Mimi sioni kosa la maelezo ya Pinda hata kidogo isipokuwa katumia lugha ambayo wengi wameshindwa kuitafsiri..
Ni kama hivi,
watu wawili waliofunga ndoa yaani Mume na Mke.. Unauliza swali kuwa kuhusiana na mmoja (martial stutas) kama anatambulika kuwa ni single.. Na mkuu Pinda kajibu hapana - sio single - Maadam Zanzibar bado kaivaa pete, yupo ktk sheria za ndoa basi bado ni mke/mme wa mtu (married).
Kwa hiyo unaweza kuona ujanja aliotumia kujibu hoja ambayo haikujieleza zaidi ya kuhoji, mbona mke/mme huyu ana kazi yake ana account yake na hata nyumba kwa jina lake?...kwa nini asiwe single!.. well ukweli ni kwamba Zanzibar sio nchi kwa tafsiri ya nchi ila ni sehemu ya nchi inayoitwa Tanzania..that is the fact.
States zote za Marekani ziliungana kuunda nchi moja inayojulikana leo kama USA, huwezi kuuliza kama New York au California ni nchi..

Swala la Utawala kama kuwa na rais ni makubaliano tu ambayo kesho tunaweza sema toka leo Tanzania haitakuwa na rasi isipokuwa waziri mkuu.. Kwa kufanya hivyo hatuwezi kupoteza hadhi ya kuwa NCHI kwa sababu hatuna rais.
 
Inajulikana hata ramani ilikwisha kutaarishwa kuonyesha kuwa Zanzibar ni Mkoa ila ilipingwa vibaya sana wakati wa Aboud Jumbe yule aliejenga kiwanda cha Ulevi mahonda.
Kwa upande wangu mimi sitolifuatilia hilo la Zanzibar ni Nchi au ni Mkoa ikiwa na mkuu wake wa Mkoa Mh.Karume.
Ni pale Mheshimiwa Pinda aliposema wakati akijibu suali la kwa nini wananchi wasiulizwe kuhusu kuunda serikali ya Kitaifa huko ZImbabwe kupitia kura ya maoni kama ilivyopendekezwa na CCM chama Tawala hapa Tz lifanyike kule Zanzibar?
Akijibu sula hilo alisema .hali ya Zimbabwe na Zanzibar ni tofauti.
Suali kwa mheshimiwa Pinda Je anataka Wazanzibari wafikie hali kama iliyofikia Zimbabwe au Kenya maana hali ya Zimbabwe na kenya zinajulikana na ndio wakaunda Serikali ya umoja wa Kitaifa kwa Kenya na kupendekezwa hilo hilo kwa Zimbabwe.
Kusema kweli kuzua suala la kura ya maoni kwa Zanzibar mmekwenda mbali sana na sasa mnaumbuka.
 
SERIKALI MBILI ZENYE NCHI MOJA AMA NCHI MBILI ZENYE SERIKALI MBILI...AMA HATA UKIPENDA..SERIKALI MOJA YENYE NCHI MBILI?

SERIKALI MBILI NCHI MOJA NI KAULI GANI GANI HIYO?
SERIKALI IPI INAMTUMIKIA NANI NA KIVIPI?

JE KUNA SERIKALI MOJA KUITUMIKIA NCHI MOJA NA SERIKALI MOJA KUZITUMIKIA NCHI ZOTE?

NA KAMA THATS THE CASE THEN KUNA SERIKALI INABEBA MZIGO MZITO SANA TU!

HUWEZI KUITA ZOTE SERIKALI..KWANI UTATA WA SHERIA UTAKUWA MWINGI SANA!

MUANGALIE SANA HUO MUUNGANO MUJUWE NAMNA YA KUUREKEBISHA NA SIYO KUJA NA HIZO KAULI.

Sasa NANI ASIYEJUWA KUWA HATA PEMBA NAYO LABDA INA SERIKALI YAKE ISIYOTAMBULIWA?

NA WATANGANYIKA NAO WASHAANZA KUDAI TAIFA LAO!

DUH!KAAZI KWELI KWELI!

NB:HAYO MAMBO YA KUSEMA SI NCHI NI SEHEMU YA MUUNGANO NA HUKU WANA SERIKALI YAO NI USANII ULIOPITWA NA WAKATI!
 
