hahaha ni kweli zile sory za viatu hazikuwa imala kabisa ..sijui hao jamani waliendelea kupigaje gwaride
 
Wazanzibari hawatosheki licha ya kwamba Wabara have bent backwards ili kuwaridhisha. Unguja na Pemba hata hawanaukubwa kama mkoa mmoja wa Tanzania Bara.

Pendekezo langu ni kwamba Muungano uvunjwe au Katiba ibadilishwe ili tuwe na Serikali moja itakayotambua Unguja kama mkoa na Pemba kama mkoa.

Kupokezana kwa zamu u-Rais kama Mhe. Khatib anavyopendekeza ni kichekesho. Labda kila Mkoa Tanzania upewe zamu ya kutoa Rais. Zanzibar wameshapata zamu yao. Wangoje mpaka Rais wa 24!

Kilasara
 
nakubALIANA NA UNACHOSEMA
 
Nimevutiwa na Gwaride linaloendelea hapo uwanjani hivi sasa pongezi kwa majeshi ya Tanzania ni wakakamavu ,Gwaride zuri wamependeza sana,kweli mnastahiri pongezi ,hivi nasikia sikia huu muungano hauhitajiki tena?

Unaongelea kupendeza gani dada mi nimeona taswira mbalimbali mbona ilikua aibu...!





Hawa nao kila mtu anaangalia kwake..??



Ona wenzetu.......
 
WAKATI Watanzania wanaadhimisha ya miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, imeelezwa kuwa kuna hali ya kutoaminiana kati ya viongozi wa serikali za pande mbili. Aidha, imeelezwa kuwa wakati umefika sasa wa kuandikwa kwa katiba mpya na mkataba mpya wa Muungano kwa kuwa ndiyo msingi wa matatizo. Mbunge wa kuteuliwa, Ismail Jussa Ladhu alisema hayo katika mahojiano maalum na Mwananchi mjini Dodoma wakati alipoungana na wabunge wengine kueleza kuwa Muungano huo mkongwe una mafanikio ya kuigwa barani Afrika, lakini wakasema una kasoro ambazo ni lazima ziondolewe ili uwe imara zaidi. “Katika miaka 46 ya uhai wa Muungano huu, kuna hali ya kutoamiana kati ya viongozi wa serikali za pande mbili,” alisema Jussa. Alisema hali hiyo inadhihirishwa na mivutano baina ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Muungano, mivutano ambayo alisema imedumu kwa wakati wote tangu nchi hizo zilipoungana Aprili 26 mwaka1964 wakati rais wa serikali ya awamu ya kwanza, Julius Nyerere na rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume. Alisema ingawa wapo viongozi wachache wa SMZ waliomaliza muda wao bila kukwaruzana, upo ushahidi wa wazi wa kukwaruzana na kutoaminiana na kutaka kurekebishwa kwa hali hiyo. Alisema hayo yalisababishwa na tofauti ya mitazamo ya uendeshaji Muungano baina ya viongozi hao. “... ni wachache walioongoza Zanzibar bila kukwaruzana na Serikali ya Muungano. Upo ushahidi wa wazi wa mivutano na kukwaruzana... hata (rais wa pili wa Zanzibar) Aboud Jumbe, katika kitabu chake kuhusu Muungano, ameonyesha kuwa Nyerere na Karume walikwaruzana na hawakuzungumza katika mwaka wa mwisho wa uhai wa Karume,” alisema Jussa. Alibainisha kuwa katika kitabu hicho Jumbe, ambaye pia aliwahi kuwa makamu wa rais, ameonyesha kuwa kwa muda huo wa mkwaruzano Karume na Nyerere walizungumza kupitia yeye (Jumbe) na marehemu Bhoke Munanka. Alisema anachokiona yeye ni kuwa Muungano huo ulikuwa wa kisiasa zaidi na haukuwa na msingi mzuri wa katiba na sheria, jambo alilosema ndiyo msingi wa matatizo yake. “Muungano ulikuwa wa kushtukiza, ni wa kisiasa, hauna msingi mzuri wa katiba na sheria. Wakati umefika sasa ‘kufanyike solution’ (suluhisho) kwa kuandikwa kwa katiba mpya na mkataba mpya wa Muungano,” Jussa alisema. Katika hatua nyingine, Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amesema kuwa kuvunja Muungano si njia ya kutatua kero zinazoukabili, bali ni kusababisha matatizo. Akizungumza na waandishi wa habari juzi wakati wa hafla ya miaka 46 ya Muungano Ikulu jijini Dar es Salaam, Nahodha alisema kutokana na kutambua kuwepo matatizo ndani ya Muungano, pande zinazohusika ziliamua kuunda kamati inayoshughulikia masuala hayo peke yake. Alisema kamati hiyo yenye wajumbe kutoka Tanzania Bara na Visiwani tayari imetatua kero ya kwanza iliyokuwa ni kutozwa ushuru wa kusafirisha mizigo kwa wananchi wa Zanzibara na imemalizia na kero ya ukusanyaji wa kodi ya mapato ya kibiashara pande hizo za muungano. “Kuvunja muungano si njia ya kutatua matatizo, bali njia sahihi ni kukaa pamoja na kuangalia chanzo cha matatizo ili kuweza kulipatia ufumbuzi. Jambo hili litatuongoza kwenye makubaliano yetu, lakini watu mkianza kugombana mnaweza kufikishana pabaya wakati ni ndugu,” alisema Nahodha. http://www.mwananchi.co.tz/habari/4...iongozi-smz-muungano-hawaaminiani-asema-jussa
 
