Huwa nachukizwa sana na watanganyika wanaotetea huu muungano na Zanzibar. Zanzibar kwa nini asiachwe ajitemee mbona tuna ishi kwa amani na majirani wakorofi kama Kenya na Rwanda lakini tunaishi nao kwa amani na tunaheshimiana sote. Kwa nini Zanzibar anaitawala Tanganyika?
 
Kama kweli Zanzibar ni nchi basi wanaosema mtu katoka nchi ya zanzibar wapo sawa. Kama Zanzibar ni sehemu ya Tanzania basi sio nchi na hawana Uhuru wa kuitwa nchi. Zanzibar ingetakiwa kuwa na Governor au Mkuu wa mkoa lakini sio Raisi. Hili ndilo linachanganya watu na kuanza ku punic. Je zanzibar ni kama Puerto Rico ambayo ni sehemu ya USA lakini hawana nguvu kama nchi basi tuweke sawa.

Tatizo tulilonalo kila mtu anajua Zanzibar sio nchi lakini kwa kinafiki tuna kaa na kuita Zanzibar nchi!

Kama wewe unaamini Zanzibar ni nchi basi sio makosa mumuita mtu yeyote kwamba ni Raia wa Zanzibar. Lakini kama hatuamini hivyo basi tubadilishe sheria tuweke mambo sawa
 
MaCCM ndio hayataki kusikia Tanganyika huku yakizidi kuimega keki ya Tanganyika
 
Mwana wa Mungu ameamusha dude , mwamba kauli yake moja hapakaliki lissu hakuzaliwa kwa bahti mbaya
 
Nchi ni nini?

Na unaitafsiri Nchi kwa mujibu wa marejeo gani?

Je marejeo hayo yanakubaliwa na watu wote ambao wanajihusisha kwenye mjadala huu ?

Bila kupata muafaka wa hayo hapo juu hasa hiyo bolding basi hakutakuwa na muafaka wa mjadala huu
 
Ni nchi ambayo kupinduwa serikali si uhaini. Hii ni kwa mujibu wa Mahakama ya rufaa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…