Naanza kura yangu.........................TUVUNJE MUUNGANO,WATUACHIE KATANGANYIKA KETU.....
 
Hayo yote wangaliyajua wananchi wa Zanzibar labda wasingepiga kelele za kunyonywa wakiwa ndani ya muungano!

Kudai Zanzibar huru ni hoja isiyo na mashiko kwa raia wa Wete, Pemba. Zanzibar huru inadaiwa na wanasiasa, walichofanya ni kuwapandikiza wananchi hayo mawazo ya kukandamizwa. Viongozi wa zenji wanautaka uhuru ili wawe marais, mawaziri wakuu, na mawaziri wanaotambulika duniani na kupewa red carpet services wanazozikosa under Muungano. Kwa mwananchi wa kawaida, kuwa au kutokuwa ndani ya Muungano hakujawa na faida yoyote.
 
Nafikiri kama ni mtumiaji wa akili yako utaona kuwa huna hoja ya msingi hapa
 
Wakati tunasema bila ya kuamini kuwa Wazenj hawautaki Muungano, Je watanganyika na wao wana msimamo gani kuhusu Muungano. Watanganyika ndio wengi kwa idadi sasa kama watanganyika hatuutaki Muungano mbona tuko kimya? Tunasema tu wazenj ni mzigo, tunawabeba. Je tunapenda mzigo? Je tunapenda kuwabeba wazenj?

Mkuu Zaidi ya Rev. Mtikila na ile move ya G55 nani katika Tanganyika anasema hautaki muungano na amechukua hatua gani?

Umesema wanasiasa wanaogopa..hata CHADEMA nao wanaogopa kuzungumzia Muungano?

Kwa maoni yangu wakifanya hivyo itakuwa njia rahisi ya kupata kuungwa mkono Zanzibar. Waseme CHADEMA wata-negotiate upya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. au waseme bila kuuma meno kuwa CHADEMA watairudisha Tanganyika ili members wa Muungano wapate nafasi ya kujadili Muungano kwa uwazi....Pengine kusema kuwa watauvunja muungano kwa sasa wanaweza kumpa sababu Tendwa kukifuta lakini hizo kauli za mwanzo zitawapa wafuasi wengi Zanzibar.

Kilicho wazi ni kuwa kuna siri kubwa ya Muungano ambayo inaonekana CCM wanaijua na ndio wanalifanya suala la muungano kuwa ni nyeti na lisiguswe.

Katika arrangement ya sasa Tanganyika inatumia mamlaka ya Muungano katika hali zote,wakati Zanzibar wanalazimika kupitia serikali ya Muungano. Je kuna faida kubwa Zaidi kuliko hii kwa Tanganyika?
Huu muingiliano wa serikali ya tanganyika,kuwa ndio hiyo hiyo serikali ya muungano ndio inayowapa mwanya wazenj kusema wanaminywa,wanabanwa na kuna ukweli katika hilo. ni serikali ya Muungano ndio ina mamlaka ya mambo ya nje.

Zamani ushirikiano wa kimataifa haukuwa katika Muungano lakini sasa hili pia limeingizwa katika Muungano na hivyo kuifanya Zanzibar isiwe na uwezo wa kutafuta washirika au wabia au misaada kwa mambo yale yasiyo ya muungano wao wenyewe.kwani ni lazima wapitie Muungano.

Inawezekana sisi hatuzioni faida wazi wazi za muungano zaidi ya bughudha za wazenj na kuwabeba lakini Zanzibar wakiwa nje ya muungano au Tanganyika pia ikiwa na serikali yake inayoonekana wazi basi tutaweza kuchanganua vizuri juu ya nani anafaidika zaidi na Muungano.

