Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
TAMKO LA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) KUFUATIA TAMKO LA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM KUHUSIANA NA MAZUNGUMZO YA KUTAFUTA UFUMBUZI WA KUDUMU WA MPASUKO WA KISIASA ZANZIBAR

Tarehe 17 Machi, 2008, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama Cha Wananchi (CUF) lilifanya kikao chake mjini Zanzibar ambapo lilipokea na kuridhia makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya CCM na CUF ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Siku hiyo hiyo, CUF iliwatangazia wanachama wake na Watanzania kwa jumla matokeo ya kikao hicho cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia, mjini Zanzibar.

Hiyo ilikuwa ni hatua kubwa na muhimu kutekelezwa na upande wa CUF baada ya vyama vyetu viwili kukubaliana kuwa viwasilishe makubaliano hayo kwa vikao vya juu vya maamuzi vya vyama vyetu ili kuyaridhia kabla ya kutiwa saini. Baada ya CUF kutekeleza wajibu wake, yalikuwa matarajio na imani yetu kwamba na upande wa CCM nao ungefanya wajibu wake.

Kwa mshangao na masikitiko makubwa, jana tumepokea Tamko la Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuhusiana na mazungumzo ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar ambalo kimsingi limeyakataa makubaliano yaliyofikiwa na Kamati zetu mbili.

CCM imeamua kufanya usanii wa kisiasa kwa kutumia lugha ya mzunguko, ya ubabaishaji na ya upotoshaji kwa lengo la ama kuendelea kurefusha muda hadi mwaka 2010 au kuyakataa makubaliano ambayo wajumbe wake wameshiriki kuyaandaa katika miezi 14 ya mazungumzo kati ya vyama vyetu viwili.

Hali hiyo iko wazi kwa sababu mbili kuu zifuatazo:

1. CCM imetamka ‘kuyakubali kimsingi’ mapendekezo yaliyowasilishwa na Kamati ya chama hicho inayoshiriki mazungumzo lakini wakati huo huo inazungumzia marekebisho ambayo inataka yafanywe na hivyo kuiagiza Kamati yake kukutana na wajumbe wa CUF ili kuyajadili marekebisho hayo.

Kwanza, CCM haikutaja ni maeneo gani inataka yafanyiwe marekebisho. Pili, hoja hii inashangaza kwa sababu wajumbe wa Kamati ya Mazungumzo kutoka upande wa CCM walikuwa wakiwaarifu wajumbe wa Kamati kutoka upande wa CUF kwamba wao walikuwa wakiwasilisha taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vikao vya chama vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa na pia kwa viongozi wao wa juu, Rais Jakaya Kikwete na Mheshimiwa Amani Karume, na kupata maelekezo na miongozo inayohitajika. Hata taarifa ya karibuni kabisa ya CCM iliyokuwa ikikanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba Mheshimiwa Amani Karume si kikwazo cha kufikiwa makubaliano ya muafaka iliweka mkazo na msisitizo kwamba katika kila hatua, viongozi hao wameshauriwa ipasavyo. Hatua hii ya mwisho ilikusudiwa kubariki makubaliano hayo yaliyokuwa yakifikiwa hatua kwa hatua na siyo kufungua mjadala mpya kupitia duru mpya ya mazungumzo.

2. CCM imekuja na hoja mpya kwamba iwapo mapendekezo haya yatakubaliwa, yatakuwa yanaleta mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala katika Zanzibar na hivyo yanapaswa kuridhiwa na wananchi wenyewe kwa njia ya kura ya maoni.

CCM kuleta hoja hii ni kulifanyia mzaha jambo kubwa linalohitaji umakini wa hali ya juu kwani linagusa mustakbali wa taifa letu. Muda wote wa mazungumzo ambayo yamechukua miezi 14 na yakiwa yamehusisha vikao 21, wajumbe wa Kamati ya CCM wanaoshiriki mazungumzo hawakuleta hoja hii ya kura ya maoni. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa tofauti na ilivyoelezwa, pendekezo la kutaka kura ya maoni halikuwa limeibuliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM bali lilikuwemo katika Taarifa ya Kamati ya CCM inayoshiriki mazungumzo likiwa ni pendekezo walilotaka liridhiwe na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa. Hivyo, ni wazi liliandaliwa mapema kutokana na kile Kamati hiyo ya CCM ilichokiita “kuipiku CUF katika ubunifu wa kujenga”. Kitendo cha Kamati ya CCM kuwasilisha kitu kipya nje ya makubaliano yaliyofikiwa ni upotoshaji mkubwa wenye lengo la kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa kama hili linalogusa maslahi ya taifa na watu wake moja kwa moja. Na iwapo pendekezo hilo lina nia njema ya kuwashirikisha wananchi, kwa nini wajumbe wa Kamati ya CCM wasiliwasilishe katika vikao vya mazungumzo na badala yake wakaamua kuliingiza kama mtego wa kisiasa wenye lengo la “kuipiku CUF”?

Hoja nyengine ni kwamba kura ya maoni hiyo itaendeshwa na chombo kipi na kwa utaratibu upi hasa ikitiliwa maanani tayari CCM na CUF wamekubaliana kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura vina matatizo ya msingi ambayo yanahitaji kurekebishwa? Ni vipi basi Tume hiyo chini ya Daftari bovu liliopo itaweza kuendesha kura ya maoni ambayo itakuwa huru na ya haki?

Sisi tunaona suala hilo ni mbinu chafu tu yenye lengo la kuendelea kupoteza muda ili makubaliano yaliyofikiwa yasiweze kutiwa saini na utekelezaji kuanza. Kwa lugha yao CCM waliyoandika katika waraka wao ni njia ya “kuipiku CUF” na kamwe haikusudiwi kupata maoni ya wananchi.

Kwa msingi huo CUF haikubaliani na hoja hizo zote mbili.

Ni lazima tukiri kuwa tumeshtushwa sana na kiwango hiki cha CCM kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa kama hili. Lakini pia tumepata faraja kuwa Watanzania sasa wameweza kujua ni nani kati ya CCM na CUF asiyeitakia mema nchi hii. Wamejua ni nani kati ya CCM na CUF asiyetaka amani na utulivu katika nchi hii. Wamejua ni nani kati ya CCM na CUF asiyetaka siasa za maelewano na mashirikiano katika nchi hii.

