There is a completly diferent MIND SET in Zbr and Tnky. If we are big enough and bold enough to accept facts/reality ,you will not have any problem knowing the reason for the Union.It was formed out of a neccessity that was obvious to Mwalimu but not so obvious to the common man on both sides.(The threat of aligning to the Commuinist block;that it is now history.)Today, Zbr would be much better off on its own,economically. Aid will pour in from the Islamic states,and the Western Block.It could well become another Singapore,if it were to break away.
Wawe kama Singapore, labda tunasoma hadithi za Abunuwasi na Bulicheka. Maendeleo yanaletwa na kufanya kazi, tatizo la Zanzibar wanatafuta mchawi - hakuna mchawi bali wao wenyewe wakae chini na Wapemba wasuluhishe matatizo yao. Hayo yaliyotokea Musoma yalikuwa kati ya Zenji na Pemba, huwezi kufanya muafaka bila kuonana jicho kwa jicho na mbaya wako.
Kwanza wamependelewa sana lundo la viongozi wao wanaweza kulibeba? Bara tuko millioni karibu 40 lakini hatuna hata wabunge unaoweza kulinganisha kwa uwakilishi na wenzetu.
Kuna mjadala mwingine motomoto ambao unaendelea kama huu wenye heading ya leo ni siku ya muungano!Na nimeuliza maswali kama haya na nina subiri waungwana huko wanipe majibu!cha ajabu wanaotaka muungano na hasa toka bara hawako tayari kueleza kwa nini tuendelee kuwa na hili jambo
Hii ni kama ndo ikishindikana kila mmoja anatazama lwake
Muungano ni kama ndoa..na kama ikishindikana kuishi pamoja basi tupeane talak kila mmoja atazame ustaarabu wake.
Muungano haukuwepo na unaweza usiwepo.Kwa wazanzibari wengi wao be it CUF au CCM deep down wanaamini kuwa muungano hauna faida kwao, na zaidi ule mkutano wa Butiama ambao CCM ZNZ walimtisha JK kuwa kama anataka kuwasikiliza hao CUF basi na wao watarudi ZNZ kivyao.Na hapo bado hatujazungumzia 60/40
Bara nao wanaona kuwa watu wa ZNZ wanaishi kwa income support ya kodi wa watu wa Bara sasa je mnasemaje wana JF tuuvunje huu muungano?
Maoni yenu Tafadhali
JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY
...Today, Zbr would be much better off on its own,economically.Aid will pour in from the Islamic states,and the Western Block.It could well become another Singapore,if it were to break away.
HAPANA, TUWE NA SERIKALI MOJA TU AU TUSIWE NA MUUNGANO KABISA
Umenipa pakuanzia!
Ni kweli kama mtoa hoja alivyosema kuwa wazanzibari deep down their heart hawaupendi muungano. Hawaupendi muungano kwakuwa wanaona hawafaidiki nao. Kisiasa mtaona wanafaidika lakini ukiangalia kwa makini utaona wana point.
Rais wa zanzibar hana tofauti na Mhe Kandoro yule mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Zamani Rais wa zanzibar alikuwa makamu wa rais siku hizi hakuna hilo! mnajua kwa nini? Hii ni choyo ya CCM wanajua kuwa hawashindi ZNZ ikija tokea CUF wakiwazidi maarifa wakashindwa "kuchukua kuweka waa" Seif au mwingine yeyote wa CUF awe Rais wa ZNZ then awe makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano! hilo haliwezekani kwani wao CCM tu ndio wamezaliwa katika dunia hii watawale!
Wenyewe wazanzibari wana ZNZ yaani Zanzibar Nzuri Zamani
Wa bara wanaosema Zanzibar wananyonya mapato ya Tanzania bara au uchumi wake unategemea Bara si kweli ila naamni kama Bara inafaidika sana na Muungano kuliko Zanzibar na nina hoja. Misaada yote inayoipata Tanzania inakuja kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania yaani Zanzibar ikiwamo maana haiji kwa serikali ya Tanganyika. Kwa taarifa yenu misaada hii haifiki hata Chumbe! inaishia Dar es Salaam!
Ukiangalia hati ya muungano kuna yale mambo 11 ya awali katika yale mambo suala la mgawanyo wa pesa zipatikanazo mafuta na gesi ya asili halikuwepo limekuja kuongezewa tu baada ya kungundulika zanzibar ina neema hiyo! ndio rafiki zangu wazanzibari wanahoji mbona madini hawakuyaweka tugawane mapato pia?
Zanzibar ni nchi ikiyokuwa imepiga hatua kubwa sana wakati inaingia katika muungano.
Msiojua Zanzibari ni nchi ya kwanza kuwa na taa za bara barani barani afrika, ya kwanza kuwa na television ya rangi barani afrika.
Kwa maana hiyo Muungano umeirudisha Zanziba kimaendeleo pengine bila la Muungano Zanzibar ingekuwa Brunei
Karume baba aliwahi kusema "muungano ni kama koti ukiona linakubana livue" sasa ni hiari yao wabara na wazanzibari kulivua au kulifumua makwapani!
Naomba kuwakilisha hoja!
Wawe kama Singapore, labda tunasoma hadithi za Abunuwasi na Bulicheka. Maendeleo yanaletwa na kufanya kazi, tatizo la Zanzibar wanatafuta mchawi - hakuna mchawi bali wao wenyewe wakae chini na Wapemba wasuluhishe matatizo yao. Hayo yaliyotokea Musoma yalikuwa kati ya Zenji na Pemba, huwezi kufanya muafaka bila kuonana jicho kwa jicho na mbaya wako.
Kwanza wamependelewa sana lundo la viongozi wao wanaweza kulibeba? Bara tuko millioni karibu 40 lakini hatuna hata wabunge unaoweza kulinganisha kwa uwakilishi na wenzetu.
cha ajabu wanaotaka muungano na hasa toka bara hawako tayari kueleza kwa nini tuendelee kuwa na hili jambo
Hii ni kama ndo ikishindikana kila mmoja anatazama lwake
cha ajabu wanaotaka muungano na hasa toka bara hawako tayari kueleza kwa nini tuendelee kuwa na hili jambo
Hii ni kama ndo ikishindikana kila mmoja anatazama lwake