Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mkuu MO,

Unajua ndugu yangu katika taifa kama letu na mazingara ya uongozi wetu na siasa kwa ujumla, unapopata angalau kidogo kinacho-make sense, basi unashukuru, maana kumbuka wangeweza kunyamaza kimyaaa, au wangeweza kuleta mauza uza kibao,


Lakini kwa kusema watatafuta maoni ya wananchi, angalau sisi wananchi tunaweza kuwafuatilia kwa makelele, si unakumbuka Hosea alivyosema kuwa Richimonduli haikuwa na noma, sasa si unajua kuwa anasubiri hukumu ya Waziri Mkuu, kutokana na mapendekezo ya wabunge kuwa aondolewe, pole pole mkuu, as a nation we are making progress, ingawa sio kwa kasi ambayo wengi hapa tungeitaka!

Sasa Mkuu hapa unajua kabisa tuna discuss the inner workings ya haya masuala. I repeat there is no need for all this craziness and rubbish amateur moves being done. U have to remember we are talking about human lives that might be lost because of one reason and one reason only:: Indecisive character za mkuu.

Watu wa CUF walikuwa wameshapowa na dhuluma walizotendewa kwenye uchaguzi. Sasa hawa viongozi wetu wanacheza chess lakini wote ni amateurs wameleta issue ya kura ya maoni?/ The moment U start talking about voting in a climate like Zanzibar trust me, trouble is just around the corner.

So let me ask::::

Kura za maoni ni binding???
Nani mwenye madaraka ya kuitisha kura za maoni??
Tume ya uchaguzi imeambiwa nini??


Yaani hata Karume ameweza kumshinda mkuu wa kaya kwenye issue hii, kwa kweli tumekwisha.

So CUF unadhani imewekwa kwenye position gani na hili??
CUF uongozi wao umekubali in good faith maamuzi ya mjadala uliocost nchi yetu billions, leo wanaambiwa never mind, tunataka kura za maoni!! Unafikiri wananchama wa CUF watawaona vipi viongozi wao??

We shall see plenty kwenye hivi vicircus vyetu vya kujitakia.

U either believe in something and do it, or U keep quiet.

JF, naomba watu wa IKULU wapewe maoni kuwa mkuu wa kaya aanze zile safari zake maana kumbe akikaa hapo magogoni ni even worse.
 
Kubwa zaidi ambalo litateka fikara za waandishi wengi wiki hii inayokuja ni kuitishwa kwa kikao maalum mwezi wa tano... ambapo Kikwete kawaambia wajumbe "agenda yao ya siri waliyokubaliana jana..

Pia wamekubaliana kuwa Butiama itakuwa ni makao makuu ya wilaya mpya itakayoundwa..

Mwenzangu naona magoli yameanza kusogezwa nyuma taratibu na kwa hakika.... sitashangaa ikisemwa kuwa kura ya maoni itafanyika mwaka 2009 na hicho kikao cha siri kitatoa taarifa rasmi mwezi wa tano mwaka 2010!

mengine zaidi ..... kesho!
 
tutayaweka matangazo hayo ili mpate nafasi ya kuwasikia viongozi hao wa CCM wakitangaza maamuzi hayo ambayo yana kila dalili ya kugusa viongozi wengi.. hasa masuala ya biashara na uongozi (itabidi usikilize vizuri hapo kwani kuna maneno wameyachagua vizuri sana)...
 
Tusingalie CCM na CUF kule ZANZIBAR tuangalie zaidi TAnzania kwa ujumla ipo hadithi inayosema mtoto wa mamba alikuwa akimwambia mama yake ewe mama DOMO hilo na yule mama alimjibu Unakuja huku huku mwanagu alikuwa namaana kuwa kila siku zikienda na yeye anakuwa lile domo lake na ukiangalia kwa upeo hapa mainland sasa watu akili zimezidi kupanuka siwapumbavu tena kama walivyokuwa miaka iliyopita tusubiri na wakati utatueleza
 
Sounds to be a very wise democratic political idea, na ndio demokrasia yenyewe kuwasikiliza wananchi wanataka nini, sasa sio tena kuanza ujanja ujanja kwenye kutafuta maoni ya wananchi on the ishu,

Halafu hii tabia ya kutafuta maoni ya wananchi CCM waitumie kila kona muhimu za maamuzi ya taifa letu, sio iishie kwenye muafaka tu!

Bravo NEC kwa hili!

