Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Ukweli utabaki wazi na hakuna haja ya kuupindisha. Zanzibar mwaka 1964 ndo iliomba kuungana na Tanganyika. Hakuna Mtanganyika laiyewahi kuwaza au kufikiria kuungana na Zanzibar kwa hiyo ni hiari ya Zanzibar kujitoa. Suala la kubadili muundo wa Muungano nalo ni tete lisilokubalika kwa Watanganyika wengi kwani lina maslahi ya Zanzibar pekee. Nani atabeba gharama za serikali ya Muungano na kwa faida ya nani? Mapato ya serikali ya Zanzbar ni bilioni 50 kwa mwaka wakati mapato ya Tanganyika ni bilioni 200 kwa mwezi. Sasa nani atabeba gharama za serikali ya tatu na kwa manufaa ya nani????
Nadhani Zanzibar wana uhuru wa kutembea mbele kwa mbele kwani hatuna kitu tunategemea toka kwao. Tanganyika tunaweza kuendeleza beach zetu vizuri sana na kuvutia watalii katika maeneo ya Kigamboni n.k .... well, Zanzibar wataona utalii utakavyoporomoka kwao !!

Mkuu.
Ukiondoka Muungano ndio tutajua faida ya Muungano kwa Tanganyika.
Lakini CCM wanajua faida ya Muungano ila wanazifanya ni siri kubwa.
Nani alitaka Muungano...historia zinasema kuwa Mwalimu alitumwa kumshawishi na kumtisha Karume aingie Muungano. Mwalimu alipata msukumo kutoka Amerika na UK.
 
Kama Mtanzania na mkereketwa wa umoja, imani yangu ni kuwa kuungana kuna faida, lakini muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliwekwa kimabavu na Mwalimu (Mungu amrehemu), akiwa na ndoto za kuleta umoja wa Afrika kama alivyokuwa Dr. Nkrumah. Sababu nyengine ni ya kiitikadi kuizuwia Zanzibar isielemee mrengo wa kusho (Urusi na China) wakati wa vita baridi. Muungano ule ulikuwa wautata na bado umegubikwa na utata.
Kwa hiyo sipingi Muungano lakini unapaswa kuwa wa serikali tatu - ya Muungano itayoshughulikia mambo ya ulinzi, mambo ya nje na fedha tu, ya Tanganyika na ya Zanzibar ambazo kila moja itajiendesha wenyewe, kila moja ikiwa na mamlaka kamili ya uendeshaji wa eneo lake, ili kuondosha malalamiko baina ya Watanganyika na Wazanzibari wanaodai kuelemeshwa mzigo na mwenzake.
 
Mkuu.
Ukiondoka Muungano ndio tutajua faida ya Muungano kwa Tanganyika.
Lakini CCM wanajua faida ya Muungano ila wanazifanya ni siri kubwa.
Nani alitaka Muungano...historia zinasema kuwa Mwalimu alitumwa kumshawishi na kumtisha Karume aingie Muungano. Mwalimu alipata msukumo kutoka Amerika na UK.
Blaza!......Tunajua historia,USA hawakuwa na interest yoyote na zanzibar,waingereza walimsapoti sultani ila baada ya mapinduzi wakataka kuleta manuwari iliyokuwa gulf of edn,ni ya marines,kuondoa fujo wakatoa condition sultani apite pwani ya dar es salaam bila kusumbuliwa na nyerere ahakikishe Okello,hanga na babu hawatainfluence serikali ya zanzibar kwa kuwa wao ni wakomunisti!!!..hii data iko wazi uliza ubalozi wa uingereza wakupe mlolongo jinsi balozi wao in 1964 alivyoandika telegramu kwa waziri mkuu wake kutoa ushauri.
 
Mkuu.
Nimemwaga maji juu ya mgongo wa bata?
Kama kejeli na matusi ndio hoja... basi endelea mkuu....

Ukumbuke sisi pia tunakataa kuungana na Kenya kwa hofu ya kuwa watatutawala...watatuzidi ujanja na shirikisho la kisiasa linakuja. Kama changa moto hii inatushinda sijui itakuwaje tukifika huko.

Hebu pata muda upitie hako kajarida ...shirikisho ndani ya shirikisho...link ipo post #12.
Samahani sana kwa lugha chafu Blaza! and I appreciate your calmness.
I am not for EAC either! hii miungano itatuletea balaa kwa kuwa haijumuishi jamii.Baada ya kutangazwa soko huria la EAC,kuna jamaa aliniuliza hivi hilo soko liko wapi?nataka kwenda kununua spea!
Now tell me if there was a political will in establishing the EAC!
 
