Vunja Zenj tubaki na serikali moja!
Gharama za uendeshaji zitapungua na tutakuwa na umoja wa ukweli!
 
Vunja Zenj tubaki na serikali moja!
Gharama za uendeshaji zitapungua na tutakuwa na umoja wa ukweli!
Mkuu,

Unaelewa kuwa zenj wamefanya mabadiliko ya katiba yao?
Inakubidi uyapitie,uyasome uone kama wako tayari kuvunja Zenj.

Zamani kipengele kimoja kilikuwa kinasomeka Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Sasa hivi kinasomeka Zanzibar ni moja ya kati ya nchi mbili zilizounda Muungano wa Tanzania.

Kauli ya Pinda ndiyo iliyopelekea mabadiliko hayo, sasa hii yako sijui itawafanya waje na nini.

Jitahidi uyatie maneno yako katika kinywa cha Pinda, halafu yeye ayaseme kule bungeni halafu usikilize wazenj watakavyopiga taarabu.
 
Kula tano hapo!! Hiyo ndio njia pekee murua zaidi na sahihi kuboresha UMOJA WETU WA KITAIFA.

Mkuu,

Wewe na YeshuaHaMelech muna mawazo mazuri.If it is a wish,it is a good wish lakini basi haya ni mawazo yetu sisi tu wa upande mmoja. Je wenzetu wa Zenj wana mawazo gani?

Nafikiri tatizo hasa linaloukabili Muungano wetu ni hili la sisi huku bara ku-dictate kila kitu kinachohusu muungano na tumeacha ku-negotiate na wazenj. Hiki ndio chanzo cha msuguano uliopo na wazenj. Tusisahau kuwa huu ni muungano wa equal members; Tanganyika na Zanzibar.

Mimi nataka nitofautiane na wewe katika approach ya njia murua na sahihi. Mimi naona njia murua na sahihi ni kwa serikali ya muungano na ile ya Zanzibar kuwa wawazi katika mjadala wa Muungano. Wafungue mjadala wa kitaifa kuhusu muungano. Watu, wananchi wajisikie huru kuuchambua na kuudadisi muungano.

Halafu, ipigwe kura ya maoni kuhusu muungano na muundo wake. Hii ndio njia murua na sahihi. Hivi sasa kila kitu kinafanywa kisiri siri, unasikia tu kuna tume ya pamoja, kuna kamati ya kero za muungano.

Mwananchi wa kawaida haelewi nini kinaendelea. Hali ambayo inajenga malalamiko na manung’uniko katika kila upande na kila mtu.

Kura ya maoni kuhusu muungano na muundo wake ndio njia murua na sahihi.
 
Wao waki-dictate sawa, sisi hatuna haki...mhh!! Sounds like double standard!
Anyway, kama kweli umoja unahitajika either tuwe na serikali 3 (impractical) au tuwe na moja (practical). Hatuhitaji kuwa na nchi mbili, hilo ni kosa tangu enzi za Nyerere na ni vema likarekebishwa. Ila wazenj sometimes huwa wananiboa kwa ulalamishi usio na tija!
 

Mistari miwili ya mwisho brother you are right.
Laiti ukikaa na Wazenji, huwa wanaona kama wao ni koloni la Tanganyika,
Huona kama Tanganjika sory Tanzania bara ni kikwazo kwa wao kufanikiwa ktk mambo yao hasa kiuchumi.
La msingi atokee rais jasiri aanzishe mchakato wa kuuvunjilia mbali muungano kama kushirikiana tushirikiane tu kila nchi itakapokuwa kivyake.
Wazenji wanalalamika mno bana.
 
Vunja Zenj tubaki na serikali moja!
Gharama za uendeshaji zitapungua na tutakuwa na umoja wa ukweli!
mitego na ujanja wa Njerere na Wa Tanganyika wa kulivunja Taifa la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar iliwashinda hadi Mr Julius mZee wa aZimio La Arusha wa siasa za Ujamaa na kujitegemea ilifikia wakati wa kifo chake na styl hakufanikiwa kuli Vunjaaa Taifa La wa Zenji...Wa Zanzibari Taifa lao litakuwepo hadi mwisho wa Dunia hiiii na wataji tambulisha na ku Proud kama wao ni Wa Zanzibari na walipata uhuru wao kutoka kwa muengereza British monarch on December 1963!!! Wa Zanzibari Agenda yao na mipango yao mikubwa ni kulirudisha Taifa lao kama lilivyokuwa hapo zamani before ya kuvamiwa na wa Tanganyika katika Nchi yao na Mipaka yao!!!!!! wa Zanzibar watarudisha Taifa lao kamili na kiti chao ndani ya United Nation (UN) KAMA Ilivyokuwa hapo zamani kabla ya kufanya Muungano na Tanganyika!!! Ni mambo kidogo tu na machache waliyobakisha Wa Zanzibar Kulirudisha Taifa lao Kamili na DOLA yao UHURU...Wafuatiliee Habariiiiii Zao Upate kuchemsha Bongoooo:A S-alert1:
 


