Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Wana Jamii forum,

Mimi binafsi namuunga mkono Maalim Self ya kuwa mambo ya Wazazibari tuwaachie wazazibari wenyewe hao ni ndugu na wameamua kupatana sasa sisi tuna wasiwasi upi? ugomvi wa ndugu usiingilie, wakipatana utaonekana mchawi.

Baada ya kuona matatizo makubwa 1995, 2000. 2005 mnataka tena yatokee mengine 2010? kama wao wameamua kwamba kukata mzizi wa fitna ni kuwa na serikali ya mseto sasa tatizo lipo wapi?

Acheni wajenge zazibari mpya yenye upendo na amani, sioni tatizo la Rais kuongezewa muda ukilinganisha na vurugu na mauaji ambayo tumeshuhudia yakitokea katika chaguzi zilizopita.

Zazibari ina historia yake, sisi bara tukae kimya kama wameamua wenyewe kuunda serikali ya mseto kuelekea uchaguzi Mkuu tatizo ni nini? kwani katiba ipo kwa maslahi ya nani? si wananchi wenyewe.

Mtu mwingine anasema huko ni kuchezea katiba - kwa hiyo tuache watu waishi kwa fitna, wauane, wawe wakimbizi kwenye nchi yao kwa sababu ya katiba? Lazima tutibu upele kabla halijawa ndonda ndugu.

Hatutaki wapemba hasa wamama na watoto wawe wakimbizi kwenye nchi yao. Hongera Maalim -na Rais Karume mna upeo mkubwa sana wa mawazo.
 
Nawaunga mkono sana wazanzibari kupitia Karume na Seif kwa kuamua kumaliza tofauti zao na kuipeleka mbele zanzibar.

Ni jambo la heri na nawatakia mafanikio katika kuyafikia yale wanayoyatamani.
Ni wakati sasa kuwa na siasa za mashirikiano ndani ya Zanzibar.
 
Wana Jamii forum,

Mimi binafsi namuunga mkono Maalim Self ya kuwa mambo ya Wazazibari tuwaachie wazazibari wenyewe hao ni ndugu na wameamua kupatana sasa sisi tuna wasiwasi upi? ugomvi wa ndugu usiingilie, wakipatana utaonekana mchawi.

Baada ya kuona matatizo makubwa 1995, 2000. 2005 mnataka tena yatokee mengine 2010? kama wao wameamua kwamba kukata mzizi wa fitna ni kuwa na serikali ya mseto sasa tatizo lipo wapi?

Acheni wajenge zazibari mpya yenye upendo na amani, sioni tatizo la Rais kuongezewa muda ukilinganisha na vurugu na mauaji ambayo tumeshuhudia yakitokea katika chaguzi zilizopita.

Zazibari ina historia yake, sisi bara tukae kimya kama wameamua wenyewe kuunda serikali ya mseto kuelekea uchaguzi Mkuu tatizo ni nini? kwani katiba ipo kwa maslahi ya nani? si wananchi wenyewe.

Mtu mwingine anasema huko ni kuchezea katiba - kwa hiyo tuache watu waishi kwa fitna, wauane, wawe wakimbizi kwenye nchi yao kwa sababu ya katiba? Lazima tutibu upele kabla halijawa ndonda ndugu.

Hatutaki wapemba hasa wamama na watoto wawe wakimbizi kwenye nchi yao. Hongera Maalim -na Rais Karume mna upeo mkubwa sana wa mawazo.

Uko sahihi mkuu nakuunga mkono 100% ninachoomba nione katiba inabadilishwa na Karume anapewa nafasi ya kumalizia kile kizuru alichikianzisha yeye pamoja na maalim seif kwa maslahi ya Wazanzibari wote na si venginevyo!

