Hii habari niliirusha jana usiku na kuiweka picha nashangaa Mtu wa pwani ameirudisha na kejeli,sasa mnaboa na kuanza kufanya mambo ya ajabu ajabu au hapa pia ni ukumbi wa mafisadi katika rangi nyengine. Inabidi tuumbuane kwa ujinga huu wa kuondoa mada na kuileta tena , kama mletaji wa kwanza alikuwa hafai basi hata huyu wa pili hafai maana mada au habari ilkuwa na kichwa cha maneno sawa tofauti ni picha ya Katibu wa hicho Chama cha CUF. kwa wale waliobahatika kuiona mada hii nilipoileta hata haijatolewa kwenye magazeti wataikumbuka hii picha niliyoiweka na watasema kweli ikiwa ni wasema kweli.

Sasa Moderator suali ni kwako nipe sababu ya kuiondoa mada na halafu kuileta tena niandikie japo pembeni ili mara ya pili nifuate sheria kama zipo.
Jamaa wa JF mfuata sheria MWIBA.
 

Hatukuiona Mkuu! Samahani kwa hilo!
 
Atasababisha Wazanzibar wasiokuwa na hatia kuteseka. Kama kipindi kile kabla ya kuanza mazungumzo ya Muafaka walikuwa Wazanzibar hawapati scholarship za kwenda kusoma nje ya nchi.
Atakuwa anajipalia mkaa mwenyewe.
 
MAPINDUZI - DAIMA.
Hii ni slogan ya AAA Karume.
Je atakubali kushirikiana na Maalim Seif hata kama wananchi wakipiga kura ya maoni na kukubali Serikali ya Mseto?
MAPINDUZI - DAIMA.
 
Nasuport mapinduzi as nimegundua mtutu ndo njia pekee ya kutiana adabu na kuondokana na huu usanii wa kisiasa.
Watu wako seriuos na muafaka ninyi mwaleta usanii,kipigo tuu apo.

Au mbinyo kutoka nje nao waweza kuwa the best altenative.
 
Hapa tunatakiwa tuangalie msingi wa haya maamuzi kutokea. Mkumbuke hapa tulikuwa tunapiga kelele juu ya udhaifu wa wasaidizi wa JK.

Yeye kama Rais, pia ni mwenyekiti wa Chama. Tunafahamu kabisa, maamuzi kama haya hawezi kuyafanya peke yake kwa upande wa chama, huku akifanya majukumu ya Kiserikari.

Kama katibu mkuu wake ni Makamba, Mlitarajia atapata ushauri wa namna gani? Pili ningeshauri kwa chama cha Mapinduzi. Muda umefika sasa, si lazima Raisi ndie awe mwenyekiti wa chama. kwani, mfano mzuri kwa hili. JK asingekuwa mwenyekiti wa chama, angeingilia kati kama Rais. Ila kwa hali hii inaonekana ameshindwa kwa pamoja, kama Mwenyekiti na kama rais. Awatulize wananchi atafute njia nyingine kulimaliza hili.
 
Fundi, unajua hizi nchi zetu za kimaskini viongozi wanatafuta suluhisho la matatizo yetu nje na si kwa wananchi unajua kwa nini? huko nje wana nguvu zaidi yetu wananchi. SASA MTU KAMA ANAFADHILI BAJETI ASILIMIA 50% KWELI WEWE UNA NGUVU GANI?

Harafu ukweli mwingine ni kwamba sauti yao inasikilizwa na kuheshimiwa zaidi ya wananchi/wapiga kura. kama unabisha kawaulize wakenya watakwambia. So MAALIMU KWENDA NJE NI SAWA MAANA HUKO NDO WATATOA LUGHA AMBAYO JK ANAWEZA KUIELEWA...WANANCHI HATA UKIPIGA KURA INAWEZA ISIWE NA MAANA..FUNDI BANA..AS IF YOU DONT KNOW... Hakuna anayependa kinachotokea kuongozwa kwa remote..lakini ndo lugha viongozi wetu wa kiafrika wanaijua tuu..where else?

Why stick with a system which cant work? discard and get something which can work...
 


Hiyo kwenye font kubwa ndio basis ya safari ya Maalim Seif. Mengine haya ni longolongo la sisiem ambao wanampango wa kuua tena watu kule zanzibar kwa visingizio vya kutuliza fujo!

grrrrrrr
 
Niliongea suala hili katika thread moja na watu wameshafuta kama kawaida yao.Vyama hivi ninanipa shaka kubwa sansa kama wakipewa waongoze nchi sababu watatuletea mambo ya Neo colonoalism.kuna chama kimoja cha kikabila huwa wanapata pesa toka Ujerumani ili waongoze shughuli zao.CUF sijui zinatoka wapi.CUF-Zanzibar kuwa watu makini ila kwa hapa Bara,Upinzani Bado sana labda wajipange kwa miaka kama 50 huku wakisaidiwa na waandishi wa habari ila kama siyo hivyo bado sana..sana sana CHADEMA,hakina viongozi na kimejaa watu wabinafsi tu(Mawazo Binafsi)
Mataifa ya Nje tumeyachoka na tunahitajki kufanya maamuzi sie wenyewe.Matokeo ya kuzikaribisha nci za magharibi ni kuchochea uharibifu wa Amani.
 

