sio kwamba haihitaji tu, ni kwamba Tanganyika haijawahi kufaidika na chochote toka Zanzibar,

1. Mzanzibar anamiliki ardhi hapa bara, sisi NO.
2. Mzanzibar anaajiriwa serikali Tanganyika, sisi kwao No.
3. Mzanzibar ana vitambulisho bara na visiwani, sisi bara tu. kule ni wageni.
4. kero za wazanzibar tu zinatatuliwa, zetu hazijawahi kutatuliwa. zitajeni kama zipo.
5...............the list goes on and on.
 
umeshawahi kufika zanzibar?kajionee mwenyewe kuna wabara wangapi wanafanya kazi kwenye tourism industry, zanzibar hata inasaidia tanzagiza kujulikana nje wengi hamlijui hilo labda …
Kwani kuna mtu amesema hakuna watanganyika wanaofanya kazi zanzibar?!! Kinachozungumziwa hapa ni nani mnufaikaji mkubwa wa huu muungano, mbona lisu amefafanua vizuri, eti li ccm linakuja na hoja nyepesi eti tumeoleana!! Jibuni hoja hizo
 
Kwani kuna mtu amesema hakuna watanganyika wanaofanya kazi zanzibar?!! Kinachozungumziwa hapa ni nani mnufaikaji mkubwa wa huu muungano, mbona lisu amefafanua vizuri, eti li ccm linakuja na hoja nyepesi eti tumeoleana!! Jibuni hoja hizo
ni watanganyika gani wanafanya kazi kwenye serikali ya zanzibar? mtaje hata mmoja tu. kule hata wakitangaza ajira kitambulisho cha mzanzibar ni cha kwanza kuonyesha. wakati huku kuna maelfu ya wazanzibar wanafanya kazi serikalini. yaani kwetu wapate, sisi kwao tusipate. tunaongelea ajira serikalini, sio hizo za mtaani za kufanya kazi hotelini. serikali ya Tanganyika imeajiri wazanzibar, ila serikali yao ni marufuku kuajiri mtanganyika.
 
Bosi wa ZRA. Yusuf Juma Mwenda.
 


Naona Lissu kapiga chini ya mkanda kwenye hili swala. Wengi wanakubaliana na Lissu kwamba kuna ubaguzi mkubwa sana hasa kwenye umiliki na uongozi wa wananchi wa hizi nchi. Haiwezekani mkuu wa wilaya anaweza kuwa Mzanzibari lakini watu kutoka bara waonekane kama wageni na wasioweza kupewa uongozi
 
Bosi wa ZRA. Yusuf Juma Mwenda.
huyo alikuwa meya wa kinondoni? ongelea kwenye sector zote, ukija bara, kila sector ya serikali hii kuanzia halmashauri yadi taifa kuna wazanzibar maelfu kwa maelfu, na sisi tunaona sio mbaya wacha wafanye kazi, ni watanzania. ila sisi huko mmesema tusitume hata cv.
 
Samahani. Ulitaka utajiwe mmoja.
 
Ndio ivyo hata Mimi naunga mkono hoja, nasema Muungano ni wa ovyo sana
 
Njia sahihi ni kuitisha kura ya maoni kwa kila nchi wananchi waseme km wanataka muungano au hawautaki,wananchi ambao ndo walitakiwa kuamua hatma ya nchi yao hawajawahi kushirikishwa kamwe,ndo maana nasemaga huu ni muungano fake wa Nyerere na ccm
 
Wazanzibari nimeamini Shukrani Hawana

Nilikuwa kijiwe kimoja pale Kisiwandui Zanzibar
Baadhi ya wazanzibari walalamika Raisi Samia kuwapa wazanzibari ajira Bara kuwa wanaharibika na kuua utamaduni wa kizanzibari

Kuwa wakipata ajira Bara wanaharibika na kuwa walevi na Malaya na wasio zingatia Dini Wala utamaduni wa Zanzibari wakiharibiwa na watanganyika wanakofanya kazi au kuishi mitaani
 
Nimecheka sana πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†. Kwamba wakija bara tunawafundisha uhuni. Hata hivyo dunia ya sasa ni utandawazi, tamaduni nyingi zinakufa na huwezi zuia
 
Mtu mzima haaribiwi, anaharibika mwenyewe.
 
 
Hii clip ya mheshimiwa mmoja hapo Zanzibar ambaye anasema mzanzibari yeye automatiki ni mtanzania na ana haki ya kumiliki ardhi huku tanzania bara ila mtanzania Bara yeye sio mzanzibari na hana haki ya kumiliki ardhi akiwa Zanzibar imenipa ukakasi sana katika hili suala la muungano.. maana halisi ya muungano ni nini??
 

Attachments

  • VID-20240601-WA0002.mp4
    2.7 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…