Bila shaka asilimia zaidi ya 90 ya watanganyika hawaupendi muungano huo kwa vile umekuwa kero tupu.
 
Mi nadhan hakuna shida coz moyoni mwangu binafsi naamini wanzanzibar(tanganyika visiwani) hawana furaha na huu muungano, na sina shaka itafikia kipindi watanzania bara watadai tanganyika yao!
 
Ukweli utabaki wazi na hakuna haja ya kuupindisha. Zanzibar mwaka 1964 ndo iliomba kuungana na Tanganyika. Hakuna Mtanganyika laiyewahi kuwaza au kufikiria kuungana na Zanzibar kwa hiyo ni hiari ya Zanzibar kujitoa. Suala la kubadili muundo wa Muungano nalo ni tete lisilokubalika kwa Watanganyika wengi kwani lina maslahi ya Zanzibar pekee. Nani atabeba gharama za serikali ya Muungano na kwa faida ya nani? !!
Mkuu.
Pitia hiyo document,report iliyopo post #1.....page 7 ...Inapoanza....In Zanzibar itself,the Union.......
 
I am not for EAC either! hii miungano itatuletea balaa kwa kuwa haijumuishi jamii.Baada ya kutangazwa soko huria la EAC,kuna jamaa aliniuliza hivi hilo soko liko wapi?nataka kwenda kununua spea!
Now tell me if there was a political will in establishing the EAC!
Mkuu.
Miungano ni kitu kizuri kama itasimamiwa na kuendeshwa kwa faida ya wote.
Ubaya wa miungano tunayoifanya sisi Afrika ni wanasiasa tu ndio wanaoamua kila kitu bila ya kuwashirikisha wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa miungano hii.

Kuna msemo wa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Miungano inayosimamiwa na kuendeshwa kwa haki,usawa na mgawano wa tija kwa wanachama wake basi huwa inawavutia wengi kutaka kujiunga na miungano hiyo.

EAC si umeona Rwanda na Burundi wamejiunga karibuni tu baada ya kuona kuna faida...Huu wa kwetu sisi jee? Kuna nchi ambayo imeshawahi kutuma maombi ya kutaka kujiunga nasi? Kwa sababu gani?
 
Sam,
Unajua Wamarekani walivamia Hawaii, wakamwua mfalme wake, wakaiburuza katika USA, mambo kwisha. Hakuna hata siku moja unasikia Hawaii wanapiga kelele hiki au kile. Mwalimu alikuwa mwuungana sana. Angekuwa Nkrumah, Zanzibar hivi sasa ingekuwa mkoa tu. Hakuna kelele. Chagueni gavana wenu, mbunge wenu lakini katika Federal govenment kura yenu inalingana na idadi ya watu wenu. We should have done the same.

Yagujuu

Nyerere sio hakutaka kashindwa hasaaaa,na ever ever hamutoweza kuifanya zanzibar kuwa mkowa,na mutavitema hivi visiwa ,,mungu akipenda tutapata uhuru ambao tulionyang'anywa na muungano,tatizo kubwa sisi wazanzibari tunapinga katika huu muungano ni kiuchumi ,,,tumenyang'anywa mamlalaka yetu,sitokuchambulia sana ila sikiliza wanasheria hapa katika huu majadala wa muungano watakavyokuachambulia fudu wewe.
Sauti:Kongomano la katiba – 05 March 2011 | MZALENDO.NET
 