Kuna watu wengine wataleta hoja zao zisizo na msingi na ubinafsi eti nina wasiwasi kwa kubadilisha katiba. Wasiwasi kaeni nao kinachoangaliwa na ndicho cha msingi ni umoja wa kitaifa na maslahi ya wazanzibari wote yanazingatiwa period

Hatupendi kuona watu wengine wanapoteza maisha katika uchaguzi ujao ikiwa kuna nafasi ya kufanya marekebisho na kupatikana amani ya kudumu.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania , Mungu Ibariki Zanzibar!!
 
sawa waachiwe waamue ya kwao wenyewe kwani wao ndio wenye kuijua znz zaidi na ndio watakaokuwa affected na uongozi au matatizo ya kiuongozi. after all znz ina watu wachache wakikaa pampja wanaweza kuutumia utalii pekee wakawa very rich ka vile sheyshels, bahamas, d.republic. Ila waache uyakhe ndo unaowaangusha! wafanye kazi, wana uwezo wa kuendelea sana kuliko bara!
 
sawa waachiwe waamue ya kwao wenyewe kwani wao ndio wenye kuijua znz zaidi na ndio watakaokuwa affected na uongozi au matatizo ya kiuongozi. after all znz ina watu wachache wakikaa pampja wanaweza kuutumia utalii pekee wakawa very rich ka vile sheyshels, bahamas, d.republic. Ila waache uyakhe ndo unaowaangusha! wafanye kazi, wana uwezo wa kuendelea sana kuliko bara!

Mamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Uko sahihi mkuu nakuunga mkono 100% ninachoomba nione katiba inabadilishwa na Karume anapewa nafasi ya kumalizia kile kizuru alichikianzisha yeye pamoja na maalim seif kwa maslahi ya Wazanzibari wote na si venginevyo!

Kuna watu wengine wataleta hoja zao zisizo na msingi na ubinafsi eti nina wasiwasi kwa kubadilisha katiba. Wasiwasi kaeni nao kinachoangaliwa na ndicho cha msingi ni umoja wa kitaifa na maslahi ya wazanzibari wote yanazingatiwa period

Hatupendi kuona watu wengine wanapoteza maisha katika uchaguzi ujao ikiwa kuna nafasi ya kufanya marekebisho na kupatikana amani ya kudumu.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania , Mungu Ibariki Zanzibar!!

WE! Nadhani una damu ya kidiketa,Sidhani kwamba Karume ni mtu ambaye yuko talented kuliko wazanzibar na wana ccm wote,isitoshe anaposema amalizie mazuri aliyoanzisha ina maana hakuna wana ccm wengine wenye kuweza kuendeleza hayo yaliyoanzishwa? Maridhiano ya Karume na Maalim ni ya kiofisi zaidi kuliko mtu binafsi,hivyo hata kama Seif na Karume hawapo lazima muafaka yufikiwe.La msingi nadhani tufikie wakati wa kuacha mawazo mgando na kudhani bila A wala B nchi haitawaliki.Tafadhali bwana Zanzibar ni TANZANIA........................!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ni vigumu kusema tunawe kabisa mkono kwenye mambo ya Zanzibar kwa sababu what affects Zanzibar affects the rest of the country too. Sasa huu muungano una maana gani kama ya Zanzibar yaachiwe Zanzibar tu? Je iki tokea kuka tokea fujo pia hapo mtasema tuwa achie watatue mambo yao wenyewe? Tupende tusipende as long as tuna muungano matatizo ya Zanzibar ni yetu na tutakua wajinga kuignore yanayo tokea huko. Tatizo kuna watu pamoja na viongozi wanaogopa kusema ukweli nakuogopa baadhi ya Wazanzibar wata react vipi.
 
Mimi kama mimi na-support jinsi Maalim Seif na Karume walivyoamua kuzika tofauti zao kwa maslahi ya Zanzibar,ingawa watu wengi wanasema tatizo ni katiba lakini mimi napingana nao, katiba ina sema wazi kuwa: Kutakuwa na chombo kitakachosimamia mambo yote ya uchaguzi, mambo hayo ni yapi; kuandikisha wapiga kura, kuendesha, na kutangaza mshindi, katika kuendesha Tume ya uchaguzi imepewa mamlaka ya kuahirisha uchaguzi wowote ule inapoona inafaa, tulishuhudia uchaguzi ukiahirishwa kwa wiki moja kipindi fulani Zanzibar pia tumeshuhudia ukiahirishwa hapa Bara, kipindi gani uahirishwe inategemea na sababu kama kifo, majanga kama tetemeko mafuriko,vita na sababu za msingi.

Hata tume ya uchaguzi Zanzibar ilipoulizwa kuhusu kuahirisha uchaguzi watu hawakulielewa jibu lao, Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Zanzibar Salumu Kassim Masego alisema namnukuru "Mpaka sasa hatujapokea maombi yoyote yanayotaka kusogezwa mbele kwa Uchaguzi Mkuu ujao, lakini pia itambulike kuwa tunafanya kazi kwa mujibu wa Katiba inavyosema, na wala hatuwezi kuusimamisha kwa hali hiyo, ila kama ikitokea, tutafanya hivyo," wengi tulipoona kasema kwa mujibu wa katiba basi mawazoyetu yakaacha kufikiri zaidi, huo mujibu wa katiba ni upi wataangalia sababu kama zitakuwa za msingi wanaweza kuahirisha wanao uwezo kikatiba.

Kwa hiyo ndugu zangu wale mnaowasikia wakisema Karume kasema havunji katiba ni sawa lakini wengi wao wanafanya hivyo kwa maslahi yao elewa kuwa katiba huvunjwa kwa katiba, katiba hiyo hiyo imeipa nguvu Tume kuahirisha uchaguzi, hata Karume wengi hawakumwelewa aliposema hawezi kuvunja katiba kwa sababu katiba inamruhusu vipindi viwili tu hakusema hawezi kuendelea katiba itakaporuhusu.
 
Ni vigumu kusema tunawe kabisa mkono kwenye mambo ya Zanzibar kwa sababu what affects Zanzibar affects the rest of the country too. Sasa huu muungano una maana gani kama ya Zanzibar yaachiwe Zanzibar tu? Je iki tokea kuka tokea fujo pia hapo mtasema tuwa achie watatue mambo yao wenyewe? Tupende tusipende as long as tuna muungano matatizo ya Zanzibar ni yetu na tutakua wajinga kuignore yanayo tokea huko. Tatizo kuna watu pamoja na viongozi wanaogopa kusema ukweli nakuogopa baadhi ya Wazanzibar wata react vipi.


Asili yangu ni mtanganyika na magharibi lakini naona post yako imekaa kiukolonikoloni

Sasa huu muungano una maana gani kama ya Zanzibar yaachiwe Zanzibar tu?
Si ni sisi tuliokua tunasema wazanzibari wanabaguana waunguja kwa wapemba?

Sasa wameamua kuwa kitu kimoja kwanini ituhusu sisi watangayika?
Wacha waangalie kitu kinachowafaa wao wenyewe KIBAYA KIZURI.
Mbali ya haya yote Muungano sio kitu chakulazimishwa. Kama wazanzibari hawauoni umuhimu wa muungano ndio watakaoamua wenyewe.
 
Asili yangu ni mtanganyika na magharibi lakini naona post yako imekaa kiukolonikoloni

Si ni sisi tuliokua tunasema wazanzibari wanabaguana waunguja kwa wapemba?

Sasa wameamua kuwa kitu kimoja kwanini ituhusu sisi watangayika?
Wacha waangalie kitu kinachowafaa wao wenyewe KIBAYA KIZURI.
Mbali ya haya yote Muungano sio kitu chakulazimishwa. Kama wazanzibari hawauoni umuhimu wa muungano ndio watakaoamua wenyewe.

La hasha mkuu. Hauwezi ukakaa na mtu ndani ya nyumba moja kama wana familia halafu useme kinacho mtokea mwenzako haki kuhusu na umuachie mwenyewe completely. Sawa unampa uhuru wa kujiamulia lakini huwezi kuniambia hauta husika in one way or another. Zanzibar ni part ya jamhuru ya Muungano ya Tanzania kwa hiyo matatizo ya Zanzibar yana tuhusu sisi wote. Chochote kiki tokea Zanzibar kita tuaffect na sisi sasa uta semaje tuwaachie wenyewe tu?

Muungano siyo wa kulazimisha but last time I checked sisi bado ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. As long as that is the case matatizo ya Zanzibar pia ni ya Muungano. Wazanzibari kuamua kuwa kitu kimoja ni kitu cha kheri na cha kufurahisha. Kwa sababu kukiwa na amani Zanzibar basi hata bara kutakua na amani. Lini nyie cowards wa kusema ukweli mtaona kuwa as long as tupo kwenye Munngano our destinies are intertwined?
 
Kwani hao Wazanzibari tumewashika vinywa vyao mpaka mseme tunawaingilia? Yetu ni maoni tu, wao ndio wenye final say! Huko kwenye Baraza la Wawakilishi watakaa wenyewe Wazanzibari! Seif aache woga usiokuwa na maana! Woga wake ndio unaowafanya watu waulize maswali mengi zaidi, that man is too defensive! Kwani haya ni mambo ya misahafu ambayo hakuna kuuliza maswali? Na hivi Karume akifariki (hatuombei anyway) ina maana hicho "kizuri" alichokianzisha kitakufa vilevile? Na kama hicho "kizuri" kinamtegemea Karume na Seif pekee, hakitadumu, labda Seif na Karume waishi milele!
 
Unachotakiwa kufahamu Zanzibar si Maalim na Amani - hivyo wanapaswa kuweka hadharani kile walichokubaliana ili wananchi tuweze kuchambua na kutafakari kama ni kwa masilahi ya Zanzibar au ni mambo yao binafsi.
 
Kaeni hivo hivo mkao wa kutega sikio, subirini kikao kikianza hapo barazani tarehe 20.

Habari zinasema futa na mseto litajadiliwa na bunge letu tukufu liliopo Maisara.Hatusikii kitu safari hii ni futa letu na mseto wetu.JK hapati kitu 🙄

Just kidding, but seriously uchaguzi utavuruga kila kitu kwa Zanzibar.Na naona kwa mtazamo wangu hayo ya maridhiano/muafaka ni jambo zuri kumalizwa kushinda huo uchaguzi.

Nyie hamufahamu hali ikoje visiwani, kuna pande kubwa CCM walishalikata kwenye kuandikisha wazanzibari ili kujitengenezea ushindi wa kishindo.

Sasa ni bora bunge hilo la Maisara likapeleka mbele uchaguzi kuepuka mgogoro mwengine wa kisiasa ambao tayari kwa hali ilivyo ya daftari...ni wazi mgogoro mpya na visiwa vitaingia tena gizani...sio giza la umeme though 😀
 
KINACHOFUKUTA Zanzibar, kwa minong'ono kuwa yanahitajika mabadiliko kabla ya uchaguzi mkuu, kinaweza kuwa baraka kwa taifa hili kuliko balaa.

Hii ni kwa sababu, kuingia katika uchaguzi, wakati Zanzibar kunawaka moto, ni kumwaga petroli kwenye moto badala ya kutafuta juhudi za kuuzima kwanza.

Maangamizi ya aina ya 2001, ambako watu wapatao 40 walikufa, yaweza kurudiwa au kuwa makubwa zaidi.

Ni hivi: Visiwani Unguja na Pemba kunahitajika mwanzo mpya katika mambo mbalimbali ya kiutawala, kisheria na hata kiutaratibu. Haya bado hayajafanyika.

Ikibidi, siyo lazima kuongeza muda wa Rais Amani Abeid Karume wa kutawala kwa miaka mitatu; bali kipindi maalum cha “kuweka mambo sawa” kabla ya kuingia uchaguzi.

Kwa mfano, utaingiaje uchaguzi ikiwa matatizo ya msingi yaliyopo katika daftari la kudumu la wapigakura hayajapatiwa ufumbuzi?

Utaingiaje uchaguzi ikiwa sheria mbalimbali zikiwamo zile zinazotoa mamlaka kwa sheha (mtendaji wa kata) kuamuru nani aandikishwe na yupi aachwe, hazijabadilishwa?

Utaingiaje uchaguzi wakati vyombo vya dola vinavyotuhumiwa kuwa kiini cha mgogoro wa muda mrefu visiwani Zanzibar, bado vinaendelea kujiegemeza kwa chama kilichopo ikulu?

Utaingiaje uchaguzi wakati hakuna uhakika wa matakwa ya raia kuheshimiwa? Utaigiaje uchaguzi wakati Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ikiwa inabebeshwa tuhuma za kuendeshwa kama kampuni binafsi?

Jibu liko wazi; kwamba haiwezekani. Kila anayetakia mema taifa hili, hawezi kutamani kufanyika uchaguzi kabla ya kupatiwa ufumbuzi kwa matatizo yaliyopo.

Si lazima hayo yafanyike kwa kuongezea muda Karume. Muhimu ni kule kutendeka, tena kwa moyo mmoja. Kutekeleza hayo kwa njia ya kulipua, huku wahusika wakitanguliza maslahi ya vyama kuliko taifa, hakuwezi kusaidia Zanzibar. Kutaangamiza taifa hilo na Tanzania kwa jumla.

Tukifika hapo atakayelaumiwa hatakuwa Karume pekee. Hata Rais wa Jamhuri, Jakaya Kikwete na viongozi waandamizi katika serikali na CCM. Wote watanyoshewa kidole, tena kila kona, ndani na nje ya nchi.

Hata nchi wahisani na jumuiya ya kimataifa, watapiga kelele na pengine kuchukua hatua kama ikibidi. Hoja ya kutaka Karume aongozewe kipindi kingine cha urais, imeibuka mara baada ya kiongozi huyo kukutana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad.

Hata hivyo, tayari umezuka upinzani ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pande zote mbili za Muungano, zikipinga Karume kuongezewa muda zaidi ya kipindi kinachoruhusiwa kikatiba.

Ndani ya CCM na hata CUF, wanachama na viongozi wamegawanyika; hawa huku na wengine kule. Bali, kwa mtu anayepima mambo kabla ya kutenda, kuingiza Zanzibar katika uchaguzi mwingine bila ya kushunghulikia matatizo yaliyopo, ni kuhatarisha maisha ya raia.

Zogo la mgogoro visiwani Zanzibar lilianzia uchaguzi mkuu wa 1995. Vyama vyote viwili – CCM na CUF, vilitangaza kugomea matokeo ya uchaguzi na kutuhumu ZEC kuwa imeendesha uchaguzi kinyume cha sheria.

Kabla ya matokeo kitangazwa, CCM iliamini na kukubali kuwa imeshindwa lakini kwa njama. Ilipeleka malalamiko kwa ZEC. Lakini baada ya kutumika kile walichoita “teknolojia,” Tume ikatangaza kuwa mshindi ni Dk. Salmin Amour (“Komandoo”) na siyo Maalim Seif.

Tangu hapo, Zanzibar hakujawa tena shwari. Utawala wa Komandoo uliendeleza chuki na uhasama miongoni mwa jamii. Ulikebehi hata jitihada za kuleta maelewano zilizofanywa na jumuiya ya kimataifa kupitia Jumuiya ya Madola.

Si mara moja wa mbili, Salmin na wapambe wake walikebehi majadiliano na mwafaka uliofikiwa kati ya chama chake na CUF mwaka 1999. Machafuko na mauaji ya Januari 25 na 26 mwaka 2001 yaliyofuatia huko Unguja na Pemba, yana kiini katika kutotekelezwa kwa mwafaka huo.

Sasa swali la kujiuliza ni hili: Nani anataka turudi tulikotoka? Bila shaka, hakuna atakaye. Je, kama hayupo, marekebisho yanayohitajika kabla uchaguzi mwingine, yawezekana katika kipindi kilichosalia?

Yapo yanayowezekana. Lakini mengi hayawezi kufikiwa. Kwa mfano, Karume aweza kuamrisha masheha kupunguza munkari na ukereketwa kwa CCM na hivyo wananchi walionyimwa haki ya kuandikishwa wakapata haki hiyo.

Lakini hakuna dalili kwamba aweza kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kama ambavyo baadhi ya viongozi wa CCM na CUF wanavyopendekeza, ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu.

Akiiunda haitamaliza tatizo. Kunahitajika muda wa majadiliano ili kuhakikisha serikali inayoundwa inadumu na kuwa imara. Vinginevyo, inaweza kuwa kama Zimbabwe.