Matatizo haya yote yasingetokea kama kweli CCM inajali na kuheshimu maoni ya wananchi. Wananchi waliamua kuwa hawaitaki CCM Zanzibar na wakaipa ushind CUF, lakini wakatumia mabavu.
 
kumbe hawakuwa na jipya,kama yesu alivyo waambia wale mafisadi waliokuwa wanataka kumsulubu mwenzao na nuku "asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe" basi wale mafisadi waligeuka kila mmoja akashika njia yake.Hivi ndivyo walivyofanya leo kule butiama.
 
Sasa kwanini Kupoteza muda wote huo? Mimi ninaona hiyo kura ya maoni ni Kiini macho tu Matokeo ya Uchaguzi zoote yana toa jibu katika hiyo Kuraya maoni yao
Na jee kama watu wa cuf nao watakataa hiyo kurayamaoni itakuwajee? hawa watu kweli wasanii wa nguvu kwani hilo jibu liliwezekana katika kikao cha kwanza tu cha huo ETI Muafaka.
 
Matatizo haya yote yasingetokea kama kweli CCM inajali na kuheshimu maoni ya wananchi. Wananchi waliamua kuwa hawaitaki CCM Zanzibar na wakaipa ushind CUF, lakini wakatumia mabavu.

Mkuu pole pole, maana ilipotokea mara ya kwanza 1995, Mwalimu baba wa taifa letu alihusika, kwa kumpa okay Salimini kwa hiyo careful mkuuu!

I mean mimi sio msemaji wa CCM, lakini baada ya kuongea na viongozi wengi huko Butiama, ni kwamba zimeongelewa ishu nyigi sana za CCM kama chama na chache za taifa, as we go on zitataanza kutolewa pole pole, lakini sina uhakika kama kuna tatizo na kuamua wananchi wapigie kura ya maoni muafaka huko visiwani, which personally I could care less, lakini nilifikiri ni uamuzi wa busara, na pia ikiwezekana wai-extend hiyo tabia kwenye ishus zingine pia za muhimu kwa taifa hasa kwenye elimu.
 
Mkuu pole pole, maana ilipotokea mara ya kwanza Mwalimu baba wa taifa letu alihusika, kwa kumpa okay Salimini kwa hiyo careful mkuuu!

Mkuu niko polepole na nimecheka kidogo.
Baba wa Taifa namuheshimu sana, ila hakuwa malaika.Alifanya mengi mazuri lakini kuna aliyokosea na mojawapo ndo hilo. Sasa hapo alimpa ok Salmini kwa kuwa yeye alikuwa TUME YA UCHAGUZI au vipi? Au unataka kuniambia kuwa Rais wa Zanzibar anapatikana kwa okay ya Mwalimu na siyo kura za wananchi.
 
Sasa hapo alimpa ok Salmini kwa kuwa yeye alikuwa TUME YA UCHAGUZI au vipi? Au unataka kuniambia kuwa Rais wa Zanzibar anapatikana kwa okay ya Mwalimu na siyo kura za wananchi.

Wewe mkuu unaanza uchokozi tu, hivi mukulu alipompa Mwinyi na Mkapa, yeye alikuwa ni nani mbona mchokozi wewe?
 
mwizi siku zote atakulaharamu na pale penye halaliyake hapatiki atafanya kila njia ilihiyo halali aigeuze haramu WANGAPI WAMESHA TANGULIA sisi tunajifanya wataalamu wa maisha hii ni hatari.kura ya maoni ni mzunguko kwanini wasiunde tume tu.
 
Kawawa, hakufanya kosa lolote kushika uongozi wa taifa na kumpisha Mwalimu, alipoamua kurudi, Kawawa was just being himself na who he is as a human being, bila ya kujali power, na ni uzalendo pia,

Sasa hapa ninaona juhudi zile zile za kujaribu kusafisha kitendo cha Mwalimu, kumshusha hadhi kiongozi mwenziwe, ambayo ukweli ni kwamba ilikuwa moja ya mapungufu makubwa ya Mwalimu, ilikuwa siku zote kutowapa nafasi wasaidizi wake kufanya maamuzi ya kuwapa fursa ya kujiamini kiuongozi, matokeo yake ni taifa letu kuwa mahali lilipo sasa kiuongozi,

Ni mpaka siku tutakapokubali kuwa Mwalimu, naye alikuwa na mapungufu na ndiyo hasa tatizo kubwa la taifa letu sasa hivi, na tukayachambua wazi kwa undani, tutaendelea tu kulaumiana bila sababu. Mwalimu alimuita Kawawa mjinga, lakini akasema Mkapa ana akili na ni Mr. Clean, lakini bado tu watu wanamtetea Mwalimu ku3wa hakuwa na makosa.

Mkuu sio uchokozi na hiyo hapo juu ni maandishi yako kuonyesha kuwa Mwalimu alikuwa anakosea.
 
