Tatizo hapa ni CCM wao walisaini makubaliano hayo ila leo hii wanakuja na nyimbo mpya eti ooh haya yanaweza kuanza kutekelezwa in 2010 baada ya uchaguzi mkuu huo.

CCM wamegoma kusasini kile kipengele kinachosema kuwa makubaliano haya ya muafaka huu yaanze kutekelezwa kipindi hiki wakitaka kibadilishwe, sasa hapo wa CCM ZNZ hawapo tayuari ila wa bara wanawalazimisha kukubaliana na jambo hilo.

Karume huenda yakamkuta yale ya aliyetakiwa kuondoka in 3hrs time madarakani?

na leo hii anaishi kule kigamboni DSM chini ya ulinzi mkali sana ..
 

Tuone utekelezaji wa hili, lakini kama likifanikiwa na kuleta muafaka ambao unakubaliwa na pande zote mbili basi JK anastahili pongezi za hali ya juu, kwa kuwa bila yeye hili lisingefanikiwa.
 
Tuone utekelezaji wa hili, lakini kama likifanikiwa na kuleta muafaka ambao unakubaliwa na pande zote mbili basi JK anastahili pongezi za hali ya juu, kwa kuwa bila yeye hili lisingefanikiwa.

Kwa rekodi ya JK ni mapema mno kumpongeza hivi sasa, tusubiri tuone!!!!!!!!!
 
Haya SISIEMU hao!!!!!!!!

Chama tawala chashindwa kukanusha kauli ya CUF kuhusu mwafaka Zanzibar
Na Lilian Lucas, Morogoro

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, kuhusiana na muafaka wa vyama hivyo visiwani Zanzibar ni ya CUF.


Katibu huyo wa CCM aliyasema hayo jana mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Usambara nje kidogo ya mji wa Morogoro baada ya Seif kutaja vipengele vilivyomo kwenye muafaka baina ya vyama hivyo.


Makamba alisema kuwa, kauli alizozitoa Katibu huyo kuhusiana na muafaka huo ni za CUF na si za CCM na kusisitiza kuwa, CCM kitatoa taarifa yake kuhusiana na muafaka huo.


Alisema kama Katibu Mkuu wa CCM kwa sasa, hawezi kuzungumzia lolote kuhusu makubaliano ya chama chao, kwani jukumu hilo ni la Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM unatarajiwa kufanyika hivi karibuni Butiama wilayani Musoma Mkoa wa Mara.


Alisema masuala kuhusiana na makubaliano ya Muafaka wa CCM na CUF Zanzibar yanaendeshwa na timu mbili za kutoka vyama hivyo, kila moja ikiwa na wajumbe watano, ikiongozwa na Katibu, hivyo Maalim Seif katoa taarifa ya chama chake.


Kila alipoulizwa juu ya taarifa aliyozitoa katibu huyo mkuu wa CUF kuhusu makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani humo, Makamba, hakutaka kuzungumzia chochote.


"Sisi taarifa yetu tutaitoa kwa wakati muafaka kwani kama CCM sasa hatuna la kusema," alisema .


Makamba yuko Morogoro kwa ziara ya siku nne kukagua shughuli za kichama na kwamba, atatembelea wilaya za Kilosa, Mvomero, Morogoro Mjini na Morogoro Vijijini.

?

Akihutibia mkutano wa hadhara ulifanyika Uwanja wa Demokrasia visiwani Zanzibar juzi, Maalim Seif alisema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Amani Abeid Karume wakati wowote kwa maslahi ya Wazanzibari.


Alisema kuwa, yuko tayari kufanya hivyo kwa vile Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani Zanzibar, itaundwa baada ya kutiwa saini Muafaka huo baina ya vyama hivyo, na si kusubiri Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.