Mimi ninavyofahamu Zanzibar ni nchi (country) lakini Zanzibar sio Taifa (Nation).

Kwa hivyo basi Waziri Mkuu ameteleza!!!
 
Mnakumbuka ile kesi ya "kubambika" ambapo Komandoo Salmini alidai watu wanataka kumpindua? Mahakama ilisema pia kwamba Zanzibar sio Nchi.
 

labda na wewe hujalifahamu suala aliloulizwa pinda.
inawezekana pia kuwa muulizaji alitaka kuuliza hivi, mie na wewe tumeoana, wewe una nyumba yako, gari yako, account yako, insuarence yako, hivi kwa nini mimi nikienda nje ya nchi lazima nitumie jina lako? wakati (kwa mila za kizanzibari) hata kama tumeoana hakuna ulazima wa mie kubadilisha jina na kutumia lako.
jibu la pinda ni kuwa madhali tumeoana lazima tutumie jina moja labda tuvunje ndoa.
 
Mnakumbuka ile kesi ya "kubambika" ambapo Komandoo Salmini alidai watu wanataka kumpindua? Mahakama ilisema pia kwamba Zanzibar sio Nchi.

Mahakama ilisema mengi tu mle. Walisema Muungano wenyewe hau make sense!

Ile kesi kila Mtanzania inabidi aisome.
 
Wakuu,

Mimi binafsi naamini Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili zilizoungana kwa kukubali kupoteza mamlaka yao kikatiba kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Wakati Zanzibar haikuridhia baadhi ya mambo yake kuendeshwa na serikali ya Muungano, ilibaki na serikali yake ya kuendeshea mambo hayo. Tanganyika iliridhia mambo yake yote yaendeshwe na serikali ya Muungano. Hicho ndicho kisa cha kuwapo kwa serikali mbili Tanzania.

Ingawa kikatiba na kimataifa Zanzibar na Tanganyika hazitambuliwi kisheria, lakini bado zinaeleweka kuwa nchi mbili zilizoungana. Na hata kwa miaka 1,000,000 nchi hizi mbili zinaweza kujirejeshea mamlaka yake ema kwa maelewano au hata kwa nuksani. Mifano tumeiona nchi za Mashariki ya Ulaya na Urusi.

Kutoa mfano wa mke na mume na mmoja wao kuulizwa kama uko single kunachekesha. Mtu akiolewa au akioa hapotezi utu wake, bado anabaki kuwa mtu. Kuna baadhi yetu tunaogopa hata kutaja tu jina Tanganyika. Tunaiita Tanzania Bara. Ni sawasawa na mbuni kutia kichwa mchangani akiamini kwa kuwa yeye haoni basi na wengine hawamwoni. Tanganyika siku zote itakuwapo na Zanzibar hali kadhalika. Huwezi kuwa na Muungano wa nchi moja. Ni lazima iwe ni Muungano wa nchi zaidi ya moja.

United States of America ni Muungano wa nchi 50 za Marekani. States maana yake ni nchi. Tanganyika nchi na Zanzibar ni nchi zilizoungana chini ya katiba ya nchi moja ya MUUNGANO. Sheria za Zanzibar haziwezi kukiuka sheria za Muungano, lakini bado ina sheria zake na ukiwa kule ukazikiuka, jasho litakuporomoka. Hali kadhalika, ukikiuka sheria za state yoyote ya Marekani unapokuwa kwenye state hiyo, utakiona cha mtema kuni.

Hatusemi kweli tunaposema Zanzibar si nchi. Zanzibar ni nchi (state) ndani ya nchi ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kama ilivyo Tanganyika ambayo serikali yake imo ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Hatuwezi kuifanya nchi ya Zanzibar kuwa ni mkoa kisheria. Wala hatuwezi kuifanya Tanganyika kuwa ni mkoa. Tanganyika itakuwa na mikoa ndani yake na Zanzibar itendelea kuwa na mikoa ndani yake. Na hapa Zanzibar maana yake ni Unguja na Pemba.

Hata tukifumbia macho Jamhuri ya Muungano ya Tanzania siku zote itabaki kuwa nchi moja ya muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar. Maelezo yote mengine hayatabadilisha ukweli huu hata tukiwa na serikali moja tu ya Muungano.