Mkuu pole pole, maana ilipotokea mara ya kwanza 1995, Mwalimu baba wa taifa letu alihusika, kwa kumpa okay Salimini kwa hiyo careful mkuuu!

Mkuu hapa umenikumbusha jambo muhimu sana.

Sasa kama CCM inajua kwamba kuipa nafasi CUF kule Zanzibar si uamuzi wa busara ni njia gani sahihi ya kuwapa hao Wapemba na wa-Unguja uwezo wa kujitawala wenyewe?
 
Makosa mawili yalifanyika tangu awali ambayo itakuwa ngumu sana kujichomoa nayo:

i) Zanzibar ni nchi, lakini siku zote mambo mazito wamekuwa wakiamuliwa na watu wa bara. Mambo kama haya ya mwafaka hayakupaswa kuamuliwa na watu wa bara. Hili ni jambo linalohusu utawala wa Zanzibar na linapaswa kuamuliwa na wazanzibar. Kibaya na cha kutisha kuliko yote ni pale ambapo mnaamua jambo hili liimuliwe na chama cha siasa badala ya kuamuliwa na vyombo vya kikatiba kama BUnge. Zanzibar wana bunge lao, kwa nini hili jambo wamekuwa wakilikwepa. Ok, sasa wanasema wanapeleka kwa wananchi, iweje jambo kama hili waliamua upande mmoja tu bila kuwashirikisha wenzao? Nafikiri umefika mahala mambo ambayo hayahusu muungano, watu wa bara tuwaachie wenzetu wa Zanzibar wayaamue, tunaweza kusaidia wakituomba. This means that it was wrong in the first place kwa JK kujitapa kwamba angemaliza mgogoro wa Zanzibar kama Rais wa Muungano; it was wrong then and it is even more wrong today given his upward trend of indecisiveness and incompetence.

ii) Hili ni la muhimu zaidi, nalo ni kuwahusu CUF. Maalim na CUF wanacheza. Wanataka kuanzisha dunia yao ya mapambano. Sijaona popote duniani hapa hasa katika bara letu ambapo mabadiliko makubwa kama haya ya kugawana madarakani yalifikiwa bila upande mmoja kulazimishwa. Kitendo cha CUF kuvua viatu na kurudi vyumbani lilikuwa ni kosa kubwa ambalo watalijutia. Hakuna njia ya mkato katika jambo hili zaidi ya wananchi wenye uchungu, ambao Zanzibar wamejaa tele, kuingia barabarani. Yaani, watu wakubie ushindi wako, ukakubali mzungumze, mkakubaliane, wanakwenda wanajibanza sehemu halafu wanaibuka,wanakwambia subirini kwanza tukawaulize wenzetu tulioiba nao kama wanaona ni sawa tugawane mali tuliyokuiba, na wewe unasema hewala baba na unataka tukwambie una akili? Maalim, baba, ningekuwa ni mwanachama wako ningeandika barua ndefu ya kukuomba ujiuzulu, lakini kwa kuwa sio, inabidi nikupe pole tu yatosha.

Na sisi jamani hapa JF tuache kushangilia mafanikio hewa. Hivi hasa watu wengine mnachokishangilia hapa ni kipi? Tutaacha lini hasa kuwa mateka wa CCM kwa kiwango cha kutisha namna hii?
 
Mbwe mbwe zote zile hawakuwa na muafaka wala maamuzi ? Haya wananchi wenzangu tuendelee kuvumilia .Wamesema kura za maoni je zitaendeshwaje ili kufikia makubaliano ?Hakuna watu walio jiandaa kwamba hakuna MSETO huko kweli ?

Ati nini,KURA YA MAONI? Subirini matokeo yake...kama atutaambiwa X% ya wazanzibari wamekataa serikali ya Mseto,Kura Y% zimeharibika!!
 
Mbwe mbwe zote zile hawakuwa na muafaka wala maamuzi ? Haya wananchi wenzangu tuendelee kuvumilia .Wamesema kura za maoni je zitaendeshwaje ili kufikia makubaliano ?Hakuna watu walio jiandaa kwamba hakuna MSETO huko kweli ?

Hiyo inayodaiwa kuwa "kura ya maoni" kuhusu serikali ya mseto Zanzibar nadhani itasubiri uchaguzi mkuu ujao (kama kweli itafanyika). Hawa jamaa nawaheshimu kwa danadana, wanazijua kweli! Baada ya uchaguzi mkuu huo (ambao CCM itashinda kwa kishindo zaidi hasa iwapo Seif atagombea tena), natabiri kuwa tutatangaziwa kwamba mazingira ya kisiasa yamebadilika na hivyo hakuna tena mantiki ya kura ya maoni. Kwa hiyo vyote havitakuwepo: kura ya maoni haitakuwepo na wala serikali ya mseto haitakuwepo Zanzibar katika miaka hii ya karibuni. Na itabidi heshima iwepo maana somo la Anjouan limeeleweka vizuri!
 
