Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mwenye kujua hisa kwenye kampuni au bank, sharti ajue ana-kiasi gani? hizi hisia ndugu zangu ni Tatizo...
 
Kasheshe,

..hili suala la hisa za ZNZ BOT bora aulizwe gavana wa mwanzilishi wa BOT Edwin Mtei.

..Mtei pia atakuwa anajua mambo mengi kuhusu mgawanyo wa mali za EAC kwasababu alikuwa ndiyo katibu wa mwisho wa EAC na baada ya hapo Waziri wa fedha.

..pia kulikuwa na msimamizi wa kimataifa kuhusu mgao wa mali za EAC akiitwa Dr.Victor Umbrich. huyo naye atafutwe atufafanulie ni nini kilichojiri.

..kuna habari kwamba ZNZ ilikuwa na akaunti yake ya fedha za kigeni nje ya BOT. nadhani IMF ndiyo waliokuja kulazimisha Tanzania tuwe na akaunti moja/ya pamoja ya fedha za kigeni.

..nadhani kipengele hicho hapo juu ndicho kilichopelekea kutengwa kwa nafasi ya Naibu Gavana maalum kwa M-ZNZ au M-TGK kutegemea na upande anaotokea gavana.

..naibu gavana toka ZNZ ameteuliwa kwa mara ya kwanza wakati wa Ugavana wa Dr.Idris Rashidi. Naibu gavana wa mwisho toka Bara alikuwa Ndewirwa Kitomari.

..vilevile kuna habari kwamba ZNZ ilitusaidia TGK kifedha wakati wa vita vya Kagera. sasa najiuliza fedha hizo zilitoka wapi kama tulikuwa na benki kuu na hazina moja?

..kama kulikuwa na hazina au Benki Kuu moja je iliwezekana vipi kutofautisha fedha za ZNZ kutoka zile za Tanzania au hata Tanganyika?

..pia hii Benki wa wananchi wa ZNZ ilianzishwa mwaka gani na imekuwa ikifanya shughuli gani?
 
Kwanza kabisa alieandika ni hodari, na kujua mambo yote aliyoandika kama yanaukweli basi tosha kua ni Phd yake huyu mwadnishi.

Ila hali inavyokwenda hivi sasa Tanzania, mafisadi kuweza kuvitumia vyombo vya umma na kufanikisha mambo yao - watakua walijifunza sehemu - na kutokana na huyu mwandishi hapo juu hakuna shaka hawa mafisadi walijifunza kwa Baba wa Taifa - Taifa la mafisadi!

Kuna usemi unaosema kwamba - ukila na kipofu usimshike mkono!

Well, mkono wa Zanzibar inaonekana kwatika haya yanayotokea ni mafuta.
 
kwani tatizo nini? ni kwasababu kule pemba ndo kuna mafuta sasa wapemba ndo wamiliki mafuta yale peke yao? mbona hata bara kuna mafuta kule pwani ya kusini wamegundua na jana tu wameona dalili kubwa sana ya mafuta kwenye bonde la ziwa Rukwa? kama vipi, waacheni wapemba walale mbele na mafuta yao, na sisi wabara tutalala mbele na vyetu tulivyopewa na Mungu. tatizo kubwa ambalo ni moja ya hata kimegeo kinachomega muungano ni mafuta ya pemba. Je, kama mafuta yasingekuwapo pemba na yakawepo bara tu, kungekuwa na misukosuko yote hiyo?, basi muungano wetu ni wa siku za faida tu, siku zisizo na faida ni ugomvi. tunachowang'ang'ania sana wazanzibar ni nini? kwani sisi wabara hatuna nini? tunakosa nini, tunafaidika nini na wao kama sio wao kufaidika na sisi zaidi? you think we need them more than they need us? No, I don't think so. let them take their way and go. watuache watanganyika vyovyote watakavyo tuita, na sisi tutachimba mafuta vilevile. period.

Unawafanya wanaoingangania Zanzibar ni wapumbavu? - sio hivyo kabisa na kinachotakikana Zanzibar si rasilimali yeyote iwe mafuta au chochote kile - kuna agenda kubwa sana ambayo kusema kweli imeshafanikiwa nayo ni kuuwa maaadili na hulka za Kizanzibari na kupunguza na kama sio kuuwa Uislam katika visiwa hivyo. This is long term planned strategy ambayo mtu wa kawaida si rahisi kuitambua ndio maana wewe unashangaa kwa nini Bara ambayo ni tajiri maradufu kuliko Znz bado wanangangania Muungano.
 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unakufa, kama siyo kwa kumezwa na EAC basi kwa kuvunjika, halafu baada ya hapo Pemba na Unguja zinaweza kujitenga vile vile.
 
