CCM imezidi kujimaliza huko Zanzibar ,hivi sasa wanasema waliopinga wazo la serikali ya mseto sio wanaCCM kutoka Zanzibar bali ni wabara kwani kumbukumbu zinaonyesha ,maamuzi ya CCM bara ndio yanayosimamia mambo yote yanayofanywa na CCm Zanzibar kwa mafano ambao ni hai ni wa huyu raisi wao Karume wanavyosema kwamba hawakumchagua na alikuwa ni wa mwisho katika kutafuta nani akamate uraisi wa Zanzibar ,na walipofika Dodoma CCM bara ikayapangua na kuwapangua wote na kumueka kibaraka wao wanaemtaka ambae ni Karume mtu aliekuwa hakupata hata ridhaa za wanachama wenzake kutoka Unguja hivyo utaona ,CCM Bara wamewagawa wanaccm na wanawatawala na kuwaendesha wanavyotaka.
Ikumbukwe tu Wazanzibar fujo wanaliweza hata ikibidi wapoteze roho zao lakini wakiamua na viongozi wa CUF wakajifanya kama hawaoni basi hawa kina Karume hawachukui hata muda kukaa ila watapanda boti na kuja kujificha Bara kama walivyofanya katika uchaguzi uliopita.tusidanganyane inajulikana wazi kuwa Wazenji wote chama chao ni CUF hakuna cha mpemba wala waunguja ila wamekaliwa na nguvu za dola ,na leo nimesikia wakimpa salamu Kikwete aanze kutayarisha polisi na majeshi mambo tayar au msimu tayari na wengine wanasema zamu yake ya kuja kuwaua wazanzibari ishafika.
 
Mtu wa Pwani,

Kwani unadhani Kibaki na PNU yake walikubali kufanya hayo mabadiliko kwa hiari? Ama wewe hukuona damu za watu zilivyomwagika? Labda waulize CUF kama wako tayari kuwalazimisha CCM wafanye mabadiliko kama ilivyotokea Kenya.

Bw Keil kwa faida ya nani. Au kwa sababu hakuna Bibi na Shangazi zako kule Unguja na Pemba. Peleka siasa hizo na kwenu kama unaona ni zenye kuleta kheri.
 

Hiyo sio serikali mkuu, Kampuni, NGO ni CHAMA nasisitiza ni CHAMAna wenye chama ni wanachama!!! Kiongozi wa Chama anawaongoza wanachama kufikia maamuzi yao. Ndio maana kwenye CCM kila kitu kinaamualiwa na vikao vya chama... Mwenyekiti hata kama Kipanga kama Kitila... hawezi kuamua mambo mwenyewe... well true he can convince members... lakini alitakuwa awa-convince nini kwenye hili... i don't see it brother.

So, long as JK remains unable to take tough decisions on our nation's fate and wants to be directed what to do by his cronies, to me, he is simpy and disturbingly incompetent!
Najua unapata tatizo wapi?

Unataka decision za namna hii hapa chini:-
  • Kupora mamlaka ya wanachama kwenda kwa mwenyekiti wa Chama
  • Kupeleka watu mahakamani au magerezani bila kufuata sheria,,, hili halitatokea kwa serikali ya Kikwete subiri ya Mrema au Mbowe!
  • Kufanya mambo bila kufuata utawala bora na haki za binadamu...
 

Zoezi la mwaka 1995, halikufanikiwa, Wapemba wamerudi tena Mji Mkongwe na wanaendelea kuishi katika majumaba hayo. Ingawa sasa kuna mchanganyiko mkubwa na wafabiashara ndogo ndogo toka Bara.

Ngome nyingine kubwa ya CUF katika Unguja ni Chumbuni, Jang'ombe Urusi na Magomeni maili nne
 

Hilo ndilo wanalolitegemea CCM kuambiawa wamejaribu , pengine kura ya maoni itapangwa karibu ya uchaguzi Julai au Septemba 2010 halafu watasema serikali haina hela kwani zinataka kutumika katika uchaguzi au kisingizio chengine chochote na watu kama wewe watasema sawa sawa Mheshimiwa JK tuko nyuma kama si mbele yako tunakuunga mkono kwa juhudi zako kwani unawaelewa Wazanzibari umekaa nao miaka mitatu( binadamu haeleweki licha ya miaka 3 hata 10)una nia njema. Baada ya hapo utafanyika uchaguzi kwa staili nyengine ya kuvuruga matokeo na badala yake ni muafaka - yaani ni mzunguko usokuwa na mwisho.