Hivi wakuu naomba kuuliza, huu muafaka maana yake hasa ni nini?

Ninataka kuamini kwamba uchaguzi ulifanyika, CCM wakashinda, if this is true then muafaka ni wa nini hasa? Ninaomba mwenye kuelewa vizuri anifahamishe kuhusu huu muafaka, kwa sababu to me this thing inakaribia na insanity, I mean kuna aliyeshinda huo uchaguzi na aliyeshindwa, kama CUF walishinda wanamuafaka kitu gani haswa na waliowashinda yaani CCM? Kuna ishus za bongo huwa sizielewi ni muungano na huu muafaka ni mojawapo, can somebody please help me!

Mbona bara hakuna muafaka?
 
Chama cha Mapinduzi hakijaridhia mapendekezo yote ya kamati ya muafaka na hivyo kwa kupitia kikao chake cha kamati kuu kimerudisha mjadala tena kwa wajumbe wake ili wazungumze tena na CUF kwa kufuata maelekezo hayo.

Mojawapo ya mapendekezo hayo ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Zanzibar wanapewa nafasi ya kuamua mwelekeo wa kisiasa visiwani humo kwa kutumia kura ya maoni.

Na pia CCM imeazimia kuitisha kikao maalum (angalia makala yangu ya leo kwenye Tanzania Daima) kwa kuwa kuna mambo mazito ambayo yanalihusu Taifa na kikao hicho agenda yake imetajwa kuwa ni "siri" kubwa.

Baadaye leo tutaweletea KLHN Exclusive ripoti nzima ya maazimio kama ilivyosikika live kupitia klhnews na Bongoradio na pia hotuba ya mwisho ya Rais Kikwete.

We set the Standard, others follow...

Pia wametoa maagizo kadhaa kuhusu suala la maadili, Richmond, nidhamu n.k

Je Wazanzibar wakisema kura ya maoni wanayotaka wao ni ya kuamua kama waendelee kuwemo kwenye Muungano au wajitenge na wawe nchi huru, JK na CCM watawaruhusu?Hapa kutakuwa na kazi kubwa sana na inaonyesha dhahiri kuyumba kwa JK katika maamuzi yake.
 
Sounds to be a very wise democratic political idea, na ndio demokrasia yenyewe kuwasikiliza wananchi wanataka nini, sasa sio tena kuanza ujanja ujanja kwenye kutafuta maoni ya wananchi on the ishu,

Halafu hii tabia ya kutafuta maoni ya wananchi CCM waitumie kila kona muhimu za maamuzi ya taifa letu, sio iishie kwenye muafaka tu!

Bravo NEC kwa hili!

Mkuu wangu ningeomba hapa unifafanulie zaidi. Kwa maoni yangu ni kuwa kama mchakato wa siasa za Zanzibar ukiendelea kwa style ya chaguzi tatu zilizopita, tutakuwa tunaishia palepale pa CUF Kushinda na CCM kuingia madarakani na watu kuuawa na chuki kuendelea kupandikizwa, na maendeleo ya Zanzibar ambayo ni rahisi kabisa kuendelezwa yatakuwa nyuma kila siku.
Democracy sounds good, lakini tuwe realists hapa. Watakaoulizwa kuhusu mwafaka ni wazanzibari au ni wana CCM wa visiwani, na wana CCM wa Zanzibar ni kina nani hao? Salmin Amour na wenzake, au ni kambi mbili za CCM visiwani? Na hayo makundi ni sehemu gani ya idadi ya watu wa Zanzibar nzima na wanawakilisha maoni ya kina nani, na wanawakilisha na wanapigania maslahi ya kina nani?
Binafsi naona kuwa hilo litakuwa ni uchu wa watu wachache wa uroho wa madaraka, na kujaribu kuendeleza chuki na kukipolarize kisiwa. Naona ni ujinga kabisa, huku bara tunaona ufisadi ndio utaka kuua nchi, lakini visiwani tunaona kuwa uchu wa madaraka na chuki vitaka kusambaratisha kisiwa. Hailo ni hatari, hapa nimeanza kuona hatari ya Salmini ku-bounce back, na kama JK akionesha kulegalega kwenye hili, bado ataonesha udhaifu sana.
Huyu JK sasa hivi ana-persoanl issue na Salmin, naona sasa Salmin ataka kujibu mapigo, sijui hali halisi itakuwaje!
 
Back
Top Bottom