Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Nonda,

..suala la kujitambulisha kama Mtanzania au Mtanganyika ni suala ambalo naweza kusema ni la "mafundisho" na "mapokeo."

..binafsi nimezaliwa na kukulia Arusha, lakini wazazi wangu wamezaliwa mkoa mwingine.

..sasa kutokana na mafundisho na malezi ya ndani ya nyumba yetu, leo hii ukiniuliza natokea mkoa gani ktk Tanzania/Tanganyika, bila shaka yoyote ile nitakwambia nimetokea kule walikozaliwa wazazi wangu.

..kutokana na experience yangu hiyo, ndiyo maana nime-conclude kwamba, kwa wenzetu wa-Zanzibari hazikufanyika juhudi zozote zile za kuwaelimisha kwamba baada ya muungano basi ni vema wakachukua identity/utaifa mpya wa TANZANIA.

..naamini pia kuna mambo mengi ya KIHISTORIA na KISIASA yaliyosababisha muungano wetu uchukue sura iliyoko sasa hivi. kwa mfano, kuna tetesi za Wazanzibari kuogopa "kumezwa" kama kikwazo cha kuwa na nchi moja, serikali moja.

..kwa kweli kipengele hicho hapo juu sina jibu la uhakika la kukutosheleza. lakini ngoja nijaribu:

..je, tuna uhakika kwamba Rwanda,Burundi, etc hawajaomba kujiunga nasi kutokana na kuona matatizo tuliyonayo sisi, au kutokana na matatizo yao wenyewe, haswa ya viongozi wao?

..is it easy kwa kiongozi aliyekwisha onja madaraka ya Uraisi, akaitumbukiza nchi yake ktk muungano, huku yeye akiwa hana uhakika na nafasi yake ktk muungano huo?

..kwa sababu tunaelewa kabisa kwamba kuna baadhi ya wananchi wa Rwanda na Burundi ambao ilibidi waondoshwe kwa nguvu kuwarudisha nchini kwao.

..binafsi nadhani wakati mwingine haya masuala ya kuunganisha nchi yanahitaji viongozi kuonyesha njia. vilevile zaidi ya viongozi kuonyesha njia kunatakiwa kuwepo na jitihada za makusudi na za muda mrefu kuhakikisha kwamba wananchi wanakubaliana na hatua zilizochukuliwa na viongozi wao. reference nzuri kwa hoja yangu hii ni matatizo yaliyotokea Yugoslavia.

..again, sina jibu la uhakika kwa swali lako hili. sijachimba vizuri kujua muungano kama wa USSR au ule Yugoslavia ulikuwa wa namna gani.

..inawezekana ukawa na hoja kwamba hakuna muungano ambao umefanikiwa kuzifuta nchi zilizounda muungano huo.

..lakini haya vilevile ni masuala ya kisiasa na kijamii. kushindwa kwa mataifa mengine kuungana na kuunda utaifa mpya, isiwe kisingizio cha wa-Tanganyika, au wa-Zanzibari, kuukana u-Tanzania. nini kinachotuzuia sisi kuwa wa kwanza, na mataifa mengine kuiga kutoka kwetu?

Nilikuunga mkono kwa hoja zako lakini hili la kufikiri kuwa Watanganyika wanajiona kuwa ni Watanzania na Wazanzibari wanajiona ni Wazanzibari halitokani na kazi ya kuelimisha bali inatokana na mfumo wenyewe wa Muungano wetu ulivyo.

