Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Dream to have a Country (Tanzania) without Mafisadi shall never die naikubali ila kuna probelm kubwa Watanzania lazima wakubali CCM imemaliza kuitafuna nchi na mafisadi wameimaliza CCM kama ilivyomalizwa KANU ya KENYA kwa 10% Kitu Kidogo like Eric Waina ina Songs Taifa la Kitu kidogo hii ndio njia CCM inakoipeleka Bongo Watanzania siku wakikubali maneno ya MWalimu Nyerere kuwa upinzani wa CCM utatoka ndani ya CCM basi Tanzania itakua na weak political parties like Kenya na hapo ndio Demokrasia itakapoanza kuota mizizi huwezi kuwa na Chama kinacho shika kial kitu , Court , Parliament , and state house hutoweza kuondoa mafisadi milele , Watanzania lazima wawape Wapinzani nguvu ya Bunge kuwapa majority na hapo ndio Wafisadi watakapokuwa challnged with out that itakuwa Wadumu mafisadi milele , na Idumu CCM kwani Kenya imetoka huko huko kwenye Powerful KANU na sasa iko kwenye transition ya kujibadilisha hakuna mwenye nguvu zote Kenya mda huu.
Kwa wale wanaotaka Zanzibar iwe mkoa Nafikiri kuna wengine watasema Kigoma iunganishwe na Burundi kwani Waha pia wako Burundi na ni nchi ndogo Pia Rwanda iwe Mkoa wa watanzania hapa ndipo Kila mtu atakapowaogopa Watanzania kwani East African community Zanzibar lazima ipewe uwakilishi kama Burundi na Rwanda licha ya ukubwa au udogo wake kwanini Watanzania hawakupewa nafasi mbili kwenye Jumuia kwa vile ni nchi kubwa kuliko RWanda au Burundi na ina population kubwa kuliko Rwanda yenye 8.5 Millions wakati Tanzania ina watu milioni Sitini vipi iwe na stautus sawa na Rwanda au Burundi ?
 
Kutatua matatizo ya muungano mbona rahisi tu.
Zanziba iwe mkoa/Mikoa, KJ ateue wakuu wa mikoa na Wilaya, Jengo/Majengo ya Baraza la wawakilishi yawe Museum au yageuzwe kuwa Library.
 
Tunashangazwa sana na matamshi ya Mh Kikwete kusema kuwa yuko kwenye harakati za kutatua mpasuko wa Zanzibar na kurekebisha kero za muungano.Kutokana na viongozi wa Zanzibar walivyo na itikadi zao zilizojaa woga na hofu ya kupoteza ajira zao, au sababu zengine binafsi za kutetea matumbo yao na kutojali utaifa wa Zanzibar, wazanzibari tumeamua kuchukua hatua ya kutumia mitandao na kueleza maoni yaliyoko rohoni mwetu.Tunaamini, kuwa maoni yawe mazuri au mabaya yanahitajika kusikika, na huu ni uhuru wetu kuachiwa kuzungumza.Pengine hili la kuachiwa au kupewa uhuru wetu litasaidia kurudisha magazeti binafsi Zanzibar.

Napendelea kuruka moja kwa moja na kutoa maada, yangu ambayo inaeleza kwa uwazi kabisa nini tunachofikiria kuwa ni moja kati ya kero zilizoko kwenye nyoyo zetu kama wazanzibari.Kwa kweli tumeshachoka hatutaki tena kuweko kwenye Jamhuri ya watu wa Tanzania, tunataka dola yetu ya Zanzibar irudishwe.

Sasa unaposema kuwa mgogoro wa Zanzibar au kero za muungano ambazo umezitengenezea kigurupu nje ya bunge, sie wengine hatukufahamu kabisa.

Wakati vyeti feki tuu umetengeneza kamati ndani ya bunge, vyereje kero za muungano utengeneze kamati nje kabisa ya bunge.Wakati haya ni mambo ya kujadiliwa ndani ya bunge, na kama katiba kurekebishwa irekebishwe au muungano kuvunjika uvunjike.

Tutafurahi zaidi na hili la mwisho la kuvunja muungano, maana tunaamini hapa MZALENDO.NET kuwa kero zenyewe ndio huo muungano.

Tunaomba utufahamu kama wengi wetu tunatarajia kuondosha kero za muungano ni kuvunja muungano uliopo sasa na kuingia makubaliano mapya au pengine kurudisha mataifa ya Zanzibar na Tanganyika kama ilivyokuwa huko zamani.

Tunashangazwa kuona kuwa Tanganyika inakimbia sana kuvunja muungano na kuunda uhusiano mpya, hili ni jambo jema kabisa la kudumisha udugu na kuepuka uhasama usio kuwa na umuhimu wowote. Au tunasubiria hadi tuuwane kwa ajili ya kuuvunja huo muungano ambao una matatizo yasiyoweza kurekebishika?

Huu muungano uliopo sasa hauna mkataba wowote, kutokana na majibu ya Mh Khatibu yeye hajawahi kuona waraka wa mkataba wa muungano huu na sisi weneywe hapa MZALENDO.NET umetushinda kuupata mkataba huo.Hii inatufanya sisi vijana wa leo kufikiria zaidi kama Tanganyika imelivamia taifa la Zanzibar, na kulikalia kijeshi au kimabavu. Hatuna imani ya kuwa kuna makubaliano ya aina yoyote baina ya nchi mbili hizi. Sisi binafsi wananchi hatujahusishwa na kufanya maamuzi ya muungano huo, na hatuna maana ya kuwa mutupigishe kura za maoni halafu mutwambie kuwa wazanzibari washakubali muungano. Laah!

Muungano huu uvunjwe kwanza, halafu serekali ya Zanzibar iachwe ifanye maamuzi kama itapendelea muungano au kubakia kama ni taifa huru. Tunaamini kama Zanzibar ikiwa kama nchi inayojitegemea itafanya vizuri tuu kiuchumi, na kimashirikiano na Tanganyika kwa aina moja au nyengine. Lakini hakuna haja yoyote ya kulazimisha mashirikiano ya aina hii yaliyopo sasa baina ya Tanganyika na Zanzibar, tunaomba Mungu kila leo atukubalie dua zetu za kutupatia taifa letu.Wazanzibari tumekuwa kama watu tuliopungua kitu katika nyoyo zetu kila tunapotoka nje ya nchi tukiulizwa munatoka wapi?Jawabu tunakuwa hatuna, tuna hamu sana ya kujivunia kama ni wazanzibari, lakini hatuna fursa hii badala yake tumebebeshwa huu utaifa ambao si wetu wa Kitanzania.

Tafadhalini viongozi tunakupeni heshima zenu, wazanzibari tumeshachoka kufanywa kama vikaragosi wa Tanganyika!

Na Mrfroasty http://www.mzalendo.net/barua-kwa-jk-“wazanzibari-tushachoka-kufanywa-kama-vikaragosi”
 
Pengine hili la kuachiwa au kupewa uhuru wetu litasaidia kurudisha magazeti binafsi Zanzibar.

Sina habari kwamba Zanzibar imekatazwa kuwa na magazeti binafsi.

Tuvunje Muungano? Itakuwa kheri.

Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi!!
 
Poleni kwa hayo yote yanayowasumbua kwani naamini si nyie bali ni Babu yenu Karume ndo aloona kuwa inafaa iwe hivyo,Hata mkija na sababu kibao kwetu sisi tunawaona kama vijana wazamia meli ambao siku zote hudhani kuwa ulaya na America ndiko kwenye maisha mazuri.Hivi huwa mnajiuliza kisawasawa kweli kabla ya kutoa mawazo yenu mbele ya watu.

Ni kweli mnajiona kama mnaonenewa lakini ki ukweli Wanzanzibar wengi mmejaa mawazo ya aina moja. Binafasi huwa nawasifu hao walioamua kutuunganisha kwani hakika nawambia Zanzibar daima ingekuwa chini ya taifa jingine hata kama si TANGANYIKA.

Mna nini cha kuwapa jeuri ya kutaka muwe na taifa lenu peke yenu ili hali mpaka nyanya na kabichi tuna waleteeni toka bara wiki iliyopita ndo nimesikia mnahimizana kuanza kujifunza kulima nyanya ili muepuke kuagiza toka bara, poleni sana tena poleni mno.

Ningekuwa mimi ni Mzanzibar ningekuwa nalaumu kwanini tuendelele kuungana na Bara wakati hakuna utawala wa sheria,kwanini Bara Viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza ndio wezi na MAFISADI wakubwa na hakuna jitihada zozote zinachukuliwa kuwaondoa madarakani kama ambavyo Zanzibar tulivyo,kwanini Bara CCM Imebinafishisha Chama kwa Wafanyabiashara na kuwanyima fursa Wakulima na Wafanyakazi kuamuamustakabari wa chama chao,Kwanini Bara kila anaejitahidi kupigana na mafisadi ndio anakuwa adui wa chama.

Hapo mimi na nyie ningesema kweli bora CCM zanzibar ijitenge ili ibaki kuwa safi kama ilivyoachwa na Waasisi wetu Karume na Nyerere.

Sasa BASI angalizo langu kwenu WAZANZIBAR WOTE KWA PAMOJA ILI ZANZIBAR ITAMBULIKE KIMATAIFA KUWA NI TAIFA IONDOWENI CCM MADARAKANI NA IPATIENI CHAMA CHA UPINZANI NAWAAMBIA HAYO YOTE MNAYOTAOKA YATAKUJA AUTOMATICAL NI NANI ATAKUWA TAYARI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI INAYOLEA UONZO UFISADI.BADALA YA KWENDA MBELE TUNAJADILI KILA SIKU NANI KAFISADI PALE,HATA BUNGE NALO LISHAMEZWA NA MAFISDI MIJADALA HAISHI KILA SIKU NO CONCLUTION ,IKITOKEA INAGUSA MASLAHI YA WACHACHE SIO TAIFA BALI KIKUNDI CHA WACHACHE BASI HOJA HIYO ITAZIMWA KWA NGUVU ZOTE.

Narudia tena CCM zanzibar haiwezi kuleta mabadiko ya kweli mpaka BARA IONDOKE CCM MADARAKANI.
 
].....Mnanini cha kuwapa jeuri ya kutaka muwe na taifa lenu peke yenu ili hali mpaka nyanya na kabichi tuna waleteeni toka bara wiki iliyopita ndo nimesikia mnahimizana kuanza kujifunza kulima nyanya ili muepuke kuagiza toka bara.poleni sana tena poleni mno....[/[/SIZE]SIZE]
Mkuu,
Kabla ya kuweka huu upuuzi wako hapo juu,ungejiuliza kwanza...kabla ya April 1964, Zanzibar ilikuwa ina nini cha kujivunia kama taifa?
Ungejiuliza kabla ya wakati huo,ambao mimi nauita ni mbaya katika historia ya zanzibar kuliko wakati wowote ule,Watanganyika walikuwa na lipi kubwa wanaisadia zanzibar?
Ungejiuliza,kiwango cha hatua za maendeleo kabla ya wakati huo kilikuwaje baina ya mataifa haya mawili, halafu ndo uje hapa na hoja zako za nyanya na mabilinganyi.
Mkuu, poleni nyie wenye ardhi kubwa yenye utajiri lakini mnakula vumbi tu...watu wanaondoka na mchanga wa dhahabu.
Poleni, nyinyi mliokaa na chama cha ufisadi...kwa miaka 47 na hamjawahi hata mara moja kuthubutu kukipa changamoto ya kushindwa hata kwa kusingiziwa...poleni sana...unalolihofia ndo linakuja hilo
 
TUMSUBIRI AKITOKA JAMAIKA ATAKUJA NA UFUMBUZI WA MATATIZO YETU, amakweli nikiipigia kura CCM nifie kwenye kibanda cha Kura.
 
Ndugu mleta hoja,
Ulichoongea kina 95% ya ukweli na bila shaka wewe kama Mzanzibar una kila sababu ya kupata uchungu.

- Nyie kama vijana wa kizanzibar mna kila sababu ya kuoneshwa mikataba iliyokuwepo ama iliyowekwa mpaka kutokea muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hilo lingeweza kusaidia sana katika kupata ukweli.

Mimi ni kijana wa Tanzania Bara na bila kuficha naona wazi kwamba muungano uliopo una kasoro, hivyo ilikuwa ni busara na hekima kuzishughulikia kasoro hizo ili kuimalisha muungano na wala si vyema kuvunja muungano.

