Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Mbona hauna saini wala nembo au ndio jamaa wakasema hauna uhalali
 
Na kwa kuujadili kwa kina unahitajika uliopo sasa ambao wanasema umiongezwa viraka na kufanyiwa ukarabati bila ya kuulizwa wananchi ,hapo ndipo palipowaangusha CCM na kuwauliza wananchi juu ya muwafaka wao na CUF eti wakidai unagusa masuala muhimu katika uongozi wa Zanzibar ,sasa sijui lipi litakuwa linagusa na kuweza kusababisha kifo cha kunaswa na umeme.
 
Uhuru wa Zanzibar ulipatikana
10 Decemba 1963, kutoka kwa Uingreza kama mamlaka kamili chini ya Sultan. Hapa ilikuwa baada ya muungano wa chama cha Zanzibar National Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba peoples party, kuwa na serikali ya mwafaka wakiunganisha viti vyao kama serikali ya mwafaka na kuwa na jumla ya viti 13, dhidi ya viti 10 vya Afro Shirazi Party (ASP).

Utawala huu haukudumu baada ya serikali iliyoshinda katika uchaguzi wa kidemokrasia kupinduliwa Januari 12, 1964 katika mapinduzi yaliyoongozwa na Mganda John Okello. . Sheikh Abeid Amani Karume akatangazwa kuwa rais wa People's Republic of Zanzibar and Pemba.

Watu kati ya 5,000-12,000 wakiwa wazanzibari wenye asili ya uarabu na wahindi waliuawa na mali zao zilitaifishwa katika mapinduzi hayo.

Mpaka hapo CCM kama mtoto wa ASP haina asili ya serikali ya mseto, maana ni chama hicho ndicho kilichoipindua serikali ya mseto inayodaiwa kuingia madarakani kidemokrasia. Na hiyo tarehe ya uhuru Mhh!

mkuu hayo maneno ya upande mmoja wa akina wapenzi wa sultani sasa upande wa pili huyataki? au na ww ni mpenzi wa hao masultani?

ule ni uhuru wa bandia, tulifanyiwa kiini macho na ss tuling'amuwa
 
kama ndio huu basi sio mkataba bali hi makubaliano. mkataba bila sahii ni null and void ab initio
 
Hivi hili suala la kuuliwa jamii za kiasia (Waarabu na wahindi) kwa wingi huo mnaziamini ,ni kweli waliuliwa lakini si kwa kiasi hicho maana idadi ya watu wa Zanzibar ilikuwa haifiki hata Laki wala haikaribii kwa wakati huo.
Je katika kupekua pekua mnawajua ni akina nani walioongoza Mapinduzi au machafuzi ? Kwa ufupi ni vijana wa kiarabu ambao nao pia walikuwa na usongo na watawala na ndio waliokuwa wakiongoza na kuonyesha wapi pa kupigwa nani na nani ni wa kukamatwa ,kwa ufupi ni mapinduzi kama mapinduzi mengine kusema ilikuwa ni kuwaondoa waarabu hilo jambo linavaliwa tu kama kutaka kuyaficha na kuyafunika mengine ,lakini ukweli unabaki pale pale kuwa mambo yalikuwa ni wenyewe kwa wenyewe na sio kumwondosha Muarabu ,Hebu nendeni mkajisomee kwa kituo mujionee namna serikali ya Mapinduzi ilivyouwa wengi waliouliwa baada ya Mapinduzi ni wana Mapinduzi wenyewe.

http://www.fortunecity.com/victorian/abbey/313/ukweli8.html#NAMNA WALIVYO ULIWA
 
Huu ni original pamoja na kuwa hauna sahihi na ndomaana wanalinda sana wenye sahihi usionekane kwa watu wa CUF kuna ambao umerekebishwa sana kama kuna mtu anao anweza kutuwekea hapa tuine tofauti. Wenye sahihi uwezi kuupata maana ndo uhai wa Tanzania otherwise ni Tanganyika na People's repulic of Zanzibar
 
Kwa kuanzia,,

Kimsingi Zanzibar ilikosea kujiunga na OIC miaka ya mwanzoni wa tisini kwa sababu mambo ya nje ni mambo ya Muungano..na kwa maana hiyo ilipaswa bunge la Muungano likae lijadili hiyo hoja.....
 
Shukrani, mwenzetu aliyepost hii humu JF(Jamco_za). Sasa nnaendelea kuupitia kusoma kama ipo clause ya kusema kuwa Muungano unaweza kuvunjwa au la

lakini kwa sasa mkataba wenyewe ni huuu na sioni kwa nini ulikuwa unafichwa na kwa manufaa ya nani

anyway tuendelee na mjadala

Hakuna kitu....
Hakuna haja ya kusoma soma huo mkataba mambo yalisha isha...
1.Viongozi walio bariki muungano wetu wamesha kufa...na kutokana na utamaduni wetu ....hiyo ni nati namba moja..

2.Nyerere alichanganya Udongo *mchanga wa aridhi ya Zanzibar na Tanganyika... sijui uo mchanganyiko upo wapi..?Labda ulimwagwa baharini ... hii ni nati namba mbili

ok!! someni na Lakebisheni maandishi ili twende sawa lakini kwenye kuvunja muungano haito wezekana...Labda Mkachambue mchanga kwenye kibuyu...

au msubiri viongozi wafufuke...
 
