kwamba mafuta sio suala la muungano usitudanganye ila wanataka litolewe kwenye mambo ya Muungano. Tujulishe hiyo serikali ya Tanganyika itaboreshaje maisha ya mtanzania au unataka tu jina Tanganyika lionekane kwenye Katiba na watu waanze kujiita mimi mtanganyika na yule mzanzibara. Hiyo bendera ya Tanganyika ikiwepo ndio itatujengea barabara, hospitali, shule, nk?
 
Naamini kila jambo lina wakati wake. Mtoto hazaliwi na kuanza kutembea ila hupitia hatua mbali mbali. Wamedai bendera wamepewa na wimbo wa taifa. Mafuta wanasema ni ya kwao na kesho kutwa bahari ya kwao. Naona kwa mwendo tuwaache watafika mahali watajitoa wenyewe. Bora iwe hivyo kama watajikata lawama iwe kwao. Waachie wembe. Nawatakia michango mema.
 
Waziri(SMZ) DR. Asha Abdallah Juma anasema hata kama yakipatikana kidogo japo saizi ya kigeleni, yatatosha hayo hayo kwa akina mama wa zanzibar kujipaka walau wapendeze, wan'gare babu we khah!


Hawa wavivu wamezoea TAARABU.

Mwarabu akinkopwa asilipwe................ Tunataka mtambo wa shirahhh!!

Gahawa gahawaaaaaaaaaaa. LOL

Ngoja tuwatumie POPO B..... LOL
 
Kila nikiangalia sherehe za muungano hususani zile za mwaka 1964 ambazo huonyeshwa na vituo vya television karibu vyote kila tunapoazimisha sikukuu hiyo, huwa nashindwa kupata jibu kama kweli Karume aliridhia muungano huu au la!

Nasema hivyo kwa sababu tendo la kuchanganya udongo lilifanywa na Mwalimu peke yake huku Karume akiwa pembeni yake akishuhudia sambamba na watu wengine kama akina Kingunge.

Kwa tafsiri ya kawaida ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilitakiwa Mwalimu ashike kibuyu kimoja na Karume ashike kingine halafu wamimine udongo kwa pamoja. Au mnasemaje wakuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…