Jee Muungano una faida au hasara kwa Zanzibar YES/NO?
Hii ni haki ya kila Mzanzibar kujiuliza na kutowa rai ya kufanya ili tutatuke katika jambo gumu hili? Wznz tuweke pembeni utashi wa vyama kwa vile vyama vyote vina wafuwasi Zanzibar na Tanganyika?lakini jambo la Utaifa na Uzanzibar unawahusu Wzanzibar tu na hatma ya nchi yao na kizazi chao cha baadae.
Kwa maoni yangu mimi binafsi ukiniuliza faida na hasara nitakwambia hasara ni nyingi kuliko faida, na nasema hivi sio kwamba sipendi tungane au siwapendi Wtanganyika no. Mimi naona Wzanzibar tuna mapenzi zaidi kuliko ndugu zetu waTanganyika walivyo, na kuna mifano mingi hai inaonyesha sisi tuulivyoo wastahamilivu na kuvumilia mengi ? Lakini inaonekana upole wetu na ukarimu wetu wenzetu ndio hushukuwa advantage ya kuimeza nchi yetu kidogo x2 kwa kutumia kigezo cha Muungano na katiba ya Tanganyika ambayo ndio hii ya Tanzania imefanyiwa marekebisha kidogo tu.
Kama kwela ndugu zetu wa Tanganyika wangekuwa na nia safi na Muungano wangeweza Kuufuata makubaliano halali ya Muungano(Artcle of Union) waliokubaliana wasisi wawili Rais wa Tanganyika Julias Kambarage Nyerere na Rais wa Zanzibar Mh Abedi Amani Karume lakini wapi?.
Nikipindi kifupi tu bada ya kufariki Mh Abedi Amani Karume ndipo Rais wa Watu wa Tanganyika akanza kutubadilikia na kujifanya Super power Baba wa Taifa Mama Kafaa?.
Jambo kubwa Wzanzibar lililo tutia shaka na kutushtuwa ni pale Wenzetu Ndugu zetu Wtanganyika walipo itana na kuwa kitu kimoja na kuitisha Bunge lao la Tanganyika likiongozwa na Rais wa Tanganyika Julias, Na kwa nia yao mbaya ya kutaka kutukolonazi na kuimeza Zanzibar kimipango, ni kumsikiliza Nyerere kuwa kila balipo andikwa Tanganyika andikeni Tanzania na Tanganyika ikavaa Koti la Tanzania na Katiba ya Tanganyika ikafanyiwa marekebicho ikawa ndio hii ya Tanzania na nembo zote za Tanganyika kineme Adam na Hawa ndio hizi za Tanzania.
Huu ndio ujanja wao waliohisi Utafanyaa kazi kuimeza Zanzibar ktka Tumbo la Tanganyika ambayo ndio hii Tanzania kilisho badilika ni jina tu Nisawa na Zaire kuita Kongo au Kusema Paka kanywa mchuzi,mchuzi umenywewa na Paka ni imla hio hio tu.
Kuanzia hapo Nyerere akatukuzwa na watu wake kuwa Papa wa Taifa la Tanzania ambayo ni Tanganyika na Mipaka ya Tanzania ikawa ni Tanganyika Bara na Tanganyika visiwani?.
Baada ya hapo ikawa Zanzibar inanyoyolewa kwa kutumia katiba ya Tanganyika kwa faida ya Watanganyika na Wzanzibar tukaanza kugonganishwa vishwa vya Usultani,uwarabu,upemba na Unguja na mwisho mapinduzi daima lakini wenzetu wana lengo jengine.
Kwa hio hivi sasa Wzanzibar tumeungana na tumejifunza mingi na hatuko tayari kukaribisha fitna zakutugawa hazina nafasi tena na kiwiliwili cha kila Zanzibar hivi sasa nikimoja tu na nikupigana na aduwi fitna na kudai maslahi ya nchi yetu kwanza kwa faida ya kizazi shetu.
Ukitaka ujuwe kuwa Wtanganyika lao moja awe ccm,awe cuf awe Chadema,awe Muislam awe mkristo lao moja, mimi nashangazwa na Chadema eti wanasema cuf wamevuja katiba ya Muungano ambayo sera yake ni Serekali mbili kuelekea moja 2-1? Na hivi juzi ktk Kongamaano la Prof Shevi na Jeneral Ulimwengu wanasema Zanzibar imeshavunja makubaliano ya Muungano ni pale ilipobadilisha Katiba kifungu no 10 kinasho sema Rais wa Zanzibar ni Rais na mipaka yake ya nchi na mikowa yake? Kwa hio imevunja Muungano tayari. Sasa Wzanzibar tunasema kidogo ya Wzanzibar ni udogo wa Nyuki kujenga asali na wingi wenu ni Wanzi hauna faida yoyote ile.
Njoni Zanzibar tuwafundishe maisha, na ikiwa tumeshavunja Muungano na katiba ya Muungano Jee nyiyi mumefanya nini?nyiyi mumejisahau na Papa wenu wa Taifa na kuiuwa Tanganyika yenu na katiba ya yenu kwa Zamira yakuimeza Zanzibar kirahisi? Yaguuju Zanzibar ipo kabla ya Tanganyika na historia ya Zanzibar katu kufa na ndio itakayo wasuta. Kama uhuru wa Tanganyika ndio wa Tanzania muta jiju.sisi hivi sasa tunavuta kamba moja na ishaallah M/mungu atatusaidia kwa haki yetu kututoka.Mungu ibariki Zanzibar.

Jee nembo hii ya Adam na Hawa si ile ya Tanganyika kabla ya Muungano?huyu ni Rais wa Tanganyika na katiba mulionayo ni ile ile ya Tanganyika musitudanganye