Sasa ni wazi kwamba CCM iliingia katika mazungumzo haya ikiwa haina dhamira ya kweli na ya dhati ya kuupatia ufumbuzi wa kweli mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Inaonekana lengo pekee la CCM katika mazungumzo haya lilikuwa ni kuwahadaa Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwa kujidanganya kwamba wangeweza kuidhibiti kisiasa CUF kupitia utaratibu wa kuwapa matumaini ya uongo (strategic engagement) na kuyarefusha mazungumzo hayo kadiri inavyowezekana hadi kipindi kinachokaribia uchaguzi mkuu ujao pasina kuchukua hatua zozote za maana zenye kulenga kutoa ufumbuzi wa kweli wa mpasuko uliopo. CCM imeonesha wazi wazi kuwa haiitakii mema Tanzania yetu na wala haitaki kuona umoja wa kitaifa na utulivu wa kudumu vinapatikana Zanzibar ambayo ni sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa upande mwengine, Watanzania wote na jumuiya ya kimataifa ni mashahidi kuwa CUF imefanya kila liliomo katika uwezo wake kuinusuru hali tete ya kisiasa Zanzibar isichafuke. CUF imechukua kila juhudi kuona mazungumzo haya yanafanikiwa. Imetoa kila ushirikiano unaohitajika kwa CCM na hata kuachia madai yake makuu (kutoa ‘concessions’) ili kuyanusuru mazungumzo hayo na kuyafanikisha.

CUF imeonesha ustahamilivu, ustaarabu na uelewa mkubwa katika mazungumzo haya. Tumeweza kukubaliana na CCM kwa kila hatua tuliyoombwa tuwe na subira ili kupisha mambo kadhaa ya kisiasa yapite. Mara nyengine, hata bila ya kutuomba, sisi wenyewe tumeonyesha uelewa na kuwapa nafasi pale yalipoibuka matukio ya kisiasa ambayo hayakutarajiwa na ambayo tulihisi yanahitaji tuwape muda wenzetu. CCM haionekani kujali au kuthamini juhudi hizo na imeamua kuzipiga teke.

Kama tulivyowahi kusema, hatukufanya hivyo kwa sababu CUF ni dhaifu kisiasa kama ambavyo CCM wangependa kujidanganya. Tulifanya yote hayo kwa sababu tunaongozwa na dhamira njema ya kuhakikisha nchi yetu inabaki katika hali ya amani na utulivu huku tukiamini kwa dhati kwamba mazungumzo ndiyo njia pekee ya kistaarabu ya kumaliza tofauti au migogoro ya kisiasa na kijamii. Lakini ni lazima tusisitize kuwa mazungumzo yenye lengo hilo ni lazima yawe mazungumzo makini yanayoongozwa na utashi wa kweli wa kisiasa uliojengeka juu ya nia njema na kuheshimiana baina ya pande zinazohusika. Hilo limekosekana kwa upande wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Kufuatia misukosuko iliyoyakumba mazungumzo haya mwaka jana, Rais Kikwete, alitoa taarifa kwa umma tarehe 14 Agosti, 2007 akiuomba upande wa CUF ukubali kuendelea na mazungumzo na akiwahakikishia Watanzania kuwa angechukua hatua kuona yanakamilishwa na yanafanikishwa. Wakati akiwahutubia Mabalozi wa nchi za nje wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya, mapema mwaka huu, Rais Kikwete aliwaeleza kwamba mazungumzo yamefikia ukingoni na kwamba karibu suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar litakuwa historia. Kauli hiyo ilipokewa kwa matumaini makubwa na wananchi ambao wamekuwa wakifuatilia kwa makini kila hatua ya mazungumzo yetu. Ni bahati mbaya kwamba Rais Kikwete ameyaangusha matumaini hayo ya Watanzania kama ambavyo ameyaangusha matumaini yao katika masuala mengine yote aliyowaahidi wakati anaomba kura na anaingia madarakani.

CUF imevunjwa moyo sana na Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM. Imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa nchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa imetetereka sana. Kitendo cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya Uenyekiti wake kukataa kupitisha makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya CCM na CUF na badala yake kuja na hoja mpya za ajabu ajabu zenye lengo la “kuipiku CUF” kisiasa kunamwonyesha Rais Kikwete ama hakuwa mkweli na mwaminifu tokea mwanzoni na kwamba alikuwa akifanya usanii wa kisiasa wakati alipotangaza kuwa anasononeshwa sana na mpasuko wa kisiasa Zanzibar au ni kiongozi dhaifu asiye na udhibiti wa chama anachokiongoza. Yote mawili hayampi sifa za kiongozi ambaye nchi inamhitaji inapopita katika vipindi vigumu.

Kama tulivyofanya mwaka jana, ni vyema tumkumbushe tena Mheshimiwa Jakaya Kikwete kauli yake mwenyewe aliyoitoa wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 16 Septemba, 2003 wakati anafungua Mkutano wa Kumi na Moja wa Hali ya Siasa Tanzania ambao ulihusu ‘Udhibiti na Utatuzi wa Migogoro’, pale aliposema:

“…[N]aelewa kuwa utaratibu wa kung’amua dalili za migogoro hauwezi kuwa na manufaa kama haukuambatana na vitendo vya haraka. Taarifa za dalili za uendelezaji wa migogoro zinapopatikana zitakuwa hazina manufaa katika uzuiaji wa migogoro hiyo kama zitashughulikiwa kwa njia ya mlolongo wa uamuzi wa kirasimu ambao unaweza kuchelewesha utekelezaji hadi migogoro inapotokea. Kwa hiyo ni wazi kuwa upatikanaji wa taarifa za dalili za migogoro unakuwa wa maana katika uzuiaji wa migogoro kama mara zipatikanapo, zinatafsiriwa kwa vitendo. Mtiririko wa hoja hapa unapaswa kuwa “dalili za mwanzo kujumlisha na vitendo halisi ni sawa sawa na uzuiaji wa migogoro.” Ili haya yatokee unahitaji kuharakisha au kurekebisha utaratibu wa utoaji wa maamuzi ili dalili za mwanzo ziweze kutafsirika kwa vitendo haraka iwezekanavyo.”

Maamuzi ya Chama chake kupitia kikao alichokiongoza yeye mwenyewe akiwa Mwenyekiti wake hayaonyeshi kuwa anayazingatia haya aliyowaasa wenzake mwaka 2003 maana maamuzi ya Halmshauri Kuu ya Taifa yanawakilisha hasa “mlolongo wa maamuzi ya kirasimu” ambayo kama alivyosema hayawezi kuwa msingi wa utatuzi wa mgogoro. Inasikitisha zaidi kwa Rais Kikwete kuwatangazia Watanzania na ulimwengu kuwa amefanikiwa kuwakutanisha Rais Mwai Kibaki na Mheshimiwa Raila Odinga wa Kenya na kufanikisha kufikiwa kwa makubaliano kati ya ODM na PNU nchini humo lakini anashindwa kulifanikisha hilo nchini mwake ndani ya chama anachokiongoza mwenyewe na kati ya CCM na CUF. Rais Kikwete anaona fakhari kuwa Tanzania imeongoza Jeshi la Umoja wa Afrika (AU) katika operesheni ya kijeshi iliyopewa jina la “Operesheni Demokrasia” kisiwani Anjouan, nchini Comoro lakini ameshindwa kuongoza operesheni ya kisiasa ya kusimamisha demokrasia visiwani Zanzibar.

