Nipo Zanzibar, hivi punde nimetoka kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Dharif Hamad. Ajenda kuu ilikuwa kauli iliyozua mjadala ya Pinda kuwa Zanzibar si nchi.
Maalim amemtaka Pinda awaombe radhi wazanzibari hadharani kwa kauli hiyo ambayo imewahuzunisha, kuwakwaza na kuwafadgaisha wazanznibari wote.
Lakini kikubwa, Maalim ameitumia kauli hiyo ya Pinda kuonyesha kuwa muungano wa sasa unaendeshwa kwa hila za kutaka kuiua Zanzibar. Anasema hili lilianza tangu awali na lilianzishwa na Nyerere ambaye alionyesha kuichukia Zanzibar tangu mwanzo.
Amesema Nyerere alitumia ghilba kumshawishi Karume (Original) akubali Muungano na alipokataa alimtishia kuwa ataondoa askari wake.
Kwa kuwa nchi ilikuwa changa (siku chache baada ya mapinduzi) karume alikubali lakini kwa sharti kwua Zanzibar iendelee kuwa nchi.
Maalim Seif anasema lakini hila za kuiua Zanzibar zilianza wakati huo na ndio maala masuala ya Muungano yameongezeka kutoka 11 ya awali hadi 23 hivi sasa.
Anasema kuongezeka kwa masuala ya muungano kunamaanisha kupungua kwa madaraka ya Zanzibar na hilo haliwezi kukubalika.
Amemtaka Shamsi Vuai kutangaza katika Baraza la Wawakilishi kuwa Zanzibar ni nchi na hiyo itasababisha kuwepo kwa mgororo wa kikatiba. Ameitaka SMZ itangaze mgogoro huo wa kikatiba na CUF itaiunga mkono.