......Alihoji ni jambo gani linalokwamisha utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba ya kila upande kuchangia mfuko wa pamoja wa Muungano.
Awali, Mkullo akisoma hotuba ya bajeti yake kwa mwaka 2010/2011, alisema serikali ya Muungano na ya Zanzibar zimeendelea na uchambuzi wa taarifa mbalimbali za tume hiyo kuhusu vigezo vya kugawana mapato na kuchangia gharama za Muungano kwa ajili ya kuyafanyia maamuzi.
Mwiba, choko choko mchokoe pweza, binadamu huta muweza!, hata kuku ukimchambua sana, utashindwa kumla! Hapa wataka tena kuuchoka Muungano halafu mkiambiwa ukweli, hamweshi kulia lia.
Ni kweli Zanzibar na Tanzania bara zinatakiwa kuuchangia mfuko wa Muungano, ikumbukwe Serikali ya Jamuhuri ya Muungano pia ndiyo ile ya Tanganyika, ila Zanzibar ndio yenye serikali yake.
Kama hapa tulipo, Zanzibar inatumia umeme bure, nani anayegharimia, ni serikali ya Muungano. Kama umeme tuu mnashindwa kulipa, itakuwa mtoe mchango kuchangia muungano?. Kwa uwezo upi nyie Zanzibar mlionao?!. Au ni hiyo jeuri ya mafuta ya kinibu ndio mtatumia mapato hayo kuuchangia mfuko wa Muungano?.
Na kama mfuko huo ungekuwepo, serikali ya Zanzibar ikatoa fungu kuuchangia, na serikali ya Muungano ikatoa fungu kuuchasngia kwa niaba ya bara, halafu hilo fungu likatumiwa na serikali ya Muungano kwa niana ya mambo ya Muungano, si ndio mgepiga kelele mpaka mbinguni kuwa mnanyonywa!.
Hoja ya Zanzibar ambayo ni kilio cha msingi, ni hoja kuhusu mgao halali wa Zanzibar ambao ingetakiwa kupata kutokana na misaada mbalimbali kwa Tanzania inayoipata toka kwa wafadhili na washitiri mbalimbali ambayo Tanzania inatia ndani.
Tukirudi kwenye issue za Muungano, kwa vile muungano huu unamatatizo kwenye structure, there is no way out, ni kukubali kubomoa na kujenga upya muungano imara, vingevyovyo tutaendelea kuziba nyufa na kutia viraka wee na bado nyufa zitaendelea mwishowe tutajenga ukuta.