Mgogoro wa Katiba si ajenda iliyoanzishwa na Seif Sharifu mwaka 1994 bali ni ajenda iliyoanzishwa miaka 10 kabla (1984) na waasisi wa ASP. Seif Sharifu analijuwa hilo lakini halisemi kwa vile yeye alikuwa mmoja wa walioisaliti harakati hiyo.
Muungano wa Tanzania ulipoanzishwa ulikuwa uwe kwa kipindi cha miaka 10 na baadae kuwepo paper itakayotathmini Muungan huo na kuangalia uwezkano wa kuendelea au la. Baada ya miaka 10 ya mwanzo hilo halikufanyika na baada ya kuunganishwa ASP na TANU hali ya kutotendewa haki kwa Zanzibar kulikithiri na kuwafanya waasisi wa ASP kudai hatua ya kurekebishwa Muungano. Katika hatuwa hizo Wazanzibari walitaka Muungano wa Serikali tatu.
Kwa bahati mbaya waraka wa madai hayo ulivujishwa na kufikia mikononi mwa WanaCCM vijana kina Seif Sharifu na kuupeleka kwa Nyerere.
Kilichofuata ni mchafuko wa Siasa Zanzibar uliowatowa madarakani kina Jumbe na Wazirui Kiongozi wake Brigedia Ramadhani Haji ( SOTE TUNAIKUBUKA KEJELI YA NYERERE KWA RAMADHANI HAJI YA HESABU YA MOJA NA MOJA TATU). Seif Sharifu na wenzake walitumiwa na Nyerere kama wasemaji wa matakwa ya Wazanzibari kupinga hoja ya Serikali Tatu.
Baadhi ya Waasisi wa ASP walimkabili Nyerere kwenye Kikao na kutaka kutangaza mgogoro wa Katiba na kilichofanyika ni kuwakamata baadhi yao na kuwatia gerezani na wale walionekana wana ushawishi Mkubwa kwa Wazanzibari wakatakiwa kujiuzulu. Baadhi ya Waasisi hao pia waliwasaliti wenzao.
Kwa hivyo Sera ya serikali tatu ni ya Wazanzibari wenyewe (ASP) lakini kikubwa ni kuwa Viongozi wa sasa wa CCM Zanzibar wameshafadhiliwa sana na wenzao Bara ili waweze kutumiwa kuiumiza Zanzibar na kutokana na unyeti wa Utaifa wa Zanzibar wananchi wako tayari kuwasikiliza CUF ili tuone utatuzi wa Tatizo hili.

Hao waasisi unaosema wao walishtuka kuwa madaraka yao waliokuwa nayo ambayo yalijikita katika kila aina ya madhila ikiwemo kupotea kwa watu bila kujulikana waliko, kutandikwa mikwaju n.k, ndio wakataka kuvunja Muungano na kwa yeyote yule ambaye alijua madhumuni ya waasisi hao basi angelifanya kila njia wasifanikiwe kuwarudisha Wazanzibari katika hali hiyo.

Seif alilofanya ni sawa na kwa vyovyote kama ni kuangalia sheria za nchi hao waasisi walikwenda kinyume na utaratibu ulowekwa.
 
Joka kuu

Kwa nini aulizwe Mtei kwani walikuwa wanafanya haya mambo kwa siri? Unataka kuniambia tulifika kwenye hatua ya kufanya biashara kama Kariakoo? Benki sidhani kama wanafanya biashara namna hiyo - Wabunge kama wanapenda ni swala la kuomba documents tu. Kila kitu kipo wazi. Tatizo kubwa lililopo ni Zanzibar kuona kwamba wanadhulumiwa lakini hawana proof ya hilo hivyo wanalialia kama chiriku.
 
Katika kipindi cha leo cha masuala ya papo kwa papo, mh, PINDA alikataa kujibu masula yanyohusiana na masula ya Muungano kwa maelezo kuwa anaogopo kuonekana mbaya kwenye muungano.

Masuala hayo yalihusu,
1. Nini kiliopo juu kati ya KATIBA na Makubaliano ya MUUNgano (Article of Union)
2. Kwa nini suala la Muungano halipelekwi kwa wanachi na Kujadiliwa baada ya majadiliano hayo kufanywa na CCM pekeee.
 
Hajakwepa; amesema suala hili amelikabidhi kwa Wanasheria Wakuu wa pande zote mbili. Spika akamuunga mkono.
 
Kweli JF ni shule!
Thanks wachangiaji.. maana hapa napata mambo ambayo sikufundisha shule, chuo wala mtaani!
Lol,

Ndo maana nikaamua kuiunganisha hii ili watu wajue tulikotoka na tulipo na wafikirie kwa mapana ni wapi Zanzibar inakwenda.

Haitopendeza mtu kuandika hivihivi bila kujua wapi tulipotoka na nini kimewahi kujadiliwa hapahapa JF!
 
Hilo litatusaidia sana hasa sisi ambao tumejiunga JF miezi michache iliyopita. Litapunguza kwa kiasi kikubwa threads na posts kujirudiarudia. Invisible, iangalieni na zile za CHADEMA.
 