Kwa kuanzia,,

Kimsingi Zanzibar ilikosea kujiunga na OIC miaka ya mwanzoni wa tisini kwa sababu mambo ya nje ni mambo ya Muungano..na kwa maana hiyo ilipaswa bunge la Muungano likae lijadili hiyo hoja.....

Hawakukosea kwani yale yalikuwa ni mashirikiano ya Kimataifa na hilo lilijuilikana ndio maana ikaundwa Wizara ya Mambo ya Nje na Mashirikiano ya Kimataifa na kulibandika katika clause za Muungano ikawa Zanzibar haina tena nafasi ya kufanya mazungumzo au kushirikiana na Taasisi yeyote ya Kimataifa bila kupata baraka za Wizara hiyo.
 
Itakuwa vema ukifafanua zaidi hapo kwenye rangi nyekundu

Nini cha kufafanua hapo na ulisema Mapinduzi ni faida ya Waafrika wa Visiwani ndio nikakuuliza Waafrika wa upande gani na hizo takwimu ni za kuonyesha nani ana serikali na nani anapata manufaa.

Au unataka nikuongezee kuwa kati ya wanafunzi waloenda masomoni mwaka 2007 nchini Malaysia wote walitoka Unguja au Pemba hakuna walio na sifa au hawastahili hiyo faida ya Mapinduzi - fanya utafiti mdogo tu katikavyuo vya Ellimu ya kati na vikuu wanafunzi wa Zanzibar waliopata nafasoi kupitia SMZ ni nani anayefaidi Mapinduzi ya 64 utajua.
 
Hawakukosea kwani yale yalikuwa ni mashirikiano ya Kimataifa na hilo lilijuilikana ndio maana ikaundwa Wizara ya Mambo ya Nje na Mashirikiano ya Kimataifa na kulibandika katika clause za Muungano ikawa Zanzibar haina tena nafasi ya kufanya mazungumzo au kushirikiana na Taasisi yeyote ya Kimataifa bila kupata baraka za Wizara hiyo.

Sijui kama nimekuelewe lakini nikisoma naona kama unakubaliana na mimi kuwa hilo suala lilipaswa lipate baraka za wizara ya mambo ya nje ambayo ni ya muungano...walifanya hivo?
 
The question starts with who is "WE" Is it Nyerere and Karume? Is it the people of Tanganyika and of Zanzibar, what is the motive behind the whole thing.
Kama kweli ni huo huo tu, kuna mambo mengi naona kama hayamo, kama vile distribution ya resources.
 
GT kuna kitu kimo kwenye huu mkataba nitakiunganisha wiki ijayo na nina uhakika watu wanaweza kushtuka sana maana yake.... Ukikiangalia kwa haraka haraka kwenye mkataba huwezi kukiona..

asante sana yaani umenifanya niunganishe dots mbili ambazo kwa karibu mwaka mzima zimekuwa zikinipiga chenga.
 
Mojawapo ya vitu vilivyoleta matatizo ni hilo la resources distribution, lakini baadae walifanyia malekebisho na kukubalina jinsi ya kugawana misaada na madeni ya muungano, lakini walisahau natural resources kama mafuta mpaka zanzibar ikadai mafuta sio mali ya muungano. Je pesa kutoka kwenye dhahabu haitumiki zanzibar?
 
Sijui kama nimekuelewe lakini nikisoma naona kama unakubaliana na mimi kuwa hilo suala lilipaswa lipate baraka za wizara ya mambo ya nje ambayo ni ya muungano...walifanya hivo?

Ukumbuke kuwa wakati huo nani alikuwa Rais wa Zanzibar - Mwalimu aliwahi kumwita mbogo - Salmin alijua kuwa Ushirikiano wa Kimataifa mwanzo haukuwa katika kipengele cha Muungano na kiliwekwa kkinyemela kama yalivyowekwa mambo mengine kama suala la Madini, Fedha nk.

Sasa yeye kwa vile pale alitaka kufanya uhusiano na OIC hakuwa na haja ya kuomba ruhusa ya Wizara ambayo yeye anajua haikuwa na mamlaka hayo - alolitaka yeye na uhusiano na Shirika la Kimataifa na wala sio kutakakutambulika kuwa kama nchi awe na ubalozi na vitu kama hivyo.

Ndio nikakwambia hawakukosea.
 
Ahaa! Sasa nimekuelewa...kumbe suala la wizara ya mambo ya nje pia lilichomekwa kinyemela...then ina maana huu wa sasa uko so diluted...ule original uko wapi?
 
Mojawapo ya vitu vilivyoleta matatizo ni hilo la resources distribution, lakini baadae walifanyia malekebisho na kukubalina jinsi ya kugawana misaada na madeni ya muungano, lakini walisahau natural resources kama mafuta mpaka zanzibar ikadai mafuta sio mali ya muungano. Je pesa kutoka kwenye dhahabu haitumiki zanzibar?

Kinachozungumzwa hapa sio pesa inatumika vipi ni jee hicho kipengele kilikuwepo na kama hakikuwepo kwa ninni kilipoingizwa yakatajwa mafuta tu na zisitajwe dhahabu, almasi , Tanzanite , Uranium, gesi na natural resource zote - kama ni matumizi wacha waachiwe mafuta yao na wao ( kama wanayo) na halafu pesa zinazopatikana nazo zitatumika tu Tanzania hii.Na halafu Mkuu neno kusahau hakuna ila ilikuwa imeachwa makusudi kuleta utata au tuseme loop hole ili wajanja waitumie hiyo nafasi.
 
Back
Top Bottom