Unachosema hapa kina tofauti gani na alichofanya Kikwete juzi na rafiki yake Bush na mkataba wao wa kuuza nchi?!?!?

Inaonekana unahitaji dawa ya ubongo maana very soon utakuwa beyond repair!
 
chama chake si kimejiondoa kwenye muafaka, sasa anaenda kusema nini? heheee, nilidhani ataisemea CCM kwa wananchi kumbe anaenda ulaya! Sasa sijui wapiga kura wake wapo ulaya, au vipi, i dont get it !

Ndugu yangu u-kada usikufanye kupoteza busara zako, nyumbani watu ambao unaweza kuwaambia ndio wa NEC wenyewe, sasa kama watu wenyewe wa NEC ndio hao wamekuwa wansanii, sasa unataka akawambie nani? Wenye busara hapa Bongo wanaonekana kama wameishiwa au wamekiwasha sasa awaambie kina nani? Kwani kuna ubaya gani wa kwenda kuwaambia wadau wengine? Usalama wa Tanzania sio kwa interest ya Tanzania peke yake ni pia kwa interest ya sate holders wengine? Wana CUF wako sehemu nyingi duniani sio Tanzania tu, kama ilivyo wana CCM wako London, NEw York kila sehemu.
Wakati mwingine uweke busara zako mbele kuliko ushabiki wa kisiasa. Kama ulivyoona EPA iko hapa ilipo na itakuwa pale itakapokuwa kutokana na hao wa nje unao wakejeli!
 
Inaonekana unahitaji dawa ya ubongo maana very soon utakuwa beyond repair!

naomba uniitumie dozi ya dawa ambayo itanifaa,siwezi kuwa kuathirika kwa jina la Yesu na ushindwe naulegee..

The Truth should be accepted.
 

Mkuu Msanja,
Umetoa majibu safi kabisa ila naomba tu kuongeza kidogo.
Watanzania wanapotumia nafasi yao kusuluhisha matatizo yao kwa njia ya kura, CCM hukataa kwa kuwa usuluhishi huo hauwapendezi na kukidhi matakwa yao.CUF ilipopewa mandate ya kutawala kule visiwani,CCM waliwadhulumu.Lakini bado CUF walikubali kukaa na kujadiliana na Mwizi wao CCM.Badala ya kutatua CCM wakawadanganya. Sasa CUF hawaezi kukaa tu akakunja mikono, inabidi aende kwa wale ambao CCM inaweza kuwasikiliza, na watu hao ni donors.

Watanzania siku zote tumekuwa ndumila kuwili. Baada ya machafuko kule Zanzibar. CUF walikiita chama cha fujo,leo wameamua kukaa kwenye meza safari zote tatu Wanaonwa wajinga.Mimi nasubiri nione 2010.
 
naomba uniitumie dozi ya dawa ambayo itanifaa,siwezi kuwa kuathirika kwa jina la Yesu na ushindwe naulegee..

The Truth should be accepted.

Kuna madakitari wawili waliokuwa certified na JF... Nyani Ngabu na SteveD..... Na kuna mwingine ambaye amekuwa certified na the great state ya Masachuseti --- YourNameIsMine.

Ongea nao kabla hujashindwa na kulegea!
 
Kuna madakitari wawili waliokuwa certified na JF... Nyani Ngabu na SteveD..... Na kuna mwingine ambaye amekuwa certified na the great state ya Masachuseti --- YourNameIsMine.

Ongea nao kabla hujashindwa na kulegea!

Steve D is much grown than you..shetani flani,badilika na utoe maneno ya maana.Tusubiri Maalim Arudi
 

mkuu nakuwia radhi, mie hio mada sijaiona.

na kama nimetumia maneno ya kejeli niswamehe maalim.


ila mie nimeliweka jamvini tulichangie kama unaona kejeli unaonyesha wapi pa kejeli na ss waungwana tutafahamu.

kumanisikia bwa mkuu?
 
Hawa Wazanzibari naona wameamua kuharibu dili zima!

Tunarudi kwenye siasa za jino kwa jino; ukimwaga ugali namwaga mboga tukose wote.
 
Harufu ninayoisikia kutoka ZNZ sio nzuri jamani,tafuteni manukato mapema ya kuondo harufuu hii mbaya.
 
MAPINDUZI - DAIMA.
Hii ni slogan ya AAA Karume.
Je atakubali kushirikiana na Maalim Seif hata kama wananchi wakipiga kura ya maoni na kukubali Serikali ya Mseto?
MAPINDUZI - DAIMA.

Mapinduzi aliyotaka kufanya Seif yameshindwa. Wanaume wamemgutukia. Angechukuwa Uwaziri Kiongozi kwa mujibu wa Katiba ya hivi sasa ya Zanzibar angekuwa ameshijitwalia Serikali. unajua hilo? Sasa na akae bench, na hata ukija mseto, atapewa Umakamo wa Rais 1 (kilemba cha ukoka). Basi ndo yale yale- atapata nyumba , gari, king'ora - na abakie kunywa kahawa na kuhudhuria taarab asikilize mipasho. Siye tnamsubiri na kikundi chetu cha (Sabri-bachan), tumtuimbuize Bwana mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…