Zanzibar ni taifa (nation) na sio nchi/jamuhuri (state).
Ni taifa kwa sababu kuu mbili: Ina mipaka inayotambulika,
Ina watu wanao share historia, lugha na utamaduni moja.
Sio nchi kwa sababu zifuatazo:
Haina jeshi lake peke yake, haina fedha yake peke yake, haina uhuru wa kutunga sheria zihusuzo mambo yote bila kuingiliwa, nk.
Same applies to Tanganyika/Tanzania bara.
Tanganyika au Tanzania bara haipo katika huu mjadala. Hiyo ondoa.
Mjadala ni Tanzania na Zanzibar.
Zanzibar sio Nchi wala sio Taifa.
Kuna nchi moja. Na Taifa moja. Na Dola moja.
Tanzania ni nchi moja. Ni Taifa moja. Ni Dola moja.
Maneno 'State,' 'Nation,' 'Country,' 'Sovereignty' na mengine ya kizungu, hayatakiwi kuingia katika mjadala kwa sababu Katiba halali ya Tanzania ni ile ya Kiswahili.
Haya niliyoyasema hapo sio maoni yangu. Ni tafsiri ya Katiba iliyoamuliwa na jopo la Ramadhani (J.A.), Kisanga (J.A), na Lugakingira (J.A) wa Mahakama ya Rufaa.
Katika mfumo wa Sheria za Kiingereza tuliourithi, Common Law, maamuzi ya mahakama katika kutafsiri sheria ndio yanakuwa sheria ya mwisho, ama sheria mpya,
Stare Decisis.
Baada ya kusema kuna nchi moja, Taifa moja na Dola moja, ambayo ni Tanzania, Majaji ikabidi waeleze sasa Zanzibar ni nini?
Hitimisho lao, Zanzibar ni Serikali tu.
Tofauti ni nini? Serikali ambayo sio Taifa, sio Nchi, na sio Dola, haiwezi kujiamulia mambo kivyake, kama vile, pamoja na mengine, kusaini treaty. Pia, haiwezi kujiunga na vyombo ambavyo vinataka members ambao ni Nchi au Taifa, au Dola. Haina Amiri Jeshi wa kuipeleka vitani kisheriai. Haiwezi kufanyiwa Haini.
Ndio maana Zanzibar ilijitoa UN na IOC mwaka 1964 na 1993. Ndio maana Zanzibar sio member wa AU. Ndio maana hakuna haini dhidi ya Zanzibar.
Kwa hiyo, tunaweza tukajadili Zanzibar inatakiwa iwe nini, au ingependeza iwe nini, au Pinda na Pandu wanasema Oxford Dictionary inasema Zanzibar ni nini. Lakini hakuna mabishano kuhusu Zanzibar ni nini.
Zanzibar sio Nchi wala sio Taifa. Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa.
_______________________________________
Reference: S.M.Z. vs. Machano Khamis Ali & Others (Criminal Application No. 8 of 2000) [2000] TZCA 1 (21 November 2000); Session Case No. 7 of 1999
Link: http://www.saflii.org/tz/cases/TZCA/2000/1.html