SIKU moja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mohammed Seif Khatib kupendekeza mrithi wa Rais Jakaya Kikwete atoke Zanzibar, wanasiasa wamemjibu kuwa fursa ya Mzanzibari kuongoza Serikali ya Muungano kwa sasa haipo baada ya Dk Salim Ahmed Salim kukumbana na vikwazo mwaka 2005. Juzi Waziri Khatib, ambaye amekuwa akitajwa kuwemo kwenye kinyang'anyiro cha urais wa Zanzibar, alipendekeza kuanzishwa kwa utaratibu wa kupokezana urais kwa zamu baina ya Wazanzibari na Wabara ili kuimarisha Muungano, ambao juzi ulitimiza miaka 46 tangu ulipoasisiwa. Hadi sasa Ali Hassan Mwinyi ndiye Mzanzibari pekee aliyewahi kuongoza Serikali ya Muungano baada ya kuongoza serikali ya awamu ya pili kuanzia mwaka 1985 hadi 1995, lakini wanasiasa wanaona kuwa wazo la Khatib halifai. Juma Dun Haji, mwanasiasa machachari visiwani na ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na rais, alipingana na kauli ya Khatibu akidiriki kuiita kuwa ya kinafiki, akimtuhumu waziri huyo kuwa alikuwa miongoni mwa watu waliofanya propaganda chafu dhidi ya Dk Salim alipogombea urais mwaka 2005. “... ni unafiki; 2005 ilikuwa fursa na nafasi ya Mzanzibari kuongoza Tanzania, lakini Seif Khatib na kundi lake wakamtuma bibi mmoja wa Kikwajuni, Zanzibar ambaye alililewa katika familia ya Dk Salim aende kusema Dk Salim ni mmanga, Hizbu,” alidai Duni. “Kauli hii ilimfanya Dk Salim karibu kuzimia katika mkutano mkuu wa CCM Chimwaga. Leo miaka minne baadaye Seif anataka aonekane mwema kwa Wazanzibari; haiwezekani, ni mnafiki tu,” alidai Duni. Alidai kuwa hata Mzee Nassor Moyo aliwaeleza kuwa wamefanya jambo baya sana kwa Wazanzibari kwa kuvunja utaratibu aliouweka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wa kupokezana urais. “Nafasi ya wazanzibari kuongoza Tanzania ilikuwa mwaka 2005... sasa tunaitaka haipo tena, Seif aache unafiki,” alisema Duni. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema fursa ya Wazanzibari kwa nafasi ya urais wa Muungano kwa sasa haipo kwa kuwa hamna mwanasiasa ambaye anaweza kutoa changamoto hiyo, ndani ya CCM. “Kwa chaguzi zijazo na mwelekeo unavyoonyesha ndani ya CCM, fursa ya Wazanzibari kuongoza urais wa Muungano haipo. Ni vigumu sana kwa Mzanzibari kuwa rais wa Muungano,” alisema Profesa Lipumba. “Fursa pekee ya Wazanzibari kuongoza urais wa muungano ilikuwa mwaka 2005, baada ya Rais Benjamin Mkapa ambapo mzanzibari pekee ndani ya CCM mwenye kila sifa ya kuongoza Tanzania anayekubalika kitaifa na kimataifa alikuwa Dk Salim Ahmed Salim, lakini alitengenezewa fitna na kuangushwa,” aliongeza Lipumba. Alisema hoja ya Waziri Khatib ni ya msingi, lakini imeegemea zaidi katika mgogoro wa kikatiba na sehemu ya kero ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964. “Kama Waziri Khatibu anajiamini kisawasawa basi hoja hiyo inapaswa kutolewa katika vikao halali vya chama chake na sio kuitoa katika vyombo vya habari,” alisema Profesa Lipumba. “Hoja hii imegemea zaidi katika mgogoro wa kikatiba na kero ya Muungano, kwa hiyo CCM wenyewe ambao ndio wapo madarakani kwa sasa ndio wanajua namna ya kulishughulikia,” aliongeza Lipumba, ambaye ameshagombea urais mara tatu. Hata hivyo, alisema ni vigumu kutekelezeka kwa Tanzania kwa kuwa inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa na rais wake anapatikana kupitia kura anazopigiwa moja kwa moja na wananchi. “Maana ingekuwa rais hana mamlaka makubwa (ceremonial), ambaye anapatikana kwa kupigiwa kura na wabunge, basi ingekuwa rahisi lakini kwa mfumo huu tunaofuata sisi utaratibu huo hautekelezeki,” alisema Profesa Lipumba. http://www.mwananchi.co.tz/habari/4...4-kauli-ya-waziri-khatib-yawakera-wazanzibari
 

