Huyu jamaa kaenda ulaya ,sasa CCM wameanza kuona yale yaliyotokea miaka ya iliyopita yatarudi upya na safari hii sio Zanzibar tu bali hata upande wa pili ,huyu anapokwenda huko na kuonyesha kuwa haki imeborongwa basi hata zile funguo za misaada hupewa yeye ,yaani kuna watu wana bahati ya kusikilizwa na wazungu na Seif ni mmoja wao ,na vile kumezuka uzushi wa Ufisadi basi ndio kabisa CCM wajitayarishe kutumia rasilimali za mifukoni mwao au watu watazidi kufa na njaa,Sefu Sharif mwisho kwa hatua za kuzuia misaada ,nafikiri Wazanzibari bado hawajamsahau.
Ikiwa tunakumbuka sababu ya kuanguka kwa uchumi wa Nchi ya Zimbabwe ambayo kimaendeleo ilikuwa mbele kuliko Tz kwa masafa na kumfanya Rasi Mugabe aone hata misaada ikizuiwa basi hawatababaika ,tusijidanganye na kusema misaada ya wazungu si lolote si chochote tunaiona leo majigambo ya Mugabe yalipofikia ,ukibadili dola 40 unapata milioni 400 za kizimbabwe ,maana wazungu hawana haraka mambo yao ni mahesabu tu wanajua tulichowapa kitawachukua kama miaka mitano au sita lazima maji wataita mee...!! Na hapa Tz CCM wasione kama wazungu wanawapenda na watawawacha wafanye wanachotaka,hilo ni jambo la kujidanganya na kujipa moyo ,kwamba hawatoachiwa kufa njaa kwa sababu za kisiasa ,wazungu hawana huruma na mtu wapo tayari kuona watu wanakufa na kuuwana lakini usawa wanaoutaka wao unapatikana,mnajua hadi hii leo bado wanawashangaa WaTanzania kwa nini hawawachangamkii mafisadi au hawaichangamkii hii serikali ya mafisadi ,hii ni serikali ambayo inatakiwa ijiuzulu mara moja si ya kuachiwa muda hata dakika.
Serikali iliyooza kwa rushwa na utapeli haina nafasi katika kuongoza nchi inahesabiwa kuwa ni serikali ya kidikteta ,inawaburuza wananchi vile wanavyotaka wao wezi wa mali ya uma wanatamba na kutembea kifua mbele ,hii si serikali ya kuongoza wananchi bali ni serikali ya wachache wanaohifadhiana kwa kutafutiana njia mbali mbali za huyu ni mwenetu au mwenzetu.
Majaribu mangapi serikali ya Kikwete imepata..Ukianza na yule kiongozi alieua dereva wateksi kama sikosei akiitwa Ditopile ,kesi yake inazunguushwa huku na kule.Ukifuata yule Mkuu wa Polisi alietia mimba mfanyakazi wa nyumba kesi yake ipo wapi ? Wizi wa fedha za Umma zimefikia wapi mabilion kwa mabilion
,raisi kufanya mradi akiwa Ikulu ,na wakuu na mawaziri karibuni wote kujihusisha na ubadhirifu wa mali ya umma ,kila kukichwea kunabadilishwa tu huyu anapelekwa huku yule anahamishiwa kule utafikiri wanacheza CHESS ole wao wakumbuke tu kuwa kuna CHECKMATE,huu ni usanii na uhuni dhidi ya wananchi kwa kuwa tu wanainchi wamekaa kimya hawana ubavu na hawana wa kumshitakia hivyo Raisi hawezi kuwatia hatiani eti ni marafiki zake wa karibu kwa habari zinazoandikwa kila siku.Na hili ndilo linalowaangusha viongozi wengi wanaweka urafiki na kazi wanasahau kuwa katika biashara hakuna cha rafiki wala ndugu ,waswahili tunasema cheza na mwenyemali usicheze na mali. Viongozi wa CCM ambao ndio wapo serikalini wanacheza na mali ya Watanzania ipo siku wenye mali wataweka uswahiba pembeni kama Raisi hakuwajibika katika kuwatia hatiani wale wote wanaocheza na mali ya Taifa hili.Maalim Seifu endelea na msimamo wako huo huo na choma utambi kwa baruti kwa upande wako na Wazanzibari na wao watachoma kwa upande wao.Halali mtu.