kuvunja muungano ni mawazo finyu sana, kama alivyosema MZEE ES, muungano unahisotria yake, ni kielelezo cha ukombozi wa mtu mweusi dhidi ya ubaguzi wa waarabu,
tutaendelea kukilinda kisiwa kile kwa nguvu zote.
pia tunawapongeza viongozi wetu kwa kuziingiza rwanda na burundi kwenye jumuiya ya afrika mashariki, it is a positive move na lazima utendelee mpaka africa yote iwe kitu kimoja.
aluta continue.
 
swala la zanzibar ni bom linalo subili kupasuka,sababu za nyerere kufanya muhungano kwa sasa hazipo tena moja wapo ikiwa ni ulinzi. zanzibar lazima tuachane nayo.ina matatizo mengi sana .kwanza vizazi cha sasa cha wazanzibar kinapotea wengi wapo canada ,uk ,usa,nk.nchi imeuzwa kwa waitaliano.baada ya miaka 40 zanzibar itakuwa kama palestina wazawa watakuwa awana ardhi watabakia kurusha mawe. kuhusu maalim seif ni tatizo kwa wazanzibar jamaa huyu ni ccm tena wa nguvu ameweza kuisaidia ccm mpaka leo bila kugundurika na wana caf.utaona wakati wa kampein maneno mengi kwa mfano mara hii hatukubali,jino kwa jino 'ngangari,tukishindwa hatuondoki.vitisho tu .matokeo yakitoka utaona anasema wanakafu rudi nyumbani niachieni mie ,basi huyu bwana akisha vuta cheki yake kwa kikwete anasuri miaka mingine mitano awafeck tena wapemba.
 
Zanzibarians ni watu wa ajabu, wana rais wao na wanapanga mikakati yao wenyewe. kama wameshindwa kuwa na amani kiasi cha watu laki kumi wataweza kweli kuhimili misukosuko ya kimataifa?

Mimi kwa maoni yangu binafsi kama Zanzibar hawataki huu muungano basi bora uvunjike hatuwezi kila siku kusikia hadithi ileile ambayo haina kichwa wala mkia.
 
Hivi kasoro za Muungano ni zipi ambazo hazisemwi hapa ? Na zitarekebishwa lini na nani ?
 
Hivi kasoro za Muungano ni zipi ambazo hazisemwi hapa ? Na zitarekebishwa lini na nani ?

Swali zuri sana hili ndugu Lunyugu.
Kila mara tunaambiwa kero za Muungano, Rais mwenyewe kaunda Wizara kushughulikia masuala ya Muungano (bila shaka kero) lakini hata siku moja hakuna nayetwambia kero hizo ni zipi. Muungano una kero moja tu nayo ni baadhi ya Wazanzibari wanaodhani nje ya bara maisha yatakuwa peponi. Muungano hauwei kuvunjika kwa sababu yeyote iwayo sana sana Zanzibar itaja kuwa mkoa kama hawataridhika na autonomy waliyo nayo. Haya ya undugu na weusi sijui kucha za Waarabu ni bay the way tu zaidi ni Uchumi. Ingekuwa shauri ya undugu kwa nini hatukuungana na Kenya, ambako kote kuna Wajaluo na Wamasai? Au Malawi na Msumbiji kwa Wamanda na Wamakonde?
 
DrWHO,
Nilifikiria kuwa wewe unawawakilisha ndio maana hawamo humu? Muungano utadumu na Zenj haiwezi kuingia IOC kwa sababu sio sovereign state.
 
Kutokana na nionavyo mimi huu muungano utakuja kufa, kinachofanyika ni kuwa CCM na serikali zinachelewesha tu. Binafsi napendelea muungano uendelee kuwepo, ila kutokana na ukweli wenyewe wa mambo na historia za nchi zote ambazo zilikuwa au zenye miungano ya ku force huwa zinaishia kutengana, hivyo hata kwa bara na visiwani ni vivyo hivyo.

Kitu kingine ni kuwa ukweli wenyewe ni kuwa sote hatupendani kiasi hicho!!, Imekuwa kama zile ndoa ambazo kila leo mke anakung'utwa na mumewe na anasema ati anabakia kwa ajili ya watoto!! Inasikitisha lakini ndo ukweli wenyewe huo. Ukienda nje ya nchi wa bara wana makundi yao na wa zenji wana yao, kila kundi linasema kundi jingine vibaya, je huo ni muungano?? Humu ndani katika mjadala mingi inayogusa Zenji tunaona jinsi ambavyo emotions zinapanda!!

Wengi wetu wanachosahau ni kuwa Zanzibar ilikuwa nchi na muungano huo walibambatizwa tu, kama bara ambavyo nao tulibambatizwa, hakuna hata aliyepiga kura.

Nionavyo au ninavyodhani ni kuwa muungano unaweza usivunjike kama kutakuwa na serikali tatu na kila kitu kitaweka wazi, siyo ubabe wa CCM au wa CUF.
 
Muungano hautavunjika kama CCM wataendelea kuongoza Zanzibar, kwa hilo sahau. Ila kama CUF wataingia haitachukua hata wiki. Kwa sasa ukivunja Muungano na Jumuiya ya EAC na SADC zinaendelea, itakuwa vigumu Zanzibar kufanya biashara na EAC au SADC maana tarriff za import duty zitapanda from 2% to 25%, that means Zanzibar will rely on Falme za Kiarabu, ambapo lile "Baraza la Mapinduzi" litakufa. Ndio maana nasema Muungano utaendelea.