Kama Zanzibar si nchi na ni mkoa tu wa Tanzania, hebu tujaribu kuwa na Rais wa Mkoa wa Tanga na wimbo wake wa Taifa na baraza lake la wawakilishi na bendera yake kama hakufungwa mtu kwa kosa la uhaini.

Disclaimer: Mimi si Mzanzibari, mimi ni Mtanzania wa Tanganyika.
 
Inatakiwa wabunge wawe na minimum knowledge ya mambo ya taifa kabla hawajaingia bungeni. Bunge sio shule ya kumfundisha mbunge muundo wa serikali zilizopo. Inapaswa mheshimiwa Sitta amrudishe huyo mbunge shuleni akajifunze kwanza. I thin he did not have a question to ask!
 
Zanzibar ni semi-autonomous part of URT.Na kwa sababu URT ni muungano wa nchi mbili,basi academically muungano huo hauzifanyi nchi hizo ziache kuwa nchi lakini politically nchi hizo zinakuwa hazipo tena.

Ugumu unakuwepo pale academicians wanapojadiliana na politicians!
Wakati academicians wanafocus on logical facts, politicians wanafocus on fulfilling particular needs.
 

Tatizo la Katiba, na Standing Orders (sheria za Bunge), ni kwamba zinasema Mbunge anaweza kuiuliza Serikali swali lolote lile.

Sasa unakuta Mbunge anauliza Serikali kitu ambacho ni wabunge wanatakiwa kukijua zaidi kuliko Serikali kwa sababu wao ndio wanatunga sheria.

Sasa Pinda angesema Zanzibar ni Mkoa wangemwambia nini? Wangemwambia Katiba haisemi hivyo. Halafu Pinda nae angeweza kuwaambia "sasa mbona mnauliza kama mnajua."

It's almost ridiculous.
 
``Umewasikia viongozi wenzako namna wasivyoridhika na uchaguzi nchini mwako,`` alisema Membe akimkariri Mwenyekiti wa AU, Bw. Jakaya Kikwete.

Chanzo:NIPASHE

Hiyo ni kauli ya mwenyekiti wa umoja wa Afrika ambaye pia ni rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

Aliitoa kauli hiyo mbele ya viongozi wa nchi wanachama wa AU huko Misri lakini alikuwa akimlenga Dikteta Robert 'Mbabe'.Ni kauli ya kijasiri inayoonesha kukerwa kwa mwenyekiti wa AU na viongozi wengine wa Afrika na unyama unaoendeshwa Zimbabwe kwa baraka za ZANU-PF.

Suala linalonisukuma mie siyo matatizi ya Zimbabwe, hayo nawaachia wwengine kwa sasa.Hoja ni suala la Zanzibar kuhusu mpasuko wa kisiasa.
Kwa miaka kumi na tatu hapajawahi kuwepo nia ya kweli kwa upande wa CCM kumaliza mpasuko huo.Kila wakati maraisi wamekuwa wakiunda tume na kutumia mabilioni ya fedha za umma lakini hakuna suluhisho lililopatikana.

Rais Kikwete aliahidi kumaliza mpasuko wa kisiasa na kwa mbwembwe nyingi tume yake ikaanza kazi lakini chakushangaza ni kuwa hoja ya kumaliza mpasuko huo imetaifishwa na kufanywa agenda ya CCM.Ndiyo maana mapendekezo ya tume ile yalipingwa na wahafidhina walioko ndani ya CCM kwa kejeli na sababu nyingi zisizokuwa na msingi wowote.

Hata Kikwete huyuhuyu alishndwa kufurukuta ndani ya vikao vile ambavyo wahafidhina wale waliligeuza suala la Zanzibar kuwa mali yao na kuageuza mapendekezo ya tume ya rais kuwa porojo.

Leo hii tunapomsikia Kikwete anamkaripia Mugabe kwa kutawala kibabe na kumnyooshea kidole kuwa anaendesha siasa za kibabe tunashtuka sana na kujiuliza ni yuleyule au ni mwingine?
Yanayotokea Zanzibar kwa miaka 13 yanatofautiana nini na yale ya Zimbabwe na Kenya ambako Kikwete hakulala na angali halali usingizi akitafuta suluhisho?

