Nonda,
..suala la kujitambulisha kama Mtanzania au Mtanganyika ni suala ambalo naweza kusema ni la "mafundisho" na "mapokeo."
..binafsi nimezaliwa na kukulia Arusha, lakini wazazi wangu wamezaliwa mkoa mwingine.
..sasa kutokana na mafundisho na malezi ya ndani ya nyumba yetu, leo hii ukiniuliza natokea mkoa gani ktk Tanzania/Tanganyika, bila shaka yoyote ile nitakwambia nimetokea kule walikozaliwa wazazi wangu.
..kutokana na experience yangu hiyo, ndiyo maana nime-conclude kwamba, kwa wenzetu wa-Zanzibari hazikufanyika juhudi zozote zile za kuwaelimisha kwamba baada ya muungano basi ni vema wakachukua identity/utaifa mpya wa TANZANIA.
..naamini pia kuna mambo mengi ya KIHISTORIA na KISIASA yaliyosababisha muungano wetu uchukue sura iliyoko sasa hivi. kwa mfano, kuna tetesi za Wazanzibari kuogopa "kumezwa" kama kikwazo cha kuwa na nchi moja, serikali moja.
..kwa kweli kipengele hicho hapo juu sina jibu la uhakika la kukutosheleza. lakini ngoja nijaribu:
..je, tuna uhakika kwamba Rwanda,Burundi, etc hawajaomba kujiunga nasi kutokana na kuona matatizo tuliyonayo sisi, au kutokana na matatizo yao wenyewe, haswa ya viongozi wao?
..is it easy kwa kiongozi aliyekwisha onja madaraka ya Uraisi, akaitumbukiza nchi yake ktk muungano, huku yeye akiwa hana uhakika na nafasi yake ktk muungano huo?
..kwa sababu tunaelewa kabisa kwamba kuna baadhi ya wananchi wa Rwanda na Burundi ambao ilibidi waondoshwe kwa nguvu kuwarudisha nchini kwao.
..binafsi nadhani wakati mwingine haya masuala ya kuunganisha nchi yanahitaji viongozi kuonyesha njia. vilevile zaidi ya viongozi kuonyesha njia kunatakiwa kuwepo na jitihada za makusudi na za muda mrefu kuhakikisha kwamba wananchi wanakubaliana na hatua zilizochukuliwa na viongozi wao. reference nzuri kwa hoja yangu hii ni matatizo yaliyotokea Yugoslavia.
..again, sina jibu la uhakika kwa swali lako hili. sijachimba vizuri kujua muungano kama wa USSR au ule Yugoslavia ulikuwa wa namna gani.
..inawezekana ukawa na hoja kwamba hakuna muungano ambao umefanikiwa kuzifuta nchi zilizounda muungano huo.
..lakini haya vilevile ni masuala ya kisiasa na kijamii. kushindwa kwa mataifa mengine kuungana na kuunda utaifa mpya, isiwe kisingizio cha wa-Tanganyika, au wa-Zanzibari, kuukana u-Tanzania. nini kinachotuzuia sisi kuwa wa kwanza, na mataifa mengine kuiga kutoka kwetu?
Nilikuunga mkono kwa hoja zako lakini hili la kufikiri kuwa Watanganyika wanajiona kuwa ni Watanzania na Wazanzibari wanajiona ni Wazanzibari halitokani na kazi ya kuelimisha bali inatokana na mfumo wenyewe wa Muungano wetu ulivyo.
Unategemea nini iwapo Tanganyika iliamuwa kubadili jina tu na kujiita Tanganyika na kubaki na kila kitu chake. Unafikiri jina lina maana katika Utaifa, Chukulia Congo (Zaire) hakuna anaejali iwapo Zaire au Jamhuri ya Congo mradi imeshaamuliwa hivyo. Watanganyika wanataka nini kuitwa Watanganyika wakati kila kitu cha Tanganyika kimo ndani ya hiyo inayoitwa Tanzania? Wanakosa nini kwa kujiunga na Zanzibar? Jawabu ni kuwa hakuna!
Sasa natuje kwa upande wa Zanzibar na tuone kama kweli ni kutooelimishwa au kumefanywa makusudi kuwafanya watu wa visiwa hivi wabaki kama Wazanzibari. Msingi wa Zanzibar kujitia katika umoja huu haukuwa hata siku moja kuwa na lengo la kuiondowa Zanzibar bali ni kutafuta usalama kwa taifa changa. Tamko la Serikali mbili kwenda moja halikuwahi kutamkwa na Kiongozi wa Zanzibar zaidi alishawahi kutamka matamko ya kuonesha kuwa Muungano huu ni wa makubaliano ya muda na hali isiporidhisha basi uvunjwe.
Itakuwaje pia kuiachia Zanzibar na Rais wake na vyombo vyake kamili vya dola halafu utegemee kuwa Zanzibar kama utaifa uondoke? Si ukosefu wa kutoelimishwa bali ukweli halisi wa mambo ndio uanaowafanya Zanzibar waendelee kujiona ni Wazanzibari. Kwani wananchi wa Zanzibar huhudumiwa na serikali gani? Ni Serikali ya Zanzibar ndiyo mtoto wa Visiwani huwa anafunulia macho, ni Rais wa Zanzibar ndie raisi wake, ni wizara za serikali za Zanzibar ndio zinazomuhudumia, sasa unategemea ajihisi vipi kama si Mzanzibari? Mtoto huyu kila anapokuwa anasikia na kusoma kero zinazosababishwa na Muungano huu kwa Visiwa hivi bado unategemea ataona fahari kwa Tanzania?
Watanganyika hawaitaki Tanganyika yao kwa vile kwa kurudi kwa jina la Tanganyika itabidi nao wabanane na wenzao wa zanzibar katika Serikali ya Muungano. Hivi sasa kwa kuvaa koti la Tanzania wanapata na kufanya yao na ya wenzao (Zanzibar). Sifikiri ni busara kuachia bure hii!