Unategemea nini iwapo Tanganyika iliamuwa kubadili jina tu na kujiita Tanganyika na kubaki na kila kitu chake. Unafikiri jina lina maana katika Utaifa, Chukulia Congo (Zaire) hakuna anaejali iwapo Zaire au Jamhuri ya Congo mradi imeshaamuliwa hivyo. Watanganyika wanataka nini kuitwa Watanganyika wakati kila kitu cha Tanganyika kimo ndani ya hiyo inayoitwa Tanzania? Wanakosa nini kwa kujiunga na Zanzibar? Jawabu ni kuwa hakuna!
Sasa natuje kwa upande wa Zanzibar na tuone kama kweli ni kutooelimishwa au kumefanywa makusudi kuwafanya watu wa visiwa hivi wabaki kama Wazanzibari. Msingi wa Zanzibar kujitia katika umoja huu haukuwa hata siku moja kuwa na lengo la kuiondowa Zanzibar bali ni kutafuta usalama kwa taifa changa. Tamko la Serikali mbili kwenda moja halikuwahi kutamkwa na Kiongozi wa Zanzibar zaidi alishawahi kutamka matamko ya kuonesha kuwa Muungano huu ni wa makubaliano ya muda na hali isiporidhisha basi uvunjwe.
Itakuwaje pia kuiachia Zanzibar na Rais wake na vyombo vyake kamili vya dola halafu utegemee kuwa Zanzibar kama utaifa uondoke? Si ukosefu wa kutoelimishwa bali ukweli halisi wa mambo ndio uanaowafanya Zanzibar waendelee kujiona ni Wazanzibari. Kwani wananchi wa Zanzibar huhudumiwa na serikali gani? Ni Serikali ya Zanzibar ndiyo mtoto wa Visiwani huwa anafunulia macho, ni Rais wa Zanzibar ndie raisi wake, ni wizara za serikali za Zanzibar ndio zinazomuhudumia, sasa unategemea ajihisi vipi kama si Mzanzibari? Mtoto huyu kila anapokuwa anasikia na kusoma kero zinazosababishwa na Muungano huu kwa Visiwa hivi bado unategemea ataona fahari kwa Tanzania?
Watanganyika hawaitaki Tanganyika yao kwa vile kwa kurudi kwa jina la Tanganyika itabidi nao wabanane na wenzao wa zanzibar katika Serikali ya Muungano. Hivi sasa kwa kuvaa koti la Tanzania wanapata na kufanya yao na ya wenzao (Zanzibar). Sifikiri ni busara kuachia bure hii!
 
Nonda,

..suala la kujitambulisha kama Mtanzania au Mtanganyika ni suala ambalo naweza kusema ni la "mafundisho" na "mapokeo."

..binafsi nimezaliwa na kukulia Arusha, lakini wazazi wangu wamezaliwa mkoa mwingine.

..sasa kutokana na mafundisho na malezi ya ndani ya nyumba yetu, leo hii ukiniuliza natokea mkoa gani ktk Tanzania/Tanganyika, bila shaka yoyote ile nitakwambia nimetokea kule walikozaliwa wazazi wangu.

..kutokana na experience yangu hiyo, ndiyo maana nime-conclude kwamba, kwa wenzetu wa-Zanzibari hazikufanyika juhudi zozote zile za kuwaelimisha kwamba baada ya muungano basi ni vema wakachukua identity/utaifa mpya wa TANZANIA.

..naamini pia kuna mambo mengi ya KIHISTORIA na KISIASA yaliyosababisha muungano wetu uchukue sura iliyoko sasa hivi. kwa mfano, kuna tetesi za Wazanzibari kuogopa "kumezwa" kama kikwazo cha kuwa na nchi moja, serikali moja.

..kwa kweli kipengele hicho hapo juu sina jibu la uhakika la kukutosheleza. lakini ngoja nijaribu:

..je, tuna uhakika kwamba Rwanda,Burundi, etc hawajaomba kujiunga nasi kutokana na kuona matatizo tuliyonayo sisi, au kutokana na matatizo yao wenyewe, haswa ya viongozi wao?

..is it easy kwa kiongozi aliyekwisha onja madaraka ya Uraisi, akaitumbukiza nchi yake ktk muungano, huku yeye akiwa hana uhakika na nafasi yake ktk muungano huo?

..kwa sababu tunaelewa kabisa kwamba kuna baadhi ya wananchi wa Rwanda na Burundi ambao ilibidi waondoshwe kwa nguvu kuwarudisha nchini kwao.

..binafsi nadhani wakati mwingine haya masuala ya kuunganisha nchi yanahitaji viongozi kuonyesha njia. vilevile zaidi ya viongozi kuonyesha njia kunatakiwa kuwepo na jitihada za makusudi na za muda mrefu kuhakikisha kwamba wananchi wanakubaliana na hatua zilizochukuliwa na viongozi wao. reference nzuri kwa hoja yangu hii ni matatizo yaliyotokea Yugoslavia.