Pengine Kikwete anakuwa mwepesi kushughulikia masuala ya kimataifa kwa kutaka kujenga international recognition?sitaki kuamini hivyo ingawa yawezekana ndivyo.Basi tusemaje sisi tunaoona mwafaka wa Zanzibar ukigeuzwa suala la kisanii na mustakabali wa wapemba uliwekwa pabaya.

Kikwete anapasawa kukumbuka kuwa kati ya mambo ambayo hayati mwalimu Nyerere aliyapigania ni suala la Wazanzibari na watanganyika kuwa kitu kimoja.Nje ya wazanzibari kwa maana ya wale wa unguja na wale wa pemba hakuna uzanzibari bali kuna u-pemba na u-unguja.Hapo ndipo visiwa vile vilipofikia hata kama ukweli utapingwa.

Kikwete anastahili kuona aibu pale anapoacha wanyumbani kwake wanaendelea kupigana vikumbo na kuacha kuzikana na kuuziana ili hali yu kiguu na njia nymbani kwa watu akiwahimiza wapatane.

Historia inatabia ya kusema ukweli, hata hii ya mpasuko wa Zanzibar itasema tu siku moja.

Muungwana siku zote ni vitendo na siyo maneno na mwenye kukutakia mema daima atakupasha ukweli japo unauma.
 
Tofauti kati ya Zimbabwe na Zanzibar ni kubwa sana; wakati Zimbabwe matatizo yao yanatokana na kila walichokipigania miaka 28 iliyopita, na kupambana na wajukuu wa kina Rev. Muzolewa na Ndabaningi Sithole wakisaidiwa na Wazungu ambao kwao ni kupoteza kama watawapa Wazimbabwe kile wanachostahili; Zanzibar ni muendelezo wa ubaguzi wa waarabu dhidi ya waafrika, sasa hivi kati ya Waunguja dhidi ya Wapemba, wakisaidiwa na serikali iliyojaa mafisadi Bara.
 
Mimi ninavyofahamu Zanzibar ni nchi (country) lakini Zanzibar sio Taifa (Nation).

Kwa hivyo basi Waziri Mkuu ameteleza!!!

Hajateleza,hadi sasa definition inayoongoza kuhusu maana ya nchi(state) ni ile ya mkataba wa montevideo,1939 kama sikosei mwaka,ambayo inadefine state na sio taifa.Taifa neno hilo linahusisha zaidi uasilia au link to a certain society of people.Ila kisiasa na kitaaluma kwa maana ya state ni ile yenye dola,watu,mipaka,uwezo wa kusaini mikataba(capacity to contract)ya kimataifa.Vipo vigezo vidogo kama bendera lakini cha msingi ni hivyo vitu vinne. Zanzibara inakosa kimoja au viwili kwenye dola inakosa jeshi,na capacity to contract haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa kama nchi isipokuwa kama jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Hakuna nchi ya Zanzibar.........
Someni katiba yetu (na ndiyo aliyoinukuu Mhe. Pinda).
"1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano."
 
Ipigwe kura ya maoni waulizwe wananchi maana kumbukumbu hazionyeshi kama wananchi waliulizwa kupitia kura ya siri kama wanautaka Muungano au hawautaki nafikiri hapa panatakiwa papigwe mstari, ili ipatikane suluhu kwa pande zote kama Watanganyika hawautaki na WaZanzibari wanautaka itakuwa hakuna muungano na kama Wazanzibari hawautaki na WaTanganyika wanautaka bado kutakuwa hakuna Muungano ,Muungano utakuwepo ikiwa wote watasema wanautaka ,haya shime tudai kura ya maoni.
 
[QUOTE----------bila Zanzibar kusingekuwa na Tanzania--[/size][/color][/QUOTE]

Sasa huyu mbunge anafikiri kuwa bila Tanganyika,Tanzania ingekuwapo?Au kwa upeo wake anafikiri Zanzibar ni muhimu kuliko Bara?Kama yeye haelewi mambo na maana ya muungano,akina yakhe wenzake huko jimboni kwake si balaa zaidi.Mhe spika kazi unayo
 
Nchi na Taifa ni kitu kimoja? Je yawezekana sehemu kuwa nchi na isiwe Taifa, na je Taifa laweza kuwepo bila kuwa nchi? Mifano...???

Clue: Someni Azimio la Uhuru la Marekani hasa sehemu ya mwisho linapotangaza kuvunja uhusiano wake na Mamlaka ya Mfalme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…