Rais anapaswa ajue kuwa heshima ya ofisi yake na uadilifu wake binafsi ameutia doa kubwa kutokana na kushindwa kusimamia kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa kwa Watanzania kupitia hotuba yake ya Desemba 30, 2005 Bungeni na pia ahadi aliyoitoa na kuirejea mara kadhaa kwa marafiki wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika ziara zake za nje ya nchi kila mara pale alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa Zanzibar.

MSIMAMO WETU:

1. Chama Cha Wananchi (CUF) hakiko tayari kushirikiana na CCM kuwafanyia Watanzania usanii wa kisiasa. Huu sio utaratibu wa CUF katika uendeshaji wa siasa. Kwa CUF, siasa si proaganda zilizopitwa na wakati bali ni utumishi wa dhati na uliotukuka kwa umma uliowaamini viongozi wake. Kwa msingi huo, CUF haitakubali kurejea katika mazungumzo kwa utaratibu inaoutaka CCM.

2. CUF kinakitaka CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya vyama vyetu viwili na endapo kweli Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho “ imeyakubali kimsingi” makubaliano yaliyofikishwa kwake kama ilivyosema taarifa yake, basi kikubali kutia saini makubaliano hayo na utekelezaji wa yaliyokubaliwa uanze mara moja.

3. Kinyume na hayo, CUF inatoa wito kwa marafiki wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti, za uhakika na za haraka kuingilia kati suala hili ili kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa yanatiwa saini. Baada ya Tanzania yenyewe kushindwa katika utatuzi wa mgogoro wake huu wa muda mrefu, sasa ni wakati muafaka kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati kwa kuchagua Mpatanishi wa Kimataifa anayeheshimika kuja kuyasimamia hadi kuyafikisha ukingoni kwa kuhakikisha makubaliano ya dhati yanafikiwa yatakayotoa ufumbuzi wa kweli na wa haki wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar.

4. CUF inatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuepuka fedheha iliyoipata katika nchi nyengine za Kiafrika ambazo iliziachia hadi hali ikachafuka na ndipo ikaingilia kati. Hali ya Zanzibar ni mbaya. Ilitulia kwa sababu ya matumaini ya Wazanzibari na Watanzania kwamba mazungumzo ya CCM na CUF yataleta suluhisho la utulivu na umoja. Makubaliano yaliyofikiwa yanapokosa uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuyakamilisha, yanahitaji kuona jumuiya ya kimataifa inaingilia kati kwa hatua za wazi na madhubuti kuinusuru Zanzibar na Tanzania isitumbukie kule nchi nyengine za Kiafrika zilipotumbukia.

5. Wakati tunawashukuru kwa dhati viongozi wa vyama vyengine vya siasa, viongozi wa dini, taasisi na jumuiya za kijamii, mabalozi wa nchi za nje wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania na vyombo vya habari hususan magazeti huru kwa mchango wao mkubwa walioutoa na ambao ulisaidia kuyafikisha mazungumzo hadi hatua ya kukamilishwa, CUF tunatoa wito tena kwao kuendelea kutoa ushirikiano wao na kutimiza wajibu wao kuona mgogoro huu unamalizwa kwa njia za amani na za haki.

6. CUF inawataka wanachama na wapenzi wake pamoja na Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki wakijua kuwa CUF iko upande wa amani, ukweli na haki na siku zote upande wa amani, ukweli na haki utashinda.

7. Kwa jinsi inavyoyachezea masuala mazito yanayohusu maslahi ya taifa kama ilivyodhihirika kwa mambo yote makubwa yaliyojitokeza hivi karibuni, ni wazi kuwa CCM imepoteza uhalali wa kuongoza nchi na wakati sasa umefika wa Watanzania kuchagua chama makini kitakachoipa Tanzania uongozi makini unaohitajika.

HAKI SAWA KWA WOTE

SEIF SHARIF HAMAD
KATIBU MKUU – CUF

Dar es Salaam
01 Aprili, 2008
 
Attachments

Sisiemu ilijitoa (na kutaka kuipeleka kwa wananchi) kabla ya kaf, haishangazi!
This is our tz.
 
Finally they went for the jagular.. Kikwete.. ameshindwa kusuluhisha mgogoro wa Zanzibar na ameonesha udhaifu wa uongozi.
 
waliokuwa wanalitaka tamko napenda kuwataarifu rasmi kuwa nimeliweka, nimelianzishia thread yake, nimelimwaga kama lilivyo na pia kuna document ya attachment.
soma elewa, changia
 
Iam not a CUF supporter, but Iam greatly dissapointed by my President for failure to take serious and meaningful decision at the critical juncture of our nation. Make no mistake all these countries in conflicts on our continent, it was a result of such selfishness and short sightedness of their leaders. This is a tragedy!

For how long shall we Africans suffer from our own greedy and selfishness? is there any mad person who believe that a president who wins election by a margin of 1% can rule without his challenger?-not even in the Western World, sembuse Africa? I guess Makamba siyo Msomi lakini surely he should use his form four education to understand what is at stake in Zanzibar.

As a Tanzanian, I strongly believe CCM and CUF must make painful and hard decisions for Zanzibar to be credibly governable. Short of that we should brace for unknowns.

Walioishiwa hoja wataanza kusema eti CUF ni wadini, lakini kwa wanaoona mambo, CCM must realize that Tanzania is for Tanzanians and not for CCM faithfuls only.
 
Tatizo la CCM ni wahuni na tatizo la CUF ni wachochezi wa uvunjaji amani.

Kwanini CUF wasipoelewana na CCM wanakimbilia maneno ya uvunjaji Amani??? kwani Amani imejingwa na CUF??? Viongozi gani hawa wanaposhidwa kuelewana yani alternative yao ni VITA na kuvunja amani.Inamaana hata hawana plan B wao ni maguvu tu Ni rahisi sana kuona CUF hawana kitu na msiwape nchi .

Chama chenye kilicho na maono ya kivitavita kisipewe nafasi

Naona sasa tunaachakujadili hoja na tunaleta ushabiki, unajuaje kuwa hiyo ndiyo plan B ya C.U.F? maana tumeona mara nyingi viongozi wakirudisha maamuzi kwa wananchi. Suala la nguvu naamini kila mtu anajua chama gani kina nguvu.
 