Ahahaha Ana Wakati Mgumu Sana Maana Mmmm Muungano Umemlalia Yeye Na Kauli Zake.....ama Ujengwe Au Uboreshwe Ama U............zote Hi Hatma Tokana Na Kauli Zake..bw Pinda
 
Ahahaha Ana Wakati Mgumu Sana Maana Mmmm Muungano Umemlalia Yeye Na Kauli Zake.....ama Ujengwe Au Uboreshwe Ama U............zote Hi Hatma Tokana Na Kauli Zake..bw Pinda
Du. Hamumtendei haki Mheshimiwa Pinda. Ama kweli kamba hukatikia ..... Lakini haya masuala (mtafaruku katika Muungano) yapo , ni ya muda mrefu na lazim (sasa) yajadiliwe kwa uwazi . Mheshimiwa Pinda amekuwa chahcu tu (chambo) cha mjadala. Asibabaike ni Mtu mzuri na jasiri.
 
Muungano tulionao uko fragile/delicate sana,uamuzi wa pinda kutojibu tena na hivyo kuacha suala hilo lishughulikiwe ''kisiasa'' na wanasheria wakuu nafikiri ni uamuzi sahihi.Upande ule wa pili wa muungano jamani unabalaa duuuh acheni tu! ndiyo hapo huwa najuliza maswali mengi ambayo sipati majibu yake.mojawapo likiwa ni kwamba kama tanganyika tunafaidika nini na huu muungano?
 
Hao waasisi unaosema wao walishtuka kuwa madaraka yao waliokuwa nayo ambayo yalijikita katika kila aina ya madhila ikiwemo kupotea kwa watu bila kujulikana waliko, kutandikwa mikwaju n.k, ndio wakataka kuvunja Muungano na kwa yeyote yule ambaye alijua madhumuni ya waasisi hao basi angelifanya kila njia wasifanikiwe kuwarudisha Wazanzibari katika hali hiyo.

Seif alilofanya ni sawa na kwa vyovyote kama ni kuangalia sheria za nchi hao waasisi walikwenda kinyume na utaratibu ulowekwa.

Nafikiri tuwe waadilifu katika kuyaongea matatizo. Kwa bahati mbaya hao Waasisi unaosema wewe hawakuwa kwenye madaraka wakati huo. Tunaishi katika nyakati za Demokrasia na utawala bora hivyo hao waliotenda mabaya wangeadhibiwa kama kungekuwa na ushahidi. Kilicho na ushahidi ni kuwa Seif Sharifu alivunja harakati za kuikomboa Zanzibar kwa tamaa ya uongozi kwa vile wakati ule alikuwa bado ni mgeni wa siasa na hakumuelewa Nyerere.
Nafikiri suala hapa halikuwa kujadili kitendo cha kina Seif bali ni kuomyesha kuwa harakati za nmgogoro wa Katiba na Sera ya Serikali TATU si sera za Wapinzani kama ilivyodaiwa na wengi hata CCM Bara bali ni kujuvya watu kuwa harakati hizo ni muendelezo wa muda mrefu wa harakati za Wazanzibar katika Muungano huu usio wa haki.
 
Dua said:
Joka kuu,
Kwa nini aulizwe Mtei kwani walikuwa wanafanya haya mambo kwa siri? Unataka kuniambia tulifika kwenye hatua ya kufanya biashara kama Kariakoo? Benki sidhani kama wanafanya biashara namna hiyo - Wabunge kama wanapenda ni swala la kuomba documents tu. Kila kitu kipo wazi. Tatizo kubwa lililopo ni Zanzibar kuona kwamba wanadhulumiwa lakini hawana proof ya hilo hivyo wanalialia kama chiriku.

Dua

..njia uliyoelekeza ifuatwe ktk kuchunguza suala hili ni sahihi kabisa. wabunge wanaweza kuyapitia makabrasha ya BOT na East African Currency Board kujua kilichojiri.

..pamoja na pendekezo lako, ambalo ni zuri tu, nafikiri kuna umuhimu wa kuwahoji wahusika wakuu ktk kuvunjwa kwa East African Currency Board na kuanzishwa kwa BOT. sasa hoja hiyo ndiyo iliyonifanya nichomeke jina la Edwin Mtei, gavana wa kwanza wa BOT.

..vilevile kuna mgogoro/malalamiko kuhusu mgawanyo wa mali za Jumuiya ya Afrika Mashariki. katika hili Wabunge wanaweza kufuata ushauri wako wa ku-trace documents. again mimi naona ingekuwa vema kumhoji Dr.Victor Umbrich ambaye alikuwa msuluhishi wa kimataifa ktk zoezi la kugawana mali za EAC.

..off course mambo mengi sana yamekuwa yakiendeshwa kienyeji-enyeji ktk huu Muungano. hebu fikiria sheria ya ambapo Raisi wa ZNZ alikuwa Makamu wa Raisi wa Tanzania nzima. Lakini wakati huohuo Makamu huyo alikuwa hapigiwi kura na sehemu yoyote ya Muungano. Baada ya hapo Makamu wa Raisi akawa akipigiwa kura na upande mmoja tu wa Muungano.

..tabia ya kuendesha Muungano kienyeji-enyeji ndiyo leo inawafanya wa-ZNZ kuja na madai ya kulazimisha Raisi wao awe Makamu wa Raisi wa Muungano. hawafikirii kabisa kwamba waliompigia kura Raisi wa ZNZ hawafiki hata 10% ya population ya Watanzania.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom