Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Binafsi huwa nawashangaa sana wabara wenzangu. Kuna ugumu gani kuwaachia wazanzibari wajiamulie mambo yao? Wenyewe wameamua kupatana baada ya kuona ugomvi wao hauwasaidii chochote zaidi ya kuendelea 'kupokea instructions' kutoka 'Dar es Salaam'!
 
Aya = paragraphs?

Mara baada ya mwafaka kati ya Karume na Seif kumekuwa na kauli mbali mbali zinazojichanganya kuhusu Karume kugombea tena au kuongezewa muda ili "alee" makubaliano yake na Seif! Hilo ni jambo jema sana kwa mustakabali wa visiwa hivyo.

Hata hivyo kumekuwa na kauli zinazotaka kuwa mambo ya Zanzibar yasiingiliwe, waachiwe wenyewe, watayamaliza. Mimi kwa upande wangu niko tofauti na kauli hizo.

Kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 inavyosema na kwa kuwa suala la Ulinzi na Usalama ni la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ipo haja ya kujua na kutoa maoni kwa kile kinachoendelea huko, si kwa kuwalazimisha wafanye tunayotaka bali kutoa maoni kama wafanyavyo observers wengine kwenye masuala mbalimbali! Mbona Jumuiya ya Kimataifa na hata JK mwenyewe alitoa pongezi kwa mwafaka wa Seif na Karume? Hizo pongezi sio maoni kwamba mlichokifanya ni kizuri? Mbona hatukusikia malalamiko kwamba tunaingiliwa?

Hakuna anayependa Wazanzibari wauane au kuchukiana. Ndio maana Wazanzibari wengi wanaishi Tanzania Bara na hakuna anayewabughudhi wala kuwachukia! Wazanzibari wengine wameajiriwa kwenye Taasisi ambazo si za Muungano na wanaishi vizuri na Wabara. Sijazungumzia wale ambao wameoana na Wabara na hakuna unyanyapaa wowote!

Sasa hizi kauli za akina Seif anapodai kuwa "kajitu toka Bara" (akimaanisha Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba) kuhoji mambo ya Zanzibar hazionyeshi nia njema na zinawafanya watu kuanza kuhoji kulikoni!

Kwani hakuna lugha ya kistaarabu ya kutamka, hata kama kweli Wazanzibari wameingiliwa? Hizi ni kauli za "kusahau yaliyopita na kujenga mapya" kweli? Hapa watu wataendelea kuhoji maana Seif mwenyewe ndiye anayejenga mazingira hayo ya "kutaka kuhojiwa!"

Otherwise, mimi naona kuwa maamuzi ya kuwa na uchaguzi au la wanayo Wazanzibari wenyewe hata kama watu hawatapenda, ila wasikilize maoni ya watu wengine, ndio maana ya demokrasia, si kutoa kauli za chuki, hakutajenga, kutabomoa!
 
Binafsi huwa nawashangaa sana wabara wenzangu. Kuna ugumu gani kuwaachia wazanzibari wajiamulie mambo yao? Wenyewe wameamua kupatana baada ya kuona ugomvi wao hauwasaidii chochote zaidi ya kuendelea 'kupokea instructions' kutoka 'Dar es Salaam'!

Acha ugumu wa kuelewa! Kesho wazenj wakikaa kwenye Baraza la Wawakilishi na kuamua kumwongezea Karume aongoze mpaka atakapokufa kuna mtu atawakataza? Mbona wazenj wanapoajiriwa katika Taasisi ambazo si za Muungano hatusemi kuwa wanaingilia mambo ya Bara? Mtu toka Bara akipiga chafya tu eti "unaingilia mambo ya Wazanzibari!"
 
MrFroat, Nakubaliana na wewe kwa hili kuwa amani ya Zanzibar ndio priority no.1, hata ikibidi uchaguzi usogezwe.

Kwa vile maridhiano ya Karume na Seif ni dhima, muda uliopo kati ya sasa na October, unatosha kuyafanya yote hayo na kufanya uchaguzi huru na wa haki.

Pia naungana na wale wote wanaoshauri mambo ya Wanzibari, waachieni wenyewe, ila hili la kuahirisha uchaguzi au kuuzogeza mbele sio lenu, hata sisi bara tukifanya uchaguzi wetu tarehe ile ile, kuanzia rais wetu, bunge letu, serikali yetu, vyote vitakosa uhalali 'legitimacy' bila kura ya Mzanzibari.

Kama Baraza litakapokuta na kupitisha kwa kauli moja kusogeza mbele uchaguzi, Bara italazimisha uchaguzi wa rais na wabunge wa Bunge la Muungano uendelee, jee unajua kitakachotokea ni nini?.

Hivi nyinyi Wazanzibari hamjifunzi tuu na kilichomkuta Jumbe alipotaka kuikomboa Zanzibar toka mkoloni Tanzania?. Hamjifunzi tuu Salmini alipotaka badili katiba kuongeza kipindi cha urais, sasa hizi kelele za kutaka kusogeza uchaguzi, zitawatokea puani.

Dawa ya kuimarisha Muungano wetu, ni kufanya serikali moja, Zanzibar na Pemba itageuka mikoa, kelele na chokochoko zote kuhusu muungano zitaisha, si mnaona kisiwa cha Mafia kilivyotulia?. Nacho kilikuwa himaya ya Sultani na sehemu ya Zanzibar, pamoja na Kilwa, Lamu mpaka Mombasa enzi hizo.
sasa mkuu,
unakubaliana pia ni vyema karume akaendelea ''kula kuku'' mpaka biashara ya amani zanzibar itakapokwisha?i mean kwasababu yeye na maalim wameshaanzisha huu mchakato wa amani zanzibar SASA ILI KU-MAINTAIN UNIFORMITY ya hii kitu na pengine kuokoa muda ni bora karume akaendelea ''kula bata''?
 
halafu wahishimiwa,
haya maswala ya zanzibar haya.......
HIVI JUNIUS YUPO WAPI?
...au amebadili aidii?😀
 
Acha ugumu wa kuelewa! Kesho wazenj wakikaa kwenye Baraza la Wawakilishi na kuamua kumwongezea Karume aongoze mpaka atakapokufa kuna mtu atawakataza? Mbona wazenj wanapoajiriwa katika Taasisi ambazo si za Muungano hatusemi kuwa wanaingilia mambo ya Bara? Mtu toka Bara akipiga chafya tu eti "unaingilia mambo ya Wazanzibari!"

Hapo kwenye bluu nenda pole pole! Kwenye nyekundu umenisikitisha kidogo. Kama dhana yako ya 'kuingilia mambo' ndio hiyo basi huu mjadala hauna maana.
 
Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ni batili au sahihi? Hiyo habari ya Yesu hapa si mahali pake, kama unataka tufungue thread kwenye Jukwa la Dini ili tuhabarishane! Ukianza kuruka hoja na kulazimisha mambo na pia kuleta yasiyohusika (Yesu Kristo) hutaeleweka ndugu!
Kama na wewe utaweza kujibu errors zote katika mfumo wa muungano basi tutakuwa even.

Obviously, huu muungano una makosa mengi na unahitajika ufanyiwe ukarabati.Sasa hizo katiba ndio matatizo yenyewe, kama ingelikuwa katiba ziko sawa mbona saa hizi pangekuwa hapakaliki.

Kwa hiyo katiba ya Zanzibar ambayo mpini umeshikwa na Bunge la Zanzibar, ina uwezo wa kufanya maamuzi haya yote ya kumpatia muda wa ziada Karume na kutengeneza serekali ya mseto.

Wala hakuna mtu ndani ya TZ atakayeweza kufanya chochote.Soma habari hii ya Citizen utaona kama hiyo agenda tayari iko barazani na itajadiliwa kesho...na hao wawakilishi wa CCM washaikubali kabla ya hata hilo baraza kujadili maada.

http://thecitizen.co.tz/newe.php?id=16958

Sasa kwa ufupi haya masuala yana umuhimu kwa Zanzibar, na yoyote mwenye kuitakia mema ataungana na wazanzibari kuimarisha amani na SIO KULETA UCHAGUZI KABLA HATA WATU HAWAJAJIPANGA VIZURI!!!

Kwanza acha watu wajipange vizuri kwenye hiyo miaka 2, then tutafanya uchaguzi tukiwa tayari tumejipanga vizuri na kuweka mazingira ya watu kukubali na kuiamini hiyo tume.

Sasa kaka zangu na dada zangu kutoka Tanganyika kaeni kando na acheni kutoa comments na critics kwa kulazimisha lazima tuende kwenye uchaguzi ili mupate nafasi ya kumueka kibaraka mwengine.Hiyo nafasi haipo safari hii, maana mukipewa nafasi ya kueka kibaraka na futa letu limeenda harijojo.

Ndio nikasema mutakula harufu tuu, tutakula mseto na futa letu huko huko jikoni huko kwenu itakuja harufu tuu...kama mulivyofanya kwenye madini na vitu vyengine.

Cheers
 
Al Qaeda, Taleban au Al..?
Utakavyopenda wewe, lakini nchi itakuwa haikaliki.Sasa hivi tunaacha kwanza hiyo SMZ, lakini ikifutwa tuu hiyo kazi itakuja mikononi mwetu wananchi.

Na vita ya wananchi unaijua, nishakueleza msimamo wangu juu ya hili suala la ugaidi kuwa mimi siuiti ugaidi.Naona ni sawa na vita yoyote ile, kwa hiyo kwangu hakuna kitu kinaitwa ugaidi.