..again, sina jibu la uhakika kwa swali lako hili. sijachimba vizuri kujua muungano kama wa USSR au ule Yugoslavia ulikuwa wa namna gani.

..inawezekana ukawa na hoja kwamba hakuna muungano ambao umefanikiwa kuzifuta nchi zilizounda muungano huo.

..lakini haya vilevile ni masuala ya kisiasa na kijamii. kushindwa kwa mataifa mengine kuungana na kuunda utaifa mpya, isiwe kisingizio cha wa-Tanganyika, au wa-Zanzibari, kuukana u-Tanzania. nini kinachotuzuia sisi kuwa wa kwanza, na mataifa mengine kuiga kutoka kwetu?

Mkuu,

JokaKuu nimependa jawabu zako ingawa wewe mwenyewe umesema ni za kubahatisha, kujaribu.
Imani yangu ni kuwa utajibebesha jukumu la kusoma historia ya nchi yetu. Napendekeza ,soma historia ya Tanganyika kama nchi na taifa, Zanzibar kama nchi na taifa, pia Muungano wa mataifa haya mawili, tokea ulipoundwa mpaka leo hii.

Mimi sioni ubaya kwa nchi kuungana, lakini matatizo yanakuja inapokosekana haki na usawa.

Pia mataifa,nchi zinapoungana hufanya hivyo kupitia mikataba ya kimataifa na kwa hiyo panapotokea sitafahamu, manung'uniko baina yao ambayo wao wenyewe watashindwa kuafikiana basi kimbilio lao linakuwa mahakama ya kimataifa lakini inapokuwa members wa muungano hawa-exist utatatua vipi mzozo huo? Litakalotokea ni vita au annexation.

Kwa hiyo, tukubali kuwa waliotuundia muungano huu walifanya madudu tokea mwazo na tusipofanya juhudi za makusudi kuweka sawa palipoharibika basi ni kusema tunakalia time bomb. Hata kama itachukua miaka 70 kuna siku lita-explode na kuleta maafa.

Jambo ambalo mimi naliona ni kiini macho katika muungano huu ni kuwepo kwa mambo ya Tanganyika tu, ingawaje hatuisikii Tanganyika kutajwa(badala yake inatajwa Tanzania bara. When did Tanganyika change the name to become Tanzania bara?), kuwepo kwa mambo ya Zanzibar tu, hii ipo na kuwepo kwa mambo ya Muungano(Tanzania)hii pia ipo.

Hebu pata muda kufikiria haya, kwa nini mwanachama mmoja katika Muungano aamue kupoteza jina lake la asili,kiasi iwe ni dhambi au kama kosa la jinai kulitaja jina lake? Na hapa nakusudia Tanganyika.
Jee kuna faida gani kuwafanya watu wauchukie utaifa wa awali?

Katika muungano wetu kuna pande mbili na kila upande unategemea kutetea maslahi yake ndani ya muungano, jee kukosekana kuonekana kwa uwazi wawakilishi wa upande mmoja kunasaidia vipi kuudhofisha muungano huu?
Kuna kitu gani hapa ambacho viongozi wetu wanakifanya kuwa ni siri kubwa sisi wananchi wa kawaida tusijue,tusielewe?

Mfano huu tunaweza kuusogeza kwenye EAC. Tanzania ni member hapo jee tutanufaika vipi kama hatuna muwakilishi wetu huko? Au tukijifanya kuwa Tanzania hai-exist?

Je umeshajitayarisha kuachana na utanzania pale Comoro itakapojiunga nasi kama anavyodokeza Buchanan? Utaifa wetu mpya utakuwa Utanzancomia! Tan-zan-com-ia

Je umeshajitayarisha kuwa mui-east afrika na kuachana na utanzania litakapokuja East African federation?

Asante, mkuu kwa kuendeleza mjadala.

PS, Mkuu,
Ona hii, mchango wa mbu sugu,nimeiopoa katika thread, JK kupangua baraza la mawaziri
Re: JK kupangua Baraza la Mawaziri........