After all any idiotic idea of breaking the union is not welcomed in this century. Kinachotakiwa ni kuweka mezani "all junk calaims" about the union na tuzijadili bila ya kuangalia huyu ni CUF au CCM au Kulinda upande mmoja wa muungano.
 
wema unapo kuwa mwigi ndugu yangu ni hatari kwani sio wotewanakuja kwako na Nianjema mpeleke mjaluo pale akaponde upinzani kwa sana na kumsifu karume na mapinduzi yake ASUBUHI YAKE UTAAMBIWA HUYO NI MKUU WA MKOA.
 
ebwana eee nani kakwambia kuwa wazanzibar wana taka muungano wanao taka muungano ni wabara.

Kumbe hujui hivyo?
 
Ni kweli ukiongea na wazanzibari wengi utasikia hawana haja na muungano, ila viongozi wa huo muungano wameung'ang'ania kama vile uliletwa na Mungu, na kututia pande zote migogoroni. Pengine watanzania kabla hatujaenda East Africa Federation tuangalie hili linalotuhusu zaidi kujiuliza kwa kura za maoni kama tunautaka. Tusiung'ang'anie tu eti kwa vile Nyerere na Karume waliutengeza...Tutumie sayansi ya maoni!!!
 
Nashangaa sana kuona viongozi wanawadekeeza hawa wazenji, kama hawataki muungano si tuwateme?

HAYATI Baba wataifa alishasema, KAMA MUUNGANO UTAVUNJWA BASI KUTAIBUKA WAZANZIBARI NA WAZANZIBARA, Na nikweli kutokana na historia ya PEMBA (CUF) na UNGUJA (ccm).

Sitaki kuelezea saana ila tu nawabipu hawa viongozi ya kwamba kama ni vipi tuwape wazenji walio wengi wanachokitaka! AU SIO jamani. Tukuwang'ang'ania watatuadhiri!

Ni mawazo yangu tu sababu katiba ya Tz inasema kila mtu ana haki ya kuchangia/kusema anachodhani ni sahihi ilimradi tu asivunje Katiba.

Rgrds/Abdallah Issa!
 
Ziara ya Makamba yazua hofu Z’bar

na Mwandishi Wetu

 
Na sasa mgogoro wa Zanzibar ndio utakuwa mkubwa kuliko zamani!...

Hawa viongozi wote wanagombea - KULA, iwe CUF ama CCM tumbo kwanza na maslahi ya wananchi yatafuata. Mkutano huo hauna ridhaa ya wananchi kwa sababu kama kweli JK alitaka ku-solve matatizo ya Zanzibar zingeandikwa mapendekezo ya mkutano wa (CUF na CCM) kisha yakapigiwa kura na wananchi. Wananchi wangejulishwa kwa undani kipi kinawasaidia wao ktk yale wanayopigania.
Kuunda kwa serikali ya mseto ni udanganyifu mkubwa kwa wananchi na viongozi wote wanahaha kwa sababu ya ajira zao zaidi na sio kabisa hatma ya makubaliano hayo kwa faida ya Zanzibar.
 
CCM wanaogopa kutibuliwa mbinu zao za kuingia kwenye Umoja wa EAC wakati soo la Zanzibar bado halina utatuzi. Wanakimbilia kwenye EAC ili wajifiche vizuri.
 
Z`bar not sovereign country-AG

2007-01-25
By Mwinyi Sadallah, Zanzibar


Zanzibar Attorney General Idd Pandu Hassan has said that Zanzibar cannot join the East African Community as independent country because it lacks the status of sovereignty.

The AG made the clarification yesterday in the House of Representatives, which kicked off its sessions yesterday, after being pinned down by house members to explain why Zanzibar is not an independent member of the regional bloc.

The law that established the EAC, he explained, required member countries to have the status of sovereignty, which Zanzibar, being part of the United Republic of Tanzania, is lacking.

"Zanzibar will continue to be represented in the regional grouping by the United Republic of Tanzania, said Hassan.

The AGs reaction came after Gando legislator Said Ali Mbarouk (CUF) sought clarification on a recent statement made by Prime Minister Edward Lowassa that Zanzibar could not join the EAC as independent nation.

Mbarouk had wanted to know if the statement came out of Union meetings that discussed ambiguities in the union structure or if it originated from Lowassa himself.

However, Hassan said that both governments had made significant progress in resolving the ambiguities and two joint meetings had already been conducted both on the Mainland and in Zanzibar.

Responding to a basic question from Ali Usi (Chaani, CCM), who had wanted to know the exact number of union ambiguities resolved so far, Hassan said five issues had been discussed, namely distribution of foreign aid, Bank of Tanzania interest rates and loan issues.

Others are double taxation on goods from Zanzibar, implementation of the Commission for Human Rights and Good Governance, oil and gas exploration and management of fishing activities on the Indian Ocean shores.

He said the issue of oil exploration had been forwarded to the Union government because it required change of the countrys Constitution.

The Union Parliament had already amended the law that established the Commission for Human Rights and Good Governance, basing on recommendations from joint meetings before implementing the same in Zanzibar.

He said the House of Representatives had approved the establishment of a fishing authority and that 40 percent of revenue to be generated would go to Zanzibar and 60 percent to the Mainland.

According to the AG, a joint Financial Commission has already compiled its preliminary report on modalities of sharing foreign aid coming to Tanzania and interest of the Bank of Tanzania.

The report had been presented to the Chief Minister, while discussions on other issues are still going on, he said.

The EAC Union constitution is a big secret WHY?
 


Mawazo ya wananchi? Hiyo siyo kwa CCM!
 
Haya jamani nimewawekea mkataba unaounda Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Hadi hivi sasa hakuna Katiba ya Shirikisho la Afrika ya Mashariki kwani Shirikisho hilo halipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…