Ni muhimu ifahamike mapema CUF wanapewa nafasi ngapi na zipi ndani ya serikali? CCM nao wanabaki na ngapi na zipi? Je, wanaishia katika baraza la mawaziri tu au wanashuka hadi chini kwa mawaziri na wakurugenzi?

Aidha, serikali ya umoja wa kitaifa, pamoja na kuhitaji kuwepo kwa sheria, ni sera ya chama kilichopo ikulu?

Sera ya sasa ya CCM haitaji serikali ya mseto Zanzibar. Kuiunda ni lazima utumie vikao halali vya chama chenyewe. Haya hayawezi kufanyika kwa mtindo wa kufumba na kufumbua.

Mpaka sasa inadaiwa Karume hajakiambia chama chake wamezungumza nini na Maalim Seif? Hajasema kipi kilichowafanya wazungumze, wakati ni yeye na wafuasi wake waliokwenda Butiama kwa lengo la kuzika mwafaka ulioandaliwa na chama chao?

Vinginevyo Karume atende kwa njia ya kuasi CCM. Abebe suala hili kwa njia ya kupeleka muswada kwenye Baraza la Wakikilishi la Zanzibar, ambapo kwa kutumia wingi wa wajumbe wa CUF na baadhi ya wafuasi wake, waweza kulipitisha.

Lakini ni vema kwenda ndani ya chama. Huko atapata nafasi ya kueleza kwa ufasaha alichojadili na Seif. Kueleza hata idadi ya ajenda zao na zililenga maeneo gani.

Je, ni kitu gani kimesababisha kushindwa kutekeleza hayo kwa miaka minne iliyopita? Kipindi kilichosalia hakitoshi kwa ajili ya kitu gani? Kitu gani kinahitaji muda zaidi? Hii ndiyo njia ya utekelezaji.

Akifanya hivyo, hakika atafanikiwa. Atajenga heshima kwa sasa na siku zijazo. Hata wanaaompinga wataishia kujifunika nyuso. Lakini hilo litawezekana iwapo atakuwa na dhamira ya dhati ya kumaliza tatizo, si kwa kutaka hayo kwa maslahi yake binafsi.

Matatizo ya Zanzibar ni mengi. Kwanza, kuna Katiba mbili na sheria mbili tofauti zinazosimamia chaguzi. Kuna Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na sheria yake ya uchaguzi, pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano na sheria yake ya uchaguzi.

Katiba ya Zanzibar hailazimishi mtu kuwa na kitambulisho cha ukaazi. Inataja kitambulisho cha uraia. Si uraia wa Zanzibar – kwa sababu Zanzibar si Jamhuri, ni uraia wa Jamhuri ya Muungano.

Kitambulisho hiki bado hakijapatikana mpaka sasa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha kuingilia mchakato wa zabuni kinyume cha taratibu na kusababisha ucheleweshaji.

Lakini katika sheria ya uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambapo ZEC inasimamia upande wa Zanzibar, hakuna mahali panapotajwa kitambulisho cha ukaazi.

Yapo madai yanayoweza kuthibitishwa kwamba baadhi ya masheha wametumia vibaya madaraka yao. Wapo waliogomea kuandikishwa hata ndugu zao wa karibu – wakwe zao, dada zao, shangazi zao na hata maimamu wa misikiti wanaowaswalisha asubuhi, mchana na jioni. Kisa? Wanaotaka kuandikishwa siyo wanachama wa CCM.

Mambo yote haya yanahitaji muda zaidi kuyarekebisha. Kingine kinachohitaji muda zaidi ni marekebisho katika ZEC ambayo kwa sasa imepoteza hadhi mbele ya wananchi.

Vinginevyo, katika mazingira ya sasa ambapo ZEC inatuhumiwa, vyombo vya dola vinashutumiwa, watendaji serikalini wananyoshewa kidole, kuitisha uchaguzi ni kujitafutia mgogoro usiokuwa na sababu.

