Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uhuru wa Zanzibar ulipatikana
10 Decemba 1963, kutoka kwa Uingreza kama mamlaka kamili chini ya Sultan. Hapa ilikuwa baada ya muungano wa chama cha Zanzibar National Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba peoples party, kuwa na serikali ya mwafaka wakiunganisha viti vyao kama serikali ya mwafaka na kuwa na jumla ya viti 13, dhidi ya viti 10 vya Afro Shirazi Party (ASP).
Utawala huu haukudumu baada ya serikali iliyoshinda katika uchaguzi wa kidemokrasia kupinduliwa Januari 12, 1964 katika mapinduzi yaliyoongozwa na Mganda John Okello. . Sheikh Abeid Amani Karume akatangazwa kuwa rais wa People's Republic of Zanzibar and Pemba.
Watu kati ya 5,000-12,000 wakiwa wazanzibari wenye asili ya uarabu na wahindi waliuawa na mali zao zilitaifishwa katika mapinduzi hayo.
Mpaka hapo CCM kama mtoto wa ASP haina asili ya serikali ya mseto, maana ni chama hicho ndicho kilichoipindua serikali ya mseto inayodaiwa kuingia madarakani kidemokrasia. Na hiyo tarehe ya uhuru Mhh!
Shukrani, mwenzetu aliyepost hii humu JF(Jamco_za). Sasa nnaendelea kuupitia kusoma kama ipo clause ya kusema kuwa Muungano unaweza kuvunjwa au la
lakini kwa sasa mkataba wenyewe ni huuu na sioni kwa nini ulikuwa unafichwa na kwa manufaa ya nani
anyway tuendelee na mjadala
Kwa kuanzia,,
Kimsingi Zanzibar ilikosea kujiunga na OIC miaka ya mwanzoni wa tisini kwa sababu mambo ya nje ni mambo ya Muungano..na kwa maana hiyo ilipaswa bunge la Muungano likae lijadili hiyo hoja.....
Itakuwa vema ukifafanua zaidi hapo kwenye rangi nyekundu
Waombe hao CUF wasipate huo MKATABA WA MUUNGANO baina ya TANGANYIKA na ZANZIBAR ambao ni siri kubwa kuliko siri zote Tanzania
Hawakukosea kwani yale yalikuwa ni mashirikiano ya Kimataifa na hilo lilijuilikana ndio maana ikaundwa Wizara ya Mambo ya Nje na Mashirikiano ya Kimataifa na kulibandika katika clause za Muungano ikawa Zanzibar haina tena nafasi ya kufanya mazungumzo au kushirikiana na Taasisi yeyote ya Kimataifa bila kupata baraka za Wizara hiyo.
Sijui kama nimekuelewe lakini nikisoma naona kama unakubaliana na mimi kuwa hilo suala lilipaswa lipate baraka za wizara ya mambo ya nje ambayo ni ya muungano...walifanya hivo?
Ukumbuke kuwa wakati huo nani alikuwa Rais wa Zanzibar - Mwalimu aliwahi kumwita mbogo - Salmin alijua kuwa Ushirikiano wa Kimataifa mwanzo haukuwa katika kipengele cha Muungano na kiliwekwa kkinyemela kama yalivyowekwa mambo mengine kama suala la Madini, Fedha nk.
Sasa yeye kwa vile pale alitaka kufanya uhusiano na OIC hakuwa na haja ya kuomba ruhusa ya Wizara ambayo yeye anajua haikuwa na mamlaka hayo - alolitaka yeye na uhusiano na Shirika la Kimataifa na wala sio kutakakutambulika kuwa kama nchi awe na ubalozi na vitu kama hivyo.
Ndio nikakwambia hawakukosea.
Mojawapo ya vitu vilivyoleta matatizo ni hilo la resources distribution, lakini baadae walifanyia malekebisho na kukubalina jinsi ya kugawana misaada na madeni ya muungano, lakini walisahau natural resources kama mafuta mpaka zanzibar ikadai mafuta sio mali ya muungano. Je pesa kutoka kwenye dhahabu haitumiki zanzibar?