Ikitokea hivyo kutakuwa kuna mfumo wa majadiliano katika pande mbili ambazo zitaamua mamlaka yepi yawe kwa serikali ya Muungano na mamlaka yepi yabaki kwa serikali ya tanganyika na yepi yabaki kwa serikali ya Zanzibar.kutakuwa na mipaka ya kimamlaka inayoeleweka. sasa hivi ni shaghala baghala tu.

mkanganyo huu umezaa manung'uniko na kelele na sasa unajenga kejeli na chuki.
Siku ambayo watu wataamua kuzungumza kwa maana ya "kunegotiate" kama wabia wa Muungano basi kelele zitapungua.
 
Wewe nawe sijui umekunywa nini leo!
Unaonekana kama umekurupuka ghafla tu na kung'ang'ani Watanganyika...Watanganyika... Kama wewe ni raia wa kawaida mchango wako kuleta effect katika muundo wa muungano unazidiwa nguvu na mchango wa CUF kama chama. Unadhani watanganyika wamemzuia Seif Shariff kuitetea sera yake ya serikali tatu ndani ya serikali ya Umoja wa kitaifa?
CCM iliwafanya watanganyika kuamini kwamba safari ya Muungano ni serikali mbili kuelekea moja ndiyo maana ukaona watanganyika kutolalamikia muundo sana kama wewe. Sijui ni kwa sababu ya kuwa modest au kusoma sana lakini majority ya watanganyika hawapotezi sana muda wao kulalamikia swala hili isipokuwa wenzetu mnapoanza kutaja muundo ndiyo tunaanza kuwaona kama msioridhika maana hata huu muundo upo ili kupunguza malalamiko yenu juu ya kumezwa na Tanganyika.
If you ask me I'll tell you to end it right now because there is no way you guys will ever be satisfied with the union.
 
Nipeni faida za muungano wa tanganyika na zanzibar kuazia mwaka 1964 na hasara zake,na upande upi umefaidika na upi umepata hasara ,,,,,

Pia naomba mutathini faida kuanzia 1964 ikiwa nchi mbili hizi zingelikuwa hazina muungano,,,,jee zingelikuwa wapi ?

Mana naona wazalendo wa tanzania mumeshikiliza zanzibar ndio inafaidika kwa muungano hebu nipeni sababu ambazo tunazo faidika,,au wanaofaidika ni wachache wetu ambao kwa maslahi yao kama wabunge.

Ila nawaomba wazalendo waache kuleta hoja tunafaidika kwa mchele,nyama na viazi kwa sababu hizi sio hoja za msingi kutoka huo mchele na viazi hatuokoti huko bara,tunanunua,,,,pia hata hao wafanya biashara wazanzibari hapo tanganyika hata kama muungano hakuna basi kama wafanyaji biashara wangelifanya tu,wako wazanzbari msumbiji,uganda,kenya,congo.

Naomba leteni sababu za msingi musiropokwe.
 