Dunia ya leo mataifa yanaungana ili kuwa na nguvu. Sisi kama watanzania bara na visiwani hatuna sababu ya kuvunja muungano, tuna kila sababu ya kuuimarisha muungano ila tuzishughulikie kasoro zilizopo ndani ya muungano bila ya kuchelewa wala kuona woga kwa lengo la kuepusha machafuko huko mbeleni.
Mimi kama kijana wa Tanzania Bara siwezi kuruhusiwa kununua ardhi na kujenga Zanzibar, lakini wazanzibar wanaruhusiwa kununua ardhi na kujenga Tanzania Bara. Hapa naona wazi kwamba hii si haki hata kidogo. Huo ni mfano mdogo tu wa kasoro za muungano wetu.

Ni muhimu kushughulikia kasoro zilizopo haraka kadri iwezekanavyo.
 
Kutatua matatizo ya muungano mbona rahisi tu.
Zanziba iwe mkoa/Mikoa, KJ ateue wakuu wa mikoa na Wilaya, Jengo/Majengo ya Baraza la wawakilishi yawe Museum au yageuzwe kuwa Library.
When this happen pray to God that all Zanzibaris are dead, but if they are still alive then its no need to continue with life.

With that being said, we will officially declare JIHAD which will make your Daresalaam light up on fire just like what you wanted!
 
Habari zenu wana JF,

Tunaomba maoni yenu wana JF kwenye mchakato mzima wa mfumo gani wa muungano watanzania wanaupendelea.

Thanks guys...
 
Serikali moja tu "Serikali ya Muungano wa Tanzania"
Sbb: Kupunguza idadi ya mawaziri, wakuu wa serikali
Ila uwekwe utaratibu kwenye katiba kwamba rais wa Tanzania "asipochaguliwa na Wazenj kwa 50% anakuwa hafai kuongoza Tanzania ili kulinda maslahi ya wa Zanzibar.
 
Mkuu nimeiruka hiyo possibility ya serekali moja, na sioni option za kuedit hiyo poll.

Pengine mode wanaweza kusaidia kuongeza option ya serekali moja.

By the way mimi kama mzanzibari sikubaliani na wazo la serekali moja, hiyo ni kutokana utendaji wa serekali SMT ni mbovu na wenye sera za centralization economic strategy.Hii akilini mwangu ndio sababu ya msongamano hapo Dar, kwamba SMT inashindwa kuendesha uchumi sehemu zengine inalamizika kuuwa kila kitu na kukisogeza Dar.

Ikiwa mikoani hali ni mbaya mno, mimi kama natoka Zanzibar, kuelekea serekali moja ni manaake nijitayarishe na kufanya uhamiaji Dar....

By the way, nilishawahi kuchukua mawazo ya mtandao wa MZALENDO.NET ambao wengi ni wazanzibari mawazo juu ya mfumo wa muungano ni kama ifuatavyo:

Muungano gani unaopendelea?

Serikali 3(SMZ,TANG,TZ) (44%, 96 Votes)
Sitaki muungano (42%, 93 Votes)
Sitaki mabadiliko (10%, 21 Votes)
Serikali 4(SMZ,PBA,TANG,TZ) (4%, 9 Votes)

P:S
**Again naomba radhi sikufikiria uwezekano wa serekali moja, nilisahau kabisa 😀
 
Hakuna problem mkuu
ila hiyo ya serikali nne ..nimecheka sana???

Serikali moja ni jambo zuri kwa nchi..nikuangalia jinsi ya wazenj wanaweza ku marais kikatiba..
 
Mkuu nimeiruka hiyo possibility ya serekali moja, na sioni option za kuedit hiyo poll.

Pengine mode wanaweza kusaidia kuongeza option ya serekali moja.

By the way mimi kama mzanzibari sikubaliani na wazo la serekali moja, hiyo ni kutokana utendaji wa serekali SMT ni mbovu na wenye sera za centralization economic strategy.Hii akilini mwangu ndio sababu ya msongamano hapo Dar, kwamba SMT inashindwa kuendesha uchumi sehemu zengine inalamizika kuuwa kila kitu na kukisogeza Dar.

Ikiwa mikoani hali ni mbaya mno, mimi kama natoka Zanzibar, kuelekea serekali moja ni manaake nijitayarishe na kufanya uhamiaji Dar....