Mimi najuwa kuna badhi ya Watanganyika hua hawapendi wala hawataki kuitwa au kuskia jina la Tanganyika kutajwa au kutumiwa kwa ajili yao? hii nikutokana na Nyerere (SLEEPING PILLS)alizo wapa,Na pindipo ukimwita Mtanganyika ugomvi au nongwa tayari?.
Sasa tuseme Wzanzibar tukisema Muungano baasi nyiyi mutatambulikana kwa jina gani? Sisi Wzanzibar tumeikana na kuuikataa kabisa Tanzania au kuitwa Watanzania tokea miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Hii ni kutokana na Zanzibar ndio nchi ilio ungana na mshirika wake Tanganyika na ktk miundo yote ya miungano huwa hivi mfano cheko/slovakia,southkorea/northkorea,Sene/Gumbia na hii ni kutokana na kuwa nchi za Muungano mara zote huwa hazifi hubakia vile vile unaweza kubadilicha jina lako lakini huwezi kubadilicha jina la mwenzako mpaka umulize mwenyewe.
Sasa sisi Wzanzibar tumebakia na jina letu lakini lenu mumeuwa bila kutuliza.
Kwa hio mshirika wa Zanzibar ni Tanganyika ikiwa Tanganyika haipo na Muungano umekufaa,kilichobaki hivi sasa ni ujirani mwema lakini inaonekana nyiyi baado mumengagania Muungano? Muungano umechakufa na walouwa ni nyiyi wenyewe mulipo kaa na kuiticha Bunge la Tanganyika kuuwa Tanganyika na Katiba yake? sisi Wzanzibar tunasema kifo cha Tanganyika nichakujitakia wenyewe.
ikiwa sisi Wzanzibar kama munavyo sema tuna Rais wetu,bendera,wimbo wa taifa,mahkama etc sasa nani nyiyi alio wazuwia kufanya hivyo? akili nyingi mbele kiza bada ya kufa kwa Tanganyika Wzanzibar tulijuwa hakuna tena Muungano kuna mkubwa kumeza mdogo na kutawaliwa kimbinu Wzanzibar na sisi kutawaliwa hatutaki kama vile Mulivyo pigania uhuru wenu December9 1961 na sisi Wzanzibar tulijigomboa 1963 sasa ni mataifa mawili huru?.
Vipi leo nyiyi mututawale sisi wakati sisi uhuru wetu ni wakumwaga damu na kupoteza vizazi vyetu ili kuigomboa ardhi yetu ya Bibi zetu na Babu zetu,kama kutawaliwa kutamu kwa nini hamukubakia ktk utawala wa kutawaliwa?.
Kama Munataka Muungano turudi ktk meza ya mazungumzo kwa pande zote 2 Serekali ya Tanganyika na ya Zanzibar kujadili Muungano wa pande mbili wananchi wanao utaka sihivyo bakini na Tanzania yenu mulioipigania uhuru na sisi tutabaki na Zanzibar yetu finish.
Watanganyika wenye akili zao na wenye kujuwa haki wanajuwa kuwa Muungano tulokuwa nao hautofika mbali kila mtu hayuko tayari kupoteza utaifa wake wa asili, sio nyiyi wala sio sisi? udgo wa nchi yetu na watu wake sio hoja ya kumezwa kwa asili yetu Zanzibar ni nchi na ina historia yake refu na nitabu kuimeza historia ya Zanzibar.
Kufaa kwa Tanganyika na katiba ya Tanganyika kumeleta Comfuse ktk Muungano, ndio ukaona hivi sasa Bara wanazungumzia kuandikwa kwa katiba mpya? Zanzibar wako mbali na hilo wao wanazungumzia makubaliano ya Muungano.
Sasa hii ni fursa mzuri ikiwa Wana wa Tanganyika mutataka kurudicha Tanganyika yenu na katiba yenu kusimamia mambo yenu yasio ya Muungano? katiba mpya kwenu itawasaidia nini ikiwa hamuna nchi kama musemavyo? au nchi yenu ni hio Tanzania?.
Kama nchi ni Tanzania sisi wzanzibar hatumo jitambulicheni wazi kuwa mumebadili jina la Tanganyika kuita Tanzania ili mujulikane sio mbaya ni sawa na Zaire kuita Kongo na kama tutazungumza kuhusu Muungano itakuwa Muungano wa Tanzania na Zanzibar?. Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote.
 
Kwa kuwa ilikuwa ni ridhaa ya watu wawili TU, huku wananchi wakiachwa bila kutoa ridhaa yao kama wanaridhia au hawaridhii muungano wa Tanganyika na Zanzibar sasa ni wakati muafaka wa kufanya mchakato wa kura za maoni juu ya muungano wa nchi mbili hizi ili kukata mzizi wa fitna.

Naomba zoezi hili liende sambamba na mchakato wa kura za maoni za katiba mpya.

Ili tujue mbichi na mbivu.

BNN
 
..lakini hiyo inaweza kuwa gharama isiyo na ulazima kwa wa-Tanganyika.

..bora kura hiyo wapige wa-Zenj halafu watuletee majibu, then wa-Tanganyika tutajua la kufanya.
 
Wazanzibar hawatakubali kwani Zanzibar inafaidika zaidi na muungano kuliko Tanganyika, muungano ukivunjika WAMEKWISHAA.

