Haya SISIEMU hao!!!!!!!!
Chama tawala chashindwa kukanusha kauli ya CUF kuhusu mwafaka Zanzibar
Na Lilian Lucas, Morogoro
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, kuhusiana na muafaka wa vyama hivyo visiwani Zanzibar ni ya CUF.
Katibu huyo wa CCM aliyasema hayo jana mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Usambara nje kidogo ya mji wa Morogoro baada ya Seif kutaja vipengele vilivyomo kwenye muafaka baina ya vyama hivyo.
Makamba alisema kuwa, kauli alizozitoa Katibu huyo kuhusiana na muafaka huo ni za CUF na si za CCM na kusisitiza kuwa, CCM kitatoa taarifa yake kuhusiana na muafaka huo.
Alisema kama Katibu Mkuu wa CCM kwa sasa, hawezi kuzungumzia lolote kuhusu makubaliano ya chama chao, kwani jukumu hilo ni la Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM unatarajiwa kufanyika hivi karibuni Butiama wilayani Musoma Mkoa wa Mara.
Alisema masuala kuhusiana na makubaliano ya Muafaka wa CCM na CUF Zanzibar yanaendeshwa na timu mbili za kutoka vyama hivyo, kila moja ikiwa na wajumbe watano, ikiongozwa na Katibu, hivyo Maalim Seif katoa taarifa ya chama chake.
Kila alipoulizwa juu ya taarifa aliyozitoa katibu huyo mkuu wa CUF kuhusu makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani humo, Makamba, hakutaka kuzungumzia chochote.
"Sisi taarifa yetu tutaitoa kwa wakati muafaka kwani kama CCM sasa hatuna la kusema," alisema .
Makamba yuko Morogoro kwa ziara ya siku nne kukagua shughuli za kichama na kwamba, atatembelea wilaya za Kilosa, Mvomero, Morogoro Mjini na Morogoro Vijijini.
?
Akihutibia mkutano wa hadhara ulifanyika Uwanja wa Demokrasia visiwani Zanzibar juzi, Maalim Seif alisema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Amani Abeid Karume wakati wowote kwa maslahi ya Wazanzibari.
Alisema kuwa, yuko tayari kufanya hivyo kwa vile Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani Zanzibar, itaundwa baada ya kutiwa saini Muafaka huo baina ya vyama hivyo, na si kusubiri Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
?Napenda kuwafahamisheni kuwa utaratibu mpya tumekubaliana tugawane nafasi mbili za juu, yaani Rais na Waziri Kiongozi?ili kuhakikisha haya tuliyokubaliana yanatekelezwa, mara baada ya kutiwa saini kwa muafaka, CUF itaingia katika Serikali hakuna kusubiri mwaka 2010," alisema.
Alisema katika makubaliano hayo, wamezungumziwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar utakaofanyika mwaka 2010, ambao baada ya kumalizika itaundwa Serikali ya Mseto kwa kushirikisha vyama vingi ambavyo vimepata idadi maalumu ya kura majimboni.
?
Alisema katika makubaliano ya mazungumzo, vyama vya siasa ambavyo vitashiriki katika Uchaguzi huo na kufanikiwa kupata kura, navyo vitashirikishwa katika kuunda Serikali kwa kupewa uwaziri.
?
Alisema Serikali itakayoundwa itatokana na wingi wa kura na chama kitakachopata kura nyingi kitatoa Rais na cha pili kwa kura kitatoa waziri kiongozi na vingine mawaziri ili kuondoa ukiritimba wa chama kimoja.