Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mazingira yaliyounda Muungano huo hayapo tena, kwa hiyo sidhani kama kuna ulazima wa kuendela kuung'angania ilhali nchi nyingine zilizokuwa zimeungana kaika mazingira yale zilishavunjika. Ni miungano thabiti tu kama ule wa marekani ndiyo iliyodumu; wa kwetu ni kujidanganya tu iwapo tutatumia nguvu nyingi sana kujadili malalamiko kuliko kuangalia maendeleo.
 
Lets call spade a spade! Why mince words? Now the president of the United Republic of Tanzania has no power over the President of the Revolutionary Government of Zanzibar. The exception is that the latter has no power to declare war. I can see that happening in a near future. So May I take this opportunity to congratulate the People of Zanzibar for re-gaining their independence! By the way, what is THE SECOND country the clause in the constitution of Zanzibar referring to? May be Tanganyika. Sooner or later Rev. Mtikala may be a victor! Even though the recent ruling warned us over questioning political issues, I think one can go to the Court to seek to know which is the other country...Mtikila are u out there?
 
Mazingira yaliyounda Muungano huo hayapo tena, kwa hiyo sidhani kama kuna ulazima wa kuendela kuung'angania ilhali nchi nyingine zilizokuwa zimeungana kaika mazingira yale zilishavunjika. Ni miungano thabiti tu kama ule wa marekani ndiyo iliyodumu; wa kwetu ni kujidanganya tu iwapo tutatumia nguvu nyingi sana kujadili malalamiko kuliko kuangalia maendeleo.

muungano tulionao ni Hoax. Ndiyo maana hata articles zake hazijulikani zilipo. There were nothing called kuungana kati ya tanganyika na zanzibar. it could be siku hiyo there was coup zanziba mzee karume alikimbilia kwa nyerere. And they proclaimed Tanzania ili kumlinda Karume.

If there was at all that muungano we need that histocial document to be open to the public.
 
Baraza jipya la Wawakilishi (BLW), ambalo mabiliko ya Zanzibar mpya yanafanyika asubuhi hii ya Jumatatu, tarehe 09/08/2010. Picha inamuonyesha rais wa Zanzibar Mh. Amani Karume akiwa na wajumbe wa BLW, wadhamini wa ujenzi kutoka Saudi Arabia, Mkewe, mgombea mwenza wa Kikwete, Dr.Bilal, pamoja na rais wa Zanzibar mtarajiwa Maalim Seif Sharrif Hamad (anayependeza kwenye picha hiyo) n.k Jengo hilo lipo eneo la Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar eneo ambalo linapulizwa na upepo mwanana wa bahari ambayo haipo mbali na hapo
 

Attachments

  • new HR opened aug 2010.JPG
    new HR opened aug 2010.JPG
    195.6 KB · Views: 46
So mkuu do you know anything about the role this first-vp will play within the government?



You got it right, ceremonial! Ama kuhusu kama Zanzibar ni taifa au nchi, sioni kama ina maana sana. Chenye maana ni kuhakikisha Rais wao (Zanzibar) hawezi kuingiliwa na yule wa Muungano kwa vyovyote vile...successfully done!
 
AG Werema,
Tuambie basi kama hizi clauses zinazotaka kupitishwa hapa hazibatilishwi na Katiba ya JMT? Kwani Baraza la Wawakilishi bado lipo?
 
Zanzibar kuwa nchi

na Hassan Shaaban, Zanzibar


SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inafanya marekebisho ya katiba ya mwaka 1984, ambayo yanaipa Zanzibar hadhi kamili kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano.

Marekebisho hayo ya katiba yanatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoanza leo Zanzibar, ambapo pia yataruhusu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.


Kwa mujibu wa rasimu ya marekebisho ya katiba hiyo, sura ya kwanza ibara ya kwanza iliyokuwa ikisomeka, Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefutwa chini ya marekebisho hayo.


Rasimu hiyo ambayo itawasilishwa na Mwanasheria Mkuu, Idd Pandu Hassan, inapendekeza kifungu hicho sasa kisomeke ‘Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguuka na bahari yake, ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar'.


Aidha, marekebisho hayo ya katiba yamegusa kifungu cha pili na kueleza kuwa Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Marekebisho hayo pia yamegusa mamlaka ya rais katika kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.


Kabla ya marekebisho hayo kifungu cha pili cha Katiba ya Zanzibar kilikuwa kikisomeka ‘kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano akishauriana na rais anaweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa'.


Marekebisho hayo pia yamempa uwezo Rais wa Zanzibar kuteua wakuu wa mikoa bila ya kushauriana na Rais wa Jamhuri ya Muungano, kama ilivyokuwa kabla ya marekebisho hayo.


Marekebisho hayo ya 10 ya Katiba ya Zanzibar iwapo yatapitishwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi yatamaliza msuguano uliokuwa umejitokeza kuhusu nafasi ya Zanzibar katika Jamhuri ya Muungano, baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kudai kuwa "Zanzibar si nchi".


Hata hivyo, baadaye Rais Jakaya Kikwete akitoa ufafanuzi wa suala hilo alisema Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano, lakini "Zanzibar si nchi nje ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyo kwa Tanganyika. "


Aidha, marekebisho hayo ya katiba yanampa uwezo Rais wa Zanzibar kuteua makamu wawili wa rais, akiwamo makamu wa kwanza ambaye atateuliwa baada ya rais kushauriana na chama kilichoshika nafasi ya pili katika kura za rais kwenye Uchaguzi Mkuu.


Rais pia atamteua makamu wa pili wa rais ambaye atakuwa ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za serikali ndani ya Baraza la Wawakilishi

Wakati wajumbe wa Baraza la Mawaziri watateuliwa kwa uwiano wa viti vya wajumbe ndani ya Baraza la Wawakilishi.

Pia mswada huo unafuta wadhifa wa Katibu Mkuu Baraza la Mapinduzi na kuweka Katibu Mkuu Kiongozi, ambapo pia kutakuwa na makatibu wakuu wa ofisi ya makamu wa kwanza wa rais na katibu mkuu ofisi ya makamu wa pili wa rais.


Source: Tanzania Daima
 
..Raisi wa SMZ asiwe Makamu wa Raisi wa Muungano, unless anapigiwa kura na pande mbili za muungano.
 
8D6U9904.JPG


Ndio,

Ninaongelea serikali ya muungano wa ccm na cuf.

Rais wa JMT - Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)
Makamo wake - Bilal (CCM)
Waziri Mkuu - Lipumba (CUF)

Rais wa Zanzibar - Seif (CUF)

Wadau endelezeni majina hapa chini.
 
Malaria Sugu - Waziri wa Propaganda na uenezi (CUF)

Tumaini - Waziri wa sheria na mahakama ya Kadhi ( CCM)
 
Waziri wa fedha - Mkullo (CCM)
Usalama wa taifa - Othman (CCM)

Inaendelea....
 
Mwanakijiji - Waziri wa habari

Mwafrika wa Kike - Waziri wa wanawake

David Solomon - Waziri wa Kazi

Bi Centi50 - Waziri wa Mifugo

Maxshimba - Waziri wa Miundo Mbinu

Mzee Mwafrika - Waziri wa Mawasiliano

Bibi Ntilie - Waziri Nishati

Madilu Madela - Waziri wa Mazingira

................... to be continue
 
Jamani mmesahau kumpa Kanda 2 cheo katika serikali hii tukufu!
 
Ndugu wana JF ,napenda kuwauliza ,hili suala ambalo linaonekana kuchangiwa na kutetewa na watu wa aina kwa aina, hivi ni nani anaepaswa kuitetea uwepo wa serikali ya Tanganyika ,Zanzibar na Hii serikali ya Muungano ?

Karibuni vyama vyote vya upinzani vinasema ikiwa vitashinda basi vitahakikisha kuwa zinakuwepo serikali tatu ,kwa maana kuu kuwa serikali ya Tanganyika ,serikali ya Zanzibar na serikali ya Muungano ,zinakuwepo kikamilifu.

Hapa ukumbini nimeona waZanzibari wanapojaribu kujadili mambo au wanapoweka wazi mambo ya Serikali yao ,kunatokea watu hufanya nongwa na kukasirika vibaya sana kama vile kumesemwa tusi au maneno yasiyostahili kusemwa,kwa ufupi wengine mnaonekana kama kuchanganyikiwa na mnapoteza muelekeo.

Ajabu kwamba nyie msiekuwa na serikali mnakuwa wakali sana kwa kuonyesha kuitetea serikali ya Muungano serikali ambayo hata WaZanzibari inawahusu ,tena wao inawahusu zaidi kuliko nyie wengine ambao serikali yenu, nikimaanisha ya Tanganyika haipo,mlipaswa kukaa kimya ,WaZanzibar wanapanga na kurekebisha yale ambayo wanaona yanafaida kufanyiwa hivyo na wanafanya hivyo kwani wananyo haki kamili ya kufanya hayo.

Haionekani kama mnachangia au kuonyesha kuwa mnajali yale ambayo WaZanzibari wanayafanyia ukarabati zaidi ya kuonyesha kuwa mnachukia au hamupendi kuona maendeleo yao.
 
Haionekani kama mnachangia au kuonyesha kuwa mnajali yale ambayo WaZanzibari wanayafanyia ukarabati zaidi ya kuonyesha kuwa mnachukia au hamupendi kuona maendeleo yao.

Hakuna anayechukia Znz au maendeleo yake, watu wanachukia unafiki wa wznz! mfano wameanza harakati za kuvunja muungano kitambo tu, lakini kwa unafiki hawatamki, wanafanya mambo uani uani tu!
 
Rais wa Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania ndiye mwenye wajibu no. 1 kuitetea serikali ya Mwungano. Asipofanya hivyo anafanya usaliti kwa katiba aliyoahidi kuitetea.
 
Back
Top Bottom