Jarida hilo limechelewa na liko nyuma ya wakati. Wizara walizopewa Sitta na Tibaijuka ni miongoni mwa Wizara nyeti hapa Tanzania na za kuheshimika kama mtu ataamua kufanya kazi kama alivyoanza mama Tibaijuka. Ulaya hawana wizara ya Afrika mashariki na suala la ardhi kwao halina utata lakini huku kwetu bila ardhi wanyonge wangi watakosa haki zao. Wazungu hawajajua kwamba tunahitaji mtu makini sana wa kutetea maslahi ya Tanzania katika muungano wa Afrika Mashariki.....
 
..binafsi nadhani wakati mwingine haya masuala ya kuunganisha nchi yanahitaji viongozi kuonyesha njia. vilevile zaidi ya viongozi kuonyesha njia kunatakiwa kuwepo na jitihada za makusudi na za muda mrefu kuhakikisha kwamba wananchi wanakubaliana na hatua zilizochukuliwa na viongozi wao. reference nzuri kwa hoja yangu hii ni matatizo yaliyotokea Yugoslavia.

..again, sina jibu la uhakika kwa swali lako hili. sijachimba vizuri kujua muungano kama wa USSR au ule Yugoslavia ulikuwa wa namna gani.

..inawezekana ukawa na hoja kwamba hakuna muungano ambao umefanikiwa kuzifuta nchi zilizounda muungano huo.

..lakini haya vilevile ni masuala ya kisiasa na kijamii. kushindwa kwa mataifa mengine kuungana na kuunda utaifa mpya, isiwe kisingizio cha wa-Tanganyika, au wa-Zanzibari, kuukana u-Tanzania. nini kinachotuzuia sisi kuwa wa kwanza, na mataifa mengine kuiga kutoka kwetu?[/QUOTE]

JokaKuu,

Mataifa mengine yatatuiga kama kuna zuri la kuiga. jee kwa kelele hizi tunazopigishana kuwa huyu ananuafaika zaidi, huyu ananibana, huyu nambeba kama yatima, huyu ananimeza! Ndio kuna zuri la kuiga hapo?
Au amani na utulivu wakati kila raia ni fukara,maskini ila wachache tu? Lipi la kuigwa hapa ?

Tatizo hapa sio Utanzania. Ukiachilia wachache, Wazanzibari wanajijua kuwa wao ni watanzania. Huu ndio utaifa common kwa jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania). Lakini hii haiwafanyi wao wasiwe Wazanzibari. Pia sisi watanzania wa upande huu haitufanyi tusiwe watanganyika. Kama unauelewa juu ya pasi za EU basi ni rahisi hii dhana kuielewa. Au US au UK na kwa sasa China na Hong-kong. Pitia mifumo yao uone kama itaweza kutusaidia katika kuufanyia marekebisho muungano wetu.

Hapa Tz utapata mtu ambaye ni mtanzania, mtanganyika, mnyamwezi.
Au,Mtanzania, mtanganyika, mchaga, mmachame.

Pia hapa Tz utampata mtu ambaye ni mtanzania, mzanzibari, mpemba
Au, mtanzania. Mzanzibari, mtumbatu.
Kuna watanganyika waliohamia Zanzibar na wamepata sifa huko ya kuwa mzanzibari kwa sheria za uchaguzi za huko, basi leo utampata mtu, mtanzania, mtanganyika-mzanzibari, mnyamwezi.

Kama hilo litakushangaza, leo duniani, watu wana dual citizenship. Mtu ni mmarekani wakati huo huo ni mcuba na hapa kwetu,kuna watu walio nje wanaisubiri kwa hamu sheria itakayoruhusu utaifa wa nchi mbili. Si umemsikia Membe? Kwa hiyo ,tutapata watu ambao watakuwa, wamarekani,watanzania, watanganyika, wabondei au (British)mbritania,mtanzania,mzanzibari,mkojani.

Huu ni uhalisia katika dhana ya utaifa.
 
Comoro wanataka kujiunga na sisi, kama unafuatilia matukio! labda nikuulize tukijiita mtanganyika itatusaidia kujenga zahanati, shule, barabara, nk?

Wacha utoto mwanangu utanzania ulio nao umekusaidia kujenga shule na zahanati? kinacho takiwa kwanza kujitambua hiki ni changu baadaye utakipenda na kukilinda mwanangu dhidi ya aina yeyote ya hujma na ufisadi Wanakushinda hata wazenj ambao WANAJITAMBUA hawakubali mtu yeyote kuchezea utaifa wao jaribu leo uone watakavyo kuzomea bila kujali huyu cuf ccm ima chadema wote wanaungana Kutetea kwa maslahi ya nchi yao na utaifa wao Leo huendi na chakula hospitali kuona mgonjwa Angalia shule zao zinavyo boreshwa pamoja na makazi Jiangalie mtanganyika ulivyo laniwa tunakufa sanda kiroba kwa kukosa dawa kwa magonjwa yanayo tibika Wanetu badala ya kusoma wanacheza gololi! Wakati hatuna upungufu wa mali asili JITAMBUENI MWANA WATANGANYIKA!!
 
Eti nisaidieni,au Tanganyika ndio Tanzania? Hapana,Tanzania ni acronym ya majina mawili,Tanganyika na Zanzibar.Sasa mbona Zanzibari bado inaishi!!,tanganyika siioni!!
Hata ktk mashindano ya soccer ya challenge yanayoendelea,mbona timu ya Zanzibar jezi zake zimeandikwa ZANZIBAR na timu inaitwa zanzibar? Timu ya bara inaitwa kilimanjaro staz,jezi zake hazijaandikwa jina la nchi,kili staz inawakilisha nchi gani?kwa nini zisingeandikwa Tanganyika? au tanganyika imekufa? Sasa si zingekufa zote Zanzibar na Tanganyika! Au mnaonaje linapokuja swala la pande hizi mbili za muungano kushiriki kila moja kivyake kama ilivyo ktk soccer,tutumie bara kwa upande mmoja na visiwani kwa upande wa pili,hata jezi zionyeshe hivyo.Kuna nini hapa chafichwa?Mie nabata ushungu.

Mkuu,

wenye nchi, yaani CCM katika mwaka 1977 kama hii kumbukumbu iko sawa Tanganyika ilibadilisha rasmi jina lake kutoka Tanganyika na kuwa Tanzania bara.

Kwa sababu gani?

Nafikiri mtu ambaye ataweza kujibu suali hili ni Jaji Warioba. yeye ndiye muandishi wa katiba ya 1977 na ndipo Tanzania bara ilipoanza kutumika rasmi.

wewe tapata ushungu mpaka tazaa!!!

..kwanza tuvunje muungano, halafu turejeshe Tanganyika.

..kuirudisha Tanganyika ndani ya muungano, kutatuongezea gharama za uendeshaji serikali.

..wa-Tanganyika tutalazimika kuhudumia serikali ya Tanganyika, pamoja na ile ya Muungano.

..kumbuka kwamba tutalazimika kuwa na bunge la muungano, na bunge la Tanganyika.

..juu ya hayo wakati mwingine SMZ wanakuwa so irresponsible kiasi kwamba huacha kulipa madeni yao kwa mashirika kama Tanesco, na pia kulipa watumishi wa serikali "tarehe 45 ya mwezi." katika mazingira kama hayo wa-Tanganyika hulazimika kuchukua mzigo wa gharama za kuendesha SMZ.

..narudia: rudisha Tanganyika; vunja Muungano; imarisha mahusiano na Zenj kupitia East African Community.
 
mkuu,

Mkuu usipate tabu katika hili, Kilimanjaro stars inawakilishisha nchi iliyopata uhuru 09,Disemba. lakini ni dhambi, uhaini kuitaja kwa sauti. Na ile timu iliyovaa jezi zilizoandikwa Zanzibar, ni kuwa wazenj wanatushinda sisi huku “Tanzania” kwa uzalendo!

Kwa hiyo "uzalendo" ni kuheshimu mipaka iliyowekwa na Wakoloni badala ya ile tuliyoiweka sisi?
 
..kwanza tuvunje muungano, halafu turejeshe Tanganyika.

..kuirudisha Tanganyika ndani ya muungano, kutatuongezea gharama za uendeshaji serikali.

..wa-Tanganyika tutalazimika kuhudumia serikali ya Tanganyika, pamoja na ile ya Muungano.

..kumbuka kwamba tutalazimika kuwa na bunge la muungano, na bunge la Tanganyika.

..juu ya hayo wakati mwingine SMZ wanakuwa so irresponsible kiasi kwamba huacha kulipa madeni yao kwa mashirika kama Tanesco, na pia kulipa watumishi wa serikali "tarehe 45 ya mwezi." katika mazingira kama hayo wa-Tanganyika hulazimika kuchukua mzigo wa gharama za kuendesha SMZ.

..narudia: rudisha Tanganyika; vunja Muungano; imarisha mahusiano na Zenj kupitia East African Community.

Faida ya kiuchumi ni ipi ya kuwa na serikali ya Tanganyika? Je, barabara zitajengwa, mafisadi watapelekwa mahakamani, etc?
 
Mkuu,

wenye nchi, yaani CCM katika mwaka 1977 kama hii kumbukumbu iko sawa Tanganyika ilibadilisha rasmi jina lake kutoka Tanganyika na kuwa Tanzania bara.

Kwa sababu gani?

Nafikiri mtu ambaye ataweza kujibu suali hili ni Jaji Warioba. yeye ndiye muandishi wa katiba ya 1977 na ndipo Tanzania bara ilipoanza kutumika rasmi.

wewe tapata ushungu mpaka tazaa!!!

Kwani jina Tanganyika ambalo hata hatujui asili yake lilitakiwa lisisbadilike?
 
oooh!jamani mbona mnaotonesha moyo wangu. Mi nadhani kuna kila ya haja ya warioba kuulizwa na kutupa majibu ya siri ya kuivunja tanganyika yetu. Mi nasema tanganyika ni nchi huru iliopata uhuru tar 9 dec 1961 na hiyo tanzania sio nchi ila ni muungano ambao hauna tija na faida zaidi ya majungu. Mungu ibariki tanganyika yetu, mi na wewe ndio wa kuirudisha tanganyika yetu iliyo uawawa bila kosa.
 
Nchi maana yake nini? Wakoloni waliacha maagizo kwamba tusiweke mipaka mingine isipokuwa "urithi" waliotuachia?
 
Kama halieleweki sasa hivi basi hata huko mbeleni halitaeleweka!
Buchanan
user-online.png
JF Senior Expert Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

Join DateTue May 2009Posts5,663Thanks1,267Thanked 2,174 Times in 1,336 PostsRep Power34

Did you find this post helpful? |
icon1.png
Re: Taja mapungufu ya Katiba

1. Rais apunguziwe madaraka ili baadhi anaowateua wathibitidhwe na Bunge!
2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwe huru, ie cmposition ya wajumbe wa tume ijumuishe pia wapinzani.
3. Tanzania sio tena nchi ya Ujamaa na Kujitegemea kwa kuwa njia kuu za uchumi zote haziko mikononi mwa Serikali. Kwahiyo Katiba ifanyiwe marekebisho kuondoa kipengele hicho!
4. Katiba ifanyiwe marekebisho iendane na Katiba ya Zanzibar, km kuondoa cheo cha uwaziri kiongozi!
5. Viti maalum vya ubunge na udiwani viondolewe, havina kazi yoyote.
6. Rais asiwe na mamlaka ya kuteua Wabunge, kwa kuwa hao wabunge hawawakilishi chochote.
7. Matokeo ya urais yawe challenged mahakamani, kwa hiyo kile kipengele kwamba Tume ikishatangaza matokeo basi hakuna mahakama yoyote yenye uwezo wa kuyachunguza kiondolewe!
8. Rais asiwe na uwezo wa kubadili Wizara mara kwa mara, idadi ya wizara ziwekwe kwenye Katiba na kama ataona kuna haja ya kuziongeza Bunge liridhie. Hii itapunguza Rais kubadili Wizara kila mara, kwa kutaka kuwapatia maswahiba wake vyeo! Pia Wizara ziwe chache ili kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali.
9. Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana kazi waondolewe na badala yake wabaki Wakurufenzi watendaji wa Majiji, Miji, Manispaa na Wilaya!
10. Muundo wa Muungano uwe wa Serikali tatu!
11. Kuwe na equal distribution ya resources badala ya kuconcetrate tu kujenga Dar es Salaam na baadhi ya mikoa. Kwa hiyo iwekwe mechanism kwenye Katiba, eg Swrikali za Majimbo zenye baadhi ya mamlaka juu ya resouces zilizopo maeneo yao.
13. Mgombea binafsi aruhusiwe Kikatiba!
14...
Last edited by Buchanan; 18th December 2010 at 07:15 AM.
 
Faida ya kiuchumi ni ipi ya kuwa na serikali ya Tanganyika? Je, barabara zitajengwa, mafisadi watapelekwa mahakamani, etc?

Buchanan,

Serikali mbili tayari zipo. je ya tatu utaipa jina gani?
Usijifanye umesahau,tizama mapendekezo yako ya katiba mpya. nambari 10 hapo.
 
Kwa hiyo "uzalendo" ni kuheshimu mipaka iliyowekwa na Wakoloni badala ya ile tuliyoiweka sisi?

Mkuu,

Tulipigana vita ya Kagera kwa nia hiyo hiyo, kuheshimu mipaka ya mkoloni.vyenginevyo tungelimwachia Idi Amin, kipande kidogo tu cha ardhi, sehemu tu ya Kagera. Au umelisahau hili?
 
mkuu,

Mkuu usipate tabu katika hili, Kilimanjaro stars inawakilishisha nchi iliyopata uhuru 09,Disemba. lakini ni dhambi, uhaini kuitaja kwa sauti. Na ile timu iliyovaa jezi zilizoandikwa Zanzibar, ni kuwa wazenj wanatushinda sisi huku "Tanzania" kwa uzalendo!

WAZAZI WETU 'JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA' NA 'ZANZIBAR', KUISHI HUKU KAMA VIMADA MPAKA LINI???

Nimependa sana hilo!!

Ni hapa JF tu ndiko tunakodiriki si kulitaja tu jina Tanganyika bali hata kulifanyia uchambuzi wa kina.

Kwa kwaida Serikali ya Ubia Kati ya Mheshimiwa Tanganyika na Mheshimiwa mwenzake Zanzibar (Baada ya kuzaa jina zuuuuuri duniani la Mama yetu Tanzania basi ni vema wakaishi CHUMBA KIMOJA KWA KILA NYANJA YA MAISHA.

Kweli kabisa kama waliamua kwa hiari yao kuoana basi ni vema kuonekane maisha ya kifamilia wanaoishi kwa kuvumiliana katika shida na raha.

Kwetu sisi vijana hatufurahishwi kuendelea tu kuishi bila hata kujua mzazi wetu mwingine aliendaga wapi zaidi tu ya kuhadithiwa kwamba asubuhi moja alipokwenda sokoni hakurudi tena nyumbani.

Kama Tanganyika alikufa basi katuonyesheni kaburi lake ili tukubaliane na matokeo. Na kama kageuka MSEKULE nako tuambiwe ili tukasali dua na rozari na kumrudisha katika hali ya kawaida.

Kitendo cha sisi kulazimika kuishi kama yatima miaka nenda rudi katika jumba hili zuri liitwalo Tanzania kamwe halitufurahishi. Maana maisha tunayoyaona sisi watoto kati ya Mama yetu wa Kambo Zanzibar na Mzazi Tanzania ni kama maisha ya KUWEKA KIMADA VILE.

Iweje kwamba wameona na kila siku majirani wanatuambia kwamba mama mdogo Zanzibar bado anakilipia chumba chake cha ujanani kule mtaa wa pili na hata vyombo vyake vya kulala, samani na vile vya kupikia anavitunza tu hukohuko LAKINI nako hapa nyumbani akija anadai chumba cha baba yetu ni halali yake???

Jamani siku hizi maradhi ni mengi sana na mzazi pekee tuliobaki naye ni Baba yetu Tanzania ambaye tukimpoteza ndio basi tena, hivyo tunamuomba mama yetu mdogo Zanzibar chagua kukaa na Baba moja kwa moja kama mke na mume na kwa kuzingatia heshima ya ndoa maana sisi vijana wenu tumeshakua watu wazima na mnapoishi KIUJANJA UJANJA hivi wenzenu huzuni hauishi moyoni na hasa tunapomkumbuka mama yetu Tanganyika ambaye hajulikani aliko hadi leo hii.