Tanzania ilipata uhuru lini? kutoka kwa nani?
Nauliza hivyo kwa sababu Tanganyika ilipata uhuru Desemba 9 1961. Uhuru wa Tanzania unanipa utata, labda historia inanipiga chenga.
 

Sadakta mwanangu heri ya wote wanaoliunga mkono! kwa wasio ona tuwaonyeshe kuwa hili ni BOMU na litalipuka wakati wowote TATIZO ni wanasiasa mf leo mtu ni rais wa tanzania anaona dhahiri tanzania ikifa atakuwa raisi wa nchi gani? hajui hatma yake itakuwa vipi!
 

Mkuu,

Nipe mfano au mifano ya wazenj Ku-dictate. Kitu gani au jambo gani ambalo wao wame-dictate kwetu?

Ukinipa mfano wa mabadiliko ya karibuni ya katiba itakuwa si sahihi,kwani ni CCM ndio walikuja na rai ya kura ya maoni.

Mimi najua mifano michache ambayo sisi tunajifanyia tu mambo na kuwaburuza wao.

Moja,Kuwachagulia nani aongoze Zanzibar.

Mbili, marekebisho ya katiba ambayo yalimuondoshea rais wa zanzibar kuwa makamo wa rais wa TZ

Tatu, Uundwaji wa TRA na ufanyajikazi wake.

Shirika la uchimbaji wa mafuta kujipa hadhi ya kimuungano bila ya ridhaa ya Zanzibar.

Ushirikiano wa kimataifa, kuongezwa katika wizara ya mambo ya nje ili ku-preempt Zanzibar kuwa lazima ipitie Wizara ya mambo ya nje hata kwa mambo ambayo si ya muungano.

Kama haya yote , tunayafanya basi ni lazima wazenj watalalama tu, watapiga kelele.

Siku ambayo tutakubali kuwa Zanzibar ni washiriki sawa katika Muungano basi kelele zitapungua au kwisha, kwa sababu tutakuwa tuna-negotiate nao na sio kuwaburuza, ku-dictate.

Vyenginevyo ni vyema kuuvunja ,halafu Tanganyika na Zanzibar kujiuanga EAC kama individual members kama ilivyofanya Rwanda na Burundi.

Sisi kama Tanzania hatukubali Kenya au Uganda kutuburuza katika EAC. We negotiate.
Vipi leo tutegemee kuwa Wazenj watakubali kuitikia yes, boss!.tumewajengea mazingira ya kulalamika. Tuyaondoshe!
 

Mkuu,

Hapo kweye red nafikiri kuna kaukweli ndani yake.
Unajuwa katika eneo dogo la Zanzibar(Unguja na Pemba) kuna more that 20 kambi za Jeshi.

Kwa nini iwe hivyo?
Kam huelewi , fikiria kauli ya CCM,”ushindi ni lazima, mapinduzi daiama”
 
Duh! Hili la Zanzibar kuwa mama una hakina nalo? Na huyu Baba sasa naona kwa kumkosa mama anatafuta la witi kwa mababa mengine (Kenya na Uganda.
 


Hana lolote huyu na kwa kujua hilo ndio akakurupuka. Unatumia akili iwapo jambo ni serious kwako!
 

Unajuwa nini ? Wewe huwa unatuchefua kwa husuda zako!!
 

Kibaraka! Umegusa ndipo hasa! hayo unayoyafikiria na kuona kama ni chumvi ni ukweli ni ukweli hasa. Nyiny ni watawala na ni kiwazo kama mlivyo mkoloni yoyote ulimwenguni!i
 
there are few associations that kept the word Tanganyika and it reminds me that Tanganyika just exists and soon it will regain independence from Tanzania.

On my list
  1. Tanganyika Farmers Association
  2. Tanganyika Law Society
  3. Tanganyika Instant Cofee Ltd
 
Tunaukaribisha uhuru wa Tanganyika kwa mikono saba.

Thats a matured attitude.There is nothing wrong to have Tanganyika/Zanzibar as separate nation(s).That will provide more room and focus in eradicating hunger instead of dealing with complexity of union matters.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…