Maoni ya katuni.



Kinachofurahisha ni kwamba Watanzania wengi hawaongelei kuhusu kuvunja Muungano na kama wapo basi wanayasema hayo kichini chini, isipokuwa kinacholalamikiwa na wengi ni kero katika Muungano huo unaotumiza miaka 46 leo. Ni kero, kero kila siku kero.
Kwamba muungano wetu huu wa damu, licha ya kuwa wa aina yake duniani, unatoa fursa kibao zenye manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili ni ukweli usiokuwa na pingamizi. Pengine ndio maana tunadhani kwamba mwenye mawazo ya kutaka uvunjike ana matatizo kichwani ama ana lake jambo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, wasomi na wanasiasa wa hapa nchini na wenzao kutoka nchini jirani zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, walikutana jijini Dar es Salaam, nao wakaishauri Tanzania kutatua kwanza kero zilizoko katika Muungano kabla ya kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC) miaka miwili ijayo.
Baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakitajwa kuwa na kero ni pamoja na uendeshaji wa nchi, masuala ya kodi na biashara pamoja na rasilimali kama vile za mafuta na gesi. Yamekuwepo pia malalamiko kuhusu ukiukwaji ama uongezwaji wa mambo ya Muungano bila wananchi kushirikishwa, na pia Wazanzibari wamekuwa wakilalamika kwamba hawanufaiki sana na Muungano kama wenzao wa Bara. Suala la Rais wa Zanzibari kuwa waziri katika baraza la mawaziri, nalo limekuwa likitajwa kama kitu kinachowachefua Wazanzibari wakiona kama linampunguzia hadhi raisa huyo. Haya yote ni mambo yanayoweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.
Licha ya kuwepo kwa wizara maalum inayoshughulikia masuala ya Muungano iliyo chini ya ofisi ya Makamu wa Rais, kinachoonekana ni kwamba kero hizi zimeendelea kuwepo. Ni vigumu pia mtu leo hii kusimama akaona waziwazi namna wizara hii ilivyotatua kero za Muungano kwa muda wa takriban miaka mitano toka Rais Jakaya Kikwete aiunde.
Lakini, kwa mujibu wa wasomi na wanasiasa waliokutana mwishoni mwa wiki, msingi wa kero hizi uko kwenye sheria za nchi yetu, hususan sheria mama, yaani Katiba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Utafiti wa masuala ya siasa kutoka Uganda, Agustine Ruzindana, alitoa taarifa ya utafiti wao ikionyesha kwamba matatizo ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar yanatokana na baadhi ya vipengele vya Katiba kushindwa kueleweka kwa pande hizi mbili za muungano.
Alisema ili kumaliza dosari hizo ni lazima katiba ya nchi ifanyiwe marekebisho ili pande zote za Muungano ziweze kuamini kwamba zinanufaika nao.