1. Wazanzibar/Wapemba wataomba uraia wa Tanganyika
2. Kiasi kikubwa cha chakula kinachoingia Z'Bar kinatoka Bara kwa uchumi walionao hawataweza kuagiza chakula kwa fedha za kigeni.
3. Umeme wanaoutumia toka bara wataweza kuulipia kwa gharama halisi? Mungu epusha, mgao wa umeme ukitokea serikali ya bara haitakubali kupeleka umeme Z"bar wakati wananchi wake wako gizani
4. Waheshimiwa wabunge wa Bunge la Tanzania toka Z'bar wakirudi kwao inakuwaje??

Hebu ongezeni athari/faida za kuvunjika muungano, nani atafaidika na nani atapata hasara, tupate picha kamili ikiwa kesho tunaingia katika zoezi la kupiga kura..
 
Hayo yote wangaliyajua wananchi wa Zanzibar labda wasingepiga kelele za kunyonywa wakiwa ndani ya muungano!
 
Wazanzibar hawatakubali kwani Zanzibar inafaidika zaidi na muungano kuliko Tanganyika, muungano ukivunjika WAMEKWISHAA.

1. Wazanzibar/Wapemba wataomba uraia wa Tanganyika
2. Kiasi kikubwa cha chakula kinachoingia Z'Bar kinatoka Bara kwa uchumi walionao hawataweza kuagiza chakula kwa fedha za kigeni.
3. Umeme wanaoutumia toka bara wataweza kuulipia kwa gharama halisi? Mungu epusha, mgao wa umeme ukitokea serikali ya bara haitakubali kupeleka umeme Z"bar wakati wananchi wake wako gizani
4. Waheshimiwa wabunge wa Bunge la Tanzania toka Z'bar wakirudi kwao inakuwaje??

Hebu ongezeni athari/faida za kuvunjika muungano, nani atafaidika na nani atapata hasara, tupate picha kamili ikiwa kesho tunaingia katika zoezi la kupiga kura..

Nyongeza:-

5. Kiulinzi na kiusalama Zanzibar haina resources za kutosha ukiongeza na jiografia yake ni balaa tupu.

6. Kipengele (5) hapo juu kinamaanisha Zanzibar itakuwa koloni/makao makuu ya akina Al-Shabaab na Al-Qaeda (in fact hii pia ni hatari kwa bara na nchi jirani).

7. Zanzibar itakuwa ni mojawapo ya njia kuu na kituo muhimu sana cha madawa ya kulevya duniani pamoja na bange kama ilivyo kule Afghanistan na Pakistan.

8. ... nk.

Ndugu zangu Mungano una faida mara mia hata kwa wazanzibari kuliko hasara. Vinginevyo, tujaribu ujinga, muda si mrefu tutaona matokeo yake na itakuwa "too late".
 
Sasa inakuwaje wa zenji wengi wanalalamika kuwa muungano unawanyonya na hauna faida yoyote kwa maendeleo ya znz, na ni kwa nini wazenji wengi wameivest Tanganyika lakini hakuna watanganyika wanao invest zenji?
 
Nyongeza:-

5. Kiulinzi na kiusalama Zanzibar haina resources za kutosha ukiongeza na jiografia yake ni balaa tupu.

6. Kipengele (5) hapo juu kinamaanisha Zanzibar itakuwa koloni/makao makuu ya akina Al-Shabaab na Al-Qaeda (in fact hii pia ni hatari kwa bara na nchi jirani).

7. Zanzibar itakuwa ni mojawapo ya njia kuu na kituo muhimu sana cha madawa ya kulevya duniani pamoja na bange kama ilivyo kule Afghanistan na Pakistan.

8. ... nk.

Ndugu zangu Mungano una faida mara mia hata kwa wazanzibari kuliko hasara. Vinginevyo, tujaribu ujinga, muda si mrefu tutaona matokeo yake na itakuwa "too late".

Ndiyo maana nikashauri kura za maoni ili tujue wananchi wa Tanzania wanamaoni gani juu ya muungano.

Wenzetu wana bendera, wimbo wa taifa, rais, nchi, mipaka, wabunge kwenye bunge letu, mawaziri kwenye baraza letu lakini bado haitoshi, tupige kura za maoni tupate suluhu.
 