Hakutokuwa na tofauti yoyote kuadapt idea za Osama kwa kupigania Zanzibar ikiwa SMZ itafutwa.Hilo liko wazi wala halina mjadala....sasa kazi ni kwenu kama mutapendelea kuzorotesha watu milioni 40, kwa ajili ya kijinchi kidogo kama Zanzibar.

Huo ndio msimamo wangu binafsi, na naamini wako wengi sana watakaunga mkono mawazo haya.

Kwa kumalizia mjadala wa serekali moja haupo wala hautakuwepo kwenye vichwa vya wazanzibari.Munataka mututie umasikini kama mikoa yenu ya Tabora sio?

Turudi kwenye maada, amani ya Zanzibar ni muhimu au tufanye haraka ya uchaguzi?
 
Akili za watu wa visiwani.......! zantia kichefuchefu mie na mafuta yao ya kusadikika na miafaka isoisha ya kila siku.Hivi ni ya kweli hayo ya maalim seif kwa mustakabari wa wazanzibar?time will tell!
 
Shida yangu, hivi ni kitu gani walikubaliana baina ya Seif na Karume? kwani inawezekana kabisa kuwa watu tunaimba wimbo kwa nia njema ila wenzetu hawa walikubaliana tofauti na tunavyofikiria.

Kama tukiruhusu katiba kuchezewa kwa kutokukubali kuweka misingi imara ya kufanyika kwa chaguzi za haki na huru, kuna siku nchi hii itaingizwa kwenye matatizo kwa ajili ya manufaa ya mtu ama kikundi binafsi .

Hapa la muhimu ni kuweka mazingira ya kila mmoja kuingia kwenye uchaguzi ambao unafanyika kwenye uwanja sawa, na sio kuongeza muda wakati hatujui Karume anaenda kufanya nini.

Je?Baraza la wawakilishi litaongezewa muda?
Je?uchaguzi wa wabunge wa upande wa Zanzibar utafanyika? kama utafanyika utafanywa katika mazingira gani?
 
Kama na wewe utaweza kujibu errors zote katika mfumo wa muungano basi tutakuwa even.

Obviously, huu muungano una makosa mengi na unahitajika ufanyiwe ukarabati.

Sasa kaka zangu na dada zangu kutoka Tanganyika kaeni kando na acheni kutoa comments na critics kwa kulazimisha lazima tuende kwenye uchaguzi ili mupate nafasi ya kumueka kibaraka mwengine.Hiyo nafasi haipo safari hii, maana mukipewa nafasi ya kueka kibaraka na futa letu limeenda harijojo.

Ndio nikasema mutakula harufu tuu, tutakula mseto na futa letu huko huko jikoni huko kwenu itakuja harufu tuu...kama mulivyofanya kwenye madini na vitu vyengine.

Sasa naona tumeshaanza kuwa pamoja: Kwamba Muungano upo lakini una kasoro, suala sasa ni kurekebisha. Mwanzoni ulidai Muungano ni batili huku ukijua kwamba Rais wa Zanzibar anapoapa hutaja kwamba "Zanzibar ni Sehemu ya Jamhuri ya Muungano" na ndivyo ilivyo Katiba ya Zanzibar, 1984, Ibara ya 1! Na hayo mafuta unayodai mtayala yako sehemu gani? Na kama yapo na mkifanikiwa ninyi sisi tuchukie, kama unavyodai, kwa sababu gani? Attitude za chuki, kama unazotoa hazijengi ndugu MrFroasty, zinabomoa! Change your attitude, a simple advice!
 
Hapo kwenye bluu nenda pole pole! Kwenye nyekundu umenisikitisha kidogo. Kama dhana yako ya 'kuingilia mambo' ndio hiyo basi huu mjadala hauna maana.

Kwenye red ukipiga picha pana utakuta niko sahihi kuhusu suala la kuingilia jambo la mahali pengine! Kwenye bluu nimekusoma!
 
Binafsi huwa nawashangaa sana wabara wenzangu. Kuna ugumu gani kuwaachia wazanzibari wajiamulie mambo yao? Wenyewe wameamua kupatana baada ya kuona ugomvi wao hauwasaidii chochote zaidi ya kuendelea 'kupokea instructions' kutoka 'Dar es Salaam'!

So far hakuna aliyewazuia, JK kisha wapongeza na wengine wako kimya. Kinachoendelea JF ni mawazo binafsi may be tusubiri tuone kama CCM wataweza kuicheza hii ngoma safari hii!!
 