Kumbukeni CCM Znz walishasema juu ya majukwaa kuwa kle kipande cha ardhi kilipatikana kwa Mapinduzi na hakitatoka kwa njia ya kura. Mutajua wapi wanataka kutupeleka.
 

Kwa hivyo sio tena asilimia kubwa ya Wapemba wanaoishi kule. Maili nne si ndio jimbo la Shamsi Vuia Nahoda hilo naona majimbo yote uloyaaja Mkuu si ngome za CUF - vipi kuhusu Mtoni, Bububu na Nungwi?
 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kambi ya Upinzani wote wametoka nje ya kikao cha Baraza hilo wakati wa asubuhi kutokana na kuitwa katika kikao cha dharaura Makao Makuu ya Chama chao kwa ajili ya kujadili tamko la Chama Cha Mapinduzi lililotolewa jana usiku.

Chama Cha Wananchi (CUF) kimelazimika kuwaita wajumbe wake wote wa Baraza la Wawakilishi kutokana na kauli iliyotolewa na Kamati ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu mazungumzo ya Mwafaka kati ya vyama hivyo viwili ambayo yamechukua mua wa miezi 14.

Wajumbe hao awali waliingia ndani ya kikao cha Baraza la Wawakilishi kama kawaida na kusikiliza maombi maalumu (Dua) pamoja na maswali na majibu lakini baadae kabla maswali hajayamalizwa kujibiwa baadhi yao walianza kuondoka mmoja mmoja na kutoka nje ya kikao hicho.

Wajumbe hao walitoka nje wakati Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati ya Ardhi Mansour Yussuf Himid akiwasilisha Mswada wa Sheria ya Kusajili Wahandisi, Wasanifu na Wakadiriaji Majengo.

Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi wa Kambi ya Upinzani, Soud Yussuf Mgeni aliwaongoza wajumbe wenzake na kutoka nje ya kikao hicho huku akisema wamelazimika kufanya hivyo kutokana na ukubwa wa jambo lenyewe ambalo linahusisha amani katika nchi.

Mnadhimu huyo alithibitisha kuondoka barazani muda mfupi baada ya kutoka ukumbini alisema kwamba wanakwenda Makao Makuu ya Chama Cha Wananchi (CUF) Mtendeni kwa kikao cha dharura ambacho pamoja na mambo mengine kitajadili kilichojitokeza Butiama.

"Tumetoka kwenye Baraza tunakwenda kwenye kikao muhimu tulichoitwa na Chama Chetu sisi tunawawakilisha wananchi kwa hivyo lazima la leo lifanywe leo hakuna kusubiri" alisema Mgeni.

Mnadhimu huyo alisema wamechukua uamuzi wa kutoka nje ya kikao cha baraza bila ya kumuarifu Spika wa Baraza hilo lakini taarifa zaidi atazipata atakapoangalia upande wanaokaa wajumbe wa Kambi ya Upinzani.

"Spika hatujamuarifu rasmi lakini bila ya shaka atajua tu baadae kwa sababu akitupa jicho ataona hakuna mtu upande wetu kwa hivyo…atajua ..atajua tu" alisema Mgeni kwa haraka haraka huku akiingia ndani ya gari ndogo kuelekea Mtendeni.

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho alisema hajapokea taarifa zozote huhusiana na wajumbe wa Kambi ya Upinzani ambao wameondoka kwa ghafla katika kikao hicho.

"sina taarifa ya kuondoka kwao, kwa sababu wakiingia kwanza na baadae kutoka wote, sina taafsiri juu ya kitendo hicho, hata hivyo kwa upande wangu wa kulia wapo waliowahi kuingia na baadae kutoka bila ya taarifa ukiachia wachache, na pia baadhi hawajaja hadi sasa bila ya taarifa" alisema Spika.

Hata hivyo baada ya kuwasilishwa mswaada wa Waziri mansour na baadae Mwenyekiti wa Kamati Spika aliwataka CUF kuja kuwasilisha maoni ya kambi yao huku kama kwamba hajaona upande wake wa kushoto hakuna kiti chenye mtu jambo lililozua vicheko kwa wajumbe wa kulia (CCM).
"Mheshimiwa njoo uwasilishe maoni ya kambi ya upinzani" aliwachekesha wajumbe wa CCM.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Professa Ibrahim Lipumba anatarajiwa kuitisha Baraza Kuu la Uongozi wa Chama hicho na kutoa tamko lake rasmi kuhusiana na kauli ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo.