Written by Nassor20 // 24/03/2011 // Habari // No comments

Ama kweli Muungano huu ni Muungano wapekee?,hivyo kweli Wzanzibar tuko tayari kufyonzwa na watu million 44 na kufunga ndowa bila Wali?
Katika kesi iliofunguliwa na Wzanzibar ktk mahakama kuu ya Zanzibar kutaka kujuwa jee kuna ushahidi wowote ktk Serekali ya Mapindudhi ya Zanzibar (SMZ)inayo sibitisha kimandishi yani Mkataba wa Muungano(Artcle of Union) kwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar kuwa Zanzibar iliungana na Tanganyika na makubaliano yalikuwa ni nini na nini hakuna?.
Jawabu la Mwanasheria wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mahkama kuu ya Zanzibar nikuwa hana mkataba wa Muungano ktk ofisi yake kabisa.
Sasa kinacho wachanganya akili Wzanzibar nikuwa Zanzibar hakuna mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ? na Tanganyika haipo wala watu wake hawaitaji? Inayo julikana ni Tanzania ambayo hata ungekuwepo huo mkataba basi neno Tanzania lisingalikuwemo?.
Mimi nauliza Wzanzibar wezangu na Watanganyika kwa ujumla huu utata wa Muungano na mkataba kuwa siri kubwa ya kufika hadi kuwa hata ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Zanzibar haupo tukiashilia lebrary zetu ? .
Mimi nahisi katiba sio kitu cha kujadiliwa hivi sasa kwa pande zote mbili ikiwa zina nia safi ya kuimaricha Muungano wa kweli.,chakujadiliwa hivi sasa ni makubaliano ya Muungano ili kuondowa utata uliokuwepo wa pande zote mbili husika za Muungano?.
Hivi sasa kila upande unapiga kelele kuwa Muungano haufanyi fair? Sasa kwa nini tusiwekane sawa kwanza kama kweli tuna nia kuwa pande zote mbili ziko wazi kwa hili?.
Vipi tuweze Wzanzibar kuingia ktk marekebicho ya katiba ya Muungano wakati mkataba wenyewe wa Muungano haupo wala hatujuwi kipi cha Muungano na kipi sio cha Muungano hii sio kujitundika kitanzi wenyewe?.
Kwa upande wetu sisi Wzanzibar tunasema Muungano hautushukulii sisi kuwa ni nchi ilio ungana na nchi,wenzetu tunahisi wanatushukulia kuwa ni sehemu moja tu ya Tanzania kama vile Mafya na Lindi ?wenzetu wana tu-jaji kutokana na udogo wan chi yetu na wananchi wake , Wakati sisi hatuko tayari kuungana kwa stayle hio hakuna mtu ulimwengu huu alako tayari kuza utu wan chi yake alio toka Babu na Bibi .
Na upande mwengine wa Tanganyika wao husema Zanzibar ni dogo na ina mamlaka yote ya nchi na power zote za kuwa nchi wakati sisi hatuna hata hio Tanganyika? Sasa ili kuwe na fair ya Muungano nilazima Tanganyika na katiba yake irudi kutatua utata huu wa Muungano kwa mambo yasio ya Muungano.
Ikiwa tutajadili katiba bila ya kuwa na Serekali 3 yani Tanganyika kwa mambo ya Tanganyika ya sio ya Muungano na Zanzibar kwa mambo ya Zanzibar yasio ya Muungano basi Muungano tunaweza kuenzi.
Lakini ikiwa Wenzetu wa Upande wapili hawato taka hivyo hio watataka kutujaji sie kwa udodo wan chi yetu na udogo wa watu wetu basi sisi hatuko tayari na Muungano huu na itafika pahali tutasema mamudhi ni kura ya maoni kuvunja Muungano na kila mtu kuwa na nchi yake? Sasa ikiwa Mutapinga mamuzi ya Wzanzibar kujitowa katika Muungano itakuwa ni kututawala kimabavu na tuta ji-declear kuwa tuko chini ya ukoloni wa Tanganyika.
 
