Hivi kumbe Zanzibar wakati wa Karume ilikuwa inaitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar? mie nachanganyikiwa!

Jamhuri ya watu wa Zanzibar

Serikali ya mapinduzi Zanzibar
 
Binafsi huu wote ni Upuuzi mtupu!.. mtanisamehe wakuu, kwani hawa viongozi walitegemea kitu gani haswa!...Ombi lolote lina majibu mawili...hakuna sheria.
Hili swala lilitakiwa kushughulikiwa baada tu ya matokeo ya Uchaguzi..

Na Ni upuuzi haswa!!!
 
Swali kwa wadau mnisaidie: Hivi hawa akina Mrema, Lipumba, Maalim Seif n.k ndiyo watu pekee kwenye vyama vyao wanaoweza/stahili kushika madaraka ya Urais kiasi kuwa ni lazima kila kipindi wagombee wao tu?
yaani hapo ndio unaniwacha hoi kwa mbali ukitazama utaona huko CCM kuna vizee vinafika kuanguka lakini vimekuwa vinganganizi ,alafu ka unasahau vile kusikia wazee wang'atuke sijui nani ameng'atuka makamba manyororo mangunge na sasa pinda yaani inaonyesha sasa CCM wanakata kona ila madereva na makonda ni walewale tokea iundwe.
 
Hivi kumbe Zanzibar wakati wa Karume ilikuwa inaitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar? mie nachanganyikiwa!

Jamhuri ya watu wa Zanzibar

Serikali ya mapinduzi Zanzibar

Nafikiri huu sio wenyewe wanasema ulikuwa na mambo kumi na moja tu.
Halafu sidhani kama Karume alikuwa anakijua kilugha cha kizingu
 
Nafikiri huu sio wenyewe wanasema ulikuwa na mambo kumi na moja tu.
Halafu sidhani kama Karume alikuwa anakijua kilugha cha kizingu

Una maana gani? Unajua kwamba wakati huo Karume alikuwa amezungukwa na watu kama Abdulrahman Mohammed Babu, Abdulla Kassim Hanga, na wengineo. Hawa wakijua hicho kizungu kushinda wakina Kambona waliokuwa wakimsaidia Nyerere. Wacha dharau Bwana..
 
Sikuandika kimasai ...Yero sovai... ni kiswahili ambacho kipo wazi kwa ufupi nimeuliza ..sidhani kama Karume anakijua Kizungu.. sasa naona mnakuja kiajabu ajabu hivi kuuliza ni ujinga ? . Ningetarajia jawabu kama alikuwa anajua au hajui ..that is all ,jaribuni kusoma between the line ili muone kina cha suali neno kwa neno mstari kwa mstari ,nimeridhika na alieeleza kuwa alikuwa amezunguukwa na wasomi na hapo unaweza kupima kwa nini wasomi aliwaua na kama hamfahamu ugonvi wa matatizo yaliopo Zanzibar si Waarabu na Wazalendo bali ni wenyewe hao wanamapinduzi kati ya wasomi na mbumbumbu ,wasomi wengi wakiwemo hao mliowataja waliuliwa na wengine waliwahi kukimbia na hapo ndipo mgawanyiko ulipoanza ,kuna watu wa mrengo wa waliouliwa ambao hawakuridhika na mauaji ya wasomi ambao walikuwa msatari wa mbele katika mapinduzi...natumai mnaweza kupata picha halisi ya matatizo ya Zanzibar na kuondokana na lile shombo la waarabu wanataka kurudishwa na Seif na wenzake ila mkiambiwa ndani ya CUF kuna ASP kuliko ndani ya CCM-Zanzibar mnaona ,watu wanaipenda CUF ,hapana wandugu wote ni Wazanzibari ambao tatizo na chimbuko la yote hayo ni huku kuuliwa kwa watu wasomi na wengine kukimbia ,ila sasa vita ni kati ya ndugu hawa , natumai kila atakae soma hili dondoo atafunguka kichwa na akili na ubongo wake kuanza kufikiri upya na kuondokana na dhana ya waarabu ,hapa hapana cha muarabu hii ni dugu moja ,hivyo kazi kwenu.
 
Mwiba,
Acha uhuni mkuu, kuuliza kitu hakiwezi kutanguliwa na neno SIDHANI!.. hii ina maana umesha mweka chini Karume uwezo wake kusoma ama kuongea Kiingereza... Pamoja na yote haya Bongo wamejaa watu kibao ambao wanaweza kusoma na kuelewa kiingereza lakini inapofikia kuzungumza inakuwa ngumu, mtihani mwingine kabisa.. Anayeongea kiingereza pia sio lazima ajue kusoma..
Sokomoko,
Mkuu wangu inakuwaje huelewi kuwa Zanzibar ilikuwa Jamhuri kabla ya Muungano kisha unakuja pinga tarehe ya Uhuru wa Zanzibar! - vipi mkuu unachanganya siku ya Muungano na Uhuru wa nchi hiyo?
 