Baadhi ya wananchi mbali mbali waliotoa maoni yao wamewatupia lawama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kutokana na kuwaendeleza wahafidhina wa Zanzibar ambao hawataki mabadiliko wala nchi kuwepo katika hali ya amani.

Wamesema kwamba Rais Kikwete angepaswa kusimama na kauli yake bila ya kujali wahafidhina kwa kuwa tayari alikuwa ameshaawahidi wananchi wa Zanzibar kushughulikia na kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa na sio kuanza kupoteza muda hivi sasa kwa kuleta sababu za kura ya maoni.

Zakia Omar ni miongoni mwa wenye mawazo hayo ambaye amesema hakuna dhamira ya kweli katika kuutatua mgogoro wa Zanzibar kwani baadhi ya maamuzi yamechukuliwa bila hata ya kuwashirikisha wananchi inakuwaje katiak hili washirikishwe wananchi.

"maamuzi mengi yameamuliwa bila ya kutushirikisha sisi wananchi leo wanatwambia kupigwe kura ya maoni ..si wana bytime tu sioni kama kuna umuhimu sana wa jambo hilo kwa sababu mwaka 1995 tulisema kupigwe kura ya maoni lakini wenzetu walikataa leo hii wanatujia na kutaka kura ya maoni…hatuwafahamu" alisema kwa hasira.

Akitaja maamuzi yaliowafikiwa bila ya kuwashiriksiha wananchi alisema aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi, alitakiwa kujiuzulu wadhifa wake bila ya kuchukuliwa maoni ya mtu yeyote.

Alisema kwa mujibu wa hati ya muungano Rais wa Zanzibar anakuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM lakini kufuatia mabadiliko ya 11 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wamepitisha vifungu na kumuondoshea madaraka bila ya kuwepo kura ya maoni pamoja na maamuzi mengi yakiwemo yale ay kupeleka majeshi ya Tanzania katika vita vya Somali na Comoro.

Mansour Ali Yussuf alisema inaonekana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijali wananchi na badala yake wanaenesha serikali kama mradi wa watu wachache ambao wana maamuzi yao kwa kusaidiwa na Serikali ya Muungano ili kuwadanganya wananchi kuwa suala hilo ni gumu na haliwezi kupatiwa uamuzi wa haraka bila ya kuwepo kura ya maoni.

Yussuf alisema sio kweli kama Kikwete hawezi kutafuta suluhu isipokuwa anachofanya ni kuwalinda wahafidhina ambao wana lengo la kuleta machafuko katika nchi.

Wananchi wa Zanzibar jana walikuwa katika mijadala mikali katika kila sehemu ambapo baadhi yao walisema sasa Rais Kikwete anataka kucheza na amani kwa kuwaachia viongozi wa Zanzibar kufnaya maaamuzi ya kihuni.

"Kilichoamuliwa Butiama ni uhuni na sasa wanataka kutuchagulia nchi maana hatutakubali kama waliona ya Kenya sasa wanataka yaje Zanzibar sawa…" alisema Mzee mmoja
 
Unazo data? Abdalla Rashid alihamisha watu wachache sana tena kwa faida yao kwa sababu wakikaa kwenye magofu yaliyokuwa yakianguka na hivyo wakihatarisha maisha yao. Wengi wao baada ya nyumba hizo kukarabatiwa (chini ya mradi wa Mji Mkongwe uliopata ufadhili) walirejeshwa kwenye makaazi yao. Ndugu zetu hao wapo. Tembelea Malindi, Shangani, Baghani,Funguni, Mchambawima. Vuga,etc. Sina hulka za kibaguzi na nachukia kueleza haya lakini tunajenga hoja tu. Wakaazi wa Mji Mkongwe ni rahisi kudanganywa kwani wao ndio waliokuwa wakidanganywa na Seif na kulazimishwa kuingia mababarani kuandamana na hata pale walipojua kuwa watapambana na nguvu za dola na kuhatarisdha maisha yao. Wengine waliambiwa watafanyiwa mpango waje Ulaya kama ni wakimbizi na hivyo watatimiza zile doto zao za kuishi majuu. Tembelea wapo tele huko Miji ya UK. Mji Mkongwe una asilima 5 (TANO)ya wakaazi wa Mji wa Zanzibar. Mbona CUF hawajapata ushindi katika majimbo mengine ya Mjini Znz (majimbo 12 yaliyobakia sehemu kama Magogoni, Jan'gombe, Mtoni, Daraja bovu hawakushinda?) Jenga hoja Yakhe.
 