Na Dkt. Harith Ghassany,
Wzanzibar tunafuatilia step moja moja ya mkataba wa Muungano ulivyo kwenda kimataifa tukigunduwa kuwa kulifanyika Fraud yaTanganyika ku-forgery Artcles of Union Internatinal Papes.
Ant-Union tutaishtaki Serekali ya Tanganyika kimataifa na hilo linafuatiliwa na Wzanzibar kila kona ya ulimwengu ukweli utazihiri tu.Hata kama Mwalimu amesha fariki wako waloko hai kwa pande zote za Muungano wataweza kueleza hatuwa zilivyo kwenda.
Mawasiliano yote kuhusu kiti cha Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar cha Umoja wa Mataifa yalifanywa na “Ministry of External Affairs, P.O.Box 9000, Dar es Salaam, United Republic of Tanganyika and Zanzibar”, kwa sababu kwa mujibu wa Khati za Muungano “Mambo ya Nchi za Nje” yalikuwa ni ya Muungano na Muungano ulikuwa ni wa Tanganyika na Zanzibar, na kwa mpangilio huo, Tanganyika iliyatawala mawasiliano yote na Umoja wa Mataifa bila ya kuihusisha Zanzibar.
Kwenye “Interoffice Memorandum” yenye kichwa cha maneno “Registration of the Articles of Union between the Republic of Tanganyika and the People’s Republic of Zanzibar in accordance with article 102 of the Charter” ya tarehe 14 May 1964, Mr. Jose Rolz-Bennet, Deputy Chief de Cabinet alimuandikia C.A. Stravropoulos, Under-Secretary, Legal Counsel:
As you are aware, Article 102 of the Charter requires Member States to register all treaties by them “as soon as possible” with the Secretariat. The same Article also provides that unregistered treaties cannot be invoked before any organ of the United Nations. Although the sanction just mentioned has never, as far as I know, been enforce, I think that, in the interests of full compliance with the Charter, the attention of the Government of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar should be drawn to the registration requirement of Article 102 of the Charter with respect to the Agreement containing the Article of Union giving rise to the United Republic. I should therefore suggest that a cable along the following lines be sent by you to the TAB representative in Dar-es-Salaam for communication to the Government.
“PLEASE DRAW ATTENTION OF GOVERNMENT TO PROVISIONS OF ARTICLE 102 OF CHARTER REQUIRING UN MEMBERS TO REGISTER AS SOON AS POSSIBLE WITH SECRETARIAT AGREEMENTS CONCLUDED BY THEM, AS THIS REQUIREMENT APPLIES TO AGREEMENT CONTAINING ARTICLES OF UNION BETWEEN TANGANYIKA AND ZANZIBAR. REGULATIONS TO GIVE EFFECT TO ARTCLE 102 OF CHARTER REQUIRE REGISTERING GOVERNMENT TO SUBMIT TO SECRETARIAT ONE COPY OF AGREEMENT CERTIFIED (my emphasis) TO EFFECT IT IS TRUE (my emphasis) AND COMPLETE COPY INCLUDING ALL RESERVATIONS (my emphasis) MADE BY PARTIES THERETO (my emphasis), TWO ADDITIONAL COPIES OF AGREEMENT, AND STATEMENT REGARDING DATE AND METHOD OF ENTRY INTO FORCE.”
Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilitakiwa izisajili Khati za Muungano kunako Seketeriet ya Umoja wa Mataifa, na si kuzisajili tu, bali hizo Khati za Muungano zithibitishwe na pande mbili za Muungano, yaani Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Serikali ya Watu wa Zanzibar, kama ni za kweli, yaani si za bandia, na kama kuna jambo lolote ambalo upande mmoja haujarithika nalo litoe maelezo. Memorandum hiyo iliandikwa tarehe 14 Mei 1964 na Muungano ulifanyika tarehe 26 Aprili 1964. Yote hayakufanywa.
Kwa mujibu wa barua pepe ya majibu kwa mwandishi huyu ya tarehe 25 March 2009 kutoka kwa Bwana Andrei Kolomoets wa Ofisi ya Mambo ya Kisheria ya Umoja wa Mataifa, hakuna ushahidi kama usajili huo ulifanywa na Serikali ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar huko Umoja wa Mataifa. Na kwa mujibu wa maneno ya hapa chini, ni kuwa kama ulifanyika basi kungelikuwa na kumbukumbu kwenye DB (database) na shahada ya usajili ingeliambatanishwa. Bwana Andrei ameangalia na amenijibu kuwa hakuna kitu kama hicho:
There is no evidence that the Articles of Union were ever registered with
the UN Secretariat.
Had it been the case, there would have been a record in the DB with the
registration certificate attached.
I checked, it’s not there.
Andrei Kolomoets
Legal Information Officer, Treaty Section,
Office of Legal Affairs
United Nations, Office S-3200E, New York, NY 10017
 
ya nini kuhangaika kote huko.. kama hamuutaki muungano si tangazeni kwamba muungano basi.. kuliko kukimbia huku na kule!!
 
ya nini kuhangaika kote huko.. kama hamuutaki muungano si tangazeni kwamba muungano basi.. kuliko kukimbia huku na kule!!