CCM must realize that Tanzania is for Tanzanians and not for CCM faithfuls only.

Sawa ni vyema pia nawe ukaona kuwa Zanzibar ni ya Wazanzibari wote siyo ya CUF pekee. Kule wapo wengi tu(wasio CUF) ambao ni pamoja na kibao wasio na Chama chochote. Sasa kwa nini hutaki na hao wengine washiriki katika muwafaka. kwa nini wasitakiwe maoni yao?
 
Kweli kabisa. Moja kati ya makosa makubwa ambayo CCM na CUF wamelifanya ni kuhodhi mchakato wa kutafuta muafaka kana kwambza Zanzibar ni ya CCM na CUF tu. Inabidi watafute namna ya kutafuta muakaka wa kitaifa na si kati ya CUF na CCM akwa sababu matatizo yaliyopo hayawaathiri CCM na CUF peke yao
 
Naona sasa tunaachakujadili hoja na tunaleta ushabiki, unajuaje kuwa hiyo ndiyo plan B ya C.U.F? maana tumeona mara nyingi viongozi wakirudisha maamuzi kwa wananchi. Suala la nguvu naamini kila mtu anajua chama gani kina nguvu.

kwa hiyo CUF wamekubaliana na hoja ya CCM wananchi wapige kura ya maoni BIG UP!!!!!

Ama wanalirudisha kwa wananchi kwa mtindo upi na wananchi walifanyie nini ??

Nyie angaleini CUF wasipokubaliana kimasilahi suala hilo wanaliunganisha kiujanja ujanja na suala la Uvunjaji Amani ili kuamisha hisia za watu.

Mbona maalimu Seif wakati anarudishiwa fungu lake na CCM hatukusikia maswala ya uvujanji amani wala swala hilo kurudishwa kwa wananchi ili waamue maalimu SEIF apokee hizo fedha kutoka serikali ya CCM ama la!!!

Plan B ya CUF nikulirudisha wananchi waingie barabarani ili wakakutane na uhuni mwingine mkali baada ya wananchi kuumia wao wanaangalia namna ya kutumia uhuni huo kupata madaraka na fedha.
 
TAMKO LA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) KUFUATIA TAMKO LA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM KUHUSIANA NA MAZUNGUMZO YA KUTAFUTA UFUMBUZI WA KUDUMU WA MPASUKO WA KISIASA ZANZIBAR

Tarehe 17 Machi, 2008, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama Cha Wananchi (CUF) lilifanya kikao chake mjini Zanzibar ambapo lilipokea na kuridhia makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya CCM na CUF ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Siku hiyo hiyo, CUF iliwatangazia wanachama wake na Watanzania kwa jumla matokeo ya kikao hicho cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia, mjini Zanzibar.

Hiyo ilikuwa ni hatua kubwa na muhimu kutekelezwa na upande wa CUF baada ya vyama vyetu viwili kukubaliana kuwa viwasilishe makubaliano hayo kwa vikao vya juu vya maamuzi vya vyama vyetu ili kuyaridhia kabla ya kutiwa saini. Baada ya CUF kutekeleza wajibu wake, yalikuwa matarajio na imani yetu kwamba na upande wa CCM nao ungefanya wajibu wake.

Kwa mshangao na masikitiko makubwa, jana tumepokea Tamko la Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuhusiana na mazungumzo ya kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar ambalo kimsingi limeyakataa makubaliano yaliyofikiwa na Kamati zetu mbili.

CCM imeamua kufanya usanii wa kisiasa kwa kutumia lugha ya mzunguko, ya ubabaishaji na ya upotoshaji kwa lengo la ama kuendelea kurefusha muda hadi mwaka 2010 au kuyakataa makubaliano ambayo wajumbe wake wameshiriki kuyaandaa katika miezi 14 ya mazungumzo kati ya vyama vyetu viwili.

Hali hiyo iko wazi kwa sababu mbili kuu zifuatazo:

1. CCM imetamka ‘kuyakubali kimsingi’ mapendekezo yaliyowasilishwa na Kamati ya chama hicho inayoshiriki mazungumzo lakini wakati huo huo inazungumzia marekebisho ambayo inataka yafanywe na hivyo kuiagiza Kamati yake kukutana na wajumbe wa CUF ili kuyajadili marekebisho hayo.

Kwanza, CCM haikutaja ni maeneo gani inataka yafanyiwe marekebisho. Pili, hoja hii inashangaza kwa sababu wajumbe wa Kamati ya Mazungumzo kutoka upande wa CCM walikuwa wakiwaarifu wajumbe wa Kamati kutoka upande wa CUF kwamba wao walikuwa wakiwasilisha taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vikao vya chama vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa na pia kwa viongozi wao wa juu, Rais Jakaya Kikwete na Mheshimiwa Amani Karume, na kupata maelekezo na miongozo inayohitajika. Hata taarifa ya karibuni kabisa ya CCM iliyokuwa ikikanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba Mheshimiwa Amani Karume si kikwazo cha kufikiwa makubaliano ya muafaka iliweka mkazo na msisitizo kwamba katika kila hatua, viongozi hao wameshauriwa ipasavyo. Hatua hii ya mwisho ilikusudiwa kubariki makubaliano hayo yaliyokuwa yakifikiwa hatua kwa hatua na siyo kufungua mjadala mpya kupitia duru mpya ya mazungumzo.

2. CCM imekuja na hoja mpya kwamba iwapo mapendekezo haya yatakubaliwa, yatakuwa yanaleta mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala katika Zanzibar na hivyo yanapaswa kuridhiwa na wananchi wenyewe kwa njia ya kura ya maoni.

CCM kuleta hoja hii ni kulifanyia mzaha jambo kubwa linalohitaji umakini wa hali ya juu kwani linagusa mustakbali wa taifa letu. Muda wote wa mazungumzo ambayo yamechukua miezi 14 na yakiwa yamehusisha vikao 21, wajumbe wa Kamati ya CCM wanaoshiriki mazungumzo hawakuleta hoja hii ya kura ya maoni. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa tofauti na ilivyoelezwa, pendekezo la kutaka kura ya maoni halikuwa limeibuliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM bali lilikuwemo katika Taarifa ya Kamati ya CCM inayoshiriki mazungumzo likiwa ni pendekezo walilotaka liridhiwe na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa. Hivyo, ni wazi liliandaliwa mapema kutokana na kile Kamati hiyo ya CCM ilichokiita “kuipiku CUF katika ubunifu wa kujenga”. Kitendo cha Kamati ya CCM kuwasilisha kitu kipya nje ya makubaliano yaliyofikiwa ni upotoshaji mkubwa wenye lengo la kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa kama hili linalogusa maslahi ya taifa na watu wake moja kwa moja. Na iwapo pendekezo hilo lina nia njema ya kuwashirikisha wananchi, kwa nini wajumbe wa Kamati ya CCM wasiliwasilishe katika vikao vya mazungumzo na badala yake wakaamua kuliingiza kama mtego wa kisiasa wenye lengo la “kuipiku CUF”?