Mafuta sijayaona, na maji yakiungana,
Vovote tungakazana, ni huja iso maana,
Jambo lisowezekana, viwi kulishika sana,
Muhali kutangamana, lila na fila twambiwa.
 
bwana mtu wa Bara unaboa na vijishahiri vyako visivyo na kina wala mizani na lugha ngumungumu.Bora nisikilize mashairi ya Mr Blu

Nikiamka kitandani nachukua mswaki wa BLUE,
Demu wangu naye kapiga kitop cha BLUE,
Gari langu nalo ni la BLUE,
Chaofan yangu nayo ina jiaozi za BLUE
 
Nafikiri Mh. Mwiba una hoja ya msingi. Ni kweli hakuna suala la Uarabu. Kwani huyo Babu ni Mjomba wa Waarabu. na Bw. Hanga ni Mzanzibari mwenye asili ya Bara. Hivyo dhana ya Uarabu iliondolewa mara tu baada ya Mapinduzi matukufu ya 1964. Hivyo ugomvi unaondelea sasa hauchangiwi sana na suala la Uarabu. Kipo chanzo jaribu kupekua , na anzia pale wakati Mh. Jumbe alipoambiwa kachafua hali ya hewa. Seif akapewa Uwaziri Kiongozi Zanzibar chini ya Mwinyi, Akachafua hewa (yeye Seif) katika utawala wa Sheikh Idriss Abdulwakil, na hapo ndipo akafukuzwa CCM pamoja na wapambe wake. Haya endelea na ukikwama nitakuchangia.... Kwa taarifa tu wasomi hawakataliwi SMZ na CCM -Zanzibar, wamejaa tele huko wanaowazidi waliomo ndani ya CUF.
 
Historia ya Zenji tuliwahi kuijadili kule Tanzanet na wala hatukufikia makubaliano. Nikipata muda nita peruzi archives zangu niangalie angalie.
 
Shukrani, mwenzetu aliyepost hii humu JF(Jamco_za). Sasa nnaendelea kuupitia kusoma kama ipo clause ya kusema kuwa Muungano unaweza kuvunjwa au la

lakini kwa sasa mkataba wenyewe ni huuu na sioni kwa nini ulikuwa unafichwa na kwa manufaa ya nani

anyway tuendelee na mjadala


 

Mwiba maneno yako ni mwiba yanachoma kama mwiba CCM wakiona hii statment yako watakupongeza kwani huo ndio ukweli wa mambo. Mapinduzi aim yake ilikuwa kuwajali wakulima na wakwezi lakini leo hii wakubwa wa CCM hawajali watu wao wanajali maslahi yao zaidi wanataka kudumisha mapinduzi ili wawe madarakani milele wapate kuwanyonya wananchi. Kikubwa zaidi wenyewe wazanzibari wameshajua nani atakaewasaidia kujitoa pale walipo. Ndio maana CCM bila Jeshi la Bara wakati wa uchaguzi hawataweza kushinda! na kama mnabisha basi ije tume huru ya zanzibar majeshi yasiende kule wakati wa uchaguzi na kuwe na waangalizi huru wa kimataifa kisha muone aibu itaka wakumba CCM.

Shukrani sana Mwiba umetoa kitu ambacho watu wengi hawakijui mimi mmoja wao "CUF kuna ASP kuliko ndani ya CCM-Zanzibar"
 

Mkandara,

Sijachanganya mkubwa ninachouliza mbona kipo wapi? kwenye ile QUOTE nimeonyesha ilipotiwa Saini hati iliandikwa [COLOR="Red[SIZE="5"]"]"Abeid Karume the President of the Peoples' Republic of Zanzibar"[/SIZE][/COLOR] Hii ilikuwa 1964 baada ya Mapinduzi haramu yalio ondoa utu wa wazanzibar! swali wakati ule mkataba ulipo sainiwa inaonyesha ilikuwa jamhuri ya watu wa zanzibar lini serikali ya mapinduzi zanzibar ilianza?
 
tokea mapinduzi jamhuri ya watu wa zanzibar ilitawaliwa na serikali ya smz
 
Uhuru wa Zanzibar ulipatikana
10 Decemba 1963, kutoka kwa Uingreza kama mamlaka kamili chini ya Sultan. Hapa ilikuwa baada ya muungano wa chama cha Zanzibar National Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba peoples party, kuwa na serikali ya mwafaka wakiunganisha viti vyao kama serikali ya mwafaka na kuwa na jumla ya viti 13, dhidi ya viti 10 vya Afro Shirazi Party (ASP).

Utawala huu haukudumu baada ya serikali iliyoshinda katika uchaguzi wa kidemokrasia kupinduliwa Januari 12, 1964 katika mapinduzi yaliyoongozwa na Mganda John Okello. . Sheikh Abeid Amani Karume akatangazwa kuwa rais wa People's Republic of Zanzibar and Pemba.

Watu kati ya 5,000-12,000 wakiwa wazanzibari wenye asili ya uarabu na wahindi waliuawa na mali zao zilitaifishwa katika mapinduzi hayo.

Mpaka hapo CCM kama mtoto wa ASP haina asili ya serikali ya mseto, maana ni chama hicho ndicho kilichoipindua serikali ya mseto inayodaiwa kuingia madarakani kidemokrasia. Na hiyo tarehe ya uhuru Mhh!
 
niliwahi kusikia kuwa ule wa awali ulikuwa na maeneo 14 ya muungano inagwa yameongezwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…