Alisema licha ya utafiti kuonyesha kwamba Wazanzibari wanaupenda Muungano, lakini wengi wanaona kama hauwanufaishi sana. Hata hivyo, alisema wenzao wa Bara walio wengi hawaamini kama Wazanzibari wana kero ambazo pengine bila Muungano wasingekuwa nazo.
Katika mkutano huo wa wasomi na wanasiasa, Dk. Sengondo Mvungi alifafanua kwamba wakati wa kuunda Muungano, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, walikubaliana vipengele vinane, lakini kwa sasa vimeongezwa na kufikia 11.
Lakini akasema, kwa bahati mbaya sana, wananchi wa pande mbili hizi hawajui vipengele vya zamani vinasemaje na vilivyoongezwa vinazungumzia nini.
Kitu kingine ambacho kimeanza kujitokeza ni Wazanzibari, tena kupitia baraza la wawakilishi kuhoji mambo mengi ya Muungano na mwisho wa siku kupitisha maamuzi ambayo taratibu yanaonekana kama yatarudia ama yanapunguza nguvu za Muungano wetu.
Tunadhani kwamba lazima tuwe na dhamira ya kweli katika kutatua kero za Muungano kwa kukaa pamoja na kuzungumzia ikiwa ni pamoja na kupitia upya katiba na sheria za nchi yetu zinazoonekana kuwakwaza wananchi wa pande hizi mbili.
Ingawa hili linawakera baadhi ya watu, lakini si vibaya tena ukaanzishwa mjadala wa nchi nzima kuhusu aina ya Muungano ambayo wananchi wanaitaka likiwemo suala la serikali tatu.
Kitu kingine muhimu ni kutoa elimu kwa wananchi wa pande hizi mbili kuhusu mambo muhimu ya Muungano, yaani wayajue yale yaliyokuwepo na yaliyoongezwa na umuhimu wake.
Tunaamini viongozi wetu wakiamua kuweka nguvu katika eneo hilo, kero za Muungano zinaweza kuisha kabisa kabla hatujaingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.



CHANZO: NIPASHE
 
Nilkuwa namisiliza Mhe Nahodha kwa kwenye TV akihojiwa nashangaa majibu au maelezo aliyokuwa anatoa yanasikitishwa. yeye kama mmoja wa waheshimiwa ambao wanazipitia kero za muungano.asinge pashwa kusema kero zitakuwa zinztatuliwa kidogo kidogo kama vile mtoto anavyo kuwa. leo ni miaka 46 huyu mtoto hajakuwa tu. umri wa kuishi sasa tz chini ya miaka 50 ...
halafu kilichonifanye niandike ni kwa changa moto kwenye muungano hazina budi kuwepo , ansema pamoja na vitabu vya dini kuwa baada mtu kufa huenda ahera , lakini yeye haamini kama huko ahera hakuna changa moto lakini kuna changa moto. .Kwa maoni yangu hii sasa nikufika mbali.

bibilia inasema huko mbinguni watu wanafurahi na kuimba nakumshanglia na kusifu Mungu , hakuna changamoto hata moja. Ni kweli sasa viongozi watu wamelewa madaraka !!!
 
bibilia inasema huko mbinguni watu wanafurahi na kuimba nakumshanglia na kusifu Mungu , hakuna changamoto hata moja. Ni kweli sasa viongozi watu wamelewa madaraka !!!