Hoja nyengine ni kwamba kura ya maoni hiyo itaendeshwa na chombo kipi na kwa utaratibu upi hasa ikitiliwa maanani tayari CCM na CUF wamekubaliana kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura vina matatizo ya msingi ambayo yanahitaji kurekebishwa? Ni vipi basi Tume hiyo chini ya Daftari bovu liliopo itaweza kuendesha kura ya maoni ambayo itakuwa huru na ya haki?

Sisi tunaona suala hilo ni mbinu chafu tu yenye lengo la kuendelea kupoteza muda ili makubaliano yaliyofikiwa yasiweze kutiwa saini na utekelezaji kuanza. Kwa lugha yao CCM waliyoandika katika waraka wao ni njia ya “kuipiku CUF” na kamwe haikusudiwi kupata maoni ya wananchi.

Kwa msingi huo CUF haikubaliani na hoja hizo zote mbili.

Ni lazima tukiri kuwa tumeshtushwa sana na kiwango hiki cha CCM kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa kama hili. Lakini pia tumepata faraja kuwa Watanzania sasa wameweza kujua ni nani kati ya CCM na CUF asiyeitakia mema nchi hii. Wamejua ni nani kati ya CCM na CUF asiyetaka amani na utulivu katika nchi hii. Wamejua ni nani kati ya CCM na CUF asiyetaka siasa za maelewano na mashirikiano katika nchi hii.

Sasa ni wazi kwamba CCM iliingia katika mazungumzo haya ikiwa haina dhamira ya kweli na ya dhati ya kuupatia ufumbuzi wa kweli mpasuko wa kisiasa Zanzibar. Inaonekana lengo pekee la CCM katika mazungumzo haya lilikuwa ni kuwahadaa Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwa kujidanganya kwamba wangeweza kuidhibiti kisiasa CUF kupitia utaratibu wa kuwapa matumaini ya uongo (strategic engagement) na kuyarefusha mazungumzo hayo kadiri inavyowezekana hadi kipindi kinachokaribia uchaguzi mkuu ujao pasina kuchukua hatua zozote za maana zenye kulenga kutoa ufumbuzi wa kweli wa mpasuko uliopo. CCM imeonesha wazi wazi kuwa haiitakii mema Tanzania yetu na wala haitaki kuona umoja wa kitaifa na utulivu wa kudumu vinapatikana Zanzibar ambayo ni sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa upande mwengine, Watanzania wote na jumuiya ya kimataifa ni mashahidi kuwa CUF imefanya kila liliomo katika uwezo wake kuinusuru hali tete ya kisiasa Zanzibar isichafuke. CUF imechukua kila juhudi kuona mazungumzo haya yanafanikiwa. Imetoa kila ushirikiano unaohitajika kwa CCM na hata kuachia madai yake makuu (kutoa ‘concessions’) ili kuyanusuru mazungumzo hayo na kuyafanikisha.

CUF imeonesha ustahamilivu, ustaarabu na uelewa mkubwa katika mazungumzo haya. Tumeweza kukubaliana na CCM kwa kila hatua tuliyoombwa tuwe na subira ili kupisha mambo kadhaa ya kisiasa yapite. Mara nyengine, hata bila ya kutuomba, sisi wenyewe tumeonyesha uelewa na kuwapa nafasi pale yalipoibuka matukio ya kisiasa ambayo hayakutarajiwa na ambayo tulihisi yanahitaji tuwape muda wenzetu. CCM haionekani kujali au kuthamini juhudi hizo na imeamua kuzipiga teke.

Kama tulivyowahi kusema, hatukufanya hivyo kwa sababu CUF ni dhaifu kisiasa kama ambavyo CCM wangependa kujidanganya. Tulifanya yote hayo kwa sababu tunaongozwa na dhamira njema ya kuhakikisha nchi yetu inabaki katika hali ya amani na utulivu huku tukiamini kwa dhati kwamba mazungumzo ndiyo njia pekee ya kistaarabu ya kumaliza tofauti au migogoro ya kisiasa na kijamii. Lakini ni lazima tusisitize kuwa mazungumzo yenye lengo hilo ni lazima yawe mazungumzo makini yanayoongozwa na utashi wa kweli wa kisiasa uliojengeka juu ya nia njema na kuheshimiana baina ya pande zinazohusika. Hilo limekosekana kwa upande wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Kufuatia misukosuko iliyoyakumba mazungumzo haya mwaka jana, Rais Kikwete, alitoa taarifa kwa umma tarehe 14 Agosti, 2007 akiuomba upande wa CUF ukubali kuendelea na mazungumzo na akiwahakikishia Watanzania kuwa angechukua hatua kuona yanakamilishwa na yanafanikishwa. Wakati akiwahutubia Mabalozi wa nchi za nje wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya, mapema mwaka huu, Rais Kikwete aliwaeleza kwamba mazungumzo yamefikia ukingoni na kwamba karibu suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar litakuwa historia. Kauli hiyo ilipokewa kwa matumaini makubwa na wananchi ambao wamekuwa wakifuatilia kwa makini kila hatua ya mazungumzo yetu. Ni bahati mbaya kwamba Rais Kikwete ameyaangusha matumaini hayo ya Watanzania kama ambavyo ameyaangusha matumaini yao katika masuala mengine yote aliyowaahidi wakati anaomba kura na anaingia madarakani.

CUF imevunjwa moyo sana na Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM. Imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa nchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa imetetereka sana. Kitendo cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya Uenyekiti wake kukataa kupitisha makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya CCM na CUF na badala yake kuja na hoja mpya za ajabu ajabu zenye lengo la “kuipiku CUF” kisiasa kunamwonyesha Rais Kikwete ama hakuwa mkweli na mwaminifu tokea mwanzoni na kwamba alikuwa akifanya usanii wa kisiasa wakati alipotangaza kuwa anasononeshwa sana na mpasuko wa kisiasa Zanzibar au ni kiongozi dhaifu asiye na udhibiti wa chama anachokiongoza. Yote mawili hayampi sifa za kiongozi ambaye nchi inamhitaji inapopita katika vipindi vigumu.