LICHA YA ADUI HATARI ITAKAYOIUA CCM KWA HARAKA ZAIDI NDANI KWA NDANI HIVI KARIBUNI, CHAMA HIKI KIKO MBIONI KUJITWISHA MIZIGO MIPYA KUMBEBA LOWASA NA HASA KUFANYA MAUAJI YA SAUTI PINZANI KISIRI KUSAFISHA NJIA

Kama uliwahi kufikiria kwamba CHADEMA ndicho adui mkubwa itakayoiua CCM basi kumbe kweli huelewi kabisa siasa za taifa hili zilivyo lakini hivi sasa kundi dogo ndani ya CCM linaloshikilia uhai wa chama hiki kiko mbioni 'KUSAFISHA NJIA KWA NAMNA YOYOTE ILE mmoja wao kushaka dola 2015.

Kwa wadadisi wa mambo, adui mkubwa zaidi na wa kutisha ajabu tayari yuko chumbani kwao CCM na hivi karibuni italipuka kuliko KINU CHA NYUKLIA CHA JAPAN na kutuma mionzi itakayoifuta kabisa CCM bukia chama cha upinzani namba 4 baada ya NCCR-Mageuzi hapa nchini.

Kwa kugusia tu kwa uchache; adui namba moja na hatasri mno hadi hivi, kwa haki kabisa kwa misingi ya kichama walichojiwekea, ni kwamba kule Wa-Tanzania Visiwani wanakiona CCM kama Chama kilichowasaliti kushika dola baada ya Mhe Benjamin Mkapa.

Hakika jambo hili la USALITI WA CCM KWA WATANZANIA VISIWANI ni tishio kubwa hivi sasa ambapo majina zaidi kutoka Bara yaendelea kutajwa KUMRITHI Mhe Kikwete ambaye naye kwanza hata hatima yake bado haiko wazi kwa umma wa Tanzania.Kwa jinsi mambo yalivyo nchini itakavyolipua Naona baada ya CCM kuwatapeli Wa-Tanzania Visiwani nafasi ya kugombea Urais, katika ule mpango wao maalum wa SIASA ZA KUKABIDHIANA UONGOZI WA NCHI KWA ZAMU KWA WATOTO WA WAKUBWA tu Bara na Visiwani.

Kitendo cha kikundi fulani kujipenyezea fedha haramu kupitia kwa akina Rostam Aziz na Edward Lowasa katika dakika za majeruhi kushawishi maamuzi kumtosa Mhe Salim Ahmed Salim (ambaye alipendwa sana bara na kuaminiwa mno na CCM-Mwalimu Nyerere) kule Dodoma, ndipo jini dume lenye vichwa viwili lilipozaliwa na kuleta salamu za maangamizi kwa hiki chama kilichowahi kupata umaarufu wa miaka mingi sana na kuaminiwa wa wengi nchini.

Miongoni mwa hizo salamu ni pamoja na (1) Wana-Mtandao badala ya Wana-CCM (ambao nao walikujakugawanyika mbele ya safari na kuwa (i) Wanamtandao Walaji (MAFISADI WA HIVI LEO) na Wanamtandao Waliwa ambao nao mahasibu yao mazito na yanayo nuka mno tutakuja kuyaelezea siku nyingine humu, (2) Wana-CCM Bara ambao lao ni kuwatumia baadhi ya Wana-CCM maswahiba kutoka Visiwani wakiwachezesha kama mchezo wa CHESS au DRAFT KISIASA ili kuzuia Wa-Tanzania wa kawaida Bara na Visiwani kuwa na maamuzi yoyote juu ya nani awaongoze isipokua tu maamuzi yote yatatoka siku zote kwa hii CCM Bara tu kwa sura zima ya Jamhuri yetu ya Muungano Tanzania.

Sasa kwa ujio wa CHADEMA na kuendelea kupendwa sana kwa chama hiki na azma yake ya KURUDISHA UONGOZI WA NCHI MIKONONI MWA WANANCHI WENYEWE kote Bara na Visiwani, na haya madai Moto Moto ya sisi Vijana kutaka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kote ndani ya taifa letu tayari zimekua ni mwiba mchungu katika ngozi ya kikundi hiki cha WAJANJA WACHACHE Wana-CCM Bara ambao mpaka hivi sasa, kwa mujibu wa habari nyeti za ndani sana chumbani mwao, kila ramani ya kisiasa wanalolichora linagoma kabisa, fedha walizokwisha wekeza kwenye juhudi hizi zote Bara na Visiwani zakumbwa na hatari za wazi mno na migawanyiko kuongezeka kila kukicha kati yao.