Hii mada ni dini, sio siasa, au?

Changamoto mbinguni zipo, Mkuu Nahodha kapatia. Shetani aliingia vishawishi vya kupindua utawala wa Ulimwengu, akazua sokomoko Mungu akamtupa duniani. Kuna changamoto ya kushikilia imani yako ya uaminifu ukiwa ahera.

(Ni taarifa ya tukio kutoka upande mmoja, wa Mungu, shetani yeye hatujamsikia kuhusu kilichojili huko Mbinguni, usikute wakati wa uchaguzi ulifika Mungu akawa anaendelea kubadilisha Katiba ya Mbingu kusitiri himaya yake tena na tena. Shetani akaona isiwe tabu.)
 
Mnh hapa sina comments....................
 

Wewe tatizo lako ni nini? Unataka Nahodha aongee yaliyo kichwani mwako ndio tuseme kaongea vizuri?
 
mawazo matatu kweli kuna tofauti kubwa sana asante mpaka nasikia aiba kuangalia hizo picha mbili tofauti
 
Unaongelea kupendeza gani dada mi nimeona taswira mbalimbali mbona ilikua aibu...!





Hawa nao kila mtu anaangalia kwake..??



Ona wenzetu.......

naona haya kuangalia kakaangu mmh hao wa chini jinsi walivyo smart aaaaaaaaaaaaagh
 
Mi sikupendezewa kabisa. Buti za maafande zilikuwa zina acha sole za viatu Alafu ile kugonga bunduki moja ikapasuka hivi Jeshi letu nalo bado linatumia vifaa vya kichina?

Soli tena au walitumia viatu vya mitumba?
 

Sina nia mbaya ila naomba nieleweke, Muungano wa Tanganyika
Na Zanzibar ni sawa na ndoa ya kiislamu ambayo anaweza kufungisha,
Muislamu yeyete ili mladi avae kanzu na baraghshia yaani hata kama ni maamuma

Huwa haina masharti yoyote yenye kumfunga mhusika yeyote kati ya waoanaji
Na sheria za kiislamu zinatambua kuwepo kwa taraka hasa kwakuwa ndoa
Ndoa za namna hiyo ni sawa na mkataba uaoweza kuvunjwa dakika yoyote.
Endapo utakuwa hauna tija kwa wana mkataba, kama itatakiwa kufanya hivyo.

Kwa mtazamo wangu Mwolewaji ama upande mmoja wa wanandoa wa Muungano
Alikuwa hana lolote analojua zaidi ya kuitikia TAWILE, sasa ameamka na kuonekana
Kutaka kuboresha ndoa kama si kudai taraka, hii ni baada ya kugundua kuwa,
Aliingia sehemu ambayo sasa anona aburuzwa, na haki ya kuadai kile anachoona ni haki yake.
 
Yaani wewe ndio mjinga kweli kweli kujaribu kutafsiri sheria ya kiislamu hata hujui uislamu wenyewe unasema nini juu ya ndoa. Eti muislamu ye yote anaweza kufungisha ndoa, ni ujinga na dharau gani hiyo kwa dini za waumini wengine?

Halafu "taraka" na "tawile" ndio nini? Hebu jifunze kiswahili kwanza halafu ndio ulete mada inayohusu dini isiyokuwa yako usije kutukana bure.
 
usikurupuke tu, nakushauri uende tena shule ukaongeze uelewa na si hiyo ilimu yako
ya kufokafoka, kipi kilicho kupata hapo,,,,soma, zama, pambanua lugha iliyotumika,
usikurupuke tu ili mradi uonekane upo hewani na kujiongezea wingi wa posti

umeelewa nini juu ya hiyo Topiki? na kuhusianisha 'taraka' na tawile?

hapo hakuna maada ya dini labda wewe hivyo, kwa sababu ya kukurupuka tu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…