Sasa naona tumeshaanza kuwa pamoja: Kwamba Muungano upo lakini una kasoro, suala sasa ni kurekebisha. Mwanzoni ulidai Muungano ni batili huku ukijua kwamba Rais wa Zanzibar anapoapa hutaja kwamba "Zanzibar ni Sehemu ya Jamhuri ya Muungano" na ndivyo ilivyo Katiba ya Zanzibar, 1984, Ibara ya 1! Na hayo mafuta unayodai mtayala yako sehemu gani? Na kama yapo na mkifanikiwa ninyi sisi tuchukie, kama unavyodai, kwa sababu gani? Attitude za chuki, kama unazotoa hazijengi ndugu MrFroasty, zinabomoa! Change your attitude, a simple advice!

Hakuna attitude huo ndio ukweli kuwa Tanganyika chini ya CCM inapenda kuzorotesha kila chenye kheri na Zanzibar.

JK badala ya kuweka mjadala wa kero za muungano ndani ya bunge ametuletea Pinda ambae anaendelea kutonyesha vidonda vya wazanzibari.

Sasa sisi tuseme nini?Ubabe mupunguze, mtanganyika hata akitoa mfano wa muungano basi atasema ni sawa na ndoa...na Zanzibar itakuwa ndio jike...mnajifanya wajuaji sana, lakini safari hii sio siri...MSHIKAMANO hadi jua linatoka!
 
Je?Baraza la wawakilishi litaongezewa muda?
Je?uchaguzi wa wabunge wa upande wa Zanzibar utafanyika? kama utafanyika utafanywa katika mazingira gani?
Kwa mtazamo wangu uchaguzi wa JK hauna tatizo lolote, na wala sio unaoleta vugu vugu huko visiwani.Hivyo huo unaweza kuendelea bila ya matatizo, kwani hauhitaji hata ZANID hata Mmasai alie Zanzibar anaruhusa ya kuchagua rais wa TZ.

Kishindo ni uchaguzi wa ZEC huu ndio mtihani.Lakini tusiandikie mate kesho tuu baraza inarudi uwanjani Maisara.
 
Hakuna attitude huo ndio ukweli kuwa Tanganyika chini ya CCM inapenda kuzorotesha kila chenye kheri na Zanzibar.

JK badala ya kuweka mjadala wa kero za muungano ndani ya bunge ametuletea Pinda ambae anaendelea kutonyesha vidonda vya wazanzibari.

Sasa sisi tuseme nini?Ubabe mupunguze, mtanganyika hata akitoa mfano wa muungano basi atasema ni sawa na ndoa...na Zanzibar itakuwa ndio jike

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo waliomkwamisha JK asiweze kutatua suala la Zanzibar ni Wazanzibari wenyewe! Sisemi kwamba JK angeachiwa peke yake angeweza, lakini sio vema kumbebesha lawama peke yake wakati players walikuwa wengi, wakiwemo Wazanzibari wanyewe! Na huko kuufananisha Muungano na ndoa, kama kupo, (na of course inaonekana kupo kwa kuwa wewe umesema) haimaanishi ni kwa nia mbaya kama wewe ulivyoonesha. It is just your inferiority complex! Unakumbuka mlipogombana hata na ZeComedy ambao ni waigizaji kwa kuwa eti wanasema "tunabonyeza kizenj?" Hadi ZeComedy waliacha kutumia usemi huo wasije wakazua yasiyozulika! Sasa kama sio inferiority complex ni nini?
 
Huja nielewa kaka/dada. Namaanisha hivi. Sasa hivi kuna baadhi ya watu wanasema "Zanzibar isiingiliwe". Sasa kuki tokea tatizo kule nani ataombwa msaada? Maana hauwezi kusema mtu "asikuingilie" lakini kukusaidia iwe wajibu am I right? Mtoto hawezi kudai mzazi asiingilie maisha yake lakini the same time ategemee mzazi huyo huyo awajibike pindi chochote kitakapo mkuta(nime tumia msemo huu kujaribu kueleweka zaidi). As it stands ni wajibu wa SMT kwa Zanzibar lakini si ndiyo huo wajibu sasa hivi wanadai unaingilia Zanzibar? I hope nimeeleweka.
Unaeleweka sana Ndugu yangu. SMT kinarani ni JK. Katika hotuba zao mbali mbali wote Karume na Maalim wamemshukuru JK kwa kuonesha kuwaunga mkono na wamemuomba (Kiheshima-lakini ni wajibu wake) msaada wake wa dhati katika kufanikisha dhamira zao. Wanaoingilia ni watu kama Msekwa na Makamba (watu wa CCM Bara hao) ni kweli unaweza kusema hayawahusu hao kwani CCM ina watu wenye nafasi kama za kwao kwa ajili ya kuhudumia wanaCCM Zanzibar (Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar -Karume, Na Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Zanzibar, Feruzi)
 
Back
Top Bottom