Hata nako ndani ya kikundi hicho cha hao Wajanja wachache Wana-CCM kumeibuka nako Migawanyiko mikali ya KI-KANDA kwa namna ambayo hata juhudi gani zifanyike hakuwezekani kupatanishwa kitu hata wakafanya kazi kwa pamoja.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya CCM katika ujumla wake, hali si shwari hata kidogo mle!! Wapo hata wale ambao, kwa ufinyu tu wa mawazo, wamefikia mahala wamependekeza MAJINA 15 ya baadhi ya watu mashuhuri na tishio kwa maslahi yao KUUAUA. Lini wauawe na kwa MTINDO GANI usioweza kuleta tafrani kwa kile wanachokiita 'Tishio la Nguvu ya Umma' kutokuweza kuwakumba.

Japo tatizo letu Wa-Tanzania tuliowengi ni mpaka tushikishwe jambo kiganjani ndio tuamini na wakati mwingine kugutuka kukiwa kumechelewa sana, miongoni mwa HAYO MAVUNO YA MIKONO YA KI-SHETANI tayari wameorodheshwa baadhi ya vinara wa kupinga madhambi ya CCM kwa njia mbali mbali nchini.

Kati ya watu wanaolengwa wamo (i) baadha ya viongozi tishio kwa kinyang'anyiro cha kiti cha urais 2015 waliomo ndani na nje ya hicho kikundi cha Rostam Aziz na Edward Lowasa. Pia, (ii) wapo baddhi ya viongozi wa serikali za wanafunzi nchini, (iii) baadha ya Wana-JF ambao wametajwa kama 'wakorofi na waharibifu', (iii) baadhi ya viongozi wa dini katika kanda fulani ambao wameelezewa kuwa na 'vinywa pana' na kuonekana kukisaidia CDM, (iv) wafanyabiashara wanaohofiwa kukifadhili CHADEMA hivi sasa na (v) na baadhi Wanataaluma wanaoonekana kujitolea kukisaidia CDM ki-mikakati ambayo hadi sasa yaelezewa KUKIDHOOFISHA MNO hiki chama tawala.

Sasa chama hiki chaonekana kubuni (1) mkakati mpya wa UONZOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kukabidhiwa kwa zamu ile ile ila safari hii ni NDANI KWA NDANI TANZANIA BARA na vile vile ni (2) kwa KUZINGATIA AMA URAFIKI, UJIRANI AU UDINI kufanya hivyo.

Hata hivyo nako mambo si yenyewe baada ya wale wafadhali wa Uarabuni (Libya, Misri na Iran) nazo kukumbwa na matatizo kibao, yale yanayoendelea na yale ambayo yatalipukia kwao miezi michache ijayo; kikundi hiki ndani ya CCM kimechanganyikiwa kupindukia kwani kwani ufadhili wao hauna uhakika tena huku wananchi tukiendelea kulishikilia bando DOWANS na mianya mingine itakayotumika kuchota kodi zetu kuyatekelezea haya yote.

Dawa ya yote haya wanayopangwa kutekelezwa kwa mikono ya giza ni (1) kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anageuka kuwa mlinzi wa mwenzie dhidi ya juhudi hizi hatari, (2) kusimama kidete kwa KUSISITIZA Katiba Mpya ya Wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi kupitishwa Bungeni mwezi ujao, (3) kuendelea kuhakikisha kwamba UTEUZI WA JOHN MIMOSE CHEYO kushika tena ile kamati kule bungeni haiwi tena kichochoro tena cha Mafisadi kujichotea fedha kununulia kura na kutekelezea mambo machafu huku Cheyo akijifanya hajaona kitu kwenye vitabu vyetu!!
 
Nyongeza:-

5. Kiulinzi na kiusalama Zanzibar haina resources za kutosha ukiongeza na jiografia yake ni balaa tupu.

6. Kipengele (5) hapo juu kinamaanisha Zanzibar itakuwa koloni/makao makuu ya akina Al-Shabaab na Al-Qaeda (in fact hii pia ni hatari kwa bara na nchi jirani).

7. Zanzibar itakuwa ni mojawapo ya njia kuu na kituo muhimu sana cha madawa ya kulevya duniani pamoja na bange kama ilivyo kule Afghanistan na Pakistan.

8. ... nk.

Ndugu zangu Mungano una faida mara mia hata kwa wazanzibari kuliko hasara. Vinginevyo, tujaribu ujinga, muda si mrefu tutaona matokeo yake na itakuwa "too late".
ndege ni zao, meli kasa ni yao na...........pia zao wao, unaongea usio yajuwa.
 
Back
Top Bottom