By the way, nilishawahi kuchukua mawazo ya mtandao wa MZALENDO.NET ambao wengi ni wazanzibari mawazo juu ya mfumo wa muungano ni kama ifuatavyo:

Muungano gani unaopendelea?

Serikali 3(SMZ,TANG,TZ) (44%, 96 Votes)
Sitaki muungano (42%, 93 Votes)
Sitaki mabadiliko (10%, 21 Votes)
Serikali 4(SMZ,PBA,TANG,TZ) (4%, 9 Votes)

P:S
**Again naomba radhi sikufikiria uwezekano wa serekali moja, nilisahau kabisa 😀

Mkuu hayo yote yanazungumzika,ili mradi tuu mjadala uwe mpana ili kujitahidi kuziba mianya yote inayoleta migogoro na matatizo katika muungano wetu.Ingawa mie sio mzanzibar ila niliishi zanzibar na ninafanya kazi katika serikali ya mapinduzi,kwa mtazamo wangu serikali moja inaweza kuwa option nzuri zaidi.Tuikarabati katiba yetu ya muungano ili iweze kutoa majibu ya maswali na madukuduku yanayotusimbua,hakuna kusichowezekana.
 
From Tumain's signature: "Yesu siyo mungu ni mtu na mjumbe wa Mwenyezi Mungu"
1. "Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu." (Yoh. 1:1)
2. "Watu wanaotembea katika giza wameona nuru kuu, wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa: Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele. Wivu wa BWANA Mwenye Nguvu utatimiza haya." (Isa. 9:2, 6-7).
 
Mkuu pamoja na kwamba hapa umekwenda off topic, pia unaweza kuanzisha mjadala mpya kwenye thread hii tofauti na matarajio ya mwanzilishi.

Huyo mdau uliyemjibu nakushauri aiza umPM au anzisha thread umualike aje kuchangia mawazo yake ili upate nafasi nzuri na muafaka ya kumuelimisha.

maana hii mambo ya imani ni kitu cha kipekee sana inabidi ijadiliwe kipekee, na kama unavyojua kuna jukwaa la dini unaweza kumpeleka huko na kumwelimisha.

hatahivyo ahsante kwa ufafanuzi mzuri na nadhani ataitafakari hiyo signature yake!
 
mfumo wa serikali mbili uendelee.

mfumo huu hauna tatizo. matatizo mnayoyaona sasa ni matokeo ya ulegevu wa uongozi. wazanzibari wanapaswa kujisikia kama watanzania zaidi kuliko wazanzibari zaidi. viongozi wa kisiasa wana wajibu wa kuhaasisha umma na sio kuchochea hisia za upande mmoja wa muungano kupuuzwa au kuonewa.

kwa ujumla, watanzania wa bara wamepiga hatua kubwa sana katika kuukubali muungano kwani ni wachache sana bado wana kumbukumbu ya kitu kinaitwa tanganyika, wakati tanzania visiwani kila mtu anajijua kuwa ni mzanzibari! hapo ndio mama wa haya matatizo ya mpasuko wa kisiasa anapozaliwa
 
Mkuu pamoja na kwamba hapa umekwenda off topic, pia unaweza kuanzisha mjadala mpya kwenye thread hii tofauti na matarajio ya mwanzilishi.

Huyo mdau uliyemjibu nakushauri aiza umPM au anzisha thread umualike aje kuchangia mawazo yake ili upate nafasi nzuri na muafaka ya kumuelimisha.

Ok, nashukuru kwa ushauri ndugu! Naomba tuendelee na mjadala kuhusu Muungano! Najua watu wanapenda mabadiliko ya mara kwa mara. Wanapenda waone Muungano ukichukua sura mpya, only that! Wengine wanataka wajitwalie madaraka kupitia mabadiliko hayo ya Muundo wa Muungano. Lakini mimi nionavyo hata kama kutakuwa na Tatu, Nne hata zaidi, hakutaondoa matatizo tuliyo nayo! Ni afadhali basi tuwe na Serikali moja kuliko kuzidi kugawanyika! Dunia sasa hivi inazidi kuungana, huku sisi tunazidi kugawanyika kila leo. Tunahitaji basi kurekebisha mind set zetu kama watanzania, tusipelekeshwe na wanasiasa ambao wana "ulterior motives!"
 
Back
Top Bottom