Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayo yote wangaliyajua wananchi wa Zanzibar labda wasingepiga kelele za kunyonywa wakiwa ndani ya muungano!
Nafikiri kama ni mtumiaji wa akili yako utaona kuwa huna hoja ya msingi hapaWazanzibar hawatakubali kwani Zanzibar inafaidika zaidi na muungano kuliko Tanganyika, muungano ukivunjika WAMEKWISHAA.
1. Wazanzibar/Wapemba wataomba uraia wa Tanganyika
Hilo halitokuwa kosa wala ajabu kwani kuna Watanzania chungu nzima walioomba uraia nchi za nje. That is natural. pia itakuwa kwa pande mbili kwani kuna Wabara wengi sana Zanzibar nao itabidi wafanye hivyo au sivyo?
2. Kiasi kikubwa cha chakula kinachoingia Z'Bar kinatoka Bara kwa uchumi walionao hawataweza kuagiza chakula kwa fedha za kigeni.
Si kweli kuwa kiasi kikubwa ya chakula kinatoka bara! Mchele unaagizwa mwingi kutoka nje ya Tanzania. hivyo hivyo kwa sukari na unga wa ngano. Sijui unafikiri kuwa kuagiza chakula ndio utegemezi? Mbiona Kenya , Uganda na rwanda na Burundi wanaagiza chakula kutoka Tanzania. Wazanzibari hawakuwa walaji wa maharage na Sembe kwa hivyo hawatoshindwa kuishi bila ya vyakula hivyo. By the way wakati huo itakuwa ni biashara ya makubaliano mbali ya kile kinachoitwa soko la Afrika Mashariki.
3. Umeme wanaoutumia toka bara wataweza kuulipia kwa gharama halisi? Mungu epusha, mgao wa umeme ukitokea serikali ya bara haitakubali kupeleka umeme Z"bar wakati wananchi wake wako gizani
Tatizo lenu Watanganyika mnapenda kujivutia kila kitu. Kwani huo umeme ni wa TANESCO au ni wa Serikali ya Tanzania na nini Tanzania? Mmekuwa mkipiga kelele sana kwa kitu cha pamoja yaani umeme. By the waya wengi wenu hamjui kanuni za biashara kuwa unaponunua bidhaa kwa wingi bei yake si sawa na ile ya rejareja. Zanzibar wananunua umeme kwa mkataba hivyo vitu viwili vinaenda pamoja. umiliki wa pamoja na mkataba wa kibiashara. Tatizo lenu matakwa yenu mnayaweka mbele bila ya kufikiri utaratibu na sheria.
4. Waheshimiwa wabunge wa Bunge la Tanzania toka Z'bar wakirudi kwao inakuwaje??
Iweje? Kwani hawa huwa hawapigiwi kura? Kama wanapigiwa kura basi kuna wengi walikuweko huko na sasa hawako lakini maisha yao yanaendelea. Au unataka kuniambia kuwa mapato binafsi ya Wabunge wa Zanzibar yanapelekwa Serikali ya Mapinduzi??
Hebu ongezeni athari/faida za kuvunjika muungano, nani atafaidika na nani atapata hasara, tupate picha kamili ikiwa kesho tunaingia katika zoezi la kupiga kura..
ya nini kuhangaika kote huko.. kama hamuutaki muungano si tangazeni kwamba muungano basi.. kuliko kukimbia huku na kule!!
Kwa ni hujajua tu kuwa Muungano Wzanzibar hatuutaki na tunaushukia kupita kiasi lakini bado mumetupiga kabari ya roho?. Muungano unaishi Zanzibar kwa kundi dogo tu la ccm likilindwa na vikosi maulu vya uvamizi vya JWTZ lakini bado tuko katika kupapatuwa kuitowa kabari na kuwa huru.
Muungano uliundw lini 1964? hadi sasa mlikuwa wapi siku zote hizo