Umetowa maelezo yenye mapambo,urembo na nakshi nyingi.
Ilikuwa useme kwa ufupi tu kuwa unapendekeza serikali moja au tatu ndio msimamo wako. Au sikukuelewa hapa ?

Lakini pia mimi sikubaliani na watu wanaotoa mifano ya kuungana kwa nchi kutoa mifano ya ndoa. Na kutoa mifano ya mama na baba,watoto. Picha hapa haikai vizuri hasa ile ya kitandani.

Jee tunaweza kufananisha EAC katika mfano huu wa ndoa ? nani kamuoa nani ? au nani kaolewa na nani ? katika dunia ya leo kuna wanaume wanaoana, kuna wanawake wanaoana(gay/lesbian marriages). Kwa hiyo sioni kama ni sahihi kuleta mifano ya ndoa katika issue ya muungano wa Tanzania, kama tuko serious katika mijadala hii.

Issue iko simple, nchi mbili,Tanganyika na zanzibar waliunganisha baadhi ya mambo. Mambo hayo 11 yakaitwa mambo ya muungano. Na muungano huu ukaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kutokana na ujanja na usanii wa wanasiasa wetu ndio tena yametufika haya yaliyotufika. Bila ya kujua tatizo lilianza vipi basi pia ni tabu kupata ufumbuzi wake.

Ubadilishaji wa jina hili Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kuwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ilikuwa ni hatua ya mwanzo kuelekea matatizoni.

Kuongeza mambo ya muungano kila leo ni hatua nyengine inayoongeza mazonge, matata.

Kuificha au kuiua serikali ya Tanganyika, rais wake na bunge la Tanganyika ni hatua nyengine iliyotandika kiza kinene mbele yetu.

Kulifuta jina la Tanganyika kuwa Tanzania bara ni hatua nyegine iliyotupelekea sisi kuchanganyikiwa na mwishowe tuwe hatujui tunazungumza nini !

Nini cha kufanya ? Zanzibar kwa busara nzuri ya CCM,( sifikirii kama CCM really walipendekeza kwa nia njema, though) wametuonesha njia,
Kura ya maoni kuhusu muungano na aina ya muungano iitishwe kulikoni kusubiri maafa huko mbeleni au kuendeleza kupiga kelele na mayowe.
 
Nonda Shaaban Papii, nimekubaliana na wewe UTATA wa chumbani unaouona hapo.

Hakika niseme ninatolea kufia maoni yako hayo. Hata hivyo nitoe ufafanuzi kidogo kwamba katika SPEECH AND EFFECTIVE MESSAGE DELIVERY techniques, ni jambo la mbolea sana mtu kutumia lugha ya kawaida kabisa na hata kuajiri mifano ilozoeleka sana katika jamii yetu tunamoishi ili UJUMBE AMBAO OTHERWISE INAONEKANA KUWA NI MZITO kueleweka ipate kufikishwa kiurahisi zaidi.

Ukumbuke kwamba kutoka hapa jamvini JF, kwa taarifa yako tu, watu wengi sana hufutilia mijadala yetu na hata kuyafyatua kwa nakala nyingi tuu na kuzitumia kuelimishia umma juu ya mambo mbali mbali yanayotuhusu. Juzi tu nimeshuhudia mjadala kule Mbagala Zakhiem juu ya hoja ya Mhe Lema kudhalilishwa na vyombo vya dola na wananchi kubadilishana hisia kalikali juu ya hili.

Niliposogelea kupata upepo ukoje ajabu nikaanza kuona vija fulani kama watatu hivi kila wakizungumza wanaonekana kufululiza kwa sana mawazo niliowahi kuyasoma humu humu jamvini. Ikabidi niendelee kuburudishwa bila kuona sababu zozote kujitambulisha kwao kama mwana jamvini.

Kila nilipouliza kaswali kupima mambo fulani fulani juu ya mada hii ndipo nikapata kuridhika kwamba mijadala yetu ni vema yakawa kwa lugha nyepesi kweli kwa sababu tunahudumia jamii pana sana bila sisi kulitambua hilo humu.
 
Back
Top Bottom