Kama tulivyofanya mwaka jana, ni vyema tumkumbushe tena Mheshimiwa Jakaya Kikwete kauli yake mwenyewe aliyoitoa wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 16 Septemba, 2003 wakati anafungua Mkutano wa Kumi na Moja wa Hali ya Siasa Tanzania ambao ulihusu ‘Udhibiti na Utatuzi wa Migogoro’, pale aliposema:

“…[N]aelewa kuwa utaratibu wa kung’amua dalili za migogoro hauwezi kuwa na manufaa kama haukuambatana na vitendo vya haraka. Taarifa za dalili za uendelezaji wa migogoro zinapopatikana zitakuwa hazina manufaa katika uzuiaji wa migogoro hiyo kama zitashughulikiwa kwa njia ya mlolongo wa uamuzi wa kirasimu ambao unaweza kuchelewesha utekelezaji hadi migogoro inapotokea. Kwa hiyo ni wazi kuwa upatikanaji wa taarifa za dalili za migogoro unakuwa wa maana katika uzuiaji wa migogoro kama mara zipatikanapo, zinatafsiriwa kwa vitendo. Mtiririko wa hoja hapa unapaswa kuwa “dalili za mwanzo kujumlisha na vitendo halisi ni sawa sawa na uzuiaji wa migogoro.” Ili haya yatokee unahitaji kuharakisha au kurekebisha utaratibu wa utoaji wa maamuzi ili dalili za mwanzo ziweze kutafsirika kwa vitendo haraka iwezekanavyo.”

Maamuzi ya Chama chake kupitia kikao alichokiongoza yeye mwenyewe akiwa Mwenyekiti wake hayaonyeshi kuwa anayazingatia haya aliyowaasa wenzake mwaka 2003 maana maamuzi ya Halmshauri Kuu ya Taifa yanawakilisha hasa “mlolongo wa maamuzi ya kirasimu” ambayo kama alivyosema hayawezi kuwa msingi wa utatuzi wa mgogoro. Inasikitisha zaidi kwa Rais Kikwete kuwatangazia Watanzania na ulimwengu kuwa amefanikiwa kuwakutanisha Rais Mwai Kibaki na Mheshimiwa Raila Odinga wa Kenya na kufanikisha kufikiwa kwa makubaliano kati ya ODM na PNU nchini humo lakini anashindwa kulifanikisha hilo nchini mwake ndani ya chama anachokiongoza mwenyewe na kati ya CCM na CUF. Rais Kikwete anaona fakhari kuwa Tanzania imeongoza Jeshi la Umoja wa Afrika (AU) katika operesheni ya kijeshi iliyopewa jina la “Operesheni Demokrasia” kisiwani Anjouan, nchini Comoro lakini ameshindwa kuongoza operesheni ya kisiasa ya kusimamisha demokrasia visiwani Zanzibar.

Rais anapaswa ajue kuwa heshima ya ofisi yake na uadilifu wake binafsi ameutia doa kubwa kutokana na kushindwa kusimamia kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa kwa Watanzania kupitia hotuba yake ya Desemba 30, 2005 Bungeni na pia ahadi aliyoitoa na kuirejea mara kadhaa kwa marafiki wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika ziara zake za nje ya nchi kila mara pale alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa Zanzibar.

MSIMAMO WETU:

1. Chama Cha Wananchi (CUF) hakiko tayari kushirikiana na CCM kuwafanyia Watanzania usanii wa kisiasa. Huu sio utaratibu wa CUF katika uendeshaji wa siasa. Kwa CUF, siasa si proaganda zilizopitwa na wakati bali ni utumishi wa dhati na uliotukuka kwa umma uliowaamini viongozi wake. Kwa msingi huo, CUF haitakubali kurejea katika mazungumzo kwa utaratibu inaoutaka CCM.

2. CUF kinakitaka CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya vyama vyetu viwili na endapo kweli Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho “ imeyakubali kimsingi” makubaliano yaliyofikishwa kwake kama ilivyosema taarifa yake, basi kikubali kutia saini makubaliano hayo na utekelezaji wa yaliyokubaliwa uanze mara moja.

3. Kinyume na hayo, CUF inatoa wito kwa marafiki wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti, za uhakika na za haraka kuingilia kati suala hili ili kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa yanatiwa saini. Baada ya Tanzania yenyewe kushindwa katika utatuzi wa mgogoro wake huu wa muda mrefu, sasa ni wakati muafaka kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati kwa kuchagua Mpatanishi wa Kimataifa anayeheshimika kuja kuyasimamia hadi kuyafikisha ukingoni kwa kuhakikisha makubaliano ya dhati yanafikiwa yatakayotoa ufumbuzi wa kweli na wa haki wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar.

4. CUF inatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuepuka fedheha iliyoipata katika nchi nyengine za Kiafrika ambazo iliziachia hadi hali ikachafuka na ndipo ikaingilia kati. Hali ya Zanzibar ni mbaya. Ilitulia kwa sababu ya matumaini ya Wazanzibari na Watanzania kwamba mazungumzo ya CCM na CUF yataleta suluhisho la utulivu na umoja. Makubaliano yaliyofikiwa yanapokosa uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuyakamilisha, yanahitaji kuona jumuiya ya kimataifa inaingilia kati kwa hatua za wazi na madhubuti kuinusuru Zanzibar na Tanzania isitumbukie kule nchi nyengine za Kiafrika zilipotumbukia.

5. Wakati tunawashukuru kwa dhati viongozi wa vyama vyengine vya siasa, viongozi wa dini, taasisi na jumuiya za kijamii, mabalozi wa nchi za nje wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania na vyombo vya habari hususan magazeti huru kwa mchango wao mkubwa walioutoa na ambao ulisaidia kuyafikisha mazungumzo hadi hatua ya kukamilishwa, CUF tunatoa wito tena kwao kuendelea kutoa ushirikiano wao na kutimiza wajibu wao kuona mgogoro huu unamalizwa kwa njia za amani na za haki.

6. CUF inawataka wanachama na wapenzi wake pamoja na Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki wakijua kuwa CUF iko upande wa amani, ukweli na haki na siku zote upande wa amani, ukweli na haki utashinda.

7. Kwa jinsi inavyoyachezea masuala mazito yanayohusu maslahi ya taifa kama ilivyodhihirika kwa mambo yote makubwa yaliyojitokeza hivi karibuni, ni wazi kuwa CCM imepoteza uhalali wa kuongoza nchi na wakati sasa umefika wa Watanzania kuchagua chama makini kitakachoipa Tanzania uongozi makini unaohitajika.

