abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
FIKIRIA unahisi vipi unapokuwa unapita katika vichochoro vya mitaa ya Zanzibar na kumkuta mtoto mdogo amekaa nje ya nyumba yao anachezea mchanga na wenzake.
Inawezekana wakati huo mzazi au mlezi wake huwa anafua nguo za huyo mtoto au anamtayarishia chakula chake kabla ya kuanza kulia, kama ishara ya kuonyesha kuwa ana njaa.
Ukifikiria zaidi utaweza kukumbuka, ijapokuwa kwa mbali, kuwa na wewe ulipokuwa mdogo kama yeye, ulifurahia sana mchezo kama alivyokuwa yule mtoto aliyekuwa anachezea mchanga kwani kwa mtoto mdogo mchezo ndio furaha yake ya maisha.
Lakini mara baada ya kuachana nacho hicho kitoto, mara unasikia kelele za mtoto analia na unaporudi nyuma kuangalia unakikuta kile kitoto uliokuwa ukikiangalia na kujikumbusha zama za utoto wako, kinagaragara chini na damu imetapakaa mkononi mwake.
Unashangaa kwa vile sekunde chache kabla ulikiona kile kitoto kinachezea mchanga kwa kuutia kwenye kifuu na kumimina chini na kurudia hivyo mara mbili au tatu.
Kwanza unafikiria labda amejikata na kitu kikali. Kumbe si hivyo, bali katokea kiumbe katili na jahili aliyeamua si tu kumnyima raha ya mchezo yule mtoto kwa wakati ule, bali raha katika maisha yake yote. Kilichotokea ni kwa huyo jahili kumdunga yule mtoto sindano iliyokuwa haina damu salama, ili amuambukize virusi vya ukimwi.
Huu ndiyo unyama na ujahili wa aina yake unaosemekana kutokea katika baadhi ya sehemu za mji wa Zanzibar katika siku za hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa ya kipindi cha matukio mbalimbali kijulikanacho kama Mawio cha Sauti ya Tanzania Zanzibar, matukio mawili ya aina hii yameripotiwa.
Wazimu huu mpya wa baadhi ya vijana ni unyama usiokuwa na kifani na tabu kuufikiria na kuamini. Hivi watoto wa miaka miwili au mitatu wamefanya kosa gani hata kupewa hiki unachoweza kukiita adhabu ya kifo?
Lakini ukichunguza kwa undani utagunduwa kuwa huu ni mtiririko wa kuendelea kwa kasi kuporomoka kwa utu, imani, huruma na maadili Visiwani. Lakini kiwango cha mporomoko huo kilichoonekana hivi karibuni si tu ni cha kusikitisha, bali ni cha kutisha.
Iwapo haitadhibitiwa haraka hali hii, na iwapo itafanyiwa mzaha wa kuonekana kama mchezo wa kuigiza, inaweza kuwa na athari kubwa hapo baadaye kwa Zanzibar. Kwanza inawezekana ikasababisha watoto wengi Visiwani kuambukizwa virusi vya ukimwi na hawa wendawazimu wanaosaka watoto wadogo ili wawadunge sindano za damu yenye virusi vya ukimwi.
Kwa vyovyote vile, matukio haya yatasababisha wazazi kuanza kufungia watoto wao majumbani kama ndege waliomo kwenye tundu, hali ambayo itawakosesha watoto wadogo raha yao ya kucheza kutokana na wazazi kuhofia kwamba hata nje ya nyumba zao si tena salama.
Hili suala ni zito sana na linahitaji kushughulikiwa kwa haraka sana na kwa nguvu zote, si tu za kisheria, bali pamoja na wana jamii wa Visiwani kushirikiana kuwabana hawa majahili wanaofanya unyama huu wa kuhatarisha maisha ya watoto wadogo.
Kwa muda mrefu imani na maadili ya watu wa Visiwani yamekuwa yakiporomoka kwa kasi ya aina yake na kuja kwa huu unaoitwa unga, yaani mihadarati, ndio kumeongeza zaidi hiyo kasi.
Hivi sasa katika kila pembe ya mji wa Zanzibar wapo vijana walioathirika na dawa hizi hatari na wanaonekana wakisinzia ovyo na udenda kuwatoka kama kuku wenye kideri. Maeneo mengi wanayokaa vijana hawa wanaotumia dawa hizi hatari na kuitwa Colombia, Peshawar, Kandahar na Jalalbad yanaeleweka vizuri.
Kama vijana wanaotumia mihadarati wanajua wapi wanaweza kuzinunua, inakuwaje iwe shida kwa askari polisi kufahamu dawa hizi hatari zinauzwa wapi?
Lilio baya zaidi, kama matukio ya kuwadunga sindano za damu yenye virusi vya ukimwi hawa watoto wadogo wasiokuwa na hatia, ni kuwa baada ya hawa vijana waotumia mihadarati kuathirika na maisha yao kuvurugika, wao sasa wameamua kumaliza maisha ya watoto wadogo.
Kama watu wa Visiwani wamekuwa wakiona taabu kuwabana wanaoziingiza dawa hizi nchini, wanaoziuza na wanazozitumia kwa vile ni jamaa, ndugu na marafiki zao, sasa waelewe kuwa mbali ya kuwa na vijana wengi kuharibikiwa akili madhara ya dawa hizi sasa yanahatarisha maisha ya hata watoto wadogo ambao hata hayo maisha yenyewe bado hawayajui.
Jamii inapaswa ielewe kuwa kama upo wakati wa kusema adui mkubwa wa Zanzibar hivi sasa ni hizi mihadarati na si jambo jingine lolote lile basi ni huu. Ni lazima mapambano dhidi ya dawa hizi hatari yakolezwe moto na pasiwepo na huruma kwa vile hao wanaoonewa huruma sasa wanafanya ujahili na unyama wa hali ya juu.
Katika miaka ya nyuma, mtoto Visiwani alilelewa na watu wote mtaani na mzee aliweza kumuacha mwanawe nyumba ya jirani bila ya wasiwasi na kuangaliwa ipasavyo na majirani na wapita njia. Kinachoonekana sasa ni kuwa kumuacha mtoto acheze nje ya nyumba ni kosa na kuhatarisha maisha yake.
Ni vizuri kwa Wazanzibari kuitafakari hali hii ya kusikitisha na kutisha kwa makini na kuchukuwa hatua madhubuti za kuwabana wanyama hawa wanaohatarisha maisha ya watoto kabla ya kila mzazi katika nyumba kubaki analia.
Hii ni changamoto nyingine kwa Jeshi la Polisi. Ni kweli hivi sasa Jeshi la Polisi lina kazi kubwa ya kulinda usalama wa raia na mali zao, lakini huu usalama wa watoto wadogo unapaswa kupewa umuhimu mkubwa.
Lakini itakuwa ni kosa kutegemea askari polisi peke yao kuweza kuifanya kazi hii kwa uadilifu na ukamilifu. Wanajamii lazima watoe ushirikiano na wao wenyewe wafanye juhudi za kuwasaka wanaofanya ushenzi huu.
Tukumbuke kuwa watoto, kutokana na umri wao mdogo, akili zao zikiwa bado hazijakamilika na udhaifu wao wa mwili, hawawezi kujilinda wenyewe. Ni wajibu wa kila mtu kuchangia kuwalinda kwa hali na mali.
Hili ni jukumu la kila mtu, mzazi na kila mwenye kuthamini maisha. Unyama huu lazima ukomeshwe haraka.