Ndivyo Ilivyo
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 243
- 4
U have got a point. Cheers up.Taratiiibuuuu naanza kuoana MPASUKO WA MUUNGANO wetu na Zanzibar.........
Soon mabadiliko makubwa yatakuwa muhimu kama tunataka Muungano UDUMU.
kwani tatizo nini? ni kwasababu kule pemba ndo kuna mafuta sasa wapemba ndo wamiliki mafuta yale peke yao? mbona hata bara kuna mafuta kule pwani ya kusini wamegundua na jana tu wameona dalili kubwa sana ya mafuta kwenye bonde la ziwa Rukwa? kama vipi, waacheni wapemba walale mbele na mafuta yao, na sisi wabara tutalala mbele na vyetu tulivyopewa na Mungu. tatizo kubwa ambalo ni moja ya hata kimegeo kinachomega muungano ni mafuta ya pemba. Je, kama mafuta yasingekuwapo pemba na yakawepo bara tu, kungekuwa na misukosuko yote hiyo?, basi muungano wetu ni wa siku za faida tu, siku zisizo na faida ni ugomvi. tunachowang'ang'ania sana wazanzibar ni nini? kwani sisi wabara hatuna nini? tunakosa nini, tunafaidika nini na wao kama sio wao kufaidika na sisi zaidi? you think we need them more than they need us? No, I don't think so. let them take their way and go. watuache watanganyika vyovyote watakavyo tuita, na sisi tutachimba mafuta vilevile. period.
Mgogoro wa Katiba si ajenda iliyoanzishwa na Seif Sharifu mwaka 1994 bali ni ajenda iliyoanzishwa miaka 10 kabla (1984) na waasisi wa ASP. Seif Sharifu analijuwa hilo lakini halisemi kwa vile yeye alikuwa mmoja wa walioisaliti harakati hiyo.
Muungano wa Tanzania ulipoanzishwa ulikuwa uwe kwa kipindi cha miaka 10 na baadae kuwepo paper itakayotathmini Muungan huo na kuangalia uwezkano wa kuendelea au la. Baada ya miaka 10 ya mwanzo hilo halikufanyika na baada ya kuunganishwa ASP na TANU hali ya kutotendewa haki kwa Zanzibar kulikithiri na kuwafanya waasisi wa ASP kudai hatua ya kurekebishwa Muungano. Katika hatuwa hizo Wazanzibari walitaka Muungano wa Serikali tatu.
Kwa bahati mbaya waraka wa madai hayo ulivujishwa na kufikia mikononi mwa WanaCCM vijana kina Seif Sharifu na kuupeleka kwa Nyerere.
Kilichofuata ni mchafuko wa Siasa Zanzibar uliowatowa madarakani kina Jumbe na Wazirui Kiongozi wake Brigedia Ramadhani Haji ( SOTE TUNAIKUBUKA KEJELI YA NYERERE KWA RAMADHANI HAJI YA HESABU YA MOJA NA MOJA TATU). Seif Sharifu na wenzake walitumiwa na Nyerere kama wasemaji wa matakwa ya Wazanzibari kupinga hoja ya Serikali Tatu.
Baadhi ya Waasisi wa ASP walimkabili Nyerere kwenye Kikao na kutaka kutangaza mgogoro wa Katiba na kilichofanyika ni kuwakamata baadhi yao na kuwatia gerezani na wale walionekana wana ushawishi Mkubwa kwa Wazanzibari wakatakiwa kujiuzulu. Baadhi ya Waasisi hao pia waliwasaliti wenzao.
Kwa hivyo Sera ya serikali tatu ni ya Wazanzibari wenyewe (ASP) lakini kikubwa ni kuwa Viongozi wa sasa wa CCM Zanzibar wameshafadhiliwa sana na wenzao Bara ili waweze kutumiwa kuiumiza Zanzibar na kutokana na unyeti wa Utaifa wa Zanzibar wananchi wako tayari kuwasikiliza CUF ili tuone utatuzi wa Tatizo hili.
Hivi Zanzibar wana mafuta ?
Lol,Kweli JF ni shule!
Thanks wachangiaji.. maana hapa napata mambo ambayo sikufundisha shule, chuo wala mtaani!
Du. Hamumtendei haki Mheshimiwa Pinda. Ama kweli kamba hukatikia ..... Lakini haya masuala (mtafaruku katika Muungano) yapo , ni ya muda mrefu na lazim (sasa) yajadiliwe kwa uwazi . Mheshimiwa Pinda amekuwa chahcu tu (chambo) cha mjadala. Asibabaike ni Mtu mzuri na jasiri.Ahahaha Ana Wakati Mgumu Sana Maana Mmmm Muungano Umemlalia Yeye Na Kauli Zake.....ama Ujengwe Au Uboreshwe Ama U............zote Hi Hatma Tokana Na Kauli Zake..bw Pinda
Ziara ya Makamba yazua hofu Zbar
na Mwandishi Wetu
Hao waasisi unaosema wao walishtuka kuwa madaraka yao waliokuwa nayo ambayo yalijikita katika kila aina ya madhila ikiwemo kupotea kwa watu bila kujulikana waliko, kutandikwa mikwaju n.k, ndio wakataka kuvunja Muungano na kwa yeyote yule ambaye alijua madhumuni ya waasisi hao basi angelifanya kila njia wasifanikiwe kuwarudisha Wazanzibari katika hali hiyo.
Seif alilofanya ni sawa na kwa vyovyote kama ni kuangalia sheria za nchi hao waasisi walikwenda kinyume na utaratibu ulowekwa.
Dua said:Joka kuu,
Kwa nini aulizwe Mtei kwani walikuwa wanafanya haya mambo kwa siri? Unataka kuniambia tulifika kwenye hatua ya kufanya biashara kama Kariakoo? Benki sidhani kama wanafanya biashara namna hiyo - Wabunge kama wanapenda ni swala la kuomba documents tu. Kila kitu kipo wazi. Tatizo kubwa lililopo ni Zanzibar kuona kwamba wanadhulumiwa lakini hawana proof ya hilo hivyo wanalialia kama chiriku.