HAKI SAWA KWA WOTE

SEIF SHARIF HAMAD
KATIBU MKUU – CUF

Dar es Salaam
01 Aprili, 2008

CCM is irresponsible in this matter. Congrats CUF political maturity. Now, its time to engage all partners towards a government of national unity and a sustainable solution to Zanzibar impasse!

JJ
 
Kikwete, please stop dithering. Be smart. Maana mpaka hapo ulipofika huna legacy yoyote. Kuwachukulia hatua mifasadi, umetoka kapa mpaka sasa, hata hili la muafaka nalo unashindwa kulitolea msimamo wewe kama raisi?? Sasa sijui tukuweke katika kundi gani??? No wonder mafisadi wanarusha roho zao kama kawaida.
 
Makapu kidogo umenichanganya hapa .Hivi CUF kusema maamuzi wanawaachia wananchi na wanachama wa Chama hao ni kuvunja amani? Amani nadhani inavunjwa na CCM kwa uwafanya Watanzania wa Zanzibar ni wajinga kiasi hicho .Mara zote ni CCM wamekuja na maneno mara CUF ya waarabu, mara wameleta silaha nchini , mara chama cha kidini etc etc .Nashangaa Makapu nisaidie kufafanua tafadhali.

Tunajua CCM wahuni lakini soma habari hii uone jinsi plan B ya CUF ilivyo.

Habari za kawaida
Posted Date::3/31/2008
CUF wadai Rais Kikwete anachezea amani ya Zanzibar
Muhibu Said, Dar na Salma Said, Zanzibar

BAADHI ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wa Chama cha Wananchi Zanzibar, wamedai kuwa Rais Jakaya Kikwete anachezea amani ya visiwani hapa.

Kauli hiyo, waliitoa jana kwa nyakati tofauti wakati wakitoa maoni yao kuhusiana na tamko la mwafaka wa kiasiasa lilitolewa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kilichomalizika juzi katika Kijiji cha Butiama mkoani Mara.

Mwakilishi wa Viti Maalum (CUF), Zakia Omar alisema hakuna dhamira ya kweli katika kuutatua mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kutokana na tamko hilo la CCM.

Alisema kuna maamuzi mengi tu ambayo serikali ya CCM imekuwa ikiyachukua bila hata ya kuwashirikisha wananchi, na inakuwaje hili la mwafaka, washirikishwe wananchi.

?Maamuzi mengi yameamuliwa bila ya kutushirikisha sisi wananchi leo wanatwambia kupigwe kura ya maoni... mimi naona kama wana- 'bytime' tu," alisema mwakilishi huyo.

Alitaja baadhi ya maamuzi yaliyowafikiwa bila ya kuwashirikisha wananchi kuwa ni kujiuzulu kwa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi bila ya kuchukuliwa maoni ya mtu yeyote.

Mwakilishi huyo, alisema kwa mujibu wa hati ya muungano, Rais wa Zanzibar, anakuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, lakini kufuatia mabadiliko ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, wamepitisha vifungu na kumuondolea madaraka bila ya kuwapo kura ya maoni pamoja na maamuzi mengi yakiwemo yale ya kupeleka majeshi ya Tanzania katika vita vya Somalia na Comoro.

Kwa upande wake, Mansour Ali Yusuf, alisema inaonekana kana kwamba mbinu hiyo ya kutaka kupata kura ya maoni, ni mchakato wa kuhakikisha kwamba, watu wachache wateule wanaendelea kuiongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) , wakisaidiwa na Serikali ya Muungano, iliyotumika ni mbinu ya kuwadanganya wananchi kuwa suala hilo ni gumu na haliwezi kupatiwa uamuzi wa haraka bila ya kuwepo kura ya maoni.

Naye Yussuf, alisema sio kweli kama Kikwete hawezi kutafuta suluhu isipokuwa anachofanya ni kuwalinda wahafidhina ambao kama watapata nafasi wangependa watawale milele.

Baadhi ya wananchi jana walikuwa katika mijadala mikali katika kila sehemu ambapo baadhi yao walisema sasa Rais Kikwete anataka kucheza na amani kwa kuwaachia viongozi wa Zanzibar kufanya maaamuzi ya kihuni.

? Kilichoamuliwa Butiama, ni uhuni na sasa wanataka kutuchagulia nchi. Maana hatutakubali... wanataka yale yaliyotokea Kenya sasa yaje Zanzibar,? alisema mzee mmoja wa makamu katika Soko la Darajani.

Mapema wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi wa CUF, jana asubuhi, walitoka nje ya kikao cha Baraza hilo wakati kikiendelea, kuitikia wito wa chama hicho wa kuhudhuria kikao cha dharura.

Kabla ya kuchukua uamuzi huo, wajumbe hao awali waliingia ndani ya kikao cha Baraza la Wawakilishi kama kawaida na kusikiliza maswali na majibu, lakini kabla mchakato huo kumalizika, walianza kutoka nje mmoja baada ya mwingine.

Wajumbe hao walitoka nje wakati Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati ya Ardhi Mansour Yussuf Himid akiwasilisha muswada wa Sheria ya Kusajili Wahandisi, Wasanifu na Wakadiriaji Majengo.

Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi wa Kambi ya Upinzani, Soud Yussuf Mgeni aliwaongoza wajumbe wenzake kutoka nje ya kikao hicho, huku akisema wamelazimika kufanya hivyo, kutokana na unyeti wa jambo lenyewe ambalo linahusisha amani katika nchi.

Mgeni alithibitisha wajumbe hao kuondoka barazani na kwamba, walikwenda Makao Makuu ya chama hicho Mtendeni kwa kikao cha dharura ambacho pamoja na mambo mengine kitajadili kilichojitokeza Butiama.

? Tumetoka kwenye Baraza tunakwenda kwenye kikao muhimu tulichoitwa na chama chetu, sisi tunawawakilisha wananchi, kwa hiyo, lazima la leo lifanywe leo hakuna kusubiri,? alisema.

Mnadhimu huyo, alisema wamechukua uamuzi wa kutoka nje ya kikao cha baraza bila ya kumuarifu Spika , lakini taarifa zaidi atazipata atakapoangalia upande wanaokaa wawakilishi wa Kambi ya Upinzani.

? Spika hatujamuarifu rasmi, lakini bila ya shaka atafahamu tu baadaye kwa sababu akitupa jicho ataona hakuna mtu upande wetu kwa hivyo?atajua...atajua tu,? alisema Mgeni haraka haraka huku akiingia ndani ya gari dogo na kwenda Mtendeni.

Spika wa Baraza hilo, Pandu Ameir Kificho alisema hajapokea taarifa zozote kuhusiana na wajumbe wa kambi ya upinzani kuondoka ghafla katika kikao hicho.