?Napenda kuwafahamisheni kuwa utaratibu mpya tumekubaliana tugawane nafasi mbili za juu, yaani Rais na Waziri Kiongozi?ili kuhakikisha haya tuliyokubaliana yanatekelezwa, mara baada ya kutiwa saini kwa muafaka, CUF itaingia katika Serikali hakuna kusubiri mwaka 2010," alisema.


Alisema katika makubaliano hayo, wamezungumziwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar utakaofanyika mwaka 2010, ambao baada ya kumalizika itaundwa Serikali ya Mseto kwa kushirikisha vyama vingi ambavyo vimepata idadi maalumu ya kura majimboni.

?

Alisema katika makubaliano ya mazungumzo, vyama vya siasa ambavyo vitashiriki katika Uchaguzi huo na kufanikiwa kupata kura, navyo vitashirikishwa katika kuunda Serikali kwa kupewa uwaziri.

?

Alisema Serikali itakayoundwa itatokana na wingi wa kura na chama kitakachopata kura nyingi kitatoa Rais na cha pili kwa kura kitatoa waziri kiongozi na vingine mawaziri ili kuondoa ukiritimba wa chama kimoja.
 
Kama mimi ningekuwa kiongozi ndani ya chama CCM basi muafaka huu ningeukubali haraka sana kwani ni CCM ndio wakakuwa wameshinda tena vibaya sana.
Hakuna mseto wowote unoweza fanya kazi kwa manufaa ya ama mfumo wa CUF ikiwa rais wa nchi ni kiongozi wa CCM. Mfumo huu unawezekana tu nci za magharibi ambao Bunge na mahakama zao wana nguvu kubwa kuliko rais.
NItakupeni mfano hai kabisa... CUF leo hii wana wajumbe wake ktk kamati ya Uchaguizi Zanzibar, lakini waulizeni wana sauti gani ndani ya tume hiyo na what changes ambazo wameweza kufanikisha. Na mapungufu yoyote yale yaliyowahi tokea CCM wameweza kudai kuwa sii wao kwani wajumbe wa CUF wamo pia.
It will be the same, CCM wataweza kumnyamazisha CUF kirahisi na pengine kama CUF hawatakuwa macho mwaka 2010 kuna viongozi wengi watahamia CCM kwa sababu ya kutopoteza ULAJI...
Seif Sharrif anachotafuta ni KULA yake kwani aliwahi kuwa Waziri kiongozi Zanzibar akiwa CCM na sidhani kama kuna mtu anayeweza kunambia kizuri alichokifanya kama wewe sio Mpemba!.
 

Mkandara,

mimi nilikuwa nimeanza kusherehekea ila naona Mzee Makamba anasema watu wahold their horses for now! Hii ilikuwa habari njema sana kwa Tanzania!
 
Mwafrika wa Kike,

Bila shaka itakuwa habari nzuri sana Tanzania kwani yatakuwa mazishi ya CUF, hivi sasa kinachimbiwa kaburi...Jamani ikiwa Serikali ya Mapinduzi inaweza kumkataa kiongozi Mtanzania, Mzanzibar wa CCM kugombea Urais kutokana na hisia zao tu kuwa wanafikiria bado ana Upemba (Arabnised) itakuwa chama hicho kupewa mwanya wa kujijenga zaidi.. Sio Tanzania hii.

Dada yangu niyakwambia hivi hakuna kiongozi yeyote aliyetoka Hizbu anaweza kuaminika Unguja na hata siku moja hawawezi kula meza moja ktk uongozi.
Muulizeni Kamandoo Salmin mtaipata picha halisi ya utawala Zanzibar..
 

sijakupata wataka kutwambia salmini alikuwa hizbu?
 
Bongo bado hatujafikia kwenye siasa makini kama Kenya. Bado sioni upinzani wenye nguvu. Na hii inasababishwa na uoga na umbumbumbu uliokithiri. Tukubali tu kuendelea kuburuzwa.
 