Kwa ni hujajua tu kuwa Muungano Wzanzibar hatuutaki na tunaushukia kupita kiasi lakini bado mumetupiga kabari ya roho?. Muungano unaishi Zanzibar kwa kundi dogo tu la ccm likilindwa na vikosi maulu vya uvamizi vya JWTZ lakini bado tuko katika kupapatuwa kuitowa kabari na kuwa huru.
 
Muungano uliundw lini 1964? hadi sasa mlikuwa wapi siku zote hizo
 
@abrulahsaf: mimi sijui Kama wazenji hatuutaki muungano nafikiri kitu chengine tunachotaka ni kunufaika zaidi na huo muungano! Vinginevyo tungekwushe jitoa siku nyingi tu! Sasa Kama ni mafao ya muungano basi kila mtu anataka zaidi ! Hebu tufanye kura ya maoni tanganyika na utagundua pia kwamba muungano wanaoutaka ni viongizi tu wa pande Mboni na raia wa kawaida hawanufaiki kwa sana! Wataukataa tu na haina haha kukimbilia UN ni kufanya maandanano kudai kura ya maoni scheme zote juu ya muungano huu!
 

Kaka Abd, ni lini vile tena uliniambia mnapanga kuleta ombi lenu la kujitenga na Tanganyika!!

Aisee liwahisheni upesi bwana, unajua raha jipe mwenyewe kuliko kujikomba na kupeleka chokochoko kwa jirani kupunguza maumivu

Liteni upesi msichelewe na sisi tutawaunga mkono kwa 100%
 

Nawatakia kila la heri mufanikiwe. The earlier the better.
 
Mimi hata sijakuelewa mkuu wangy kwa sababu imetafsiri kiingereza nakuongeza yako kama ilipozungumzia hati za bandia mara zinatakiwa hati mbili tofauti toka kila upande...
Nilichoelewa mimi hakuna maswala ya bandia wala hati mbili ila ni hati moja yenye kuwahusisha washiriki wa pande mbili..

Nachofahamu mimi Zanzibar ilikuwa nchi mwanachama wa UN na Tanganyika pia, hivyo huo muungano wao usingetambulika na UN kama artical 102 haikujazwa na ipaswavyo na kuwasilishwa UN...

Swala la nchi mbili kuungana halihusiani muda sawa na siku ya kuwakilisha UN kwa usajili wa nchi itakayotambulika kama ni ya muungano wa nchi mbili..

Na natambua pia UN isingeweza kuitambua serikali ya Ja,huri ya Muungano ikiwa vitu hivyo havikuwasilishwa, kwa maan hiyo unachotaka kusema kuna hila zimefanyika..

Hila ambazo hukuzitaja au pengine niseme Nyerere na Karume walicheza na UN kuisajili Tanzania pasipo kuwepo supporting documents...
Au labda mimi ndio nimekuelewwa vibaya..
 
Jamani kama kweli Muungano hamuutaki kwa nini wabunge wenu (CUF) hawapeleki hoja bungeni za kuvunja Muungano?? Msitudanganye ninyi...tunajua katika Muungano ninyi ndo wafaidika wakubwa!!
 
Tumechoka malalamiko ya wazanzibari kwenye mitandao, kama hamtaki muungano si muwaeleze viongozi wenu mujitenge hata leo. Watanganyika sidhani kama wana shida na zanzibar nchi yenyewe haina mbele wala nyuma.
 
Muungano uliundw lini 1964? hadi sasa mlikuwa wapi siku zote hizo


Elimu ilikuwa bado na ukichunguza sana wanadai huu Muungano ni WAPEMBA na ni baada ya kuelimika, kupata mateso na ubaguzi wa Elimu kutoka Unguja na kukimbilia Uingereza, Uholanzi n.k kama wakimbizi sasa ndio wamerudi na wanaanzisha ili vuguvugu, wenzao wa Unguja bado wanakula ROJO!
 
WaDanganyika wamezoea kuchakachua kila kitu hata article za Muungano.

Poleni sana WaDanganyika kwa kuzoea kwenu kudanganywa kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…