Ewe Mola wetu,tuepushe na shari zinazoweza kutokana na mgogoro huu.
Ewe Rais wetu Kikwete,mbinu ulizotumia kwa ushirikiano na Kofi Annan kuyamaliza ya Kenya zinahitajika haraka hapa.Nadhani mheshimiwa hutangoja tone jekundu la kwanza lidondoke,fanya hima.
 
I support CUF kutangaza maan wali pre empty na sasa iko wazi nani mwenye matatizo maana kama wangalichelewa ingalikuwa spinned kwamba CUF wanaleta shida .Now kila mmoja anaona .
Ni kweli kabisa CUF waliwashitukia CCM na hivyo kuwahi kutangaza na sasa wao ndio wenye turufu ,na wananchi wa Zanzibar wanasema kama kura ya maoni basi ni kuhusu Muungano na si vinginevyo ,vyama vya siasa havihitaji kura ya maoni ya wananchi,kupeleka majeshi Comoro hakukuhitaji kura ya maoni ya Wananchi ,kumwajibisha Aboud Jumbe hakukutakiwa kura ya maoni ya wananchi ,kubadili vifungu kumi na moja vya Muungano hakukutakiwa kura ya maoni ya wananchiRaisi wa Zanzibar kuondolewa umakamo wa Raisi wa Muungano hakukuhitaji kura ya maoni ya wananchi ,wanasema Tanzania kwa ujumla inaendeshwa kihuni hivyo sasa wanajitayarisha kupambana kihuni wanaamini ukichanganyisha na ufisadi wa CCM basi Tanzania kwa ujumla hakutakalika. Na sasa wanamuunga mkono Mtikila kuwepo kwa Tanganyika kwani uhuni unaofanywa na vikundi vinavyojiita vya mtandao unavuka mipaka na kuhatarisha maisha ya wengi.
 
Kwa hivyo sio tena asilimia kubwa ya Wapemba wanaoishi kule. Maili nne si ndio jimbo la Shamsi Vuia Nahoda hilo naona majimbo yote uloyaaja Mkuu si ngome za CUF - vipi kuhusu Mtoni, Bububu na Nungwi?

Mote humo CUF walishindwa. Lakini asilimia zao za kura zilikuwa kubwa walipata kati ya 30-42percent.mNa yapo majimbo Pemba ambako CCM ilishindwa lakini ilipata kura za zinazofikia asilimia 30 (Mkanyageni, Wawi, Mkoani, Mtambile ) na mengineyo.
 

I beg to reserve my comments.
 

Watakaouliwa ni wale walio wajinga. Wengi wa Wazanzibari ni watu wenye Busara. Mungu awaepushe na husda hiyo.
 
Angalizo:

Wakati mwingine, sio mara zote "maoni ya wananchi maana yake ni maoni ya baraza la wawakilishi" kuridhia jambo fulani lenye masilahi na Zanzibar...
Namkumbusha mwiba kwamba maamuzi mengi yaliyopitishwa mazito kama aliyoorodhesha yalipelekwa kwenye baraza la wawakilishi.

Issue ya kwenda kulinda amani Lebanon, Liberia, Comoro haihitaji... hayo unayoyasema, hata Hamad Rashid Mbunge makini na Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni alishasema hivyo.
 

Thanks for the defimitions. Wazannzibari walishatambua haya na ndio maana leo hii wanadai sasa wapate taifa badala ya kuwa nchi tu. Wanajua kuwa wanashindwa kufanya mambo mengi kutokana na kukwamishwa na yenyewe kuwa nchi tu na si taifa. Sasa wameanza harakati za kudai taifa na ndio maana wanakuwa wakorofi sana kwa sababu wana uzoefu kuwa nchi hiyo haitapatikana katika kisahani cha dhahabu.
 