Bongo bado hatujafikia kwenye siasa makini kama Kenya. Bado sioni upinzani wenye nguvu. Na hii inasababishwa na uoga na umbumbumbu uliokithiri. Tukubali tu kuendelea kuburuzwa.

Wewe unataka tupigane mapanga kama Kenya?Halafun aje Kofi Ana kutusulishisha au?
 



"Hakuna mseto wa mawe na chooko" Komandoo Salmin Amour
 
Taratiibu mkuu Masatu, tuhuma nzito hizo!!!!!!!!!!!!
 
changa la macho. ccm itasema tutaunda, tutaunda ......mpaka uchaguzi wa 2010 utafika hakuna lilofanywa.
they are just playing with people's mind.
 
•
CCM: Hakuna 'mseto' wala 'ugali' Z'bar

Habari Zinazoshabihiana
• Shivji: Serikali ya mseto si sawa na ya umoja wa kitaifa 14.08.2007

Na Ali Suleiman, Zanzibar

WAKATI wanachama wa CCM wakisherehekea mwaka moja tangu Rais Amani Abeid Karume ashinde katika uchaguzi mkuu mwaka jana, Waziri Mwandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Samia Suluhu Hassan, amewaondoa hofu wafuasi wa CCM akisema hakuna 'mseto' wala 'ugali' katika mfumo wa Serikali Zanzibar.

Akizungumza juzi na viongozi wa jumuiya za wanawake katika kongamano la wanawake Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri wa Uwekezaji, Utalii na Vitega Uchumi, Samia, alisema hakuna makubaliano ya kuwapo 'mseto' wala 'ugali' katika kuunda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hadi sasa.

"Sisi tulichokubaliana na wenzetu CUF ni kujenga mazingira mazuri ya kuondosha hali ya wasiwasi na chuki kati ya wananchi wetu wa visiwa vya Unguja na Pemba...unajua hapo zamani watu walikuwa hawaoleani eti, kwa tofauti ya itikadi za kisiasa hilo tumeliondoa kwa sasa," alisema Samia.


Hii ni quotation ya zamani. Lakini sitashangaa kama at the end this is how it will end up. Kama sivyo basi watu wenye mantiki kama ya Samia wanaweza kuleta matatizo makubwa huko Zenji!
 


kumbe siasa huijui wewe haya aliosema dada samia madogo sana kuna maneno yalisemwa kenya makubwa kuliko hayo na sasa tizama kuna nn .

wanasiasa ni meno ya mbwa hawatafunani.

chochote chaweza kutokea butiama ndio yenye maamuzi sio samia.
\
kwa kukumbusha mh amani ccm wazanzibar hatukumtaka na tulienda dodoma kwa vishindo tukiamini tutarudi na mh bilali lkn wapi tukapewa karume na mh takrima alinadi kua karume ni dalali tu ameinadi zanzibar akikusudia baba yake rais na bibi castico akajitapa na kutoa ndaro nyingi unajua kiliwakuta nn?

basi hio ndio siasa usishangae yeye akawa ndio wa mwanzo kusifu hio hali na kusema vyombo vya habari vimemchonganisha
 

Sadakta Balahau. Nawafiki hoja yako.
 
Ah Balahau, Mtu wa Pwani. Hiyo quotation ya Bi Samia usiichukue pekee pekee. Lakini kwa mintarafu ya hoja yetu ichukue pamoja na haya hapa juu aelezayo Bw. Mkandara. Upo Balahau?
 
Wewe unataka tupigane mapanga kama Kenya?Halafun aje Kofi Ana kutusulishisha au?

Naamini hataki hivyo lakini ndio tulivyo kama hatujaingiliana maungoni Waafrika hatukai meza moja tukazungumza na kukubaliana na kutekeleza yaliyopitishwa - mifano hai ni Msumbiji , Angola na kwengineko na Zanzibar kama ilikuwa nchi bila ya Muungano yangelikwisha fika hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…