Kuitisha uchaguzi kabla ya kutatua matatizo yaliyopo, ni kutaka nchi iandike historia nyingine badala ya ile ya mwaka 2001 ambapo Tanzania iliyokuwa kimbilio la wakimbizi, yenyewe ilizalisha wakimbizi.

Karume hawezi kukwepa lawama kwa kufikisha Zanzibar mahali ilipo. Ni serikali yake iliyogomea mwafaka mpya na CUF, badala yake ikaja na hoja ya “kura ya maoni” katika kile kilichoitwa kutaka kuipiku CUF.

Lakini Karume anajua siasa. Ajivunie nini baada ya kipindi cha miaka 10 ya utawala wake? Amani ya Zanzibar yaweza kuwa kitu pekee cha kujivunia kwa karne na karne. Atakayeachia fursa hii itoweke aweza kujuta maisha yake yote.

Chanzo:mwanahalisi
 
MrFroat, Nakubaliana na wewe kwa hili kuwa amani ya Zanzibar ndio priority no.1, hata ikibidi uchaguzi usogezwe.

Kwa vile maridhiano ya Karume na Seif ni dhima, muda uliopo kati ya sasa na October, unatosha kuyafanya yote hayo na kufanya uchaguzi huru na wa haki.

Pia naungana na wale wote wanaoshauri mambo ya Wanzibari, waachieni wenyewe, ila hili la kuahirisha uchaguzi au kuuzogeza mbele sio lenu, hata sisi bara tukifanya uchaguzi wetu tarehe ile ile, kuanzia rais wetu, bunge letu, serikali yetu, vyote vitakosa uhalali 'legitimacy' bila kura ya Mzanzibari.

Kama Baraza litakapokuta na kupitisha kwa kauli moja kusogeza mbele uchaguzi, Bara italazimisha uchaguzi wa rais na wabunge wa Bunge la Muungano uendelee, jee unajua kitakachotokea ni nini?.

Hivi nyinyi Wazanzibari hamjifunzi tuu na kilichomkuta Jumbe alipotaka kuikomboa Zanzibar toka mkoloni Tanzania?. Hamjifunzi tuu Salmini alipotaka badili katiba kuongeza kipindi cha urais, sasa hizi kelele za kutaka kusogeza uchaguzi, zitawatokea puani.

Dawa ya kuimarisha Muungano wetu, ni kufanya serikali moja, Zanzibar na Pemba itageuka mikoa, kelele na chokochoko zote kuhusu muungano zitaisha, si mnaona kisiwa cha Mafia kilivyotulia?. Nacho kilikuwa himaya ya Sultani na sehemu ya Zanzibar, pamoja na Kilwa, Lamu mpaka Mombasa enzi hizo.
 
Ni kweli kabisa MrFroasty...Amani ya Zanzibar ni muhimu...co lazima mambo yewekwe sawa kwanza kabla ya kuingia kwenye uchaguzi..once hii amani ikipote itawagharimu sana Wazanzibar..
 