? Sina taarifa ya kuondoka kwao, ingawa niliwaona wakiingia na baadaye kutoka wote, sina tafsiri juu ya kitendo hicho...,? alisema Spika.

Hata hivyo, baada ya kuwasilishwa muswada wa Waziri Himid, Mwenyekiti wa Kamati, aliwataka CUF kuwasilisha maoni ya kambi yao kana kwamba hajaona upande wake wa kushoto kama kulikuwa hakuna mtu, jambo lililozua vicheko kwa wajumbe walioketi upande wa kulia ambao ni wa CCM.

? Mheshimiwa njoo uwasilishe maoni ya kambi ya upinzani,? aliwachekesha wajumbe wa CCM.

Wakati huo huo; Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama cha Wananchi (CUF), imewaita wabunge na wawakilishi wake, katika kikao cha dharura kitakachofanyika leo jijini Dar es Salaam kujadili tamko hilo la CCM.

Mbali na kikao hicho, CUF pia inatarajia kutoa tamko lake rasmi leo asubuhi kueleza msimamo wake kuhusu tamko hilo la NEC ya CCM.

NEC katika tamko lake lililosomwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Pius Msekwa kwa wajumbe wa halmashauri hiyo na waandishi wa habari

baada ya kumalizika kwa kikao chake cha siku mbili kijijini Butiama mkoani Mara juzi usiku, ilisema imeyakubali mapendekezo yaliyomo katika taarifa ya mazungumzo ya mwafaka.

Hata hivyo, ikasema imeazimia kuwa ikiwa makubaliano hayo yatakubaliwa, yataleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa utawala wa Zanzibar na kwamba, kwa kuliangalia jambo hilo, ni lazima wananchi wote wa Zanzibar watapaswa kuliamua kwa njia ya kura ya maoni.

Kutokana na hali hiyo, NEC ilisema imeiagiza Kamati ya Mwafaka ya CCM kurejea tena katika mazungumzo na wenzao wa CUF ili kuliamua jambo hilo.

Kutokana na hali hiyo, Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya CUF Taifa, Said Miraji aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana kuwa, wamelazimika kuitisha kikao cha dharura kati ya kamati yake na wabunge na wawakilishi wote wa chama hicho.

Miraji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Blue Gurad Taifa, alisema kikao hicho, kitafanyika leo Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini saa 11:00 jioni na ajenda kuu itahusu kujadili tamko hilo la kikao cha NEC na hatua ambazo wabunge na wawakilishi wataona kuwa zinafaa kuchukua kuhusiana nalo.

"Hapo hakuna jambo la kuficha, kila kitu sasa ni wazi," alisema Miraji.

Kabla ya kikao hicho, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, atakutana na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, leo asubuhi.

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano na Umma wa CUF Zanzibar, Salim Bimani, aliliambia gazeti hili jana kuwa, katika mkutano huo, Maalim Seif ambaye atakuwa na Makamu Mwenyekiti wake, Machano Khamis Machano, anatarajiwa kutoa kutoa tamko kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusiana na la NEC CCM kuhusu mwafaka.

"Kubwa litakalozungumzwa na Katibu Mkuu, ni kutoa tamko kuhusu msimamo wa chama kama alivyoahidi katika mkutano hadhara katika Uwanja wa Garagara, Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja juzi kuhusu tamko la NEC Butiama," alisisitiza Bimani.
 
Kikwete, please stop dithering. Be smart. Maana mpaka hapo ulipofika huna legacy yoyote. Kuwachukulia hatua mifasadi, umetoka kapa mpaka sasa, hata hili la muafaka nalo unashindwa kulitolea msimamo wewe kama raisi?? Sasa sijui tukuweke katika kundi gani??? No wonder mafisadi wanarusha roho zao kama kawaida.

Huyu mkuu mimi nilimpinga kabla hajawa na hata hapata nomination.Nilijua na nina endelea kusema JK hapa nina mchezaji na Rais wa Watanzania ila true Mwenyekiti wa CCM.
 
kwa hiyo CUF wamekubaliana na hoja ya CCM wananchi wapige kura ya maoni BIG UP!!!!!

Ama wanalirudisha kwa wananchi kwa mtindo upi na wananchi walifanyie nini ??

Nyie angaleini CUF wasipokubaliana kimasilahi suala hilo wanaliunganisha kiujanja ujanja na suala la Uvunjaji Amani ili kuamisha hisia za watu.

Mbona maalimu Seif wakati anarudishiwa fungu lake na CCM hatukusikia maswala ya uvujanji amani wala swala hilo kurudishwa kwa wananchi ili waamue maalimu SEIF apokee hizo fedha kutoka serikali ya CCM ama la!!!

Plan B ya CUF nikulirudisha wananchi waingie barabarani ili wakakutane na uhuni mwingine mkali baada ya wananchi kuumia wao wanaangalia namna ya kutumia uhuni huo kupata madaraka na fedha.

Hivi wewe ndugu unaamini kuna mtanzania wa leo mwenye utoto kiasi hicho hata aweze kukubaliana n hizo porojo zako?
 
At the end of the day, wa kuwashangaa hapa ni sisi na hao CUF waliokuwa wanategemea CCM wafanye vinginevyo. Hii ndio CCM tunaoijua. CUF waliingie mkenge wakaanza kumsifu Kikwete kwamba ana nia ya dhati ya kumaliza mgogoro na kujaribu kumtenganisha na viongozi wengine wa CCM. Sasa CUF na sisi wengine tumekumbushwa kuwa CCM ni moja, akili yao ni moja-hivi ndivyo walivyo-tunapojibaragua na kutegemea makubwa kwao tunajidanganya sisi wenyewe na CCM wanatucheka na kutudharau kwamba wamefanikiwa kutujaza ujinga nasi tukajazika. Kwa hiyo tunapoendelea kushangaa, tusiwashangae CCM; tujisangae sisi ambao tulikubali kuamini kwamba eti CCM safari hii wangefanya tofauti na kuamini kwamba wameokoka!
 
Kweli kabisa Kitila,

Hata mimi nilikuwa nimeanza kuwapa ccm some kinda benefit kuwa wanaweza kufanya kitu lakini sasa wamethibitisha kuwa ni wale wale sisiemu waliokuwa wanampiga mrema mabomu wakati wa uongozi wa mkapa!

Shame on you ccm!
 
How can the kiddy us for almost ten years? This is a delay tactic for them to realise their objectives. But all this for whose interest? Shame upon them all! One of my secondary school teacher used to say, "Tanzania itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno". Is that not a reality at this particular juncture?

Where is our fate? Should we keep on waiting for nature to take its course? No we should stand up against all the powers of darkness.
 
Back
Top Bottom