Ah!! Kusema majukwaani. Jee waliyosema CUF majukwaani huko Pemba unayakumbuka. Walioyosema Kibanda-maiti, Mnazimmoja. Darajabovu Komba-wapya majukwaani unayakumbuka? Hizo ndiyo mbwembwe za malumbano ya jukwaani.
 

Malindi na Funguni sio jimbo la mji Mkongwe na walilitoa CCM katika mbinu zao za kutaka kupnguza nguvu za CUF kama ni mtu wa data zitafute na unamdanganya nani kuwa zoezi la Abdalla Rashidi lilifanyika kwa manufaa ya wakazi wenyewe wacha uongo na kasumba za KiCCM ni sawa na juzi Mkurugenzi wa Maafa alipoambiwa Micheweni kuna njaa akasema nimesikia katika vyombo vya habari lakini sijachukua hatua kwa sababu sijapata taarifa rasmi- halafu unambie CCM hasa Znz inafanya kitu kwa manufaa ya wananchi hasa wapemba - yaguju - serikali inayowapiga risasi wananchi wake halafu iwaonee huruma ya kuwahamisha na kutengeneza nyumba warudi kukaa - unbelievable - hakuna aliyerejeshwa kama umesikia au unapenda tu kutoa hizo habari ni haki yako. Mimi naweza kukutajia nyumba moja moja mtaa wa Hurumzi waliohamishwa na hawakurudishwa na wewe nitajie waliorudishwa ( tumia PM )

Kuhusu watu wa mji mkongwe kudanganywa hawakudangaywa hilo la kuwapeleka watu Ulaya linawezekana ni mipango tu nafikiri unajua lakini hutaki kukiri ukweli kuwa kuna nchi nyingi tu duniani zina makampuni halali ya kuchukua nguvu kazi katika baadhi ya nchi na kuwapeleka ulaya kwa mkataba maalum na mfano hauko mbali, sasa hivi pale Shule ya Vikokotoni kuna Wagiriki wahachukua vijana kwenda kufanya kazi za Ubaharia - Jee wanadanganywa na alopo madarakani si Seif Shariff. Wapemba kuwepo UK ni ajabu - ninavyoelewa wapemba ni wahangaikaji na yote hiyo ni shukrani ya ASP/CCM walowafunza kuwa wakikaa Zanzibar hawana lao kwani hawana haki - walishaona wazee wao walipokuwa wakisema- pya nsalama iyo kupigwa nsifungwe- yaani mtu anashukuru kutandikwa mijiledi lakini hakwenda jela. Kwa hivyo wapemba walioko UK au pengine ni sawa tu na wananchi wa nchi yeyote wanaotafuta maisha na UK ndio kichaka chenu, ni sawa tu na Wazimbabwe, wajamaica nk walioko huko.
 
Hivyo wewe hujui kuwa Zanzibar ni Taifa . Fanya reference ya hizo definition ulizopewa hapo. Zabzibar ni Tafa Bwana lililokuwa chini ya himaya ya usultani na British Protectorate. Mapinduzi ya 1964 yalifanyika katika Taifa la Zanzibar ambalo lilijitwalia uhuru wake. Na hilo Taifa likaungana na Taifa jengine la Tanzania-halisi kuunda Taifa moja kubwa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Haya mambo nashukuru kuwa wanasomeshwa watoto wetu. Haya nimenukuu katika vitabu vyake vya skuli ya Msingi.
 
Ah!! Kusema majukwaani. Jee waliyosema CUF majukwaani huko Pemba unayakumbuka. Walioyosema Kibanda-maiti, Mnazimmoja. Darajabovu Komba-wapya majukwaani unayakumbuka? Hizo ndiyo mbwembwe za malumbano ya jukwaani.

Yapi nikumbushe walilolisema CCM na linalohusu Muafaka nimeliandika na zaidi kuhusu Muafaka walisema hakuna Mseto hapa ladda wa Choroko na mchele (NWK Ali J. Shamhuna) nafikiri unakumbuaka sasa tueleze walichosema CUF kuhusu Muafaka na sio utaje viwanja wanavyofanyia mikutano.
 
Nimesoma maoni ya wanaJF na imenikumbusha usemi mmoja nao ni "mpaka wakati huo ambapo wanyama watapata mtu wa kuwaandikia hadithi zao simulizi zote za mbugani zitamfisia muindaji tu"

We need our own writter to tell our stories too. Labda hiyo kura ya maoni itaonyesha hadithi zetu kama tulivyofanya kule East Africa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…