1. Mara baada ya mwafaka kati ya Karume na Seif kumekuwa na kauli mbali mbali zinazojichanganya kuhusu Karume kugombea tena au kuongezewa muda ili "alee" makubaliano yake na Seif! Hilo ni jambo jema sana kwa mustakabali wa visiwa hivyo. Hata hivyo kumekuwa na kauli zinazotaka kuwa mambo ya Zanzibar yasiingiliwe, waachiwe wenyewe, watayamaliza.
2. Mimi kwa upande wangu niko tofauti na kauli hizo. Kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 inavyosema na kwa kuwa suala la Ulinzi na Usalama ni la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ipo haja ya kujua na kutoa maoni kwa kile kinachoendelea huko, si kwa kuwalazimisha wafanye tunayotaka bali kutoa maoni kama wafanyavyo observers wengine kwenye masuala mbalimbali! Mbona Jumuiya ya Kimataifa na hata JK mwenyewe alitoa pongezi kwa mwafaka wa Seif na Karume? Hizo pongezi sio maoni kwamba mlichokifanya ni kizuri? Mbona hatukusikia malalamiko kwamba tunaingiliwa?
3. Hakuna anayependa Wazanzibari wauane au kuchukiana. Ndio maana Wazanzibari wengi wanaishi Tanzania Bara na hakuna anayewabughudhi wala kuwachukia! Wazanzibari wengine wameajiriwa kwenye Taasisi ambazo si za Muungano na wanaishi vizuri na Wabara. Sijazungumzia wale ambao wameoana na Wabara na hakuna unyanyapaa wowote!
4. Sasa hizi kauli za akina Seif anapodai kuwa "kajitu toka Bara" (akimaanisha Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba) kuhoji mambo ya Zanzibar hazionyeshi nia njema na zinawafanya watu kuanza kuhoji kulikoni! Kwani hakuna lugha ya kistaarabu ya kutamka, hata kama kweli Wazanzibari wameingiliwa? Hizi ni kauli za "kusahau yaliyopita na kujenga mapya" kweli? Hapa watu wataendelea kuhoji maana Seif mwenyewe ndiye anayejenga mazingira hayo ya "kutaka kuhojiwa!" Otherwise, mimi naona kuwa maamuzi ya kuwa na uchaguzi au la wanayo Wazanzibari wenyewe hata kama watu hawatapenda, ila wasikilize maoni ya watu wengine, ndio maana ya demokrasia, si kutoa kauli za chuki, hakutajenga, kutabomoa!
 
bunge letu, serikali yetu, vyote vitakosa uhalali 'legitimacy' bila kura ya Mzanzibari.

Kwani hivyo vijikura viwili kutoka Zanzibar vinaweza kubadili matokeo JK asishinde?

Hivi nyinyi Wazanzibari hamjifunzi tuu na kilichomkuta Jumbe alipotaka kuikomboa Zanzibar toka mkoloni Tanzania?. Hamjifunzi tuu Salmini alipotaka badili katiba kuongeza kipindi cha urais, sasa hizi kelele za kutaka kusogeza uchaguzi, zitawatokea puani.
Subiri kesho tarehe 20, sikiza mambo ya bunge la Zanzibar.Hizo hoja za mseto pamoja na futa zitajadiliwa upya.Kama bado una mawazo mgando ya kutishana, bai naona kama uanze kukaa mkao mpya wa kutega sikio.

Jumbe na Salmin hawa watu wote hawakuwa na support ya wazanzibar.Hii issue ya Karume kuongezwa muda inahitaji 2/3 ya BLW.


Dawa ya kuimarisha Muungano wetu, ni kufanya serikali moja, Zanzibar na Pemba itageuka mikoa, kelele na chokochoko zote kuhusu muungano zitaisha, si mnaona kisiwa cha Mafia kilivyotulia?. Nacho kilikuwa himaya ya Sultani na sehemu ya Zanzibar, pamoja na Kilwa, Lamu mpaka Mombasa enzi hizo.

Sasa ndugu yangu unajua kama Zanzibar ni taifa kongwe zaidi ya hiyo Tanganyika?Maana unafananisha Mafia na Zanzibar, uko makini lakini?
Hilo la serekali moja lilimshinda huyo Nyerere ambae alikuwa anamkaribia Adolf Hiltler kwa ukatili na udikteta.Jee ataweza JK?Kwanza hebu naanze na kufukuza kazi hao wahusika na mafisadi, halafu ndio tutaweza kusema muna rais mwenye msimamo.

Mie personally, taifa langu likipotea na kufanywa mkoa basi niko tayari kujifunga bomu na kujiripua sehemu yoyote ya Dar 😀
 
Mambo ya Zanzibar hatuwezi kuwaachie tu wenyewe as if Zanzibar siyo sehemu ya Muungano. Wanaongea tu sasa hivi lakini ngoja kutokee tatizo huko tuone kama SMT haitaombwa msaada. Tatizo kuna baadhi ya watu ni wanafiki na wanaogopa kusema ukweli. Bottom line is as long as Zanzibar ni part ya muungano hakuwezi kikaendelea chochote kule tukasema tuwaachie tu wenyewe. Kinacho tokea Bara kina affect Zanzibar na kinacho tokea Zanzibar kina affect muungano. Be honest people.
 
Back
Top Bottom